Miaka Mitatu ya Samia Arusha: TANESCO Pekee ndio waliompunguzia 'point'

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
304
518
Wananchi katika Mkoa Wa Arusha wameeleza kuridhishwa na kazi inayoendelea kufanya na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Nchini hususani katika kuwaleta wananchi pamoja na utekelezaji Mbalimbali Wa Miradi ya maendeleo na kutoa ahueni ya wafanyabiashara kufanya Biashara zao Kwa uhuru. Wameyasema hayo katika Mdahalo Wa Hadhara ulioandaliwa na baadhi ya wandishi Wa Habari Wa Mkoa Wa Arusha wakiongozwa na Mwandishi Korumba Lebababazi.

Katika Mdahalo huo wananchi hao pamoja na kupongeza Rais Samia wameonyesha kutokuridhishwa na utendaji Wa Shirika la Umeme Tanesco hasa kutokana na kukatika katika Kwa umeme muda mwingi Hali inayopeleka kushindwa kushiriki kikamilifu katika uzakishaji Wa umeme

Afisa Mahusiano Kwa umma Mkoa Wa Arusha akijibu changa moto hiyo aliwaeleza wananchi hao kuwa changamoto hiyo ipo ukingoni kuisha kutokana na vyanzo vipya vya umeme Shirika Hilo inavyokaribia kuvukamilisha na kuanza kuzalisha umeme akitolea mfano bwawa na Mwalimu nyerere.

Mdahalo huo Wa wawazi uliwaleta pamoja wataalamu na maafisa Wa serikali pamoja na wananchi kutathimini Mafanikio ya miaka Mitatu ya Serikali ya awamu ya sita chini Ya Rais Dkt Samia Suluhu Hasan na ulifanyikia katika viwanja vya satandi ya Mkoa Wa Arusha na kuhudhuriwa na Mamia ya wakazi Wa Mkoa Wa Arusha.

Hivi Arusha kuna dolla za kutosha? Dolla ni Tsh ngapi?
Hivi Arusha sukari Tsh ngapi?
Hivi Arusha mafuta na nauli ziko chini?
 
Watu wanataka kuona mabadiliko ya vipato vyao na sio miradi, watu hawali miradi ni bahati mbaya sana CCM wako busy na miradi na huku wanachi wakiendelea kuwa masikini wa kutupwa. Unajua ni kwa nini wa Ethiopia wanakimbia nchi pamoja na nchi yao kuwa na miradi mikubwa mikubwa?
 
Subiri uone
Wananchi katika Mkoa Wa Arusha wameeleza kuridhishwa na kazi inayoendelea kufanya na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Nchini hususani katika kuwaleta wananchi pamoja na utekelezaji Mbalimbali Wa Miradi ya maendeleo na kutoa ahueni ya wafanyabiashara kufanya Biashara zao Kwa uhuru
Wame yasema hayo katika Mdahalo Wa Hadhara ulioandaliwa na baadhi ya wandishi Wa Habari Wa Mkoa Wa Arusha wakiongozwa na Mwandishi Korumba Lebababazi.

Katika Mdahalo huo wananchi hao pamoja na kupongeza Rais Samia wameonyesha kutokuridhishwa na utendaji Wa Shirika la Umeme Tanesco hasa kutokana na kukatika katika Kwa umeme muda mwingi Hali inayopeleka kushindwa kushiriki kikamilifu katika uzakishaji Wa umeme

Afisa Mahusiano Kwa umma Mkoa Wa Arusha akijibu changa moto hiyo aliwaeleza wananchi hao kuwa changamoto hiyo ipo ukingoni kuisha kutokana na vyanzo vipya vya umeme Shirika Hilo inavyokaribia kuvukamilisha na kuanza kuzalisha umeme akitolea mfano bwawa na Mwalimu nyerere.

Mdahalo huo Wa wawazi uliwaleta pamoja wataalamu na maafisa Wa serikali pamoja na wananchi kutathimini Mafanikio ya miaka Mitatu ya Serikali ya awamu ya sita chini Ya Rais Dkt Samia Suluhu Hasan na ulifanyikia katika viwanja vya satandi ya Mkoa Wa Arusha na kuhudhuriwa na Mamia ya wakazi Wa Mkoa Wa Arusha..
View attachment 2942947
subiria mapovu toka kwa Lema
 
WaTanzania wengi ni sehemu ya vichekesho, wakiona wamejengewa soko bila huduma ya maji wala hakuna huduma ya kuondoa taka...wao wanakenua tu meno kwa vigelegele na shangwe kama Nzi.
Mtoa mada jitafakari sana uache upotoshaji.
 
Kiufupi wewe na wanakikao wenzio ni wajinga wa kutupa,kwaharaka nilishahama Arusha lkn nikujuze MATATIZO ya Arusha niloyaacha malofa ninyi;
1.) Ajira hakuna,viwanda vimekufa vijana wasomi hawana kazi
2.) Mashamba ya maua yamekufa, tumeachiwa mapori yahovyo
3.) Watoto hawali shule masomo na njaa nitabu tupu
4.) Stand ya Arusha yahovyo na masoko machafu yasiyo na mpangilio.
5.) Jiji la utalii halina recreational center ni jambo duni lahovyo
6.) Taasisi za serikali zimefeli kuanzia NHIF,NIDA,TAKUKURU,TANAPA(Wanafuja mali),PSSSF nk.
7.) Madini hayaiinui Arusha,Jiji linanyonywa.
8.) Kilimo,ufugaji na masoko ya mazao hayo ni hovyo nikusema tuu hakuna
9.) Barabara kuu zimebomoka vibaya hata ile ya Dar-ARS nimashimo na ile double road imeishia tengeru kwanini?
Mambo nimengi sema labda mlikutana mazuz...
 
Watu wanataka kuona mabadiliko ya vipato vyao na sio miradi, watu hawali miradi ni bahati mbaya sana CCM wako busy na miradi na huku wanachi wakiendelea kuwa masikini wa kutupwa. Unajua ni kwa nini wa Ethiopia wanakimbia nchi pamoja na nchi yao kuwa na miradi mikubwa mikubwa?
Umesema kweli mwamba!
 
Back
Top Bottom