Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando: Lifti zetu hazina Changamoto kama inavyodaiwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Siku chache baada ya Mwanachama wa JamiiForums.com kudai kuwa kuna changamoto ya lifti katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando iliyopo Jijini Mwanza, hoja hiyo imejibiwa na uongozi wa Bugando.

Kusoma zaidi kuhusu Hoja ya Mdau Bonyeza hapa - Uongozi wa Hospitali ya Bugando chukueni hatua za haraka kurekebisha lifti zenu kabla hazijaleta madhara

Tamko rasmi la Bugando hili hapa:

WhatsApp Image 2024-03-22 at 18.29.15_46cbae1d.jpg

22 Machi, 2024 Mwanza.

Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando unapenda kuwatoa hofu Wananchi na kutoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kupitia kurasa za JAMII FORUMS zikiutaka Uongozi wa Hospitali ya Bugando kuchukua hatua za kurekebisha lifti zake.

Hospitali ya Bugando ina utaratibu wa kufanya marekebisho makubwa ya lifti zake kwa utaratibu uliopangwa na kuwa na wasimamizi wa lifti (Lift attendants) wanaohakikisha lifti zinafanya kazi.

Aidha, kama ilivyo utaratibu wa matumizi ya lifti Duniani kote, ndani ya lifti zetu kuna namba za simu zinazomuwezesha mtumiaji wa lifti kuweza kuwasiliana na msimamizi wa lifti pindi anapopata changamoto katika lifti hizo.

Hivi karibuni hatujapata changamoto ya lifti kutokufanya kazi, hivyo tunapenda kuwahakikishia Wananchi wote na watumiaji wa lifti kuwa lifti zinafanya kazi vizuri.

Imetolewa na;
Idara ya Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma
HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA BUGANDO

 
Kwanza niwashukuru kwa kutoa maelezo kuhusu suala hili, japokuwa ni maelezo ambayo ni mazuri lakini ni tofauti na uhalisia (wazoefu wa mambo uyaita majibu ya Serikali), niseme kwamba 'kilio kikubwa sio kufanya marekebisho tu' je, marekebisho hayo yamesaidia kwa kiwango ambacho kinawezesha watumiaji kujihisi wapo salama wanapozitumia hizo lift?

Kwenye andiko ambalo limeibua majibu hayo imeelezwa wazi kuwa marekebisho yamekuwa yakifanyika lakini bado wasiwasi umeendelea kuwepo kwa sababu ya changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikitokea nadhani hili wahusika wanalifahamu lakini wametoa majibu ya kulinda hadhi ya taasisi.

Katika suala hili wahusika wawajibike kwa kuchukua hatua wasisubiri changamoto kubwa zaidi zitokee waanze kutafuta mchawi, hili suala ni changamoto hata akipelekwa mtoto mdogo wa awali akapanda zile lifti mara mbili harafu akaambiwa hazina shida lazima atahoji.

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom