Hosea: DPP amekalia kesi 60 za vigogo...

Tumain

JF-Expert Member
Jun 28, 2009
3,154
70
MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Dk. Edward Hoseah, amemtupia lawama Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Elieza Feleshi, akisema amekalia kesi 60 za vigogo.

Dk. Hoseah aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akihojiwa na waandishi wa habari muda mfupi baada ya sherehe za maadhimisho ya Siku ya Maadili kitaifa, zilizofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.

“
Ingekuwa kila mtu anatoa maamuzi yake, ningekuwa mimi ningesema kuwa kila mtu asimamie kesi zake, kwa sasa nina kesi 60 kwa DPP, hata hivyo suala hilo kamuulizeni DPP zaidi,” alisema bila kuwataja vigogo hao.

Source: Tanzania daima
 
MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Dk. Edward Hoseah, amemtupia lawama Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Elieza Feleshi, akisema amekalia kesi 60 za vigogo.

Dk. Hoseah aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akihojiwa na waandishi wa habari muda mfupi baada ya sherehe za maadhimisho ya Siku ya Maadili kitaifa, zilizofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.
“Ingekuwa kila mtu anatoa maamuzi yake, ningekuwa mimi ningesema kuwa kila mtu asimamie kesi zake, kwa sasa nina kesi 60 kwa DPP, hata hivyo suala hilo kamuulizeni DPP zaidi,” alisema bila kuwataja vigogo hao.

source: Tanzania daima

ha ha ha, na yake ni ya 61.
 
Nadhani DPP angeharakisha hizo kesi maana inawezekana kabisa kesi namba moja ni ya Hosea mwenyewe kwa kubadilisha ripoti ya richmond, kujiuzia nyumba ya PCCB kwa bei poa na ufisadi mwingine.

Sijui kwanini DPP anamchelewesha wakati mwenyewe ameshasema hadharani kesi zinachelewa, mpelekeni kwa pilato kabla hajachukua likizo ya kustaafu.
 
Jamani, hivi Hosea katenda dhambi kuwataarifu kwamba ziko kesi 60 ambazo DPP amezikalia? Badala ya kumwandama DPP na kumuuliza kwa nini amekalia kesi hizo anaandamwa mtoa habari! We are not serious.
 
Mahakama zimefurika na capacity ni ndogo. Tunajenga mahakama kwanza subirini,......:rolleyes:
 
Nadhani DPP angeharakisha hizo kesi maana inawezekana kabisa kesi namba moja ni ya Hosea mwenyewe kwa kubadilisha ripoti ya richmond, kujiuzia nyumba ya PCCB kwa bei poa na ufisadi mwingine. Sijui kwa nini DPP anamchelewesha wakati mwenyewe ameshasema hadharani kesi zinachelewa. mpelekeni kwa pilato kabla hajachukua likizo ya kustaafu.

Serekali haina pesa kwa sasa, Uchaguzi nao umekaribia. Kwa hivyo inashughulikia "vitu mhimu zaidi"
 
Nadhani DPP angeharakisha hizo kesi maana inawezekana kabisa kesi namba moja ni ya Hosea mwenyewe kwa kubadilisha ripoti ya richmond, kujiuzia nyumba ya PCCB kwa bei poa na ufisadi mwingine. Sijui kwa nini DPP anamchelewesha wakati mwenyewe ameshasema hadharani kesi zinachelewa. mpelekeni kwa pilato kabla hajachukua likizo ya kustaafu.

Unao uhakika kuwa hiyo nyumba ya Tanesco alijiuzia??? nadhani si kweli jana nimesoma gazeti kuwa kuna matumizi makubwa ya jenereta la ofisi linalotumia KVA 59.2 nyumbani kwake wakati lile lililoko kwenye Wizara yake ni KVA 25 tu.
 
Nadhani DPP angeharakisha hizo kesi maana inawezekana kabisa kesi namba moja ni ya Hosea mwenyewe kwa kubadilisha ripoti ya richmond, kujiuzia nyumba ya PCCB kwa bei poa na ufisadi mwingine. Sijui kwa nini DPP anamchelewesha wakati mwenyewe ameshasema hadharani kesi zinachelewa. mpelekeni kwa pilato kabla hajachukua likizo ya kustaafu.

Hilo faili lake Dk Hosea ulifanya uchunguzi wake wewe mwenyewe na kulipeleka kwa DPP? Toa hoja zinazoweza kuwasaidia watu wengine pamoja na wewe mwenyewe!
 
Ama kweli kuelekea 2010 tutatoana mengi safari hiii, asie na mwana abebe jiwe!!!

Mpaka Dr. Hosea ananyoosha kidole kwa mwenzake DPP?

Jana nimeona Spika wa bunge Mh. sitta akiwa viwanja vya Ikulu akifoka kuhusu ugumu wa Muungwana kufanya maamuzi mazito juu ya maadili ya viongozi!! Naona kaamua kupiga magogoni moja kwa moja......
 
Upuuzi tu; kama hawataki mfumo huu wa kifisadi wabadili sheria. Hawabadili sheria basi wanautaka huu mfumo kwani wamejifunza kuishi ndani yake na kuchuma matunda yake haramu na kuwarithisha hata watoto wa watoto hadi kizazi cha nne cha wapendao ufisadi!
 
Nafikiri hosea ametusaidia sana...DPP amekuwa na mamlaka makubwa sana kiasi kwamba anaweza kucheza na mafisadi na asiguswe hii si nzuri kwa taifa letu
 
Katika siku ambayo ameongea point ni leo,kuwa yeye anakwamishwa na ofisi ya DPP kuwapeleka mahakamani wala rushwa mapapa, hadi apate kibari toka kwa DPP! Asionekane mbaya kwa kuwa sheria ndio inavyo mtaka kushughulikia.Yeye hakubaliani na mwanasheria mkuu wa serikali kuwa itakuwa ni kumlimbikizia madaraka mbona Kenya,Uganda wanafanya hivyo? Pia amempongeza rais Kagame kuwa yeye ni mkali ndio maana hata Rwanda kiwango cha rushwa ni kidogo,na kuwa kwa sasa anapata vitisho sana,mpaka amewekewa ulinzi!Yupo live chanel ten,kwenye kipindi cha General on monday.
Kumbe wabaya ni DPP na AG.
 
ktk cku ambayo ameongea point ni leo,kuwa yeye anakwamishwa na ofic ya dpp kuwa peleka mahakamani wala rushwa mapapa,kuwa hadi apate kibari toka kwa dpp!asionekane mbaya kwa kuwa sheria ndio inavyo mtaka kushughulikia,yeye hakubaliani na mwanasheria mkuu wa serikali kuwa itakuwa ni kumlimbikizia madaraka mbona kenya,uganda wanafanya hivyo?pia amempongeza rais kagame kuwa yeye ni mkali ndio maana hata Rwanda kiwango cha rushwa ni kidogo,na kuwa kwa sasa anapata vitisho sana,mpaka amewekewa ulinzi!Yupo live chanel ten,kwenye kipindi cha General on monday.Kumbe wabaya ni DPP na AG.

...Hapo kwenye Bold naona Kampiga Dongo Mkuu! Lakini pia tusishangae wiki hii DPP naye akijitokeza na kudai kuwa yeye mafaili ameishayashughulikia na Kuyarudisha kwa Hosea na anashangaa kwa nini Hosea hajawapeleka mahakamani wahusika! Ni Sarakasi tu! Zizuie kwanza Pongezi zako Mkuu.
 
Hii ina confirm yale tuliyoyafahamu kupitia Wikileaks!
 
Back
Top Bottom