[FONT=Palatino Linotype, serif]Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru
[/FONT]
[FONT=Palatino Linotype, serif]
Mwaka mpya tunaouanza usiku wa leo una umuhimu wa kipekee katika uhai na historia ya nchi yetu. Tarehe 9 Desemba 2011 nchi yetu itatimiza miaka hamsini ya Uhuru wa Tanzania Bara. Haya si mafanikio madogo hata kidogo. Ni mafanikio makubwa sana ambayo hatuna budi kuyafurahia na kuyasherekea kwa uzito unaostahili. [/FONT]
[FONT=Palatino Linotype, serif]
Katika miaka 50 ya Uhuru wetu tumefanya mambo mengi mazuri ya kujivunia katika nyanja mbalimbali. Tumedumisha uhuru na umoja wa nchi yetu. Kwa hakika hali yetu ilivyo leo kisiasa, kiutamaduni, kiuchumi, kijamii, kiusalama na kimaendeleo kwa jumla, ni tofauti sana na hali ilivyokuwa wakati Tanzania Bara inapata uhuru wake tarehe 9 Desemba, 1961. Natambua pia kwamba katika miaka 50 hii, nchi yetu na watu wake wamekumbana na kukabili changamoto nyingi. Zipo nyingi tulizoziweza na zipo ambazo tunaendelea kuzikabili na tunayo mipango thabiti ya kuhakikisha tunafanikiwa.[/FONT]
[FONT=Palatino Linotype, serif]
Kwa kutambua umuhimu wa aina yake wa maadhimisho ya mwaka huu ya siku ya Uhuru wa Tanzania Bara tarehe 9 Desemba, 2011, tumekubaliana na viongozi wenzangu Serikalini kuwa tusherehekee siku hiyo kwa uzito unaostahili. [/FONT]
[FONT=Palatino Linotype, serif]
Ndugu Wananchi;[/FONT]
[FONT=Palatino Linotype, serif]
Tumekubaliana pia, tufanye mambo manne muhimu katika maadhimisho hayo. [/FONT][FONT=Palatino Linotype, serif]
Kwanza,[/FONT][FONT=Palatino Linotype, serif]
nautangaza mwaka 2011 kuwa ni Mwaka wa Maadhimisho ya Miaka Hamsini ya Uhuru wa Tanzania Bara. Kilele chake kitakuwa tarehe 9 Desemba, 2011 ambapo kutafanyika sherehe kubwa na za aina yake nchi nzima ambapo wananchi watashirikishwa kwa ukamilifu. [/FONT]
[FONT=Palatino Linotype, serif]
Pili,[/FONT][FONT=Palatino Linotype, serif]
tufanye tathmini ya kina ya mafanikio tuliyoyapata, katika juhudi zetu za kujiletea maendeleo katika miaka hamsini hii. Kila Wizara, idara na taasisi za Serikali na hata sekta binafsi zifanye tathmini ya eneo lake. Tathmini hizo ziandikwe katika vitabu ili kuhifadhi kumbukumbu hizo muhimu kwetu na kwa vizazi vijavyo. Vitabu na nyaraka hizo vitakuwa kumbukumbu zenye manufaa makubwa kwa wenzetu watakaokuwepo mwaka 2061 wakati wa kusherehekea miaka [/FONT][FONT=Palatino Linotype, serif]
100[/FONT][FONT=Palatino Linotype, serif]
ya Uhuru wa Tanzania Bara. Itarahisisha kazi yao ya kufanya tathmini wakati huo. [/FONT]
[FONT=Palatino Linotype, serif]
Tatu,[/FONT][FONT=Palatino Linotype, serif]
kwamba yafanyike maonyesho maalum katika Uwanja wa Maonyesho wa Julius Nyerere hapa Dar es Salaam na kote mikoani kwenye viwanja vya maonyesho, kuelezea mafanikio yaliyopatikana katika nyanja mbalimbali katika miaka 50 tangu Uhuru wa Tanzania Bara.[/FONT]
[FONT=Palatino Linotype, serif]
Ndugu Wananchi;[/FONT]
[FONT=Palatino Linotype, serif]
Jambo la [/FONT][FONT=Palatino Linotype, serif]
nne [/FONT][FONT=Palatino Linotype, serif]
ambalo tulilokubaliana kufanya ni kuanzisha mchakato wa kuitazama upya Katiba ya Nchi yetu kwa lengo la kuihuisha ili hatimaye tuwe na Katiba inayoendana na taifa lenye umri wa nusu karne. Katiba yetu ya sasa tuliyoachiwa na waasisi wa taifa letu, imeifanyia nchi yetu mambo mengi mazuri na kuifikisha Tanzania na Watanzania hapa tulipo. Tunayo nchi moja huru, ya kidemokrasia na inayoendesha mambo yake kwa kuzingatia utawala wa sheria, kuheshimu haki za binadamu na mgawanyo wa madaraka miongoni mwa mihimili mikuu ya dola. Nchi yenye amani, utulivu na watu wake ni wamoja, wanaopendana na kushirikiana na maendeleo yanazidi kupatikana. [/FONT]
[FONT=Palatino Linotype, serif]
Pamoja na hayo, mwaka 2011, nchi yetu inatimiza miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, miaka 47 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar na miaka 47 ya Muungano wa nchi zetu mbili. Yapo mabadiliko mengi yaliyotokea katika nyanja mbalimbali za maisha ya nchi yetu na watu wake katika kipindi hiki. Kwa ajili hiyo ni vyema kuwa na Katiba inayoendana na mabadiliko na matakwa na hali ya sasa. Katiba ambayo italipeleka taifa letu miaka 50 ijayo kwa salama, amani, umoja na kuwepo maendeleo makubwa zaidi.[/FONT]
[FONT=Palatino Linotype, serif]
Ndugu Wananchi;[/FONT]
[FONT=Palatino Linotype, serif]
Ndiyo maana tukaamua kuanzisha mchakato huu na kwa ajili hiyo, nimeamua kuunda Tume maalum ya Katiba, yaani [/FONT][FONT=Palatino Linotype, serif]
Constitutional Review Commission. [/FONT][FONT=Palatino Linotype, serif]
Tume hiyo [/FONT][FONT=Palatino Linotype, serif]
itakayoongozwa na Mwanasheria aliyebobea, itakuwa na wajumbe wanaowakilisha makundi mbalimbali katika jamii yetu kutoka pande zetu mbili za Muungano. Jukumu la msingi la Tume hiyo litakuwa ni kuongoza na kuratibu mchakato utakaowashirikisha wananchi wote bila kubagua, vyama vya siasa, wanasiasa, wafanyabiashara, asasi za kiraia, mashirika ya dini, wanataaluma na makundi mbalimbali ya watu wa nchi yetu kote nchini, katika kutoa maoni yao juu ya wayatakayo kuhusu Katiba ya nchi yao.[/FONT]