Hotuba ya Rais: Tafadhali Mhe. Rais usiseme hivi.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hotuba ya Rais: Tafadhali Mhe. Rais usiseme hivi..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Apr 30, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Apr 30, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Kwa namna fulani tunaamini kuwa sisi tuna upendeleo wa aina fulani kwa Mwenyezi Mungu, kwamba nchi yetu kwa sababu upendeleo wa pekee basi haitapata majanga. Hatujajifunza kwa ajali zinazotea mara kwa mara za mabasi, hatujajifunza kwenye ajali za majini, hatujajifunza kwenye milipuko ya mabomu na kwa hakika tuko kama tumepigwa ganzi ya aina fulani hivi.

  Pamoja na kutoa pole na rambirambi, ni lazima tujiulize tutaendelea mpaka kulini kwa kutegemea rehema za Mungu? Sitoshangaa leo tutaambiwa katika Hotuba ya Rais kuwa haya yalikuwa ni mapenzi ya Mungu na ya kuwa wanaunda tume kuchunguza kitu gani kilisababisha na wananchi wasiwe na wasiwasi hali ni shwari na halikuwa tukio la kighaidi..

  Katika wazimu wetu tutasema Amen.. na kusahau kabisa mlolongo wa kutojiandaa na majanga ambao serikali ya CCM imeuendeleza kwa miaka kadhaa sasa na kutuacha tuishi kwa bahati!

  Jana, tumeikwepa risasi! Huko mbeleni (na itakuwa hivyo kwani majanga yataendelea kutokea hata kama tunaombea yasitokee, ndiyo kanuni ya ulimwengu!) tutakuja kulia kama tulivyolia kwenye MV. Bukoba na Bahi! (wengine wanajiuliza "Bahi?"! wameshasahau!

  I have more to say.. listen..

  [mp3]http://mwanakijiji.podomatic.com/enclosure/2009-04-29T23_41_36-07_00.mp3[/mp3]

  Update: Nasikia hadi hivi sasa waliokufa wamefikia 10:

  Pili: Mabomu yaliripuka wakati yakihamishwa-mengine yalikuwa yapelekwe Shinyanga na mengine yalikuwa yanaandaliwa kwa ajili ya safari ya Darfur pamoja na kikosi cha kulinda amani kutoka TZ.
  Lakini jeshi halitaki kusema kulikuwa na askari wangapi ndani ya ghala wakati mlipuko unatokea(thanks MN) - Isomeke yawezekana watu wengi zaidi wamefariki kuliko idadi ya awali kama nilivyodokeza katika taarifa yangu ya awali kwenye main thread.
   
 2. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #2
  Apr 30, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Na wanajeshi zaidi ya 20 waliokufa huwa hawahesabiki? Au ni "Confidential" ?
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Wanaficha Mkuu, hawataki kusema. lakini kuja ofisa mmoja ambaye alikuwa karibu na operesheni hii amenieleza kuwa kulikuwa na zaidi ya askari 15 (including mmoja au wawili wenye vyeo vya meja) walikuwa ndani ya ghala wakati mlipuko unatokea. Hivyo ni dhahiri kuwa idadi ya casualties jeshini itakuwa ni kubwa kuliko uraiani
   
 4. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #4
  Apr 30, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Tunaweza kuwapa hata majina ya waliokufa (askari)... Kama ni siri ya Jeshi basi itabidi tulisitiri.

  Tatizo misiba ipo uraiani na majina ya waliokufa yameshafahamika!
   
 5. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  MN,

  Toka jana najaribu kuangalia ni watu wangapi wamefariki lakini muda wote inaonyesha watatu. Hakuna kitu kibaya kama kuficha majanga.

  Watuambie wananchi ukweli mtupu ili kuwe na funzo, maana wakificha ina maana hawatajifunza kabisa na tokeo kama hili litatokea mahali pengine tena.
   
 6. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #6
  Apr 30, 2009
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Its true kwamba majanga huwezi kuyazuia kutokea lakini uharibifu wake unaweza kupunguzwa kwa kiasi kikibwa sana. Haiwezekani jamaa wa jeshi wawe na ghala lisilo na vifaa vya kutoa tahadhari za moto. Hii inaonyesha kuwa bado tunaishi zama za mawe.

  Lazima tuweke vipaumbele katika haya mambo ya maafa ili yakitokea tujue nini cha kufanya. Jana mabomu yanalipuka watu wanakimbilia huko huko kushangaa badala ya kukaa mbali. Lazima elimu itolewe watu wajua nini cha kufanya yakitokea. Pia vifaa viboreshwe na kuongezwa.

  Mfano jana kama kungekuwa na fire detectors jamaa waliokufa ndani mle wasingekufa na pia watu wa maeneo yale kama wangekuwa wamefundishwa kuwa ukisikia alarm kimbia mbali kutoka eneo unapotokea mlio wajeruhi wangepungua sana.

  SERIKALI LAZIMA IFANYE KITU KWENYE HILO SIYO MAMBO YA KUACHA YAJIENDEE TU.

  Salute MMK
   
 7. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #7
  Apr 30, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Nimeumia mno na kusikitishwa na hili janga ambalo ingawa halina kinga ila watu hawakuandaliwa kukabili mishtuko kama hii.
  Juzi juzi hapa tulikuwa tunadiskasi masuala ya majanga na precautions zake ila kama kawa WAKULU walidhani ni porojo za JF tu wala hawajafikiria kuchukua hatua.
  halafu nashangazwa kwa siasa inayopigwa hata kwenye maafa kama haya. waseme ukweli kwani hatutapanic wala nini ila wakificha tutajua tuyajuayo sisi.
   
 8. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #8
  Apr 30, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Huyu jamaa ukisikiliza katika maneno yake kumi ya mwanzo anasema ".......kama ni baruti zimelipuka zenyewe...." Baruti!!!!!!!! au Mabomu!!!!! jamaani hivi hamna tofauti hapa au labda mimi bado nipo kuzimu.
   
 9. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #9
  Apr 30, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mzee mkj,
  haya maafa ni makubwa sana tena sana. Watoto wamekufa wananchi wamekufa, askari wamekufa wananchi wamejeruhiwa na mali lukuki zimeharibiwa vibaya sana. katusha nyingine hazifahamiki ziliko, mabomu ya kurusha kwa mikono yamezagaa mitaana, silaha nyingi hazijulikani ziliko zaoidi ya watu mia tatu wamefika ER na wengine kibao hawajulikani walipo bado unaona hilibalaa sio kubwa??? ni kubwa mno.

  Ni kweli ajali za silaha ni kulipuka. Uzembe hapa ni kuweka ghala la silaha maeneo ya makazi ya watu huu ndio uzembe, pili jeshi halikutumia protected ghala kwa silaha husika , hapa tatizo ni safety jeshini ni ziro hawajali hata wanajeshi ambao wanatulinda usiku na mchana.

  Serikali haikutoa tamko mapema kwamba Katusha zimeanza kufanyiza zenyewe.Natamani zingeshuka kwenye vichwa vya mafisadi, ila huwa haiwi hivyo.

  Inawezekana hizi ni zile silaha mbovu walizo nunua mboma na Absoni wakisaidiana na mkapa, sasa zinafail. Nyingi sana zitalipuka.
   
 10. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #10
  Apr 30, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Inaelekea kuna uzembe fulani unafichwa. lakini wanachosahau ni kuwa mficha maradhi...
   
 11. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #11
  Apr 30, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,167
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Hili nalo ni siri kama ilivyo kwa mambo mengine kwa serikali ya CCM
   
 12. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #12
  Apr 30, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuuu MMK umefanya vizuri kumkumbusha, huenda safari hii akaboresha taarifa yake
   
 13. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #13
  Apr 30, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mkuu,
  Hizi ni siri za serikali, utachukuliwa hatua za kisheria mara moja kwa kuvujisha siri hizi, ikiwa ni pamoja na kutumia mtandao wako wa habari kueneza siri hizi kwa maslahi yako binafsi! Angalia usije "ukachemsha".
   
 14. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #14
  Apr 30, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,315
  Likes Received: 5,609
  Trophy Points: 280
  Kila kitu kitajulikana tu hata kwa habari zisizo rasmi maana karne hii si ya kutuficha tena tunataka kujua sababu...watu wangapi wamekufa....wanajeshi wangapi wamekufa na kuumia.....sababu kuu na mengineyo.......mpango wao wa kuhamisha makambi jirani na makazi ya watu??maswali yetu yote yajibiwe.
   
 15. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #15
  Apr 30, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na hoja kuwa mficha maradhi kifo kitamfichua. Kuna watu bado wako kwenye enzi zileee.Wanaamini wao tu ndo wanaoijua zaidi Tanzania na wao tu ndio wanaweza kutupa mustakabali wa nchi yetu, na wao tu ndo wanastahili kujua yote yanayofanyika TZ tena mara nyingine wanafanya siri ili wanufaike nayo kama sio walishanufaika nayo.Uongo uliopitiliza,Duh!
  Ukiona kwenye ajari ya kijeshi msemaji mkuu anakuwa mkuu wa mkoa, asiyejua lolote kuhusu nini kilikuwa kinaendelea ndani ya ghala, napata mashaka kwamba ipo kasoro somewhere.

  Kama ni uzembe umetokea, then somebody has come out na kusema nini kimetokea na what are in plan to rectify the current situation and avoid similar incidencies in future. Nilipata sikia kuna wakati rubani wa jeshi la marekani aliwahi kuload nuclear head bomb kwenye ndege yake. Aliirusha hiyo ndege sehemu kadhaa pengine kwa kujua au bila kujua, ingawa ilikuwa ni hatari kubwa. Walipochunguza ikaonekana kuna lapse kubwa kwenye kufuata kanuni na taratibu ndani ya jeshi la anga na kuna waliowajibishwa kwa makosa hayo.Kuwajibishwa kwao kulitokana na sababu kuwa kama kungekuwa na good procedures in place such a mistake could be identifies even before the pilot had left.Sisi hatujasoma alama za nyakati, na tumeamua kutotambua mapema makosa yetu kwa sababu tunalindana.

  Jamani au ndo ile collaboration ya mafisadi, wanunuzi wa mali za serikali ya Tanzania, imeanza kufanya kazi.Mana mafisadi wanatuletea sub standard items kwa double price ili kuwalisha wanasiasa wetu.
   
 16. Mtanganyika

  Mtanganyika JF-Expert Member

  #16
  Apr 30, 2009
  Joined: Jul 18, 2007
  Messages: 1,613
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 180
  Wengi naona mnaangalia waliokufa tuu, Jee walipoteza viungo vyao vya mwili? Miguu, Mikono, Macho na vingenevyo. What will be compasation kwa kupoteza mguu ambao umesababishwa na MWENDAWAZIMU Jeshini ambaye ni careless. I don't care ni ajali au laa but uzembe played is part.

  Najua ZEE LA NYETI kwenye speech yake leo atasema mungu ndio anapanga blah blah ( remember Bichwa Ben aliposema God loves Tanzania ndio maana treni ya Dodoma haikuuwa wengi kama India), expect the same leo. That is how CCM protocal teach wafuasi wake.

  We all agree mungu ndio mpangaji (unless your earthist), lakini kilicho muhimu ni nini tumejifuza, what policy changes will be put into place, who will be fired and etc. Hizi ndio measurements muhimu ambazo zinaonyesha kwamba tunajifunza.

  Lakini kama Zee la Nyeti atakuja jukwaani na kuanza kutusomea Long Speech iliyojaa madudu kama kawaida yake. Then the question will remain kwa Watanzania do we need more of the same?
   
 17. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #17
  Apr 30, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  Dunia sasa imebadilika sio kama miaka ile wanajeshi wetu walikufa Uganda na Mozambique lakini taarifa zilizokuwa zinakuja zilkuwa tofauti sana, lakini sasa kuna njia tofauti za kukusanya habari ambazo ni rahisi mno kutokana na teknologia iliyopo. kwa kifupi watu wa kawaida wanauwezo wa kujua ni idadi gani ya waliokufa.

  Lakini hapa tatizo lingine ni city plan, Dar es salaam kama mji mkuu wa kibiashara na ndio makao makuu ya Tanzania(statehouse, wizara almost zote, makao makuu ya majeshi yote nk) kwa hiyo basi kijeshi Dar es salaam ni brigade ambayo imekamilika yaani ina vikosi vyote vya kijeshi (airwing, marine, infantry etc), katika plani ya mwanzo kabisa ya Dar haya makambi yalikuwa mbali sana na wananchi, sasa kutokana na poor planning unakuta watu wanajenga just close to the military bases ni ni ukweli usiofichika uwezi ukaamisha silaha zote Dar es salaam na kuziweka say Morogoro, kwani chochote kitachotokea hapa Dar kutakuwa hakuna quick response.

  Hizo military base kuwepo hayo maeneo ni muhimu kwa sababu yamepangwa kulingana na support ya kijeshi kutoka kambi moja na nyingine, lakini plani sahihi kabisa hayo maeneo ambayo yamepakana na jeshi say 2km yangepaswa kuwa industrial areas au godowns na vitu kama vivyo
   
 18. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #18
  Apr 30, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,920
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Haya MMM nimekusikiliza nimekupata. Was interesting!
   
 19. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #19
  Apr 30, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hivi wale watoto wa Tabora walikufa wangapi? Hatua gani zimechukuliwa mpaka sasa? Poleni wafiwa na wahanga wa mbagala


  Asha
   
 20. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #20
  Apr 30, 2009
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  "The Anatomy of Mediocrity, Pattern of Incompetence" naisubiria hiyo Mazee.

  Zero tolerance.
   
Loading...