Hotuba ya kutisha!!!!!!!!

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,159
4,442
Nikiwa ndani ya daladala asubuhi hii, karibu nusu ya abiria walikuwa wanajadiri kitendo cha Serikali kuingilia kati matibabu ya Babu Loliondo wengine walikuwa wakipinga na wengine wakiunga mkono, wakiwa wanaendelea kubishana, ghafla nikasikia redioni mtu anahutubia Taifa sauti kama JK hivi.

"Serikali yenu mliyo ichagua itahakikisha haiingilii imani za watu maana serikali yenu haina dini, ila kutokana na ukweli kwamba serikali inawajibika kumlinda mwananchi na mambo yanayoweza kumuathiri kwa namna yeyote ile, Serikali yenu inaangalia uwezekano wa

  1. Kusitisha kwa mda matibabu ya Babu Loliondo mpaka ijiridhishe na ubora wake.
  2. Kusitisha kwa mda ubatizaji makanisani kwa kutumia maji mpaka ijiridhishe kama maji yanayotumika kubatizia ni maji safi na salama kwa matumizi ya binaadam.
  3. Kuzuia kwa mda matumizi ya ubani wakati wa kuendesha Sala na ibada mbalimbali mpaka ijirishishe kwamba ule moshi hauathiri afya za binaadamu.
  4. Kusitisha matumizi ya Biblia na Quran kwa mda tunataka kuunda kamati maalum itakayochunguza kisayansi kama yaliyomo ni ya kweli au la. Hii tunaifanya kwa makusudi ya kumlinda mlaji wa hivi vitabu."

Ghafla nikasikia kelele za "Coins" nikashtuka usingizini na kumuona konda anataka nimlipe nauli yake kumbe nilikuwa NDOTONI!!!!!!!!.

Nikiwa ndani ya daladala asubuhi hii, karibu nusu ya abiria walikuwa wanajadiri kitendo cha Serikali kuingilia kati matibabu ya Babu Loliondo wengine walikuwa wakipinga na wengine wakiunga mkono, wakiwa wanaendelea kubishana, ghafla nikasikia redioni mtu anahutubia Taifa sauti kama JK hivi.

Serikali yenu mliyo ichagua itahakikisha haiingilii imani za watu maana serikali yenu haina dini, ila kutokana na ukweli kwamba serikali inawajibika kumlinda mwananchi na mambo yanayoweza kumuathiri kwa namna yeyote ile, Serikali yenu inaangalia uwezekano wa

  1. Kusitisha kwa mda matibabu ya Babu Loliondo mpaka ijiridhishe na ubora wake.
  2. Kusitisha kwa mda ubatizaji makanisani kwa kutumia maji mpaka ijiridhishe kama maji yanayotumika kubatizia ni maji safi na salama kwa matumizi ya binaadam.
  3. Kuzuia kwa mda matumizi ya ubani wakati wa kuendesha Sala na ibada mbalimbali mpaka ijirishishe kwamba ule moshi hauathiri afya za binaadamu.
  4. Kusitisha matumizi ya Biblia na Quran kwa mda tunataka kuunda kamati maalum itakayochunguza kisayansi kama yaliyomo ni ya kweli au la. Hii tunaifanya kwa makusudi ya kumlinda mlaji wa hivi vitabu.

Ghafla nikasikia kelele za "Coins" nikashtuka na kumuona konda anataka nimlipe nauli yake kumbe nilikuwa NDOTONI!!!!!!!!.

Duu nimecheka sana, ila Ezan nitaku PM kuna kitu nataka tukijadiri if you don't mind
 
uanachekesha mkuu .
Kazi ya Wassira ni Hasira na siyo migogoro ya dini na tena anaikuza
 
ha,ha,ha,ha,ha,ha,ha,ha,ha,haaaa kumbe ulikuwa umelala ndan ya daladala ha,ha,ha,haaa
 
hahahaha!!!!!!!duh! hapo meseji shilingi...no nimekosea meseji senti.
 
ha,ha,ha,ha,ha,ha,ha,ha,ha,haaaa kumbe ulikuwa umelala ndan ya daladala ha,ha,ha,haaa

Yaa si unajua mkuu unaamka saa10 usiku kujiandaa kwenda kazini Posta, unatoka Posta saa12 jioni kurudi nyumbani Madale unafika saa4 usiku unaoga unakula mara saa6 usiku unajitupa kitandani ukipiga hesabu vizuri unajikuta umelala masaa manne tu. Kwa hiyo kulala ndani ya daladala hakukwepeki.
 
Na hayo masaa manne, moja la kufunga jicho la kwanza, moja la kufunga jicho la pili, moja la kuchagua ndoto ya kuota, nusu saa ya kushtuliwa na mbu, dakika ishirini za kulalamika kwa kuumwa na mbu, dakika kumi za kumjibu mwenzi wako kwa nini hujaomba naniii. Hapo kweli 'hakuna kulala ya Juma Nature ina mantiki'

Kuna haja ya daladala kung'oa viti na kuweka vitanda, 'it is the only confortable place for mlalahoi'

Ukizingatia ndoto hii uliiota ukiwa umesimama kutoka madale mpaka town maana viti vimejaa.
 
Huyo konda nadhani aliwahi kufanya kazi wizara ya ile inayoongozwa na wasira, ha ha ha ha ha ha ha ha nimecheka sana:lol:
 
Hii si ndoto Mkuu, ni siri iliyowazi. Tayari yote yanatokea kwa sababu Serikali yetu inatujali sana:
1. Matibabu ya Loliondo hayana usalama, yenye usalama ni ya Muhimbili unakopasuliwa kichwa badala ya mguu
2. Maji tunayotumia hayako salama, yaliyo salama ni yale tunapofungua bomba linatoka upepo na kutu
3. Matumizi ya ubani na udi, moshi wake unahatarisha maisha yetu, moshi salama ni wa diesel unaotanda anga yote, miji yote inanuka diesel... Aaaaaah, marashi gani bora zaidi!
4. Yaliyomo katika Biblia na Quran yanatia shaka, yanaweza kutuzuga na matumizi yake yakatunyima haki zetu za kibinadamu; yaliyo sahihi ni yale yaliyomo Katiba yetu ambapo hata kauli ya balozi wa nyumba kumi inakuwa sheria na matokeo ya kura yanachakachuliwa na hakuna mahakama Ulimwenguni ya kupinga matokeo. Tunataka serikali yetu ituenzi vipi tena zaidi ya hivi?
 
Kwa kweli hii thread ni bab'kubwa, sometimes ni sawa kuwa na thread kama hizi! Thanks
 
Na hayo masaa manne, moja la kufunga jicho la kwanza, moja la kufunga jicho la pili, moja la kuchagua ndoto ya kuota, nusu saa ya kushtuliwa na mbu, dakika ishirini za kulalamika kwa kuumwa na mbu, dakika kumi za kumjibu mwenzi wako kwa nini hujaomba naniii. Hapo kweli 'hakuna kulala ya Juma Nature ina mantiki'

Kuna haja ya daladala kung'oa viti na kuweka vitanda, 'it is the only confortable place for mlalahoi'

Ukizingatia ndoto hii uliiota ukiwa umesimama kutoka madale mpaka town maana viti vimejaa.

Tehe tehe
 
Hii si ndoto Mkuu, ni siri iliyowazi. Tayari yote yanatokea kwa sababu Serikali yetu inatujali sana:
1. Matibabu ya Loliondo hayana usalama, yenye usalama ni ya Muhimbili unakopasuliwa kichwa badala ya mguu
2. Maji tunayotumia hayako salama, yaliyo salama ni yale tunapofungua bomba linatoka upepo na kutu
3. Matumizi ya ubani na udi, moshi wake unahatarisha maisha yetu, moshi salama ni wa diesel unaotanda anga yote, miji yote inanuka diesel... Aaaaaah, marashi gani bora zaidi!
4. Yaliyomo katika Biblia na Quran yannatia shaka, yanaweza kutuzuga na matumizi yake yakatunyima haki zetu za kibinadamu; yaliyo sahihi ni yale yaliyomo Katiba yetu ambapo hata kauli ya balozi wa nyumba kumi inakuwa sheria na matokeo ya kura yanachakachua na hakuna mahakama Ulimwenguni ya kupinga matokeo.

Mhhhh ngoja hapa nisi-comment hapa, nisije jikuta mimi siyo raia hapa Tanzania
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom