([FONT=Palatino Linotype, serif]Ndugu Wananchi;[/FONT]
[FONT=Palatino Linotype, serif]Natambua[/FONT][FONT=Palatino Linotype, serif] kuwepo kwa mazungumzo, katika jamii kuhusu uamuzi wa EWURA wa kukubali ombi la Shirika la Umeme (TANESCO) kuongeza bei ya umeme. Wakati mwingine mazungumzo yamekuwa na hisia kali na hata jazba kutawala. Wizara, TANESCO na EWURA wameeleza kwa ufasaha misingi iliyotumika mpaka kufikia uamuzi huo. Sina maelezo mazuri zaidi ya hayo. Ninachotaka kusema mimi ni kuwaomba Watanzania wenzangu kutokukubali suala hili la kibiashara na kiuchumi kugeuzwa kuwa la kisiasa na kutafutiwa majawabu ya kisiasa. [/FONT]
[FONT=Palatino Linotype, serif]Naomba tuamini [/FONT][FONT=Palatino Linotype, serif]na kukubali maelezo ya TANESCO na EWURA kwamba katika miaka minne hii gharama za uendeshaji, uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme zimepanda kama zilivyopanda katika shughuli nyingine. Hivyo basi, kutaka bei ya umeme ibaki kama ilivyokuwa miaka minne iliyopita hautokuwa uamuzi sahihi kiuchumi na kibiashara kwa TANESCO. EWURA imefanya kazi nzuri ya kuchambua maombi ya TANESCO na kuyakubali yanayostahili na kuyakataa yasiyostahili kuwa sehemu ya bei. Kwa kufanya hivyo, watumiaji wa umeme wamelindwa wasibebeshwe mzigo usiostahili na Shirila la Umeme limewezeshwa ili lisiendeshe shughuli zake kwa hasara. [/FONT])
Mkulu JK hivi hujui kwamba gharama za uendeshaji za Tanesco zimetokana na mikataba ya kinyonyaji iliyoingia na makampuni feki na makampuni ya kinyonyaji? Kuwapa watanzania adhabu ya kulipa unyonyaji huu ni kuwaonea, mkulu tafuta namna ya kudhibiti malipo ya kinyonyaji yanayofanywa na Tanesco ili bei ya umeme ibaki kama ilivyokuwa. Heri ya Mwaka mpya.