Bajeti ya Tanzania matumizi ya kawaida makubwa kuliko matumizi ya maendeleo

Tafakari_nami

JF-Expert Member
Nov 4, 2016
779
1,514
UCHUMI: Serikali ya Tanzania imesema inatarajia kukusanya na kutumia Tsh. Trilioni 49.34 katika Mwaka 2024/25 ambapo kati ya Fedha hizo, Tsh. Trilioni 6.61 zitakopwa kutoka Soko la Ndani na Tsh. Trilioni 2.98 zitakopwa kutoka katika Soko la Nje

Wizara ya Fedha imeeleza kuwa katika mipango ya Matumizi, Tsh. Trilioni 33.55 zitatumika kwa Matumizi ya Kawaida na Tsh. Trilioni 15.79 zitatumika kwenye Miradi ya Maendeleo ikiwemo Kilimo, Elimu, Barabara, Maji, Umeme, Afya na ukamilishaji wa Bwawa la Nyerere (JNHPP)

Swali langu mbona 💰 fedha zinazo kwenda kwenye matumizi ya Kawaida ni nyingi kuliko 💰 fedha zinazo kwenda kwenye maendeleo.

Alafu matumizi ya kawaida ni matumizi ya aina gani wakuu, heri matumizi ya maendeleo wame fafanua ila matumizi ya kawaida hapa nipo njiapanda.

超级截屏_20240314_191248.png
 
Mishahara inachukua % kubwa ya matumizi yetu, katika kodi inayokusanywa na TRA, Jua kabisa 50% inaenda lipa mishahara
 
Mishahara inachukua % kubwa ya matumizi yetu, katika kodi inayokusanywa na TRA, Jua kabisa 50% inaenda lipa mishahara
Kuna wadau ambao hawaishi Kwa mishahara,wanaishi na kufanya maendeleo yao binafsi Kwa pesa za posho za ofisi.Tujiangalie.
 
TISSCCM
JWTZCCM
Mishahara na maposho ya waheshimiwa
Vitafunio ikulu

humo ndimo hela yetu inamoliwa.
 
MAtumizi ya kawaida kama kuona STK inampeleka mtoto shule,STM kwenda kumchukua mtoto anapofunga shule au interview,Serikali kusema ipo Dodoma na wafanyakazi wanaishi Dae es salaam.kutwa kukimbilia Dom.
 
Back
Top Bottom