Mvaa Tai
JF-Expert Member
- Aug 11, 2009
- 6,159
- 4,443
Nikiwa ndani ya daladala asubuhi hii, karibu nusu ya abiria walikuwa wanajadiri kitendo cha Serikali kuingilia kati matibabu ya Babu Loliondo wengine walikuwa wakipinga na wengine wakiunga mkono, wakiwa wanaendelea kubishana, ghafla nikasikia redioni mtu anahutubia Taifa sauti kama JK hivi.
"Serikali yenu mliyo ichagua itahakikisha haiingilii imani za watu maana serikali yenu haina dini, ila kutokana na ukweli kwamba serikali inawajibika kumlinda mwananchi na mambo yanayoweza kumuathiri kwa namna yeyote ile, Serikali yenu inaangalia uwezekano wa
Ghafla nikasikia kelele za "Coins" nikashtuka usingizini na kumuona konda anataka nimlipe nauli yake kumbe nilikuwa NDOTONI!!!!!!!!.

- Kusitisha kwa mda matibabu ya Babu Loliondo mpaka ijiridhishe na ubora wake.
- Kusitisha kwa mda ubatizaji makanisani kwa kutumia maji mpaka ijiridhishe kama maji yanayotumika kubatizia ni maji safi na salama kwa matumizi ya binaadam.
- Kuzuia kwa mda matumizi ya ubani wakati wa kuendesha Sala na ibada mbalimbali mpaka ijirishishe kwamba ule moshi hauathiri afya za binaadamu.
- Kusitisha matumizi ya Biblia na Quran kwa mda tunataka kuunda kamati maalum itakayochunguza kisayansi kama yaliyomo ni ya kweli au la. Hii tunaifanya kwa makusudi ya kumlinda mlaji wa hivi vitabu."
Ghafla nikasikia kelele za "Coins" nikashtuka usingizini na kumuona konda anataka nimlipe nauli yake kumbe nilikuwa NDOTONI!!!!!!!!.