Ifuatayo ni dondoo kutoka hotuba ya Kikwete kwa Taifa ya kufunga mwaka:
Ndiyo maana tukaamua kuanzisha mchakato huu na kwa ajili hiyo, nimeamua kuunda Tume maalum ya Katiba, yaani [/SIZE][/FONT][FONT=Palatino Linotype, serif]Constitutional Review Commission. [/FONT][FONT=Palatino Linotype, serif]Tume hiyo [/FONT][FONT=Palatino Linotype, serif]itakayoongozwa na Mwanasheria aliyebobea, itakuwa na wajumbe wanaowakilisha makundi mbalimbali katika jamii yetu kutoka pande zetu mbili za Muungano. Jukumu la msingi la Tume hiyo litakuwa ni kuongoza na kuratibu mchakato utakaowashirikisha wananchi wote bila kubagua, vyama vya siasa, wanasiasa, wafanyabiashara, asasi za kiraia, mashirika ya dini, wanataaluma na makundi mbalimbali ya watu wa nchi yetu kote nchini, katika kutoa maoni yao juu ya wayatakayo kuhusu Katiba ya nchi yao.[/FONT]