Hotuba ya Rais Kikwete ya mwisho wa mwaka

Ebo, na sisi tuna forecasts za uchumi kumbe?? U learn something everyday ahaha

Mimi naona pale bongo kwa kweli ni utapeli tu, yaani mtu anasingizia financial turmoil kwenye kuraise funds za infrastucture, wakati tunakubali madini yaondoke bila faida kwetu.

Jk pesa ziko hapo hapo motherland ni kufunga mkanda tu na kusaidia nchi kwa kuzuia tax evasion na kupata angalau 30% ya utajiri wa mdini.
 
Wakati wa hotuba yake ya kuaga mwaka 2008 na kuukaribisha 2009, Rais Kikwete alisema hivi kuhusu hali ya chakula nchini:

Ndugu Wananchi;
Hali ya upatikanaji wa chakula nchini ni nzuri kwa miaka miwili mfululizo sasa, yaani 2007 na 2008, na tumekuwa tunapata ziada ingawaje ni kidogo. Napenda kuwahakikishia kuwa hakuna tishio la njaa nchini. Hata yale maeneo ambayo yamekuwa yanapata upungufu wa chakula tumeweza kuyahudumia kwa kutumia ziada hiyo na akiba kutoka katika Hifadhi ya Taifa ya Chakula (SGR).

Katika taarifa ya gazeti la Guardian la leo kuna habari hii:

Ten villages in Tunduru facing shortage of food

2009-01-02 12:09:32
By Augustino Chindiye, Tunduru


Hundreds of residents from at least ten villages in Misechela and Mtima wards in Tunduru District, Ruvuma Region are facing starvation due to acute shortage of food supplies.

According to the area councillor, Mohamedi Njalanjala many families have resorted to consumption of unripe mangoes as a way of sustaining their lives.

Speaking during an exclusive interview with this paper yesterday, Njalanjala requested for immediate action by higher authorities to avert the situation and save many lives.

He named the villages as Chiungo, Mkotamo, Meamtwaro, Liwanga and Misechela, whereby families are reportedly unable to afford even a single meal a day. Others are Mtina, Nakapanya, Mbesa, Nalasi and Mchoteka.

``It is heartbreaking to see all family members running to mango trees early in the morning for the day`s collection. Human beings deserve more than that.

It is time proper and corrective measures were taken to help these people lead descent lives,`` he said.

However, the councillor also proposed a change in attitude among the residents to avoid repetition of such uncertainty in life.

He wanted the villagers to cultivate the culture of saving food instead of consuming it all during local traditional festivals.

``People`s income has been reduced to the lowest. Prices of grain have become unaffordable such that a kilogramme of maize flour is sold at 1000/- and dried cassava roots currently fetching 350/- a kilogramme, of which people cannot afford,`` councillor Njalanjala explained.

He said he was worried that the situation would deteriorate further in case the mango season came to an end, adding that he feared that the entire village would be reduced to cheap labour at farms and estates of the well-to-do people.


SOURCE: Guardian
 
Generally hali ya uzalishajki wa chakua inaonysha kuwa katika nchi hautakuwa na na upungufu, lakini kuna maeneo ambayo yatakuwa na upungufu. Lakini naamini kuwa rais amedanganywa kwani sehemu nyingi sana hali ya chakula si nzuri, wafanyabiashara wamevusha sana mhindi kwenda kenya na kwa sababu ylikuwa yanavushwa kinyemela, serikali bado inayahesabia kuwa yamo nchini
 
MpendwaRaisi wetu kwa mara Nyingine tena anaongelea nia yake ya kupigana na rushwa na viashiria vya rushwa, lakini kinacho nishangaza kuhusu nia yake ni kuchagua wasaidizi au mawaziri na viongozi wengine wenye harufu ya rushwa ili wamsaidie katika hayo mapambano, mfano Mattaka wa ATCL toka alipokuwa PPF, then Dr Idrisa Rashid, Kuna akina Masha etc, sasa kweli nia yake inaweza kuelezewa namna gani na kuwa na watu kama hawa?
 
Vijiji Moro vyakabiliwa na uhaba wa chakula
Eline Shaidi, Morogoro
Daily News; Tuesday,January 06, 2009 @20:00

Vijiji vinane vilivyopo katika kata mbili za Mkambarani na Kidugalo katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, vinakabiliwa na upungufu wa chakula. Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Said Mwambungu imeeleza kuwa vijiji hivyo vipo katika ukanda wa ukame ambapo mtawanyo na kiwango cha mvua ni kidogo chini ya wastani wa milimita 600 za mvua kwa mwaka.

Alivitaja vijiji hivyo kuwa ni Mkono wa Mara kilichopo kwenye Kata ya Mkambarani, na vijiji vya Visaraka, Magela, Kidugalo, Kisemo, Lubumu, Seregete A na Seregete B vilivyopo kwenye Kata ya Kidugalo.

Aidha, Mwambungu alisema wananchi wanaoishi kwenye vijiji hivyo wamehamasishwa kutotumia chakula kidogo walichovuna katika sherehe, pamoja na ngoma kama ilivyo desturi yao, na hivyo kutumia chakula hicho vizuri.

Pia halmashauri hiyo imewahamasisha wafanyabiashara wilayani humo kununua chakula kutoka kwenye Hifadhi ya Chakula ya Taifa na kukiuza kwa wananchi kwa bei nafuu ili waondokane na tatizo hilo la njaa katika kipindi hiki.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa katika maeneo mengine ya wilaya hiyo, hali ya chakula ni nzuri isipokuwa katika maeneo hayo machache, na kuwataka wananchi kutumia vizuri chakula walichovuna katika kipindi cha mwaka jana.

Ilifafanua zaidi umbile la ardhi katika halmashauri hiyo, ambalo limegawanyika katika kanda kuu mbili muhimu ambazo ni ukanda wa milimani ambapo huhusisha tarafa za Mkuyuni na Matombo, na kueleza kuwa wananchi wa kanda hizo hujishughulisha na uzalishaji wa mazao ya mihogo, migomba na matunda.

Kwa upande wa ukanda wa mabondeni ambao huhusisha tarafa za Mvuha, Bwakira, Mikese na Ngerengere wananchi hujishughulisha na kilimo cha mahindi, mpunga, mtama, muhogo, migomba na magimbi.

Wazo:
Kama waandishi ndani ya wiki moja wameweza kupata vijiji karibu 20 vyenye matatizo ya chakula; kweli kauli ya Rais bado inaweza kusimama?
 
Back
Top Bottom