Mwalimu naomba unisaidie hesabu kidogo..
hesabu zangu hazipandi.. where am I messing it up?
Yepi hayatatendeki?. Please yaanishe ,Tuyaone-Tuyajadili. Sio unarusha maneno Tuu?Hotuba iliyo jaa spinning si hotuba .Mie sitaisoma kwa undani ila nataka kuona aliyo tueleza hadi akapewa kitim yanatendeka
Yepi hayatatendeki?. Please yaanishe ,Tuyaone-Tuyajadili. Sio unarusha maneno Tuu?
Uelevu wangu, Hatuna adui kutoka nje!"...Tunaumaliza mwaka nchi ikiwa na sifa kubwa katika medani ya kimataifa. Uhusiano wetu na mataifa yote duniani ni mzuri. Hatuna adui.
..nilijitahidi sana kusikiliza kwa makini hotuba ya huyu kilaza..lakini i saw and heard nothing new ...nikaishia kulala...nimejaribu hata kuisoma ..and i see it doesnt even worthy kuchangia lolote....no wounder hata thread ya hotuba za jk siku hizi haipati wachangiaji kwa kasi...
remember those days tulikuwa tunakesha kwa walio ngambo..kusubiria....na walio tanzania wanakesha wana post ....siku hizi watu wanaona usanii ndani ya sanaaaaaa!
Yote tisa kumi ni Kipande hiki..
Tunaumaliza mwaka nchi ikiwa tulivu. Hii inathibitisha kuwa nchi inaweza kuwa tulivu isipokuwa pale ambapo baadhi yetu tutakapokuwa tumeamua kuwa isiwe hivyo. Naomba mwaka 2009 uwe tofauti. Tuache vitendo vya kuchochea ghasia kwa kisingizio chochote kile. Vitendo hivyo havitavumiliwa hata kidogo. Ni vizuri tukaambiana mapema tusije tukalaumiana. Naomba Watanzania wenzangu wote na hasa wanasiasa wenzangu tuyatambue hayo na tujiepushe nayo. Naomba makundi ya kijamii yatambue ukweli huo na waache kuwaendekeza wanasiasa hasidi..
.
Je, maneno haya mazito yanaweza kuwa yametokana na kitu gani haswa!..
Mwaka wa 2008 tunaoumaliza leo ulikuwa mwaka wa aina yake kwa taifa letu na katika historia ya uongozi wangu. Ulikuwa ni mwaka ambao tumepata mafanikio mengi mazuri na mengine ya kihistoria katika nyanja mbalimbali za maisha ya wananchi wa Tanzania na taifa letu. Lakini, pia kulikuwepo na changamoto au matukio machache ambayo yalisababisha baadhi ya watu ndani na nje ya nchi yetu wapate shaka juu ya hatima ya umoja, amani na utulivu wa nchi yetu. Umoja, amani na utulivu ndiyo nguzo kuu na sifa kubwa inayoitofautisha na kutambulisha Tanzania miongoni mwa mataifa barani Afrika.
Ndugu Wananchi;
Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwamba tumeumaliza mwaka huu kwa usalama, amani na utulivu. Tuzidi kumuomba baraka na rehema zake, katika mwaka 2009, ili nchi yetu iendelee kuwa na amani, utulivu na watu wake waishi kwa upendo, umoja, masikilizano, mshikamano na ushirikiano kama ndugu wa taifa moja.
Pamoja na kumuomba Mwenyezi Mungu, hatuna budi kutambua kuwa dhamana ya kuhakikisha kuwa nchi yetu inaendelea kuwa tulivu na yenye amani na upendo miongoni mwa watu wake ni yetu wenyewe. Ni ukweli ulio wazi kuwa katika mwaka huu tunaoumaliza sasa baadhi yetu tumekuwa tunafanya vitendo au kutoa kauli ambazo zilikuwa zinalielekeza taifa kubaya. Tena tulikuwa tunafanya hivyo kwa ajili ya kuendeleza manufaa binafsi ya kisiasa. Ni matumaini yangu kuwa tutajiepusha na mambo hayo katika mwaka 2009. Nawasihi viongozi wenzangu wa kisiasa na wa kijamii tubadilike, tuweke mbele maslahi ya taifa ili tuiepushe nchi yetu na mabalaa ambayo baadhi ya wenzetu yaliwakuta.