Hotuba za Rais kila mwezi

Hotuba za Rais kila mwezi

Je unaridhika na hotuba za Rais Kikwete?

  • Ndio

    Votes: 13 15.5%
  • Hapana

    Votes: 71 84.5%
  • SIJUI

    Votes: 0 0.0%
  • Sina jinsi

    Votes: 1 1.2%

  • Total voters
    84
  • Poll closed .
Ushaamini kwamba Tanzania hakuna rais wala hotuba sasa?
 
Thinking of Benjamin William Mkapa..... sio tu content bali wording ya hii hotuba ni ovyoo kabisa.

The way ilivyoandikwa ni kama Insha ya darasa la 3 hivi... kiswahili kilichotumika kibovi mpaka basi.... yaani aibu aibu hao waandishi wake hawafai kabisa.
 
Kabla ya kumaliza napenda kutumia fursa hii kuwashukuru wananchi wote kwa kuendelea kuiunga mkono serikali katika mambo yote ya msingi yanayoihusu nchi yetu. Licha ya mawimbi ya hapa na pale ambayo tunapambana nayo katika safari yetu, tumeendelea kuimarisha umoja na mshikamano wetu ambao ndio nguzo na mhimili wa taifa letu.

Kuwatukana wananchi sio lazima uwaite wajinga, unaweza kutumia maneno mengine lakini maana ikawa ile ile, kwamba unawaita wananchi wajinga.

Haiwezi ku-get lower than this.
 
It is high time now Rais akastick na issue moja au mbili kwenye hotuba yake. Hili suala la EPA alitakiwa alipe umuhimu na uzito wa kipekee, ni suala ambalo linahitaji details. Ni kama vile yuko busy kiasi kwamba hana muda kabisa wa kulipresent kinagaubaga kwa maboss wake?

Ingekuwa vema na haki kama angewatajia mabosi wake (wapiga kura) ni kina nani hao waliorudisha hizo pesa, nani ambao hawajarudisha na ni hatua gani watakazo chukuliwa i.e fulani na fulani watapelekwa mahakamani, fulani na fulani mali zao zimetaifishwa na serikali, na fulani na fulani hawana hatia. Hizi siri siri hizi.
 
Kubwa kuliko yote ni kuwa suala la OIC linafanyiwa kazi na wizara ya mambo ya NJE ili iweze kuiadvise serikali.

Kwa hiyo inamaana Wizara ya Mambo ya NJE sio serikali?? Au??

Kwa hiyo ni serikali kuiadvise serikali au??

Serikali ni nini hasa???
 
Tutaendelea kumsumbua kuhusu wezi wa EPA hadi waende mahakamani na ikishindikana yeye atasimama kama mwizi mwenzao.
Tunatafuta msaada wa kisheria jamani. Something must be done!😱
 
Da Rais hajui lini Wizara itamaliza kushughulikia suala la OIC!

Unaenda mbali huko. Sio hajui utaisha lini. Ka indicate kwamba hata hajui kama umeisha!!! Inawezekana umeshaisha yeye hajui.

"Ndugu Wananchi;

Nijuavyo mimi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa haijakamilisha kazi yake."

Anasema "nijuavyo mimi Wizara haijamaliza," as if ni uninformed citizen mmoja hivi wa mtaani. Yani hata kama hapati official daily briefings (or even montly briefings) za foreign minister kabla ya kuhutubia Taifa kuhusu kitu ambacho anasema ni foreign affairs angeweza kupata neno la haraka tu kutoka Foreign. I mean, hata waandishi wakujitegemea wa KLH News wana namba za simu za Mawaziri. Ikulu imeshindwa ku touch base na Bernard Membe kujua kama kamaliza au la!!!

Halafu notice Kikwete administration ilivyochanganyikiwa kuhusu nani aongelee hili swala kati ya Serikali na Wananchi.

"Ndugu Wananchi;

... Tuwaache Wizira ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wafanya kazi yao kwa utulivu ili waishauri Serikali kwa hekima na busara.

… tuiache Serikali yetu nayo itafakari kwa utulivu ili ifanye uamuzi ya hekima utakaojenga na kulihakikishia taifa letu umoja, amani, utulivu na upendo miongoni mwa raia wa nchi yetu.

…narudia kuwasihi Watanzania wenzangu tuiache Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ilifanyie kazi kwa ukamilifu suala hili."

Yani wako completely at sea. Ni foreign minister Membe ndio ame broach national debate on this issue:

"Uamuzi wa kujiunga au kutojiunga utakuwa chini ya wananchi, wasomi, NGOs na ninyi waandishi wa habari, ndiyo mtakaoamua." Foreign Minister Bernard Membe, 10-22-2008
 
Tayari hotuba ameitoa japo alikuwa very tense na kuonekana mchovu kuliko kawaida yake ya kucheka cheka.

In brief ni kama hivi.

Hotuba ya Kikwete imekuwa ya kitaalamu kabisa. Ameongea kuhusu suala la OIC kuwa jambo hili bado linafanyiwa utafiti na wizara ya mambo ya nchi za nje na wizara itawasilisha mapendekezo yake serklani. Ameomba watanzania wawe na subira wakati wizara ikiyashughulikia na pia wakati serkali itakapokuwa ikitafakari hatua sahihi zakuchukua kutokana na ushauri wa wizara. Pia alisema suala la OIC ni hitaji kubwa kwa Zanzibar ambao walikwishajiunga lakini ikaonekana kuwa suala hili ni la muungano hivyo lishughulikiwe na Jamhuri ya Muungano. Alimaliza kwa kujulisha kuwa serkali yake inaheshimu umoja wa kitaifa na maelewano ambayo yamekuwepo baina ya waislamu na wakrsito dini kuu hapa Tz hivyo yasiharibiwe .

Jambo la pili lilikuwa ni madai ya wallimu. Hapo pia alisema kulikuwa na maafikiano yalifikiwa baina ya walimu na serkali kuwa wasigome na serkali itaendelea kushughulikia madai yao wakiyahakiki kwa pamoja na chama cha walimu. Amedai alishangaa wakati Nkoba alipotanganza kuwa mgomo uko pale pale. Aliwaagiza viongozi wa walimu watafutwe na kuombwa wasigome ila wao walikataa. Hakukuwa na njia nyingine ya kunusuru sekta muhimu ya elimu ispokuwa kwenda mahakamani. Alisema anaheshimu sana walimu na kuwajali ndio maana katika kkulipa mafao mbali mbali huko nyuma kipaumbele kiliwekwa kwa walimu. Ameomba walimu wawe na subira wakati uhakiki utakaofanywa shule kwa shule kubaini madai ya wwalimu pamoja na kkubaini walimu hewa pamoja na waliokwisha fariki wakishirikiana na chama cha walimu.

Jambo lingine lilikuwa uchumi wa dunia. Hilo alilieleza kwa kurudia hotuba yake ya Tanga na kuwa hakuna mabadiliko yoyote hadi sasa. Aliomba kusihi jjitihada za Bush za kuita viongozi wakuu duniani wanaoathirika kwa recession hiyo waje pamoja na kutafuta suluhu la haraka. Ila ameshangazwa na kusahauliwa kwa Afrika katika mkutano huu kwani sisi pia tunaathirika kwa shida hii ya uchumi.

Aliongelea pia suala la mauaji ya albino kuwa serkali inawaomba wananchi wajitokeze kutoa taarif a za wagaga, wauaji, manunuzi wa viungo vya alibino. Alisema serkali itaendesha kkkura za maoni kama zile za wakati wa majambazi zitakazotoa taarifa kwa vyombo vya usalama ili uchunguzi zaidi ufanywe na kkubaini wahalifu hawa na kuwachukulia hatua stahiki. Alisema hii ni vita halali.

Mwisho aliongelea suala la EPA na kusema over 70% ya fedha zote zimerudishwa hadi kufikia leo mchana. (Ametaja kiasi something like 69 bn sikunukuru takwimu) Anasema inawezekana kuna wengine waliozirudisha lakini hajapata taarifa zao. Labda kufikia kesho sura itakuwa imebadilika. Akadai wote wasiorejesha wapelekwa mahakamani. Jambo hili amemkabidhi mwendesha mashtaka wa serkali. Akasema hii ni taasisi huru ambayo kutokana na mashtaka ya nayoletwa na polisi pamoja na Takukuru mwendesha mashtaka ana shughulikia mashtaka haya. Pia akasema zile kampuni 9 zilizochota over 40 bn vyombo vyetu vya upelelezi vilikuwa vinashirikiana na wenzao wa nje ili kuyabaini na kuyachukulia hatua. Ila hadi 2 wks zilizopita wale wa nje walkijuwa hawajaleta taarifa yoyote. Akasema wanaendelea kusubiri.

Fedha zilizorudishwa amesema ile kamati iliyowekwa kkushauri namana ya kuzigawa katika kilimo inakamilisha kazi yake na bila shaka itatoa mwongozo wa jinsi ya kugawa hela hizi. Amewashukkuru sana watanzania kwa kuwa na subira wkati serkali ilipokuwa inashughulikia jambo hili.

Kuhusu wastaafu wa Jumuaiya ya Afrika Mashariki amesema hatasema lolote kwa sababu waziri wa fedha atatoa tamko rasmi la serkali wiki ijayo. Kwa ufupi na kwa kweli in my understanding ndivyo alivyosema.
 
Mkuu wa kaya anasema OIC si deal,isiwanyime usingizi,....,wazenj ndio chanzo cha OIC,wanaulizia kila siku,kulikoni,....anaendelea mjadala wa OIC chini ya viongozi wa nje unalenga kudumisha MUUNGANO....mmmmmhhh

Nikuulize JK,bila MUUNGANO sie WATANGANYIKA hatulali usingizi?kwani kila watakalo wazenj lazima lifanyike?gharama zake tubebe wote?Kumbuka mzenj kiongozi alimtukana waziri mkuu wetu kwa kusema hawajibiki kwake,anawajibika kwa rais wa zenj...wawajibike basi na OIC yao,vunjeni muungano basi...kwani shida?hauvunjiki????!!!....kwanini hili ulipe nafasi?hatuna haki ya kusema nawe una hamu nalo?wazee EAC wanakufa na njaa unadeal na OIC???hahahahah

Ikiwa uko hapo kwa maslahi ya wazenj,sie wakristo tunataka MUUUNGANO ufe,soon,then utupe kipande chetu nasi yuwe na Tz yetu....Au?ingiza mjadala huu kwa wizara husika,kama ulivoingiza wa OIC.
 
1. Napenda kukumbusha kuwa mwaka 1993 Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilitakiwa kujiondoa kutoka kwenye jumuiya ya OIC baada ya kujiunga

2. Tangu wakati huo Zanzibar wamekuwa wanasubiri uamuzi wa Serikali ya Muungano.

Miaka 15, wizara ya nje bado inafanya utafiti, Membe amemaliza utafiti lakini hajaiarifu serikali, lakini ameamua kuwaarifu wananchi,

You wonder hivi Membe ameajiriwa na nani?
 
Na. KLHN News

Rais Kikwete amezungumza na Taifa katika utaratibu wake wa kuzungumza na wananchi kila mwishoni mwa mwezi. Hotuba yake hiyo iliyocheleweshwa ka karibu saa moja na nusu ilikuwa inasubiriwa kwa hamu na wananchi hasa kutokana na uzito wa mambo ambayo Rais alitarajiwa kuzungumzia.

Akizungumza katika hotuba hiyo ambayo ilionekana kuwa imerekodiwa Rais Kikwete alizungumzia mambo makubwa manne ambayo aliyatolea maelezo kwa kirefu. Hata hivyo jambo kubwa ambalo wananchi wengi walikuwa wanasubiri kulisikia ni hatua zilizochukuliwa dhidi ya makampuni na watu waliohusika na wizi wa fedha za EPA na kujua hatima ya uchunguzi mzima.

Pamoja na hilo suala jingine ambalo wananchi walikuwa wanasubiri kwa hamu ni msimamo wa serikali yake kuhusu suala ambalo linaonekana kuwagawanya wananchi kwa misingi ya dini. Suala hilo ni mpango wa Serikali ya Muungano kujiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC)

Akizungumzia suala la OIC ambalo alilipa umuhimu wa kwanza Rais Kikwete alisema kuwa mjadala wa OIC jinsi unavyoendeshwa sasa hivi ni “mjadala usiofurahisha”. Akielezea zaidi kutokufurahisha kwa mjadala huo Rais Kikwete alisema kuwa mjadala huo una “sura ya malumbano baina ya waumini wa dini zetu kuu na kupandikiza chuki baina ya serikali”

Kwa mujibu wa Rais msukumo wa kujiunga na taasisi hiyo zaidi unatoka Zanzibar ambayo ilikuwa imejiunga mwaka 1993 na kulazimika kujitoa miezi saba baadaye baada ya pingamizi toka serikali ya Muungano. “Tangu wakati huo Zanzibar wamekuwa wanasubiri uamuzi wa Serikali ya Muungano. Kila wakati wenzetu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wamekuwa wanaliuzia suala hilo.”

Hata hivyo akionekana kutofautiana na Waziri Membe Rais Kikwete alisema kuwa hakuna utafiti uliofanyika kuhusu suala la OIC na hivyo serikali bado inasubiri utafiti huo toka Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje. “Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa haijakamilisha kazi yake ya utafiti na hivyo haijawasilisha Serikalini matokeo ya utafiti wao pamoja na mapendekezo yao kwa ajili ya kutafakariwa na kuamuliwa ipasavyo.”

Hata hivyo kauli hiyo ya Rais inapingana na kauli aliyoitoa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Mhe. Bernard Membe akizungumza Bungeni Augusti 22, 2008 ambapo akizungumzia suala la OIC alinukuliwa kusema kuwa “sasa tumefanya utafiti wa kutosha na kugundua kuwa OIC ina faida kwetu na haina madhara, hivyo tunafanya mchakato wa kujiunga, lakini ni vema ikaeleweka wazi kuwa, Zanzibar wasingeweza kupata ridhaa ya kujiunga nayo kwa sababu si nchi katika uso wa kimataifa,”

Ni kauli hiyo ya Waziri Membe ndiyo iliyosababisha wimbi la shutma na malalamikko ya Taifa kuburuzwa kwenda kujiunga OIC na wakati huo huo kupata pongezi kuwa wakati muafaka umefika wa kufanya hivyo kwani “utafiti” tayari umeshafanyika.

Rais alielezea msimamo wa serikali kuwa “Serikali haijafanya uamuzi wowote kuhusu suala la OIC kwa vile hatujapokea mapendekezo yoyote kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.”
Rais amewataka wananchi wawe na subira.

Kuhusu suala jingine ambalo limekuwa mwiba kwa serikali Rais Kikwete ameeleza kuwa kufuatia hotuba yake ya Augusti 21 aliagiza makampuni yaliyolipwa bilioni 90 kuhakikisha yanarudisha fedha hizo na yale ambayo yatashindwa kufanya hivyo yatachukuliwa hatua.

“Leo ndiyo siku ya mwisho. Napenda kuwajulisha kuwa, taarifa nilizoletewa majira ya mchana leo(Ijumaa), ni kuwa kiasi cha shilingi 69,326,437,650 kati ya shilingi 90,359,078,804 zilikuwa zimerejeshwa. Hii ni sawa na asilimia 76.7.” alisema Rais.

Aliwaambia wananchi kuwa leo (Jumamosi) taarifa zaidi itatolewa kuhusu “kiasi” halisi kilichorudishwa. Kutokana na kauli yake hiyo inawezekana hesabu hiyo isiwe sahihi. Wachambuzi wa suala hili la EPA wanaonekana kushangazwa na Rais kutaja namba ambayo siyo sahihi na masaa machache baadaye iliyo sahihi itolewe.

Kuhusu wale ambao hawakuitikia wito huo Rais Kikwete alisema kuwa ametoa maagizo kuwa “Kamati (ya Mwanasheria Mkuu) ikabidhi majalada yao kwa Mkurugenzi wa Mashtaka mara moja, kwa hatua zipasazo za kisheria.” Agizo hilo alilolitoa Rais ni sawasawa na agizo alilolitoa wakati wa kuunda tume ya Mwanyika pale alipomuagiza Mwanasheria Mkuu “kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watu na makampuni yote yaliyohusika na uhalifu huu”. Haijaeleweka tofauti ya uelewa wa Agizo hilo la kwanza na la pili ni nini hasa kwa sababu ofisi ya DPP iko chini ya ofisi ya Mwanasheria Mkuu.

Uamuzi huo unahusu makampuni yale 13 kati ya ya 22 yanayohusishwa na wizi wa EPA. Kuhusu makampuni 9 yaliyosalia ambayo yanadaiwa kulipwa bilioni 40 Rais Kikwete alisema kuwa “nasubiri taarifa yao mpya kuhusu maendeleo ya uchunguzi huo. Taarifa niliyopewa wiki mbili zilizopita zinaonyesha kuwa polisi wetu bado hawajapata majibu kutoka kwa wenzao
katika nchi walizoomba msaada. Hivyo, nakusudia kuwataka waendelee kufuatilia kwa wenzao ili hatua zipasazo ziweze kuchukuliwa.”

Kwa maneno mengine uchunguzi kuhusu makampuni hayo bado haujaanza kwani Rais ndiyo amekusudia “kuwatataka waendelee” kufuatialia makampuni hayo 9. Makampuni hayo ni pamoja na kampuni inayodaiwa kuwa na uhusiano wa karibu na Mbunge wa Igunga Mhe. Rostam Aziz, ya Kagoda Agricultural.

Hata hivyo Rais aliwahakikishia wananchi kuwa utaratibu wa kuzigawa fedha hizo kwenye sekta ya kilimo Umekamilika.

Mambo mengine ambayo Rais aliyazungumzia kwa kirefu ni pamoja na suala la madai ya walimu, mauaji ya Albino, na suala hali ya kiuchumi ya dunia
 
I am not a big supporter of the opposition (Chadema, CUF, etc) but CCM needs to go otherwise nothing will ever change in this country. They have become so arrogant it's unbelievable.

The only thing left to do now is prepare for 2010.
 
...i am totally sick..sick..najisikia kutapika....na kuumwa kichwa!!....

...jangala michosho kiwete.. a total waste!!!!!
 
Rais alielezea msimamo wa serikali kuwa "Serikali haijafanya uamuzi wowote kuhusu suala la OIC kwa vile hatujapokea mapendekezo yoyote kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa."
Rais amewataka wananchi wawe na subira.

Hata hivyo kauli hiyo ya Rais inapingana na kauli aliyoitoa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Mhe. Bernard Membe akizungumza Bungeni Augusti 22, 2008 ambapo akizungumzia suala la OIC alinukuliwa kusema kuwa "sasa tumefanya utafiti wa kutosha na kugundua kuwa OIC ina faida kwetu na haina madhara, hivyo tunafanya mchakato wa kujiunga, lakini ni vema ikaeleweka wazi kuwa, Zanzibar wasingeweza kupata ridhaa ya kujiunga nayo kwa sababu si nchi katika uso wa kimataifa,"

Equal to incompetence!
 
Jamani nimeangalia na kusikiliza hotuba najiuliza amesema nini huyo jamaa?????Can someone explain plseeeeeeeeeee????Nimeona ma Rais lakini wasasa kiboko, du!!!!!!
 
Na. KLHN News

Rais Kikwete amezungumza na Taifa katika utaratibu wake wa kuzungumza na wananchi kila mwishoni mwa mwezi. Hotuba yake hiyo iliyocheleweshwa ka karibu saa moja na nusu ilikuwa inasubiriwa kwa hamu na wananchi hasa kutokana na uzito wa mambo ambayo Rais alitarajiwa kuzungumzia.

Akizungumza katika hotuba hiyo ambayo ilionekana kuwa imerekodiwa Rais Kikwete alizungumzia mambo makubwa manne ambayo aliyatolea maelezo kwa kirefu. Hata hivyo jambo kubwa ambalo wananchi wengi walikuwa wanasubiri kulisikia ni hatua zilizochukuliwa dhidi ya makampuni na watu waliohusika na wizi wa fedha za EPA na kujua hatima ya uchunguzi mzima.

Pamoja na hilo suala jingine ambalo wananchi walikuwa wanasubiri kwa hamu ni msimamo wa serikali yake kuhusu suala ambalo linaonekana kuwagawanya wananchi kwa misingi ya dini. Suala hilo ni mpango wa Serikali ya Muungano kujiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC)

Akizungumzia suala la OIC ambalo alilipa umuhimu wa kwanza Rais Kikwete alisema kuwa mjadala wa OIC jinsi unavyoendeshwa sasa hivi ni “mjadala usiofurahisha”. Akielezea zaidi kutokufurahisha kwa mjadala huo Rais Kikwete alisema kuwa mjadala huo una “sura ya malumbano baina ya waumini wa dini zetu kuu na kupandikiza chuki baina ya serikali”

Kwa mujibu wa Rais msukumo wa kujiunga na taasisi hiyo zaidi unatoka Zanzibar ambayo ilikuwa imejiunga mwaka 1993 na kulazimika kujitoa miezi saba baadaye baada ya pingamizi toka serikali ya Muungano. “Tangu wakati huo Zanzibar wamekuwa wanasubiri uamuzi wa Serikali ya Muungano. Kila wakati wenzetu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wamekuwa wanaliuzia suala hilo.”

Hata hivyo akionekana kutofautiana na Waziri Membe Rais Kikwete alisema kuwa hakuna utafiti uliofanyika kuhusu suala la OIC na hivyo serikali bado inasubiri utafiti huo toka Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje. “Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa haijakamilisha kazi yake ya utafiti na hivyo haijawasilisha Serikalini matokeo ya utafiti wao pamoja na mapendekezo yao kwa ajili ya kutafakariwa na kuamuliwa ipasavyo.”

Hata hivyo kauli hiyo ya Rais inapingana na kauli aliyoitoa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Mhe. Bernard Membe akizungumza Bungeni Augusti 22, 2008 ambapo akizungumzia suala la OIC alinukuliwa kusema kuwa “sasa tumefanya utafiti wa kutosha na kugundua kuwa OIC ina faida kwetu na haina madhara, hivyo tunafanya mchakato wa kujiunga, lakini ni vema ikaeleweka wazi kuwa, Zanzibar wasingeweza kupata ridhaa ya kujiunga nayo kwa sababu si nchi katika uso wa kimataifa,”

Ni kauli hiyo ya Waziri Membe ndiyo iliyosababisha wimbi la shutma na malalamikko ya Taifa kuburuzwa kwenda kujiunga OIC na wakati huo huo kupata pongezi kuwa wakati muafaka umefika wa kufanya hivyo kwani “utafiti” tayari umeshafanyika.

Rais alielezea msimamo wa serikali kuwa “Serikali haijafanya uamuzi wowote kuhusu suala la OIC kwa vile hatujapokea mapendekezo yoyote kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.”
Rais amewataka wananchi wawe na subira.

Kuhusu suala jingine ambalo limekuwa mwiba kwa serikali Rais Kikwete ameeleza kuwa kufuatia hotuba yake ya Augusti 21 aliagiza makampuni yaliyolipwa bilioni 90 kuhakikisha yanarudisha fedha hizo na yale ambayo yatashindwa kufanya hivyo yatachukuliwa hatua.

“Leo ndiyo siku ya mwisho. Napenda kuwajulisha kuwa, taarifa nilizoletewa majira ya mchana leo(Ijumaa), ni kuwa kiasi cha shilingi 69,326,437,650 kati ya shilingi 90,359,078,804 zilikuwa zimerejeshwa. Hii ni sawa na asilimia 76.7.” alisema Rais.

Aliwaambia wananchi kuwa leo (Jumamosi) taarifa zaidi itatolewa kuhusu “kiasi” halisi kilichorudishwa. Kutokana na kauli yake hiyo inawezekana hesabu hiyo isiwe sahihi. Wachambuzi wa suala hili la EPA wanaonekana kushangazwa na Rais kutaja namba ambayo siyo sahihi na masaa machache baadaye iliyo sahihi itolewe.

Kuhusu wale ambao hawakuitikia wito huo Rais Kikwete alisema kuwa ametoa maagizo kuwa “Kamati (ya Mwanasheria Mkuu) ikabidhi majalada yao kwa Mkurugenzi wa Mashtaka mara moja, kwa hatua zipasazo za kisheria.” Agizo hilo alilolitoa Rais ni sawasawa na agizo alilolitoa wakati wa kuunda tume ya Mwanyika pale alipomuagiza Mwanasheria Mkuu “kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watu na makampuni yote yaliyohusika na uhalifu huu”. Haijaeleweka tofauti ya uelewa wa Agizo hilo la kwanza na la pili ni nini hasa kwa sababu ofisi ya DPP iko chini ya ofisi ya Mwanasheria Mkuu.

Uamuzi huo unahusu makampuni yale 13 kati ya ya 22 yanayohusishwa na wizi wa EPA. Kuhusu makampuni 9 yaliyosalia ambayo yanadaiwa kulipwa bilioni 40 Rais Kikwete alisema kuwa “nasubiri taarifa yao mpya kuhusu maendeleo ya uchunguzi huo. Taarifa niliyopewa wiki mbili zilizopita zinaonyesha kuwa polisi wetu bado hawajapata majibu kutoka kwa wenzao
katika nchi walizoomba msaada. Hivyo, nakusudia kuwataka waendelee kufuatilia kwa wenzao ili hatua zipasazo ziweze kuchukuliwa.”

Kwa maneno mengine uchunguzi kuhusu makampuni hayo bado haujaanza kwani Rais ndiyo amekusudia “kuwatataka waendelee” kufuatialia makampuni hayo 9. Makampuni hayo ni pamoja na kampuni inayodaiwa kuwa na uhusiano wa karibu na Mbunge wa Igunga Mhe. Rostam Aziz, ya Kagoda Agricultural.

Hata hivyo Rais aliwahakikishia wananchi kuwa utaratibu wa kuzigawa fedha hizo kwenye sekta ya kilimo Umekamilika.

Mambo mengine ambayo Rais aliyazungumzia kwa kirefu ni pamoja na suala la madai ya walimu, mauaji ya Albino, na suala hali ya kiuchumi ya dunia

Mzee wa UJIKO
 
Ningependa kujua majina ya hizo kampuni 9 ili tumsaidie uchunguzi.

Hakuna cha kampuni tisa wala nini, tunajua hiyo 43 bilioni ndio hela zilizopelekwa CCM kwenye uchaguzi according to rostam & Co.

Kwa hiyo hakuna cha uchunguzi wa Nje wala nini.

Rais huna haja ya kuwasumbua vijana wenzetu walioshindwa kulipa hizo bilioni 21, waacha nao wapete kwanza hela si za serikali ok bwana.

Kama Jeetu hayupo kwenye kesi, pse tupunguzie hasira ili tusahau mambo ya EPA, umeamua noma iwe noma, sawa mkuu wa Kaya.

FREE LUKAZA, FREE MALEGESI.
 
Back
Top Bottom