Hotuba ya rais Kikwete ya kufunga mwaka 2010

Rais ameshauri tuwaepuke wanasiasa wanaoleta chokochoko ili wakifuatiliwa na vyombo vya dola, wakimbilie katika Jumuiya ya kimataifa. Pia ametuasa tuchape kazi na tusikalie POLITIKI. Kazi kwanza, politiki baadae. Zaidi ya yote ameahidi kufungua rasmi mjadala wa katiba. Inaonesha huyu jamaa amekomaa na kuiva kisiasa. Anaijua jamii yake inataka nini na kwa muda gani. LONG LIVE JAKAYA

La muhimu ni Katiba mpya, hayo ya fujo ni kuogopa kivuli cha Dr wa ukweli, Slaa!
 
Haa hhaaa hhhaaaaa !!! Usiniumize mbavu bure. Unachokitafuta kwa THREAD hii siku nyingi ishasomeka.

Kheri ya Mwaka Mpya lakini!!!!
 
Mbona hakuzungumzia malipo ya Dowans ambayo yanapingwa vikali na Watanzania walio wengi ndani na nje ya nchi?
 
ajagusia swala la dowans ambalo limegusa akili za watanzania sana na walihitaji kujua nini hatma yake lakini kakwepa hilo, hizo ni pesa amejiandalia anataka kwenda kuzitumia akishatoka madarakani na hao wenzake akina lowasa na rostan aziz
 
Kikwete: Ataunda tume itayoongozwa na Mwanasheria aliyebobea kuratibu maoni juu ya kuandikwa kwa katiba mpya. Wanajamvi naomba mnijuze Wanasheria wetu hapa waliobobea ktk KATIBA

Kivumah .... mimi concern yangu ni.... the type of Constitution review commission... would it be presidential or independent constitution review commision...?
 
Hekima na busara. ndio msingi mkuu. Ni kweli kakomaa kisiasa. Ameweka rekodi isiyosahauliwa milele.
 
Jambo lolote linalosimamiwa na Jk siliamini kabisa. mwaka 2005 aliaahidi maisha bora kwa kila Mtanzania leo kuna nini? Wakati anapokea mitambo Richmond uwanja wa ndege aliahidi kwamba mgawo wa Umeme Tz utakuwa historia lakini hadi leo ahadi yake haijatimia. Badala yake Richmond ikawa kampuni hewa na leo Dowans inatudai bil.185. Leo hata kuzungumzia Dowans hajazungumzia. tuendelee kusubiri usanii wa Jk hadi hapo atakapotuacha 2015
 
Kwa hili CDM na wanaharakati wengine wapewe hongera kwani CDM wasinge ishitua serikali katiba Tz ingekuwa ndoto.Hongera wabunge wa CDM.
 
Rais ameshauri tuwaepuke wanasiasa wanaoleta chokochoko ili wakifuatiliwa na vyombo vya dola, wakimbilie katika Jumuiya ya kimataifa. Pia ametuasa tuchape kazi na tusikalie POLITIKI. Kazi kwanza, politiki baadae. Zaidi ya yote ameahidi kufungua rasmi mjadala wa katiba. Inaonesha huyu jamaa amekomaa na kuiva kisiasa. Anaijua jamii yake inataka nini na kwa muda gani. LONG LIVE JAKAYA

Bila kuyakubali hayo (japo kwa unafiki) safari za nje atazisikia CNN
 
Unaonaje kama tungeenda kwa mrengo wa kuongelea issues kuliko mtu/watu.

Wewe mshamba kweli ,huwezi kuongelea issue bila watu.Issues haziwezi kuwepo bila kuwa na mtu.Sioni kosa la kusema Makamba aliahidi kuwa Rais Kikwete atatoa tamko ambalo litakuwa tamko la chama.Sasa Ukisema Waziri wa Sheria na Katiba ,huyo ni mtu na si mashine.

Kwa nini watu wasimuongelee Werema wakati amezungumza mara mbili kuhusu msimamo wake juu ya katiba? Huwezi kuandika kuwa fulani alisema au hilo lilisemwa na fulani jina linahifadhiwa.Ha haha aha ahaha acha woga ndugu.
 
Niliishawahi kusema kwenye posting zangu za nyuma kwamba Tanzania tuna uncoordinate government ambako mawaziri wanatamka mambo ambayo ndani ya siku chache linatolewa tamko lingine kutoka kwa aliye juu ya waziri n.k. Kama Kikwete anasema Katiba mpya haikwepeki, ni wapi Kombani na Werema walipata ubavu au maelekezo kusema vinginevyo?

Kuna tatizo ambalo labda serikali yenyewe hailioni!

Tiba


walipata maelekezo "KANISANI ILI WAMGOMBANISHE JK NA WANANCHI. NDIO MAANA KAWASHTUKIA SANA HAWA JAMAA'".
 
Kama politiki si safi tutafanyaje kazi!! kama politiki si safi Lazima tuandamane kudai politiki safi ndipo tufanye kazi kwa utulivu. Kumbuku, ardhi siasa safi na uongozi bora vikiwepo ndipo maendeleo ya kweli yatapatikana, la sivyo kutakuwa na maendeleo ya wachache tu na wengine will go to hell ya umaskini.
 
Wanajamvi wale wenye weledi kuhusu mambo ya katiba naomba mtujuze step zinazotakiwa kufuatwa hadi tupate katiba mpya

Tafadhali tusaidieni haraka hatutaki kuuziwa mbuzi kwenye gunia. Nasema tena isijekuwa tunapigwa kanyabwoya!!!!
 
Huyu naye ni kama Bagbo tu kasoro style ndo tofauti. Yule alitumia Jaji huyu katumia Tume! Kama huna nguvu na mwenye nguvu kakukanyaga utakaa kimya eti unaogopa? Bora upige kelele kulia maumivu jumuiya ya watu watamkemea aache uonevu wake, na ikibidi wenye nguvu wenzake ndo watakuja kumshushia kipondo kama anacho subiri Bagbo!
 
Shida ya watu kama Werema, Kombani na Malima ni watu wa kujipendekeza, inaelekea nafasi zao wamepewa kwa favour na sio merit ndio maana wanakurupuka kutoa misimamo ya hovyo bila ya kuangalia hali halisi ya issues. Kwa mtu kama Kombani alitoa msimamo kwamba serikali haina fedha za mchakato wa katiba mpya kabla ya Pinda kutoa maoni yake. Huyu anaweza kueleweka kidogo, lakini sio Werema ambaye alitoa maoni yake baada ya PM.

Kwa JK kuona haja ya katiba mpya na kuunda tume bado haitoshi, kinachotakiwa ni nia ya kweli ya kuleta katiba mpya. Hii inaweza kuwa ni mbinu ya kisiasa kuwatuliza wananchi, kwasababu kuna tume kama za Jaji Nyalali na Jaji Kisanga nazo zilitoa mapendekezo baada ya kumaliza kazi zake lakini mpaka sasa report zake ziko kwenye makabati tu. Madai ya katiba mpya inabidi yaendelee bila kukoma kwa kutumia, maandamano, makongamano, semina, mikutano ya hadhara etc
 
rekodi ipi aliyoweka??? tunasubiri utekelezaji wa huo mchakato wa katiba mpya na hatimaye tupate katiba mpya hapo hata mimi ntakubali kwamba kaweka rekodi isiyosahaulika. ACTIONS SPEAKS MORE THAN WORDS MR JAKAYA.T o be honest kama jakaya atafanikiwa kufanikisha mchakato wa katiba mpya atafunika mabaya yote yanayosemwa dhidi yake hivi sasa.
 
Jambo la msingi hapo ni Katiba, hayo masuala ya uchumi ni vizuri angetoa takwimu kuliko kutuambia export imeongezeka etc. Hawezi kuongoza nchi ya TZ kwani si mbunifu.
 
walipata maelekezo "KANISANI ILI WAMGOMBANISHE JK NA WANANCHI. NDIO MAANA KAWASHTUKIA SANA HAWA JAMAA'".

Agh! Nimewachoka waislamu koko wa jf. Wako tu kuvuruga na kuchochea chuki dhidi ya wakristo nadhani wametumwa kabisa!!! SHINDWA NA ULEGEE KWA JINA LA YESU
 
Wa-Tanzania ni wachapa kazi sana tena sana tu.

Upigaji wao POLITIKI, bila kuzuilika, huanzia tu pale ambapo MATUNDA YA KAZI YAO NA RASILMALI ZAO ZINAPOYOYOMEA kwa akina RA na ED bila ya vyombo husika kuwakabili.
 
Back
Top Bottom