Hotuba ya Rais Kikwete ya mwisho wa mwaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hotuba ya Rais Kikwete ya mwisho wa mwaka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpita Njia, Dec 31, 2008.

 1. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hii hapa wakuu
   

  Attached Files:

 2. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #2
  Dec 31, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Nadhani Mod atarekebisha title ye thread hii
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Dec 31, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Watafanya jambo la mbolea, unajua tena mkuu vidole vina mifupa
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Dec 31, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mwalimu naomba unisaidie hesabu kidogo..

  hesabu zangu hazipandi.. where am I messing it up?
   
 5. M

  Mtu wa Kawaida JF-Expert Member

  #5
  Dec 31, 2008
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 217
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Hizo bil 39 ni zilizotolewa kwa CRDB na NMB pekee.
   
 6. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #6
  Dec 31, 2008
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  kuna zaidi ya billion 15 haijulikani ilikotoka kwani haikuwepo kwenye kiasi kilichotengwa na pia haijulikani ni nani wamepewa si ndiyo hivyo?
  otherwise walioandika hotuba wamerikoroga na Mkuu mwenyewe hana time.
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Dec 31, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  At least kupitia htub hii Muungwana anakiri (ingawa kidiplomsia) kuwa hali nchini sasa ni ngumu na itaendelea kuwa ngumu. nadhani angekwenda hatua moja mbele zaidi na kuanza kutafuta ushair nje ya anaowatumia kupata ushair hivi sasa kwa sababu nyakati tunazoelekea ni mbaya zaidi
   
 8. share

  share JF-Expert Member

  #8
  Dec 31, 2008
  Joined: Nov 22, 2008
  Messages: 2,293
  Likes Received: 2,277
  Trophy Points: 280
  Sikilizeni hotuba yake redioni, pengine dosari hiyo itakuwa imerekebishwa. Mlio ughaibuni sikilizeni RADIO MARIA mtandaoni. Kuna tetesi kuwa Radio Maria itarusha hewani live hotuba hiyo.
   
 9. B

  Baba Mkubwa JF-Expert Member

  #9
  Dec 31, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 770
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mpaka sasa ni nyimbo za RC. Bado tumetega misikio. Thanks
   
 10. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #10
  Dec 31, 2008
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Japo najua hakuna jipya ila nikipata mda nitaipitia
   
 11. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #11
  Dec 31, 2008
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Hesabu zetu hazipandi Mkjj. Tena huyu bwana anasema fedha zilizorudishwa hazikuzunguuka hapo ndipo tunaona kuwa nchi inaendashwa kisanii. Mtu anaandikiwa akasome tu kwa wananchi, Kule UDSM tulikuwa tunasema unapika data, ili upate marks. Kama kila mkoa umetoa billioni moja swali ni je Tanzania ina mikoa mingapi? 39 au. kuna anayefahamu mikoa ya Tanzania bara kwa sasa baada ya kuanzishwa mikoa mipya ya kisiasa kama Manyara etc? ili tusahihishe hesabu zetu
   
 12. I

  Ilongo JF-Expert Member

  #12
  Dec 31, 2008
  Joined: Feb 25, 2007
  Messages: 292
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0


  labda suala la kujiuliza ni: hivi hizi pesa zilianza kutolewa lini?
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Dec 31, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,601
  Likes Received: 82,167
  Trophy Points: 280
  JK ageuka mbogo
  Shadrack Sagati
  Daily News; Wednesday,December 31, 2008 @20:19

  Rais Jakaya Kikwete ameagiza mtumishi yeyote wa serikali ambaye atahusika na wizi au ubadhirifu wa fedha za umma kufikishwa katika vyombo vya sheria. Katika salamu zake za mwaka mpya kwa taifa, Rais alisema bado hali si ya kuridhisha katika matumizi ya fedha za umma kumfanya afurahi na akaahidi kuwa mwaka huu utakuwa wa kubanana katika jambo hilo ili ufanisi uweze kufikiwa.

  Alisema amewataka viongozi wenzake na watumishi wa serikali kusoma na kuzingatia maoni na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali yaliyomo katika taarifa zake za kila mwaka.

  “Kuanzia mwaka ujao nitawaomba wakaguzi wa mahesabu ya serikali kumkabidhi kwenye vyombo vya sheria mtumishi wa serikali aliyehusika na wizi au ubadhirifu mara watakapougundua,” alisema Rais.

  Aliongeza kuwa kwa sasa utaratibu hauko hivyo lakini akataka ofisi ya CAG itazame upya utaratibu wa sasa ili isaidie kujenga nidhamu hata kama ni ya woga wa kufungwa.

  “Itasaidia kunusuru fedha nyingi za umma zinazotumiwa isivyo.” Rais pia alimtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuendeleza kwa kasi na nguvu zaidi kazi waliyoianza ya ukaguzi wa thamani ya fedha zilizotumiwa na kulinganisha na kazi iliyofanyika (value for money audit).


  Alisema ukaguzi wa asili umekuwa unahusu uandishi wa vitabu kwa mujibu wa kanuni za fedha. Lakini, inawezekana kabisa vitabu vya hesabu vikaandikwa vizuri lakini pesa zikatumika vibaya au hata kuibiwa.

  Tunataka ulinganifu sawia wa fedha zilizotumika na kazi iliyofanywa. Pia Rais ameielekeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kufanya kazi kwa karibu na ofisi ya CAG kusaidia kupambana na wasiozingatia nidhamu ya matumizi ya fedha na mali za umma hususan wezi na wabadhirifu wa fedha za umma kwa kutumia sheria ya mwaka 2007 iliyounda Takukuru.

  “Nimewataka wawe wakali kwa wala rushwa kama wafanyavyo sasa, lakini pia wawe wakali kwa wale wote wanaokiuka kanuni za fedha za serikali,” alisema Rais Kikwete na kuongeza kuwa vitendo hivyo siyo tu vinaitia hasara serikali bali pia vinapunguza uwezo wa serikali kuwahudumia wananchi walioiweka madarakani.

  “ Nimewataka waitumie vyema sheria mpya na fursa waliyonayo ya kuwaongezea uwezo wa rasilimali tuliyowapa kwa kutimiza ipasavyo wajibu wao. Nimewasihi pia kwamba katika kufanya hivyo wasionee wala kupendelea watu bali watende haki.”


  Kuhusu mauaji ya albino, Rais alisema mapema mwaka ujao itaendeshwa kura ya maoni nchi nzima na amewataka wananchi wawataje watu wanaowajua kuwa wanajihusisha na mauaji au kukata viungo vya albino. Alisema watu wawataje waganga wanaohusika, wauaji wa albino, wauzaji wa viungo vya albino na wafanyabiashara wanaotumia viungo hivyo.

  Rais Kikwete alisema taarifa hizo zitasaidia kuwafuatilia na kuwakamata watu hawa waovu. Pia alisema utaratibu kama huu ulitusaidia katika mapambano dhidi ya ujambazi nchini. “Naamini utasaidia kwa hili... tunafanya matayarisho ya zoezi hilo na wakati utakapowadia watu wataarifiwa namna ya kushiriki.”

  Katika hotuba hiyo Rais alisema serikali imeunda kikosi-kazi kinachojumuisha Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa cha kuendesha mapambano haya. Aliongeza kuwa hivi sasa wanaendelea na uchunguzi wa kina nchi nzima kuwatambua wahalifu na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria. “Mpaka sasa watu 91 wamekamatwa na kufikishwa mahakamani na mapambano yanaendelea.”

  Katika salamu hizo za mwaka mpya, Rais Kikwete alisema mwaka umeisha nchi ikiwa tulivu. Alisema hiyo inathibitisha kuwa nchi inaweza kuwa tulivu isipokuwa pale ambapo baadhi ya watu watakapokuwa wameamua kuwa isiwe hivyo.

  “Naomba mwaka 2009 uwe tofauti. Tuache vitendo vya kuchochea ghasia kwa kisingizio chochote kile. Vitendo hivyo havitavumiliwa hata kidogo. Ni vizuri tukaambiana mapema tusije tukalaumiana,” alisema Rais Kikwete na kuwaomba wanasiasa wayatambue hayo na tujiepushe nayo.

  Pia aliomba makundi ya kijamii yatambue ukweli huo na waache kuwaendekeza wanasiasa hasidi. Alitoa onyo baada ya kueleza kuwa katika mwaka huu unaomalizika baadhi ya wanasiasa wamekuwa wanafanya vitendo au kutoa kauli ambazo zilikuwa zinalielekeza taifa kubaya.

  Alisema walifanya hivyo kwa ajili ya kuendeleza manufaa binafsi ya kisiasa. “Ni matumaini yangu kuwa tutajiepusha na mambo hayo katika mwaka 2009. Nawasihi viongozi wenzangu wa kisiasa na wa kijamii tubadilike, tuweke mbele maslahi ya taifa ili tuiepushe nchi yetu na mabalaa ambayo baadhi ya wenzetu yaliwakuta.”

  Kuhusu hali ya chakula, Rais aliwahakikishia wananchi kuwa hali ya upatikanaji wa chakula nchini ni nzuri kwa miaka miwili mfululizo sasa, yaani 2007 na 2008, na nchi imekuwa inapata ziada ingawaje ni kidogo.

  “Napenda kuwahakikishia kuwa hakuna tishio la njaa nchini.” Rais pia alizungumzia tsunami ya uchumi wa dunia na kueleza kuwa tatizo hilo litafanya malengo ya taifa ya kukua kwa uchumi mwaka 2008 na hata mwaka huu wa 2009. alisema uchumi utakua kwa asilimia 7.7 badala ya 7.8 mwaka 2008 na mwakani 2009 utakua kwa asilimia 7.3 badala ya asilimia 8 iliyokadiriwa.

  Kiongozi huyo alisema kudorora kwa uchumi wa dunia kunafanya idadi ya watalii kupungua na mapato yake kushuka kwa kati ya asilimia 7 na 18. Alisema pia kuwa mauzo ya mazao kama pamba na kahawa kwenye masoko ya nje nayo yameshuka.

  Rais alisema kupungua kwa mauzo nje na bei ya bidhaa zetu pamoja na kupungua kwa watalii kuna athari kwa uchumi wa nchi kwani mapato ya fedha za kigeni yatapungua jambo ambalo litapunguza akiba ya fedha za kigeni, hivyo kuathiri uwezo wetu wa kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje.

  Aidha alisema mapato ya serikali kwa kodi zitokanazo na mauzo hayo yatapungua, hivyo kuathiri uwezo wa serikali wa kutimiza majukumu yake ya kiutawala na kiuchumi. Isitoshe ajira chache zilizopo katika sekta husika zitapungua na kusababisha watu hao kuwa na hali mbaya kiuchumi.

  Kuhusu kupanda kwa gharama za bidhaa mbalimbali ikiwamo chakula, Rais alisema hali imeanza kuonyesha kushuka kwa mfumuko wa bei lakini akasema wakati mwingine hali huwa hivyo kwa sababu ya ukaidi na tamaa ya wafanyabiashara.

  Aliongeza kuwa amekwishawaagiza mawaziri wahusika kuzibana mamlaka husika kutimiza ipasavyo wajibu wao kwa mujibu wa mamlaka waliyopewa kisheria kuwalinda wananchi dhidi ya wafanyabiashara wa aina hiyo.

  Pia alitaka wafanyabiashara watoe ushirikiano unaostahili kwa maslahi ya wateja wao na taifa. “ Aidha, nazitaka mamlaka husika kutochelewa wala kuchelea kuchukua hatua zipasazo kwa wafanyabiashara wakaidi
   
 14. share

  share JF-Expert Member

  #14
  Dec 31, 2008
  Joined: Nov 22, 2008
  Messages: 2,293
  Likes Received: 2,277
  Trophy Points: 280
  Mpole wakuu wote ukiwemo mheshimiwa Mbalawata. Labda tetesi hazikuwa za kweli au labda ratiba ilibadilika, hata mimi sikuisikia hewani kupitia Radio Maria. Samahani kwa usumbufu wowote mlioupata wakuu.
   
 15. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #15
  Jan 1, 2009
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Hivi hiyo ilikuwa "NGONJERA" au "SHAHIRI" kutoka kwa raisi?

  Sioni mtazamo wowote wa maana ambao JK ameuweka. Vyuo vya elimu ya juu vimefungwa halafu yeye anaona kweli taifa lina usalama kweli? Serikali imeagiza SUV 700? 800? halafu hata kusema "MATREKTA" mangapi yataagizwa kwa ajili ya kilimo "NEY". Hizo hela za EPA zilizoelekezwa kwenye kilimo, mbona hakuna KIONGOZI yeyote anayejua kinachoendelea? Si JK, MKULO wala WAZIRI WA KILIMO. HIZO HELA ZIPO AU MNATUZUGA TU?

  Wananchi wanakufa kila siku kwa uzembe wa "MADEREVA" na rushwa ilikithiri "POLISI" halafu bado anawabembeleza wahusika?

  ATCL, BANDARI, TRC wote wanakuwa "OMBA OMBA" wa "KODI ZA WANANCHI" halafu JK anasema eti wataboresha mpaka watu wafurahie? Tufurahie kodi zetu badala ya kutueleza hayo mashirika yatafanikisha vipi tija na huduma bora mpaka kufikia hatua ya kujitegemea na kutengeneza faida kwa manufaa ya nchi?

  Kuna maana gani ya kukusanya kodi kiasi hicho kama hela yote inarudi kwenye mashirika yasiyoweza kujiendesha kwa faida?

  Hakuna kitu chochote wala mtazamo wowote ambao JK ameweza kuuweka zaidi ya wimbo tunaosikia kila siku kutoka kwa viongozi wasiokuwa na dira wala sera mpya ya kumkomboa mwananchi.
   
 16. Companero

  Companero Platinum Member

  #16
  Jan 1, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  MAGAZIJUTO:

  Mikoa ya Tanzania Bara:

  1. Dar-es-Salaam = Bilioni 1 za Bwana Fulani
  2. Mwanza = Bilioni 1 za Bwana Fulani
  3. Arusha = Bilioni 1 za Bwana Fulani
  4. Manyara= Bilioni 1 za Bwana Fulani
  5. Dodoma= Bilioni 1 za Bwana Fulani
  6. Singida= Bilioni 1 za Bwana Fulani
  7. Rukwa= Bilioni 1 za Bwana Fulani
  8. Ruvuma= Bilioni 1 za Bwana Fulani
  9. Mbeya= Bilioni 1 za Bwana Fulani
  10. Pwani= Bilioni 1 za Bwana Fulani
  11. Morogoro= Bilioni 1 za Bwana Fulani
  12. Tanga= Bilioni 1 za Bwana Fulani
  13. Kilimanjaro= Bilioni 1 za Bwana Fulani
  14. Tabora= Bilioni 1 za Bwana Fulani
  15. Kigoma= Bilioni 1 za Bwana Fulani
  16. Mtwara= Bilioni 1 za Bwana Fulani
  17. Lindi= Bilioni 1 za Bwana Fulani
  18. Iringa= Bilioni 1 za Bwana Fulani
  19. Shinyanga= Bilioni 1 za Bwana Fulani
  20. Mara= Bilioni 1 za Bwana Fulani
  21: Kagera= Bilioni 1 za Bwana Fulani
  --------------------------------------
  Jumla=Bilioni 21 za Bwana Fulani
  --------------------------------------

  Mikoa ya Zanzibar:

  Pemba Kaskazini = Milioni 100
  Pemba Kusini=Milioni 100
  Unguja Kaskazini=Milioni 100
  Unguja Kusini=Milioni 100
  Unguja Mjini Magharibi=Milioni 200
  --------------------------------------
  Jumla= Milioni 600= Bilioni 0.6
  --------------------------------------

  Jumla Yote: Bilioni 21 + 0.6 = Bilioni 21.6 za Bwana Fulani
  -------------------------------------------------------
  Kiasi Kilichokopeshwa na Benki za CRDB na NMB = Bilioni 39 za Bwana Fulani
  Kiasi Kilichotolewa kwa wilaya 46 za Tanzania Bara = Bilioni 4.6 za Bwana Fulani
  Kiasi Kilichotolewa kwa SACCOS na watu/vikundi vingine = Bilioni ? za Bwana Fulani

  Salio= Bilioni ? za ?
   
 17. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #17
  Jan 1, 2009
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145

  Salio = Bilion 10 za "MZEE". Unajua tena, "FUNIKA KOMBE MWANAHARAMU APITE".
   
 18. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #18
  Jan 1, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwa nini sasa Mara na Kagera hawamo kwenye mgawo?
   
 19. Companero

  Companero Platinum Member

  #19
  Jan 1, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Asante kwa angalizo, tupo wengi tunaokosea mahesabu - sio waheshimiwa tu, ndio utamaduni wetu huo!Rejea magazijuto hapo juu, nimesharekebisha.
   
 20. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #20
  Jan 1, 2009
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Na hii imekaa vipi?
  Naomba mwaka 2009 uwe tofauti. Tuache vitendo vya kuchochea ghasia kwa kisingizio chochote kile. Vitendo hivyo havitavumiliwa hata kidogo. Ni vizuri tukaambiana mapema tusije tukalaumiana. Naomba Watanzania wenzangu wote na hasa wanasiasa wenzangu tuyatambue hayo na tujiepushe nayo. Naomba makundi ya kijamii yatambue ukweli huo na waache kuwaendekeza wanasiasa hasidi
   
Loading...