Hoteli ya kitalii Arusha hali tete

Hivi hizi hotel ni kweli zina vyumba mpaka 300 au kuna namba zimerukwa katikati

Nakumbuka kuna semina elekezi moja iliwahi kufanyiwa pale , sijui watu wote wa ile semina walilala pale?
 
Wahenga walisemaaa " ukiona ngoma inalia saana ,jua INA karibia kupasuka" !!!
In short kuna hali ngumu ya uchumi muda utazungumza
Hiyo hoteli tangu mmliki wake afariki imekuwa shamba la bibi... Hakuna kiendacho sawa.. Tusiweke siasa kwenye hili wenyewe wameshindwa kuiendesha. Huduma mbaya!!
 
Habari umeipata kwenye Taarifa ya Habari lkn bado unafanya SIRI jina la hotel!
 
kwani hoteli yao lazima iwe na wageni kila siku , na bila shaka itakuwa ngurudoto tu
 
Ngurudoto ni uwekezaji mkubwa sana, ni hatari kusikia hawana Wageni.
na ngurudoto ilianza kuyumba toka enzi za mwisho za mkwere,nakumbuka SADC moja ilifanyika pale wageni walikuwa ni hao hao wa mkutano.
 
Ngurudoto ni uwekezaji mkubwa sana, ni hatari kusikia hawana Wageni.
Ngurudoto sehemu kubwa ilikuwa ikivuma kwa semina makongamano,warsha Na vikao vya viongozi na wafanyakazi wa serikali Na mashirika ya umma ndio walikuwa wakiijaza .Baada ya serikali kusema vitu hivyo vifanyike kumbi za serikali na mashirika ya umma na vyuo vya umma naona hotel imekuwa mhanga.Ziko hotel zilikuwa wala hazina hata marketing officer kazi yao ilikuwa kujuana Na mtu ofisi ya serikali anakuletea seminar Na wafanyakazi.Zingine zilijengwa Na mafisadi mabosi wa serikali anatoa maagizo seminar nk lazima zifanyike kwenye hotel zake au za maswahiba Wake.Hotel zinazo survive ni zile za wapambanaji ambao hawakuwa Na godfather serikalini wa kuwapa wateja wao walikuwa wakisaka wenyewe mtaaani.Hao wengi wanadunda maisha tu.Wategemea godfather serikalini wengi wako hoi
 
Wazee wambeleko wajibebe .Hawakawii kuipiga bei
 
mkuu uko sahihi kwa asilimia 1000%
 
Alafu hapo ni Hoteli moja sijajua huko kwingine, maana hata yule Meneja alikuwa anajitetea ishu tofauti kabisa akajikuta analazimika kutoa hali halisi ya pale Hotelini....nadhani alikuwa anajitetea kuhusu mishahara ya Wafanyakazi.
hiyo ya 120000
 
Mimi hata sijasema hivooo ndugu yangu..cybercrime..sasa unategemea nini??Vyumba 300...si mchezo kikose watu..then hapo wafanyakazi walipwa nini?Unajua tuache tu unafiki kuna watu wanapitia hali ngumu sana hasa maskini.


hata matajiri nao wanapitia mle mle...looh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…