Hosea: DPP amekalia kesi 60 za vigogo...

Kama yeye si sehemu ya uovu huo basi ajiuzulu ndo tuone anachotwambia ni kweli. Au la anyamaze na aendelee kula mshahara na posho zake mpaka pale tutakapopata serikali yenye kupinga ufisadi na wizi kwa rushwa
 
Nimeshangazwa na kauli ya Dr. Hosea kudai kuwa serikali imemshika mikono ndiyo maana hawezi kushughulikia wala rushwa!. Hii ni aibu kwa msomi mwenye doctorate kutoa kauli ya kujikosha kama hii. Hakuna asiyejua kuwa Hosea ameshindwa kuiongoza TAKUKURU na ushahidi upo tukianzia na uchunguzi wa RICHMOND ambao serikali ilimpa nguvu zote lakini akaja na majibu ya aibu ya kuulinda ufisadi kwa kudai kuwa Richmond haina tatizo! Mwakyembe aliongoza kamati maalum ya bunge kuchunguza swala hilohilo na kubaini uozo mkubwa. Hivi karibuni wengi tumesikia kashfa kubwa ya Dr. Hosea kuchota mamilioni kadhaa ya ofisi na kwenda nayo Marekani kwaajili ya graduation ya mwanae. Je, alijichunguza na kuja na majibu gani?. Pia anapolalamika TAKUKURU kutoingizwa kwenye rasimu ya katiba mpya na kudai kuwa hata CAG amepewa mamlaka na PCCB kuachwa!. Ninamshauri Hosea kuachia ngamshauri Hosea kuachia ngazlamika tu. Ameshindwa hata kujidhibiti mwenyewe kuhusu tuhuma za rushwa ambazo wengi tulizisoma humu kwenye jamvi, ataweza kudhibiti wengine?
 
Back
Top Bottom