Hotuba za Rais kila mwezi

Hotuba za Rais kila mwezi

Je unaridhika na hotuba za Rais Kikwete?

  • Ndio

    Votes: 13 15.5%
  • Hapana

    Votes: 71 84.5%
  • SIJUI

    Votes: 0 0.0%
  • Sina jinsi

    Votes: 1 1.2%

  • Total voters
    84
  • Poll closed .
JK tumeona ulivyolishughulikia la Richmond na tunangoja utekelezaji wa Pinda.

JK tumeona ulivyolishughulikia la BoT na tunangoja utekelezaji wa tume.

Kwenye haya mkuu D, tuko wote yaani kwenye the same page.
 
Matatizo makubwa sana yalikuwepo kabla ya ubinafsishaji, kwa nini viwanda, mashirika, mabenki, mashamba tulivyo vitaifisha na tulivyojenga wenyewe vifikie mpaka kubinafsishwa? jibu ni rahisi sana, tulishindwa kuviendesha na vikafa ndio vikabinafsishwa. Kipi ambacho kiliweza kujiendesha kwa ufanisi na kuliingizia taifa faida kilibinafsishwa?
 
Kuhusu ujenzi wa bara bara ya kanda ya kusini, mbona mwanzo ilitangazwa kwamba itajengwa bara bara ya Tunduru - Songea - Mbambabay? hapo mbona amepunguza kilomita nyingi sana? yaani Tunduru- Namtumbo na Mbinga Mbambabay. Katika ilani ya CCM bara bara hii inatambulika na imeahidiwa kujengwa. kulikoni?

Ilani ya CCM na msaada wa GB ni vitu viwili tofauti, kwani uliambiwa GB kaja kutekeleza ilani za CCM? usichanganye mambo.
 
Sasa mlitaka ataje scandals zilizo kikumba chama chake? Huyo atakuwa sio mwanasiasa. Wanasiasa hawaongelei matatizo, wanaongelea mafanikio.

..kwahiyo kuwashughulikia richmondulis haikuwa mafanikio?

Kuhusu wananchi wa kawaida nafikiri kuna faida kwenye UKIMWI na Malaria.

..watu hawajui kesho watakula nini,unafikiri wanajali huo ukimwi na hayo manyalia?

Hizo hotuba za mwezi huwa haziwi na kitu cha ajabu na nia yake ni kurudia mafanikio yaliyokuwepo kwa mwezi au mategemeo kwa mwezi unaokuja.

..na matatizo pia! kuongoza nchi kunahitaji ujasiri! waulize cuf wanasemaje.

Naona JK ameweka mtaji wake wote kwa rais Bush, sijui kama yeye anawaamini hao akina Bush labda kama kuna kitu wanataka Tanzania.

..wala,huyo bush atasahaulika muda si mrefu. kuna burning issues to deal with!

..halafu,wanataka kipi ambacho bado hawajakipata,toka kwetu?
 
Kwanza hebu fafanua una maana gani ya kusema watu masikini

..watakapo choma gari lako au la nduguyo,au kulipiga mawe,ndio utafahamu maana yake!

..maana yake,kama kenya ilivyokuwa! waliopora maduka,waliochomeana nyumba na waliobakana hawakuwa matajiri.
 
Kama wewe mtoto wa Fisadi, au ndo Fisadi mwenyewe hutakuwa uelewi maana ya neno masikini, ila kwa jamii ya Tanzania neno ili ni kawaida,
Vipi mnashirikiana na bwana mkubwa kututia kwenye kaango la umasikini nini, mbona unamtetea huyu Fisadi? au ndo nyie anao walinda nini? Maana unanitisha kama uelewi maana ya neno Masikini wewe ni hatari sana

Huko tunapoelekea neno Fisadi litakuwa ni ujiko fulani, maana watu kama wewe mnashindwa kujua neno hilo linatunika kwa mtu wa wasifa gani...

Sikubaliani kabisa kuwa Watanzania ni maskini labda ni mafukara tu.. Kwani uwezo tunao wa kutoka katika hali hii ya maisha chini lakini yanakwamishwa na mambo chungu nzima, kuanzia elimu hadi afya.

Iwapo serikali inajua hilo na inatekeleza kwa kuweka ruzuku katika mambo kadhaa ili kupunguza ugumu wa ufukara na watu mnabeza kwa kuvuli cha ufisadi basi wewe na wenye mawazo kama yako mtakuwa ni mapunguani tu.

Malaria na Ukimwi ni majawapo ya vikwazo vya mwanzo katika kurudisha maendeleo au jitihada za mtu binafsi na jamii katika kushiriki katika kuiunua uchumi wake na taifa kwa ujumla.

Katika hotuba hiyo tumeweza kujua hatua kubwa zilizofikiwa katika kuondoa tatizo hilo. Hii ni habari nzuri kwa wananchi wote wa kawaida.

Ujenzi wa barabara, upanuzi wa kiwanja cha ndege, utafutaji wa nguvu mpya ya nishati sio mambo ya kubeza kwa wale ambao kila siku hushindwa kutekeleza jitihada zao kutokana na upungufu wa hayo yaliyotajwa hapo juu.

Njia nzuri ya kushiriki hoja hii ni kuangalia kwa namna gani jitihada hizo zitatekelezwa kwa wakati na kuchambua mafanikio yake na athari zake katika utekelezaji na ni kwa namna gani zitaweza kumnufaisha mwananchi wa kawaida.
 
Matatizo makubwa sana yalikuwepo kabla ya ubinafsishaji, kwa nini viwanda, mashirika, mabenki, mashamba tulivyo vitaifisha na tulivyojenga wenyewe vifikie mpaka kubinafsishwa? jibu ni rahisi sana, tulishindwa kuviendesha na vikafa ndio vikabinafsishwa. Kipi ambacho kiliweza kujiendesha kwa ufanisi na kuliingizia taifa faida kilibinafsishwa?

..mi nimekupenda hapo tu! kumbe ukweli unaujua ila umeng'ang'ania tu!

..wakati ule na sasa hamna tafauti! fyi!
 
Hivi kuna mtu anaweza kufafanua hii MCA acct inavyofanya kazi????

From what I know ni kuwa hizo funds USD 650 million, zitatolewa in 5yrs yaani 2008-2013 na only if congress wataaprove kila kiwango kwa kila mwaka.

From the way the us govt deficit debacle is going, and if congress and the new admin in 2009 wants to balance the budget itakuwa kazi.

JK anavyoongea utadhani ujenzi wa hivyo vitu unaanza next week.

my 1 cent.
 
Mnyika,
Thanks for the speech. I was more interested in your comments on the speech.
Naona GB amechukua muda mkubwa wa speech hiyo.
 
Matatizo makubwa sana yalikuwepo kabla ya ubinafsishaji, kwa nini viwanda, mashirika, mabenki, mashamba tulivyo vitaifisha na tulivyojenga wenyewe vifikie mpaka kubinafsishwa? jibu ni rahisi sana, tulishindwa kuviendesha na vikafa ndio vikabinafsishwa. Kipi ambacho kiliweza kujiendesha kwa ufanisi na kuliingizia taifa faida kilibinafsishwa?

jaribu NBC, BIMA
 
Katika hitimisho la hotuba yake, Mheshimiwa Rais ameongelea mafunzo kutoka Kenya kwa ufupi mno kana kwamba alimlazimu akatishe hotuba yake na asiwe mpembuzi wa kina wa tulichojifunza. Ama amekwepa kuwa mkweli kuwa tuna mambo mengi ambayo ni chumvi na pilipili zinazosaidia fukuto ambalo laweza kutufanya tufikie mpasuko na utengano kama yaliyotokea Kenya.

Nanukuu

Wakati tukiwapongeza Wakenya kwa mafanikio yaliyopatikana na kuwapa pole kwa magumu yaliyowakuta yatupasa kujiuliza mafunzo gani tunayopata. Mafunzo hayo ni muhimu ili tujiepushe na kasoro zilizowafikisha hapo. Kwa maoni yangu, fundisho kubwa sana tuliloliona ni kuwa kuendeleza ukabila ni jambo hatari sana kwa taifa. Bahati nzuri, katika nchi yetu tatizo la ukabila halipo, lakini linaweza kuwepo tusipokuwa waangalifu kwa vile makabila yapo. Nawasihi, ndugu zangu, tusiwape nafasi wale wote wanaofanya vitendo vinavyoweza kuturudisha kwenye ukabila.

Lakini, kwa nchi yetu lililo hatari la kujiepusha nalo si la ukabila tu, lipo la udini na yapo masuala ya ubaguzi mwingineo. Kenya hawakuwa na tatizo la udini lakini la ukabila lilitosha kuivuruga nchi. Je, kama lingeongezeka na tatizo la udini ingekuwaje? Tufanye kila tuwezavyo tuhakikishe kuwa tunapiga vita kwa uwezo wetu wote vitendo, fikra au hata mwelekeo tu unaoweza kutugawa kwa misingi ya makabila yetu, dini zetu, rangi za ngozi zetu, maeneo tutokako na mengineyo. Wale wenzetu wanaotaka kutupeleka kubaya tusiwape nafasi. Tusivumilie kauli zao za uchochezi au matendo yao ya kibaguzi. Misingi iliyowekwa na waasisi wa taifa letu hususan hayati Mwalimu Julius Nyerere na hayati Abeid Amani Karume daima tuienzi. Tukiipuuza ole wetu.

Kwa Tanzania, tatizo la kwanza litakalo leta machafuko ni lile la Matabaka ya WenyeNacho na WasioNacho! Mgawanyiko huu mkubwa ambao umeweka zege kali kati ya Masikini na Matajiri iko siku utafikia tamati na damu itamwagika.

La pili ni lile la Rangi/Dini (Zanzibar)! Tayari tumeshaona roho zisizo na hatia zikipoteza maisha kule Zanzibar na hata kwenye machafuko ya kidini bara.

Nitaomba nimuulize Mheshimiwa Kikwete, umesema ni muhimu tujiepushe na kasoro zilizotokea Kenya na kuleta vurugu, Je Serikali yako na Chama chako CCM vinaafikiana na kauli zako? Maana ikiwa katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiteto, Ubabe wa CCM na unazi wa Serikali kwa kuzembea haki itawale wiki mbili zilizopita kulihatarisha usalama na karibu roho zipotee je ni jitihada gani unazifanya wewe kama Rais na Mwenyekiti wa Chama tawala kutuepusha na hizo kasoro kama ulivyotutahadharisha?

Je ni lini utahakikisha kuwa kuna Muafaka Zanzibar?

Umesema "wale wenzetu wanaotaka kutupeleka pabaya tusiwape nafasi". Chama chako CCM na Serikali yake imejijenga kwa kuwa na tabaka la kung'ang'ania madaraka na zaidi kuwa na kundi la viongozi ambao wanakimbilia kujilimbikizia mali kwa njia zozote (Mafisadi) mpaka kuhujumu na kusahau dhamana yao kama viongozi na wajibu wao kulitumikia Taifa. Utafanya nini kwa nguvu zako za Kiserikali na Kichama kuhakikisha ule upenyo uliokomaa wa Uhujumu kwa makusudi au uzembe unazibwa na kuwa tunakuwa na Viongozi waadilifu ambao ni mfano chanya wa kuigwa ili kuchochea uzalishaji mali kwa njia halali kuondokana na umasikini na si kutafuta njia fupi fupi ambako kumeishia kujenga mgawanyiko wa tabaka la matajiri na masikini?

Je utaruhusu Sheria na Haki vifanye kazi yake kusahihisha makosa na uhalifu uliotokea (BOT, RICHMOND) au utaendelea kuruhusu mchakato ulioko sasa hivi wa kusameheana kimya kimya kwa kuona aibu kuumbuka?

Je Juma aliyeko Makunduchi na Bundala walioko Maswa wakijirudi makosa na kurudisha walichochokua kwa njia danganyifu, watapewa msamaha na heshima ya kuwa huru kimya kimya kama hao wanaorudisha pesa za EPA?

Kama unatamka tusiwape nafasi wale wenye kuwa vichochezi vitakavyoishia kuleta vurugu, inabidi uitumikie kauli yako kwa mifano niliyokupa hapo juu.

Nakutakia kila la heri katika kikao cha Kamati Kuu wiki ijayo!
 
Katika hitimisho la hotuba yake, Mheshimiwa Rais ameongelea mafunzo kutoka Kenya kwa ufupi mno kana kwamba alimlazimu akatishe hotuba yake na asiwe mpembuzi wa kina wa tulichojifunza. Ama amekwepa kuwa mkweli kuwa tuna mambo mengi ambayo ni chumvi na pilipili zinazosaidia fukuto ambalo laweza kutufanya tufikie mpasuko na utengano kama yaliyotokea Kenya.

Nanukuu

Kwa Tanzania, tatizo la kwanza litakalo leta machafuko ni lile la Matabaka ya WenyeNacho na WasioNacho! Mgawanyiko huu mkubwa ambao umeweka zege kali kati ya Masikini na Matajiri iko siku utafikia tamati na damu itamwagika.

La pili ni lile la Rangi/Dini (Zanzibar)! Tayari tumeshaona roho zisizo na hatia zikipoteza maisha kule Zanzibar na hata kwenye machafuko ya kidini bara.

Nitaomba nimuulize Mheshimiwa Kikwete, umesema ni muhimu tujiepushe na kasoro zilizotokea Kenya na kuleta vurugu, Je Serikali yako na Chama chako CCM vinaafikiana na kauli zako? Maana ikiwa katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiteto, Ubabe wa CCM na unazi wa Serikali kwa kuzembea haki itawale wiki mbili zilizopita kulihatarisha usalama na karibu roho zipotee je ni jitihada gani unazifanya wewe kama Rais na Mwenyekiti wa Chama tawala kutuepusha na hizo kasoro kama ulivyotutahadharisha?

Je ni lini utahakikisha kuwa kuna Muafaka Zanzibar?

Umesema "wale wenzetu wanaotaka kutupeleka pabaya tusiwape nafasi". Chama chako CCM na Serikali yake imejijenga kwa kuwa na tabaka la kung'ang'ania madaraka na zaidi kuwa na kundi la viongozi ambao wanakimbilia kujilimbikizia mali kwa njia zozote (Mafisadi) mpaka kuhujumu na kusahau dhamana yao kama viongozi na wajibu wao kulitumikia Taifa. Utafanya nini kwa nguvu zako za Kiserikali na Kichama kuhakikisha ule upenyo uliokomaa wa Uhujumu kwa makusudi au uzembe unazibwa na kuwa tunakuwa na Viongozi waadilifu ambao ni mfano chanya wa kuigwa ili kuchochea uzalishaji mali kwa njia halali kuondokana na umasikini na si kutafuta njia fupi fupi ambako kumeishia kujenga mgawanyiko wa tabaka la matajiri na masikini?

Je utaruhusu Sheria na Haki vifanye kazi yake kusahihisha makosa na uhalifu uliotokea (BOT, RICHMOND) au utaendelea kuruhusu mchakato ulioko sasa hivi wa kusameheana kimya kimya kwa kuona aibu kuumbuka?

Je Juma aliyeko Makunduchi na Bundala walioko Maswa wakijirudi makosa na kurudisha walichochokua kwa njia danganyifu, watapewa msamaha na heshima ya kuwa huru kimya kimya kama hao wanaorudisha pesa za EPA?

Kama unatamka tusiwape nafasi wale wenye kuwa vichochezi vitakavyoishia kuleta vurugu, inabidi uitumikie kauli yako kwa mifano niliyokupa hapo juu.

Nakutakia kila la heri katika kikao cha Kamati Kuu wiki ijayo!

Hili tabaka la walionacho na wasionacho ndio la kuangalia sana. Pengo kati ya walionacho na wasionacho linazidi kuongezeka kila kukicha. La udini kwa maoni yangu halina nguvu sana maana intermarriages kati ya waislamu na wakristo ni nyingi hivyo itasaidia kupunguza uwezekano wa vurugu na la ukabila pia kwa sababu ya intermarriages pia halina moto sana, bali la kuangalia ni hili la wenye nazo na wale ambao hawana kitu.
 
Sasa mlitaka ataje scandals zilizo kikumba chama chake? Huyo atakuwa sio mwanasiasa. Wanasiasa hawaongelei matatizo, wanaongelea mafanikio.

Kuhusu wananchi wa kawaida nafikiri kuna faida kwenye UKIMWI na Malaria.

Hizo hotuba za mwezi huwa haziwi na kitu cha ajabu na nia yake ni kurudia mafanikio yaliyokuwepo kwa mwezi au mategemeo kwa mwezi unaokuja.

Naona JK ameweka mtaji wake wote kwa rais Bush, sijui kama yeye anawaamini hao akina Bush labda kama kuna kitu wanataka Tanzania.

Sasa hapo ndipo wanapokosea. Wananchi sio wajinga ati! Wakadanganywe kwamba kuna mafanikio wakati hali wanaiona inazidi kuwa ngumu ukilinganisha na miaka miwili au mitatu iliyopita. Wananchi walipiga kura kwa wingi kumchagua JK kwa ahadi za maisha bora kwa kila Mtanzania, ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya. Wananchi hawajaona lolote kati ya hayo na wala hakuna dalili. Yeye anataka kuongelea mafanikio yakuja Kichaka wakati SK imegubikwa na kashfa kila kona! Kwani mwanasiasa ukisema kweli kuhusu matatizo yanayokabili serikali yako kuna tatizo gani? Hata wananchi watakuheshimu kwa kuwa mkweli. Unapoanza kuyakwepa matatizo yanayokukabili na kutotaka kuyazungumzia ndio story za kila aina zinaibuka, ukaonekana msanii na credibility yako kuzidi kuanguka.
 
Kikwete na waandishi wake wa hotuba ni zero kabisa.

Kasema kuna mambo matatu lakini kaongelea mawili tu, lile la tatu kaliogopa!

What a joke!
 
Hizo hotuba za mwezi huwa haziwi na kitu cha ajabu na nia yake ni kurudia mafanikio yaliyokuwepo kwa mwezi au mategemeo kwa mwezi unaokuja.

Naona JK ameweka mtaji wake wote kwa rais Bush, sijui kama yeye anawaamini hao akina Bush labda kama kuna kitu wanataka Tanzania.

Mimi naona tunasahau jambo moja muhimu kuwa mtegemea cha nduguye hufa maskini.

Hapa naona JK anazidi kupandikiza fikra za utegemezi miongoni mwa wananchi. Ni kitu cha hatari sana kwa mustakabali wa maendelea yetu. Believe or not, hatuwezi kufika mbali kwa kumtegemea huyo Bush.

Yaani tungojee mpaka atuletee pia na neti jamani, wakati watoto wanaendelea kuteketea kwa malaria??.Kweli serikali inashindwa kuzuia vifo vya watoto kwa kuwapatia neti wanapozaliwa?Hii ilitakiwa ipatiwe kipaumbele kama ulivyo mpango wa elimu.

Maendeleo tutayaleta kwa juhudi zetu sisi wenyewe, mtu asidanganye vinginevyo. Dunia ya sasa hakuna cha bure. Chochote tupewacho ni lazima tutalipa kwa namna moja au nyingine.

Naomba kuwasilisha
 
Yaonyesha JK na CCM yake wanavyopenda na kutegemea misaada kama ndio mkombozi number moja wa Tanzania. Kaacha ongelea hot issues zinazogusa raia kwa sasa badala yake anaongelea misaada. Kwanza hizo pesa (USD 650 million) si leo tutapewa na pia hazitatosha kwa shughuli zote zilizosemwa lakini CCM wanaendelea kututangazia matumaini hewa ili mradi waendelee kuongoza.
Tulishapewa mabillion ya dollar ya misaada na hatujufika popote, nashangaa mpaka leo CCM hawajui ukweli kua TZ itajengwa na watz wenye uchungu na nchi yao. Kenya washafanya usanii mpaka yamewakuta, na TZ ikiendelea kwa mwendo huu nasi yatatukuta licha ya joto dogo dogo tulilokwishapata. Aliyekata tamma haogopi kufa, hasa anapoona labda kifo chake kitaleta mabadiliko kwa watoto, ndugu zake na raia wengine wataobaki. TZ si shwari tena, kutokea ya Kenya si ndoto tena na CCM watambue hilo. Dawa si kushinda uchaguzi tu, bali na unachofanya kuboresha maisha ya watu.
 
Kikwete na waandishi wake wa hotuba ni zero kabisa.

Kasema kuna mambo matatu lakini kaongelea mawili tu, lile la tatu kaliogopa!

What a joke!

Pundit,

Naona unafikiri hotuba za wanasiasa ni sawa na academic papers, they are not. You are spending too much time looking for trivial mistakes instead of looking for the intended messages.

Ukiangalia hotuba nzuri duniani ni zile ambazo wahusika walikuwa hawasomi, maneno yalikuwa yanatoka moyoni with passion. Huenda mpangilio ulikuwa unakuwa sio mzuri sana lakini messages zilizokuwa zinatolewa zilikuwa zina make sense. Angalia baadhi ya speeches za Mwalimu au hata watu kama Churchill na Hitler

Siku hizi shauri ya kuogopa kukosolewa na kukosea, kila kitu kinaandikwa na kuchambuliwa na wajuzi, matokeo yake watu wanaongea vitu ambavyo hawaviamini, passion inapotea na speeches kuwa boring. Mimi nikiona mwanasiasa anasoma speech, huwa nalala baada ya dakika tano.
 
Mimi nimeisoma hotuna nzima sijamwelewa kabisa nduhu rais hadi sasa .Nimerudia kila mara lakini naona anaimba sifa za Bush kukaa Tanzania na ukarimu nk
 
Back
Top Bottom