Hotuba ya rais Kikwete ya kufunga mwaka 2010

Hotuba ya rais Kikwete ya kufunga mwaka 2010

Hotuba hii haina chochote cha kunifanya nichangie lolote!
 
Kwa mujibu wa hotuba yake ya leo, ataunda Tume ya Maalumu ambayo itaundwa na Wanasheria 'makini' kwa ajili ya kukusanya maoni ya Wananchi juu ya Katiba hiyo. Hata hivyo, hakusema Tume itaundwa lini na kazi ya kukusanya maoni itaanza lini na kuisha lini na Katiba itakuwa tayari lini!
 
Hapo ndiyo mwanzo wa kuingizwa mkenge. Hilo suala lipo kwenye ilani ya CCM? Bila shaka wamegundua kuwa wasiogolee dhidi ya mkondo wa maji, lakini mbele ya safari utasikia suala hilo litaendeshwa kiCCM na mwisho wa yote mtaona usanii wa JK.

Suala la madini aliliunda lakini mpaka leo hatujaona matokeo yake zaidi ya sheria mpya ya madini ya mwaka 2010 ambayo ni kiigizo tu. Bado nchi haijaanza kufaidika na madini.

Tusubiri tu, mwaka 2011 Juni tume itaundwa na kupewa kazi kwa muda wa miaka miwili(hadi 2013 Juni). Juni 2013 hadi Juni 2014 itakuwa muda wa kujadili na baada ya hapo wananchi wataipigia kura na hizo kura zitachakachuliwa.
 
Hongera sana Rais wa Tanzania ndugu Jakaya Kikwete,tunashukuru kwa ushauri,hatutageuzwa mbuzi wa kafara kwa maslahi ya kisiasa ya wanasiasa wabinafsi.tunashukuru kwamba unapenda tufurahi,tusikilize kwenye hili la katiba hatutageuzwa mbuzi wa kafara.Hongera sana kwa kuongoza UN Commission mambo ya watoto na wanawake,utuwakilishe vyema,natumai haitakupunguzia uwezo wa kushughulikia matatizo yetu na kukukosa sana.tunakupenda!:redfaces:
 
Huyu jamaa ni kilaza kabisa! Anatia aibu sana! Zote pumba tupu. Nimehamaki apa ile mbaya, hajui hata motion za watu. We MS ndo umeandika speech mbovu kama hii-toa taka hizi?

Wewe una matatizo maana sidhani kama hii speech ni mbovu.
 
Hivi huyu ni raisi au bomu maana hajui kukubali kupanda kwa gharama za umeme ni kuongeza hali ngumu kwa mwananchi nawashangaa hata hao wanaofurahia hii hotuba au mnadhani mtapewa ukuu wa mikoa tuwe Positive tuache UNAFIKIIIIIIII!!!!!

Rais wetu syo makini hta kdgo! Just imagine ktk speech hiyohiyo anasema gharama za shughuli/bidhaa mbalimbali zmepanda as justification ya kupanda kwa bei ya umeme, then anasema inflation imeshuka more than halfly! Mi apa sjaelewa wadau, plz nijuzeni?
 
Pembejeo za Kilimo


Ndugu Wananchi;
Mwaka huu tumeongeza mbolea ya ruzuku na wakulima wengi zaidi watapata mbolea hiyo. Tutaendelea kufanya hivyo katika miaka ijayo kwa lengo la kuwafikia wakulima milioni 3.5 mpaka 4 miaka mitano ijayo. Aidha, tutaendelea kufuatilia na kuyatafutia ufumbuzi matatizo ya upatikanaji na hasa usambazaji wa pembejeo kwa wakulima na wafugaji. Nasikitishwa sana na taarifa za vitendo vya wizi na udanganyifu vinavyofanywa na baadhi ya mawakala wa mbolea, mbegu na dawa za kilimo na mifugo wakishirikiana na baadhi ya watumishi wa umma wa ngazi mbalimbali.

Nimewataka Mawaziri husika na hasa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya na vyombo vya dola yaani Polisi na TAKUKURU kufuatilia mwenendo mzima wa usambazaji na upatikanaji wa mbolea, mbegu na dawa za ruzuku kwa wakulima na wafugaji. Wawatafute na kuwabaini wale wote wanaofanya vitendo viovu kinyume na taratibu zilizowekwa na kuwachukulia hatua za kisheria na kinidhamu. Watu hawa ni wahujumu wa uchumi, ni adui wa wakulima, wafugaji na taifa zima kwa jumla. Hawastahili na wala wasionewe huruma hata chembe.

Unafiki mtupu huu JK!!!! Unachuja mbu na kumeza ngamia!!!! (Mt. 23:24)
 
Piga ua garagaza, Maandamano ya Arusha yako pale pale!, ata mkware ajitete vipi tarehe 5 January ni tokomile tuuuu
 
WAPENDWA NAOMBENI SANA MSII-QUOTE HIYO HOTUBA NZIMA, unaonaje ukaja na hoja tu kuliko kuirudia tena hotuba nzima? Happy New year!
 
Wanajamvi wale wenye weledi kuhusu mambo ya katiba naomba mtujuze step zinazotakiwa kufuatwa hadi tupate katiba mpya
 
Wewe una matatizo maana sidhani kama hii speech ni mbovu.

ubovu wa speech upo haswa kwenye eneo la mfumuko wa bei na kukubali kupanda kwa gharama za umeme. Pale hakuna umakini kabisa. Mambo mengine tusubiri utekelezaji wake tuone.
 
Sasa Jaji Werema wakati anatoa maoni yake kuhusu katiba alikuwa ame base wapi? au alikuwa hajui ofisi yake imemshauri nini Rais? au Ikulu imeamua nini kuhusu ushauri alioutoa? Sielewi vizuri haya mambo yanavyokwenda

  1. Celina Kombani -- Serikali haina pesa wala bajeti ya kuandaa katiba mpya
  2. PM Pinda: Serikali inalipokea swala la katiba mpya, italifanyia kazi kwa kumshauri Rais
    [*]AG Werema: Katiba mpya hapana, tuweke viraka kwenye hii iliyopo kama ni lazima
  3. President: Anakubali katiba mpya ni muhimu, na ataunda tume kushughulikia hilo
Haya yote ni ndani ya siku 60 baada ya uchaguzi.


  • Celina alikuwa anajikomba kwa bosi wake, bosi wake kamtosa kifikra. Ningeshangaa iwapo pesa za kuwalipa DOWANS zipo za kumwaga halafu za kutinga Katiba zikosekane! Kwani rasimu zero ya CUF walitumia kiasi gani mpaka Taifa lishindwe kughalimia yake.

  • Pinda alikuwa hana uhakika JK atakubali, bahati nzuri JK ni msikivu ingekuwa Mkapa watanzania tungeambulia matusi na kubezwa.
  • Werema yeye akaweke viraka kwenye suti yake kama anaona viraka vinapendeza. Wote waliokuwa wanashabikia viraka JK kawa acha kwenye mataa
  • JK kuahidi amekwisha ahidi mengi, hatuwezi kumuamini moja kwa moja maana labda kama ameacha usanii awamu hii. Na sisi hatuachi kupiga kelele mpaka tuone imeandikwa siyo mipango na tume butu.
 
JK why did you betray Malaria Sugu....... he is your senior adviser ...... au umegundua katoroka Guantanamo Bay
 
JK ana sehemu yake na taratibu zake, vyombo vya dola, taasisi zoote zina taratibu zake, Bunge ambapo ndipo kwenye uwakilishi wetu kuna taratibu zake, na bado serikali kupitia mwanasheria mkuu wana taratibu zao. Hawa wote ni mihimili ya mchakato mzima wa uundwaji wa katiba.

La Mnyika litaendelea bungeni na la rais litaendelea au yatakutana mahali. Ila ikumbukwe la msingi sote na hao wengine angalau tunatambua na kukubaliana juu ya umuhimu wa katiba mpya. Mikakati itaainishwa, itachanganuliwa, itaratibiwa na kufikia kinachohitajika. Mungu ibariki Tanzania HASA WATU WAKE

NAOMBA NISAHIHISHE KICHWA CHA HABARI ILI ANGALAU KINGESOMEKA "Kiwete aonyesha msimamo, akubali katiba mpya" Hakuwahi kutoa kauli ya kukinzana au kupigana kuhusu katiba hadi asalimu amri. Tuwe fair

mkuu ...you sound balanced to perfection ... thanks for being fair
 
Rais wetu syo makini hta kdgo! Just imagine ktk speech hiyohiyo anasema gharama za shughuli/bidhaa mbalimbali zmepanda as justification ya kupanda kwa bei ya umeme, then anasema inflation imeshuka more than halfly! Mi apa sjaelewa wadau, plz nijuzeni?

Kwani uliambiwa kaacha lini usanii, itakuwaje bei za vitu vipande halafu inflation ishuke? Kwani maana ya mfumuko wa bei ni nini na kupanda kwa bei ni nini? Kama Rais tunaye!
 
Rais ameshauri tuwaepuke wanasiasa wanaoleta chokochoko ili wakifuatiliwa na vyombo vya dola, wakimbilie katika Jumuiya ya kimataifa. Pia ametuasa tuchape kazi na tusikalie POLITIKI. Kazi kwanza, politiki baadae. Zaidi ya yote ameahidi kufungua rasmi mjadala wa katiba. Inaonesha huyu jamaa amekomaa na kuiva kisiasa. Anaijua jamii yake inataka nini na kwa muda gani. LONG LIVE JAKAYA
 
Asante H.C Dr Kikwete kwa ahadi uliyoitoa.
Kwa vile watanzania ndio tunaihitaji Katiba Mpya hatutalala na kubweteka kwa ahadi hadi kieleweke cha msingi 2015 katiba iwe imeshapatikana.

Huko nyuma tulisema JK hana cha kupoteza kwa kuandika katiba mpya, anachotakiwa kufanya ni kuhakikisha anaongoka kwa matendo na si maneno ili msumeno wa katiba mpya usimlambe pindi atokapo ikulu.
JK anaweza kuua ndege wawili kwa jiwe,
(1) kwa katiba mpya watanzania hawatamsahau
(2) can stand a chance to scoop the Mo Ibrahim US $5m prize.

Hata asipopeleka meli mpya Bukoba na Mbamba Bay - akitimiza ahadi ya leo tu tutamsamehe kwa kutotimiza hizo ahadi zingine.
 
Sometimes huwa nawaza labda mkwere anamapenzi mema na nchi wa wananchi wenzie, ladba kinachomuangusha na uswahiba na udanyanyifu wa watendaji wake.
 
Back
Top Bottom