Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya yatoa ufafanuzi madai ya kukosekana kwa Mashine ya Kuchomea Taka

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Akizungumza na Jamii Forums, Afisa Mawasiliano na Uhusiano wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya, Agrey Layson Mwaijande amesema:

Tuna mashine mbili, moja ya mafuta na nyingine ya umeme, kupata hitilafu ni vitu vya kawaida, faida yetu ni kuwa ikiharibika moja tunatumia nyingine.

Hivyo, inawezekana mtu akaona mashine moja haifanyi kasi na asijue kuwa kuna nyingine ya pili.

Mdau aliyesema zimeharibika hajaweka wazi kama zimeharibika zote mbili japo hajasema ni lini, nakumbuka mashine moja tu ya mafuta ilipata changamoto ya valvu yake, haikuchukua muda, hata wiki haikisha.

Kuhusu kuchoma taka, utaratibu zoezi huwa linafanyika majira ya jioni kisha zinachomwa, hatuchomi mchana.


=========
WhatsApp Image 2024-02-23 at 11.48.35_45f9887e.jpg

WhatsApp Image 2024-02-23 at 11.48.37_8a9a776d.jpg

WhatsApp Image 2024-02-23 at 11.48.36_e4cf0079.jpg

WhatsApp Image 2024-02-23 at 11.48.37_7b3d9e89.jpg


TAARIFA YA HOSPITALI YA RUFAA
Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya unapenda kuujulisha Umma, kutokana na taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii, Taarifa ambayo imetolewa kwenye ukurasa wa Instagram wa Jamii Forums yenye kichwa cha Habari kinachosema "Hospitali ya Rufaa ya Mbeya haina incinerator, hali inayohatarisha afya za watu wanaoizunguka".

Kutokana na taarifa hiyo Uongozi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mbeya unapenda kuujulisha Umma na kuwatoa hofu juu ya taarifa hiyo kuwa si kweli kwa kuwa Hospitali inazo Incinerator (mashine za kuchomea taka) mbili za kisasa.

Pia Uongozi wa Hospitali unapenda kuwakumbusha wadau mbalimbali wa Mawasiliano na Habari kufuata sheria za utoaji wa Habari kuhakikisha zinakuwa Habari za kweli na zenye kutoka kwenye vyanzo vya uhakika ili kuondoa usumbufu kwa wananchi usio wa lazima.

Hata hivyo, Uongozi haujawahi kukataa kutoa ushirikiano wa aina yoyote kwa Chombo cha Habari chochote au mwananchi yeyote pale anapohitaji kupata ukweli wa jambo lolote linalohusu Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mbeya.

Hivyo, mtu yeyote ambaye anataka kupata ukweli wa jambo lolote Uongozi tutatoa ushirikiano muda wote.
Agrey Layson Mwaijande
Afisa Mawasiliano na Uhusiano
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya

Hoja ya Mdau kuhusu Mashine hiyo soma hapa - Hospitali ya Rufaa ya Mbeya haina Incinerator
 
Back
Top Bottom