Hotuba ya rais Kikwete ya kufunga mwaka 2010

Hotuba ya rais Kikwete ya kufunga mwaka 2010

CONGRATS kIKWETE kwa hili la katiba.Ume pre empty na naamini utaendelea kuwa msikivu.Ulishauriwa wakati wa kampeni uzungumzie ufisadi na pesa za EPA katika hali ya kukubali kosa kwani hiyo ingewafanya wapinzani wako wakose hoja lakini ukamsikiliza Makamba na mmeyaona.Naamini unajipanga upya na hili la Dowans mwaga ugali tumwage MBOGA.
 
Angalau sasa nimejua kuwa katiba mpya inafanyiwa kazi na kwamba mchakato wake unaandaliwa na raisi. Ila kinachonisikitisha ni kwamba viongozi wa chini ni waropokaji na hawana nidhamu.

Selina kombani - serikali haina hela [alishauriana na rais au waziri mkuu?]
werema - katiba ifanyiwe marekebisho tu [ aliongea na rais au waziri mkuu?]
huu ni udhaifu wa viongozi wetu kuropoka tu.

Pinda yeye alisema kuwa atashauriana na rais na nadhani amefanya hivyo. Huyu ni kiongozi makini.

Ukiacha suala la katiba bado kuna vitu vinatu ambavyo hajavisemea
1. Suala la dowans
2. Suala la barabara ya serengeti
3. Suala la mishahara ya wafanyakazi wa sekta zote. Binafsi na ya serikali
4. Suala la meremeta

hivyo bado mapungufu ni mengi sana.
 
[FONT=Palatino Linotype, serif]Nimewataka Mawaziri husika na hasa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya na vyombo vya dola yaani Polisi na TAKUKURU kufuatilia mwenendo mzima wa usambazaji na upatikanaji wa mbolea, mbegu na dawa za ruzuku kwa wakulima na wafugaji. Wawatafute na kuwabaini wale wote wanaofanya vitendo viovu kinyume na taratibu zilizowekwa na kuwachukulia hatua za kisheria na kinidhamu. Watu hawa ni wahujumu wa uchumi, ni adui wa wakulima, wafugaji na taifa zima kwa jumla. Hawastahili na wala wasionewe huruma hata chembe.

Mafisadi wangekua wanashughulikiwa ivi,,Tanzania ingekua mbali sana.
[/FONT]
 
MIGOMO VYUO VIKUU haitokani na wanasiasa,jk mwenyewe alikiri kuwa bodi ina matatizo,sa wanafunz watakula nyasi?ebo....yani mwanafunzi wa chuo kikuu atagoma bila 7bu?ye hana akili?mtu akigoma ujue kuna 7bu,hao usalama wa taifa mda mwingne wanatoa taarifa fake,wanafunzi wanapenda upinzani coz serikali imeshndwa kusimamia mambo kwa umakini
 
Ndugu Wananchi;
Ndiyo maana tukaamua kuanzisha mchakato huu na kwa ajili hiyo, nimeamua kuunda Tume maalum ya Katiba, yaani Constitutional Review Commission. Tume hiyo itakayoongozwa na Mwanasheria aliyebobea, itakuwa na wajumbe wanaowakilisha makundi mbalimbali katika jamii yetu kutoka pande zetu mbili za Muungano. Jukumu la msingi la Tume hiyo litakuwa ni kuongoza na kuratibu mchakato utakaowashirikisha wananchi wote bila kubagua, vyama vya siasa, wanasiasa, wafanyabiashara, asasi za kiraia, mashirika ya dini, wanataaluma na makundi mbalimbali ya watu wa nchi yetu kote nchini, katika kutoa maoni yao juu ya wayatakayo kuhusu Katiba ya nchi yao.
Baada ya kukamilisha kukusanya maoni, Tume itatoa mapendekezo yake yatakayofikishwa kwenye vyombo stahiki vya Kikatiba kwa kufanyiwa maamuzi. Baada ya makubaliano kufikiwa, taifa letu litapata Katiba mpya kwa siku itakayoamuliwa ianze kutumika.

Ndugu Wananchi;
Ni matumaini yangu kuwa mchakato huo utaendeshwa vizuri, kwa amani na utulivu kama ilivyo sifa ya nchi yetu na mazoea yetu ya kujadiliana bila kugombana. Wananchi watapewa fursa ya kutosha ya kutoa maoni yao kwa uhuru na pawepo kuvumiliana kwa hali ya juu pale watu wanapotufautiana kwa mawazo. Pasiwepo kutukanana, kudharauliana, kushutumiana, kubezana, kuzomeana wala kushinikizana. Naomba washiriki waongozwe kwa hoja badala ya jazba. Tukiwa na jazba, hasira na kushinikizana kamwe hatutaweza kutengeneza jambo jema. Na inapohusu Katiba ya Nchi itakuwa hasara tupu. Haitakuwa endelevu na kulazimika kufanyiwa marekebisho mengi mwanzoni tu baada ya kutungwa.

Nawaomba Watanzania wenzangu wenye maoni yao wajiandae kushiriki kwa ukamilifu katika mchakato huu. Katoeni maoni yenu mazuri yatakayowezesha nchi yetu kuwa na Katiba itakayokidhi matakwa yetu ya sasa na ya miaka 50 ijayo.

Hapa maji yamezidi unga. Let us give him the benefit of doubts kama itakuwa tayari 2015.

Time will tell.
 
Nadhani walimwonya Makamba safari hii. Hata naye amesema, mwenyekiti wake atalitolea tamko, nandilo litakuwa tamko la chama cha mapinduzi. Na hicho ndicho kimetokea leo hii.

Kikwete asingeweza kuitolea nje hoja ya katiba mpya kwa kuwa he has nothing to lose kwa sasa. Ameshaiba kura, amekuwa Rais wa magendo kwa uporaji wa haki za watanzania. May be atasimamia kipengele kimoja tu cha Rais kutoshitakiwa mahali popote kutokana na maamuzi na utendaji wake akitekeleza kazi yake ya Urais, na Uamiri jeshi mkuu.

Ushauri huu wa katiba mpya umetoka kwa Benson Bana wa Redet. Bana kamshauri JK asome alama za nyakati, kwa kuwa kuna uchaguzi wa serekali za mitaa 2014, na asingekubali katiba mpya angechemsha- Soma gazeti la mwananchi.

Hili ni shinikizo, na kabla hatujashangilia kwanza tuone hiyo commission itakayoundwa itakuwa na watu gani then ndio tujue

JK pia alijua akiongelea suala la katiba watu watamsamehe kuhusu issue ya Dowans, CDM msidnanganyike, JK aache unafiki, hawezi kuongelea suala la matumizi ya serkali akaacha kugusia suala la Dowans, ni uzandiki. Lakini kwa usanii wake kacheza karata ya katiba ili kuzima issue ya Dowans, Katiba wala hakuwa na haja ya kuiongelea kwani hilo lilishakuwa impossible kulikwepa. Watanzania JK atazidi kuzichezea akili zetu hadi lini?
 
Niliishawahi kusema kwenye posting zangu za nyuma kwamba Tanzania tuna uncoordinate government ambako mawaziri wanatamka mambo ambayo ndani ya siku chache linatolewa tamko lingine kutoka kwa aliye juu ya waziri n.k. Kama Kikwete anasema Katiba mpya haikwepeki, ni wapi Kombani na Werema walipata ubavu au maelekezo kusema vinginevyo?

Kuna tatizo ambalo labda serikali yenyewe hailioni!

Tiba

Walitumwa kupima upepo
 
Nadhani tuwe na imani na Rais wetu. Tumuombe Mungu na kwa Rehema za Mola uwenda Taifa hili likawa na mabadiliko makubwa yakisiasa na uchumi ambayo yatawavuta weng kuipenda Tanzania! Mim nikiwa kama mwanaharakati na mtu mwenye uchungu na Taifa langu sichelei kusema nina imani bado God yupo ktk control of ths nation. We are great nation.
 
baaado hatudnganyiiiki..........kama ni tume iundwe na bunge na sio yeye
dr slaa tupo pamoja nawe,ahasante na gazeti la mwanahalisi kwa kututoa matongotongo ndo tumegundua kua kumekuucha
 
Kauri ya Rais ni ya mwisho, Werema na Celina hawakuwa makini kwa kutokuangalia hali halisi na hivyo hawana sifa ya kiongozi bora. They lack "vision"
tatizo ni kua viongozi wtu ni watu wa kujipendekeeza sna ooona sasa CELINA KOMBANI uso wako utaficha wapy jamaa ndo keshasema hivo tho huwa animba ngonjera tu no actions.
 
Rais wetu syo makini hta kdgo! Just imagine ktk speech hiyohiyo anasema gharama za shughuli/bidhaa mbalimbali zmepanda as justification ya kupanda kwa bei ya umeme, then anasema inflation imeshuka more than halfly! Mi apa sjaelewa wadau, plz nijuzeni?
tatizo lake analetewa paper mezani bila hata kuipitia vizuri ye anapresent tu,kweeeli hizo ghrama za umeme tunaenda kuwalipa dowans ka anauchungu na sisi hebu basi awe anatoa nusu ya mshahara wake kila mwezi nae kuchangia hizo gharama zilizopanda
 
Afadhali hata Makamba hakuwa na papara ya kuropoka kuhusu msimamo wa CCM katika hili maana alishasoma ishara kutoka wananchi.
 
Kombani na Werema wajiuzulu. Wameropoka uongo ambao haukuwa na baraka kutoka juu! Vinginevyo washushwe vyeo.

Msidanganywe na cheap politics hizo ni mbinu za medani ya siasa kuwatwisha mizigo watu wa pembeni,Haya yalikuwepo hata enzi za Mwalimu,kuna wakati maagizo yalitolewa na Mwalimu mtekelezaji akiwa wakati huo Rashidi Kawawa,wakati wa uanzishaji wa vijiji vya Ujamaa.
 
kwa hili la katiba mpya amenena............mengine haya ni ya siku zote..........
 
Wewe una matatizo maana sidhani kama hii speech ni mbovu.
:focus::focus: hatudanganyiiiki.......iatundwa tume itaundwa tume upuuuzi tu zimeundwa tume ngapi na mwisho wake no actions taken.hvimbona hukui?nnicha kusifia kwenye ile hotuba?
NAKABIDHI
 
KIMEELEWEKA!... Kikwete amehofu kupingana na sauti ya umma. Attorney General Frederick Werema na Waziri wa Sheria na Katiba Celina Kombani wajiuzulu au wafukuzwe kazi kwa kupinga katiba mpya.

Kila mtu ana mtazamo wake, si lazima wote tukawa na mtazamo aina moja. Ndio maana watu hupiga kura, huunda tume na kadhalika, ili ipatikane suluhu kwa wenye muono tafauti.

Hakuna sababu ya kumfukuza mtu kazi au kumlazimisha ajiuzulu ati kwa sababu tu, yeye ana mtazamo tofauti na wako.
 
Ahsante Mheshimiwa Rais wetu mpendwa, Jakaya Mrisho Kikwete. Hotuba ni nzuri sana na imewafunga midomo wenye vidomo vidomo. Keep it up, you are the best.
 
Ndugu Wananchi;
Ndiyo maana tukaamua kuanzisha mchakato huu na kwa ajili hiyo, nimeamua kuunda Tume maalum ya Katiba, yaani
Constitutional Review Commission. Tume hiyo itakayoongozwa na Mwanasheria aliyebobea, itakuwa na wajumbe wanaowakilisha makundi mbalimbali katika jamii yetu kutoka pande zetu mbili za Muungano. Jukumu la msingi la Tume hiyo litakuwa ni kuongoza na kuratibu mchakato utakaowashirikisha wananchi wote bila kubagua, vyama vya siasa, wanasiasa, wafanyabiashara, asasi za kiraia, mashirika ya dini, wanataaluma na makundi mbalimbali ya watu wa nchi yetu kote nchini, katika kutoa maoni yao juu ya wayatakayo kuhusu Katiba ya nchi yao.

[FONT=Palatino Linotype, serif]Baada ya kukamilisha kukusanya maoni, Tume itatoa mapendekezo yake yatakayofikishwa kwenye vyombo stahiki vya Kikatiba kwa kufanyiwa maamuzi. Baada ya makubaliano kufikiwa, taifa letu litapata Katiba mpya kwa siku itakayoamuliwa ianze kutumika.[/FONT]

[FONT=Palatino Linotype, serif]Ndugu Wananchi;[/FONT]
[FONT=Palatino Linotype, serif]Ni matumaini yangu kuwa mchakato huo utaendeshwa vizuri, kwa amani na utulivu kama ilivyo sifa ya nchi yetu na mazoea yetu ya kujadiliana bila kugombana. Wananchi watapewa fursa ya kutosha ya kutoa maoni yao kwa uhuru na pawepo kuvumiliana kwa hali ya juu pale watu wanapotufautiana kwa mawazo. Pasiwepo kutukanana, kudharauliana, kushutumiana, kubezana, kuzomeana wala kushinikizana. Naomba washiriki waongozwe kwa hoja badala ya jazba. Tukiwa na jazba, hasira na kushinikizana kamwe hatutaweza kutengeneza jambo jema. Na inapohusu Katiba ya Nchi itakuwa hasara tupu. Haitakuwa endelevu na kulazimika kufanyiwa marekebisho mengi mwanzoni tu baada ya kutungwa.[/FONT]

[FONT=Palatino Linotype, serif]Nawaomba Watanzania wenzangu wenye maoni yao wajiandae kushiriki kwa ukamilifu katika mchakato huu. Katoeni maoni yenu mazuri yatakayowezesha nchi yetu kuwa na Katiba itakayokidhi matakwa yetu ya sasa na ya miaka 50 ijayo. [/FONT]
 
[FONT=ArialMT, sans-serif]President Jakaya Kikwete said yesterday Tanzania needed a new constitution to march with the country's 50 years of nationhood.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]In his end-of-the year address to the nation, Kikwete said: "We, in the government, have agreed to lead the process for the constitution review in order to come up with a document that accommodates the current dynamics and developments."[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]He said in fast-tracking the process he had formed a special Constitutional Review Commission. He said the body, which is led by the Attorney General, comprises members from different groups from both sides of the union - Zanzibar and Mainland.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]According to the president, the commission has been tasked to oversee the constitutional review processes by collecting views of social groups, political parties, business people, civil societies, religious organizations and experts.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]After collecting stakeholders' inputs, he said, the commission will give its recommendations which will be forwarded to the relevant organs for decision-making. [/FONT]
"[FONT=ArialMT, sans-serif]After these processes, the nation will have a new constitution," he noted, adding: "We want to have constitution that matches with the 50-years-old nation (Tanzania)." [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]This year, Tanzania will mark 50 years of Tanganyika's independence, 47 years of the Zanzibar Revolution and 47 years of the Union.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kikwete, however, defended the current constitution engineered by the founders of the nation saying it moved the country from the post-independence period to "where we are now."[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]The existing constitution, he said, contributed to the country's social, political and economic development.[/FONT]
"[FONT=ArialMT, sans-serif]But there are many changes that have occurred between the post-independence days and today, which require a constitution that accommodates all current developments and changes," said the president.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]The President's stance on the constitution has come at a time when the country was engulfed in heated debate over whether it should have a new constitution or not.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Attorney General Frederick Werema's recent remarks that the country did not need a new constitution have been received with mixed feelings with a section of the public accusing him of trying to strangle debate on the issue.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]At one time, Constitutional Affairs and Justice Minister, Celina Kombani, played down public demand for new constitution on the simple reasons that "the process is unnecessarily expensive.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kombani's provoked heated public debates, with some people calling for resignation of the constitutional affairs' minister, accusing her of undermining concerns of Tanzanians for constitutional reforms. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Prime Minister, Mizengo Pinda recently in a meeting with editors, promised to advise the president on the need to have new constitution.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Dwelling on the country's security, President Kikwete said the situation was stable with all borders safe and secure and that there was no threat from any place or people regarding the security of the country.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]On democracy, President Kikwete said it has grown tremendously, admitting that opposition parties were becoming stronger and therefore posing a challenge to the ruling party.[/FONT]
"[FONT=ArialMT, sans-serif]Last year's general election posed great challenge and the power of opposition parties has increased tremendously," admitted the president. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]On the management of public funds, Kikwete said he had directed concerned authorities to ensure they supervise revenue collection and expenditure of public funds more efficiently.[/FONT]
"[FONT=ArialMT, sans-serif]I am not satisfied with the use of public funds. The discipline in this is still wanting," he commented.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]On the economy he said the country expected the economy to grow by up to 7.2 per cent compared to 6 per cent of 2009.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]He said inflation has also gone down from 12.1 per cent in 2009 to 5.5 per cent 2010 and it was expected that it would continue to go down.[/FONT]
 
Ndugu zangu wapendwa, hivi kweli tunashaladia hiyo katina mpya wakati kuna mambo mengine huyu bwana angeyafanya kiufasana nafikiri tusingefikia kulazimisha hiyo katiba. Nimegundua kweli watanzania sometimes tunakuwa vipofu wa muda. Mungu atusaidie hiyo katiba ije vizuri siyo ihalalishe ufisadi.
 
Back
Top Bottom