Hotuba ya Rais: Tafadhali Mhe. Rais usiseme hivi..

Hivi wale watoto wa Tabora walikufa wangapi? Hatua gani zimechukuliwa mpaka sasa? Poleni wafiwa na wahanga wa mbagala


Asha

Washasahau kama tutakavyosahau hili baada ya wiki moja hivi.

Keshokutwa utasikia, Zombe, Ufisadi, Mengi habari ya mbagala kwisha kazi.

Na serikali wanatake advantage kimyaaaaaaaa! Tusubiri lingine
 
Du hii kali, Tanzania tunakwenda wapi? inaweza ikawa kama darfur sasa, hawa jamaa kama walikuwa wanahamisha hayo mabomu kimetokea nini mpaka yalipuke? Ni kitendawili ambacho jeshi wanajibu lake, ila nashauri makambi yote ya jeshi yaondolewe maeneo karibu raia mbona bado maeneo yako mengi? Nawapa pole wahanga wote wa malipuko ya mabomu, marehemu wote walale mahala pema peponi AMEN.
 
Kwa taarifa nilizozipata, Mabomu yaliyoripuka na yapo yanayoelekea kulipuka muda wowote kutoka hivi sasa yalitegwa kwa maana ya dharura hivyo kilichokuwa kinasubiriwa ni kufanya update yake kulingana na mabadiliko ya miundo mbinu kama majengo marefu na makazi ya watu. Sasa klichotokeo ni mistake wakati wa zoezi hilo na ni kweli kulikuwa na wanajeshi zaidi ya ishirini katika eneo la makombora hayo wakiwemo wenye vyeo vya juu.

ile amri ya kutoka maghorofani ilikuwa katika kuhofia mwelekeo wa makombara hayo yangeweza kufika hadi Tegeta, Bagamoyo na Tanga kwa kuwa setting ya awali ilikuwa bandari ya Tanga. Hivyo wandugu hali bado tete na kiukweli kama ingeendelea vile basi Dar, Pwani na Tanga kungenukia vifo na maafa ya kutisha. Shida ni moja tu, Jeshi haliko tayari kuweka wazi kinachoendelea kwani watu watakimbia hili Jiji kama ni waelewaji. Hapa niko njia kesho nahama huu mji kwa muda naenda kupumzika Mwanza hadi wataponidhibitishia usalama.

Kila mtu aeleke jiwe lake mwenyewe...GT upo ndugu yangu????
 
Ndiyo sababu labda Mkuu hajahutubia leo..au ni kesho? Najua alienda kuwatembelea wahanga leo..
 
Limeshapita hata kama waliokufa ni mia2 ,watu wanakufa kila siku.(Peoples are dying everyday)
Ila sisi tuliobaki tuendeleze pale tulipofikia kuchapana na mafisadi mpaka tujue zao au zetu.

Ila katika hiyo picha kuna magoigoi kibao sa mtu anatambaa wakati kuna kundi linaenda mbio ,hata kuna mjeshi mmoja kwa mbele anaonekana akikwepa mlio wa mabomu ,mguu mmoja wa suruali umo ndani ya kiatu na mwengine upo nje:D.
 
SUBIRINI UCHAGUZI; Ukifika tu 2010 wataanza kusema "VIta msiombee, kaulizeni Mbagala uchungu wa mabomo yaliyolipuka kwa bahati mbaya, vita siyo mchezo chagueni CCM ili nchi iwe na amani tuepuke maafa kupigana na watu kuumia. Wenzenu Uchungu wa vita tumejifunza Mbagala". Haya...! subirini mtaona.
 
SSSSSSSSShhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh mnajadili mambo ya usalama wa taifa hapa? hamjui kuwa ni kosa?
Hata kama kuna waliokufa au kualibiwa mali zao, hili wataliita ni suala la usalama wa taifa, hawatatoa taarifa ya kweli na hatutaruhusiwa kulijadili. Game over
 
SSSSSSSSShhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh mnajadili mambo ya usalama wa taifa hapa? hamjui kuwa ni kosa?
Hata kama kuna waliokufa au kualibiwa mali zao, hili wataliita ni suala la usalama wa taifa, hawatatoa taarifa ya kweli na hatutaruhusiwa kulijadili. Game over

Linauma kama lilivyomuuma Mkuu wa Kaya hata akashindwa Kwenda Musoma mkoani Mara kwenye sherehe za Mei Mosi jana na badala yake kaishia kumtuma Shein.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom