Hosea: DPP amekalia kesi 60 za vigogo...

c aachie ngazi kama anaona anakwamishwa na DPP? aache unafiki wa nataka ctaki
 
Na Mwandishi wetu | Nipashe | 14th February 2013


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imesema kuwa jitihada zake za kushughulikia kesi za rushwa zinakwamishwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).

Kutokana na hali hiyo, Takukuru imemshauri Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Othman Chande, kuwa ni vyema kesi za rushwa zikawa na mahakama yake ili kupunguza urasimu.

Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward Hoseah aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye semina iliyoandaliwa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Kimataifa la Mamlaka za Kupambana na Rushwa, kwa ajili ya klabu za wanafunzi wa shule za sekondari za mkoa wa Dar es Salaam za kupambana na rushwa.

Alisema kesi nyingi zinachelewa kwa sababu ya mfumo uliopo ambao Takukuru kazi yao ni kuchunguza tuhuma tu na wakishamaliza kazi hiyo wanamkabidhi DPP ambaye ndiye anaweza kutoa maamuzi ya kumpeleka mtuhumiwa mahakamani au la.

"Tungekuwa na mahakama maalum za rushwa, mambo yangekuwa tofauti na ndivyo ilivyo kwenye nchi za wenzetu, ambako kunakuwa na mafunzo maalum kwa ajili ya majaji, waendesha mashtaka, na kadhalika. Mahakama hizo zinakuwa na majaji waliobobea, kwa kweli kuna haja ya kuuboresha mfumo uliopo," alisema Dk. Hoseah.

Dk. Hoseah aliongeza: "Endapo tutapewa mamlaka ya kukamata, kuchunguza na kufungua kesi kutakuwa hakuna malalamiko kama yaliyopo sasa, naamini Tume ya Katiba itasema suala la rushwa liendeshweje kwani kesi nyingi zinachelewa mahakamani."

Akijibu swali la mwandishi aliyetaka kujua ni kesi ngapi za vigogo ambao wameshafungwa mpaka sasa kwa kosa la rushwa, Dk. Hoseah alisema suala la kutoa hukumu siyo la Takukuru kwani hukumu hutolewa na mahakama.

Akizungumzia kesi za uchaguzi zilizohusishwa na rushwa Dk. Hoseah alisema kuwa mpaka sasa kuna kesi 23 zilizopo mahakamani ambazo baadhi yake zimekwisha kutolewa hukumu.

Akizumgumzia ugumu wa mfumo uliopo sasa ambao Takukuru wakishakamilisha uchunguzi wanakabidhi majalada kwa DPP, ambaye akijiridhisha ndipo anaamua kama kesi ipelekwe mahakamani ama la, alitoa mfano kwa kigogo mmoja wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wakati wa uchaguzi wa mwishoni mwa mwaka jana aliyekamatwa na Takukuru mjini Dodoma kwa tuhuma za kugawa rushwa kwa wajumbe, Dk. Hoseah alisema:

"Kesi nyingi zimeshindikana kwa kukosa ushahidi, kuna mtuhumiwa tulimkamata chooni akigawa rushwa na hata mazingira yalikuwa yanaonyesha hivyo, lakini hakukuwa na ushahidi." Tuhuma za rushwa ambazo mpaka sasa hazieleweki zimefikia wapi kwa sababu ya mfumo huo anaoulalamikia Dk. Hoseah ni pamoja za kampuni ya mfukoni ya Kagoda Agriculture Limited ambayo inahusishwa na uchotaji wa Sh. bilioni 40 kutoka Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Uchunguzi mwingine ambao hatma yake haijafahamika unahusiana na tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi zinazowahusu aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo.

Hadi sasa Takukuru na DPP wanatupiana mpira kuhusiana na hatima ya uchunguzi wa tuhuma hizo.

Tuhuma nyingine za rushwa ambazo hadi leo hazijafikishwa mahakamani kwa madai ya kutokuwapo ushahidi ni za Kampuni ya Deep Green, Tangold, Meremeta, sakata la kujimilikisha mgodi wa Kiwira na kesi nyingine za uchaguzi.

Wakati huo huo, Tanzania imeshika nafasi ya pili katika nchi za Afrika ya Mashariki katika utawala bora na vita dhidi ya rushwa.

Kwa mujibu wa Dk. Hoseah ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Kimataifa la Mamlaka za Kupambana na Rushwa, nchi iliyoshika nafasi ya kwanza ni Rwanda kwa kupata asilimia 5.

Dk. Hoseah alisema kuwa Tanzania imeshika nafasi hiyo kutokana na ripoti iliyotolewa na Shirika la Transparency International katika ripoti yake ya 1998-2012 kwa kupata asilimia 3.5, ikifuatiwa na Uganda iliyopata asilimia 2.7, Kenya 2.6 na ya mwisho ni Burundi iliyopata asilimia 1.9.

Aidha, Tanzania imeshika nafasi ya 12 katika vita ya kupambana na rushwa pamoja na utawala bora katika nchi 53 za bara la Afrika kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Taasisi ya Mohamed Ibrahim (Mo), wakati Mauritius ikishika nafasi ya kwanza, ikifuatiwa na Cape Verde ambayo imeshika nafasi ya pili. Botswana imeshika nafasi ya tatu na Afrika Kusini imeshika nafasi ya nne.

Semina hiyo imewahusisha takribani wanafunzi 500 kutoka klabu mbalimbali za kupambana na rushwa shuleni. Moja ya malengo ya taasisi hiyo ni kuanzisha klabu hizo kwenye shule za msingi katika kipindi cha bajeti ya 2013/2014.


CHANZO: NIPASHE
 
Katika hari niliyo itegemea nimesoma kwenye vyombo vya habari kuwa mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa dr E.Hosea amemuomba jaji mkuu wa Tanzania kuwa na mahakama maalum kwaajili ya rushwa tu.
Ndiyo ni atua mojawapo lakini tatizo la TAKUKURU ni juu ya mfumo wa uongozi wao na ni nani anawajibika kwa nani,taasisi sio huru kwa matiki mtendaji wake mkuuu anateuliwa badala ajira yake ingelikuwa inatangazwa na atakaefahulu kupata nafasi hiyo adhibitishwe na bunge.hilo tuliache,hivi ktk hali ya kawaida taasisi hii inashutumiwa kwa kujihusisha na rushwa wakati wao ndio wenye dhamana ya kuzui na kupambana nayo,kwa maana nyingine wanabidi kupambana wao kwao ndani ya taasisi na kibaya zaidi imejikita kwa wananchi wanaopokea rushwa ndogo ndogo(dagaa) badala ya rushwa kubwa ambazo zinzdhohofisha ukuaji wa nchi yetu kiuchumi na maendeleo kwaujumla.Ata ukipewa mahakama yako lakini kama uwezi kubadili mfumo wa utendaji wa taasisi yako utaishia kulalama.Kwangu mimi kuwa na mahakama ya rushwa sio dawa bali ni sehemu ya utetezi usio na maana.Jambo linigine ni pale taasisi husika kuingiliwa na wanasiasa wakati ni taasisi ya kijamiii inayobidi ijitegemee inawa hili alionekani moja kwa moja. kwangu mimi ungeliPigania uhuru wa taasisi na sio kuwa na mahakama ya rushwa.
 
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) imesema kuwa jitiuhada zake za kushughulikia kesi za rushwa zinakwamishwa na ofisi ya mkurugenzi wa mashitaka ( DPP).Kutoka na kauli hiyo ,Takukuru imemshauri jaji mkuu wa Tanzania Mohamedi Othman Chande,Kuwa ni vyema kesi za rushwa zikawa na mahakama yake ili kupunguza urasimu.


Source:Gazeti la nipashe la leo,14/02/2013
 
Sijasoma gazeti la nipashe la leo,hata hivyo labda ni mleta mada au hosea wametoa hitimisho tofauti na kinacholalamikiwa. Kwa ufahamu wangu kwa mujibu wa sheria ya pccb kesi zote za corruption as opposed to bribery lazima baada ya upelelezi wa pccb zipelekwe kwa dpp ili ajiridhishe na ushahidi uliokusanywa. Sasa anaposema zinakwamishwa na dpp ni wakati upi,yaani kuamua kushtaki au kuendesha mahakamani baada ya kushtaki? Kama ni kuhusu kuamua kushtaki basi hata kama mahakama zitaanzishwa hazitakuwa na maana.
 
hosea(4).jpg

Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward Hoseah

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imesema kuwa jitihada zake za kushughulikia kesi za rushwa zinakwamishwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP). Kutokana na hali hiyo, Takukuru imemshauri Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Othman Chande, kuwa ni vyema kesi za rushwa zikawa na mahakama yake ili kupunguza urasimu.

Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward Hoseah aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye semina iliyoandaliwa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Kimataifa la Mamlaka za Kupambana na Rushwa, kwa ajili ya klabu za wanafunzi wa shule za sekondari za mkoa wa Dar es Salaam za kupambana na rushwa.

Alisema kesi nyingi zinachelewa kwa sababu ya mfumo uliopo ambao Takukuru kazi yao ni kuchunguza tuhuma tu na wakishamaliza kazi hiyo wanamkabidhi DPP ambaye ndiye anaweza kutoa maamuzi ya kumpeleka mtuhumiwa mahakamani au la. “Tungekuwa na mahakama maalum za rushwa, mambo yangekuwa tofauti na ndivyo ilivyo kwenye nchi za wenzetu, ambako kunakuwa na mafunzo maalum kwa ajili ya majaji, waendesha mashtaka, na kadhalika. Mahakama hizo zinakuwa na majaji waliobobea, kwa kweli kuna haja ya kuuboresha mfumo uliopo,” alisema Dk. Hoseah.

Dk. Hoseah aliongeza: “Endapo tutapewa mamlaka ya kukamata, kuchunguza na kufungua kesi kutakuwa hakuna malalamiko kama yaliyopo sasa, naamini Tume ya Katiba itasema suala la rushwa liendeshweje kwani kesi nyingi zinachelewa mahakamani.”

Akijibu swali la mwandishi aliyetaka kujua ni kesi ngapi za vigogo ambao wameshafungwa mpaka sasa kwa kosa la rushwa, Dk. Hoseah alisema suala la kutoa hukumu siyo la Takukuru kwani hukumu hutolewa na mahakama.

Akizungumzia kesi za uchaguzi zilizohusishwa na rushwa Dk. Hoseah alisema kuwa mpaka sasa kuna kesi 23 zilizopo mahakamani ambazo baadhi yake zimekwisha kutolewa hukumu.

Akizumgumzia ugumu wa mfumo uliopo sasa ambao Takukuru wakishakamilisha uchunguzi wanakabidhi majalada kwa DPP, ambaye akijiridhisha ndipo anaamua kama kesi ipelekwe mahakamani ama la, alitoa mfano kwa kigogo mmoja wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wakati wa uchaguzi wa mwishoni mwa mwaka jana aliyekamatwa na Takukuru mjini Dodoma kwa tuhuma za kugawa rushwa kwa wajumbe, Dk. Hoseah alisema:

“Kesi nyingi zimeshindikana kwa kukosa ushahidi, kuna mtuhumiwa tulimkamata chooni akigawa rushwa na hata mazingira yalikuwa yanaonyesha hivyo, lakini hakukuwa na ushahidi.” Tuhuma za rushwa ambazo mpaka sasa hazieleweki zimefikia wapi kwa sababu ya mfumo huo anaoulalamikia Dk. Hoseah ni pamoja za kampuni ya mfukoni ya Kagoda Agriculture Limited ambayo inahusishwa na uchotaji wa Sh. bilioni 40 kutoka Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Uchunguzi mwingine ambao hatma yake haijafahamika unahusiana na tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi zinazowahusu aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo. Hadi sasa Takukuru na DPP wanatupiana mpira kuhusiana na hatima ya uchunguzi wa tuhuma hizo. Tuhuma nyingine za rushwa ambazo hadi leo hazijafikishwa mahakamani kwa madai ya kutokuwapo ushahidi ni za Kampuni ya Deep Green, Tangold, Meremeta, sakata la kujimilikisha mgodi wa Kiwira na kesi nyingine za uchaguzi.

Wakati huo huo, Tanzania imeshika nafasi ya pili katika nchi za Afrika ya Mashariki katika utawala bora na vita dhidi ya rushwa. Kwa mujibu wa Dk. Hoseah ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Kimataifa la Mamlaka za Kupambana na Rushwa, nchi iliyoshika nafasi ya kwanza ni Rwanda kwa kupata asilimia 5. Dk. Hoseah alisema kuwa Tanzania imeshika nafasi hiyo kutokana na ripoti iliyotolewa na Shirika la Transparency International katika ripoti yake ya 1998-2012 kwa kupata asilimia 3.5, ikifuatiwa na Uganda iliyopata asilimia 2.7, Kenya 2.6 na ya mwisho ni Burundi iliyopata asilimia 1.9.

Aidha, Tanzania imeshika nafasi ya 12 katika vita ya kupambana na rushwa pamoja na utawala bora katika nchi 53 za bara la Afrika kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Taasisi ya Mohamed Ibrahim (Mo), wakati Mauritius ikishika nafasi ya kwanza, ikifuatiwa na Cape Verde ambayo imeshika nafasi ya pili. Botswana imeshika nafasi ya tatu na Afrika Kusini imeshika nafasi ya nne. Semina hiyo imewahusisha takribani wanafunzi 500 kutoka klabu mbalimbali za kupambana na rushwa shuleni. Moja ya malengo ya taasisi hiyo ni kuanzisha klabu hizo kwenye shule za msingi katika kipindi cha bajeti ya 2013/2014.
 
mi hapo kwenye siku ya maadili Kitaifa ndio imeniacha hoi,kuna viongozi wana maadili hili Tanzania kweli????
 
Jamani, hivi Hosea katenda dhambi kuwataarifu kwamba ziko kesi 60 ambazo DPP amezikalia? Badala ya kumwandama DPP na kumuuliza kwa nini amekalia kesi hizo anaandamwa mtoa habari! We are not serious.

Fungua macho kuna vijana wa DPP. Na wa MA CCM wanamkejeli makusudi kwa kuwa wanajua watakao shitakiwa ni mabosi wao.
 
Hosea na DPP wote ni wateule wa rais,kama DPP amekalia kesi hizo je amemsemea kwa boss wao? kama jibu ni ndiyo boss anasemaje kuhusu hili?
Mimi nadhani hapa mwenye shida si Hosea wala Feleshi bali aliyemsafisha Jairo na kutaka kumrudisha kazini,wakati watendaji wakuu wenzake walishauambia umma kuwa ''ningekuwa na mamlaka ya kumwajibisha ningefanya hivyo''
Watanzania tumechezewa vya kutosha,rungu pekee tulilonalo mkononi mwetu ni uchaguzi wa mwaka 2015,Tukiendekeza njaa na kupenda rushwa za jezi na kofia,hapatakuwa na wa kulaumiwa.
 
Nilishaandika huko nyuma kuwa "DPP kizuizi cha vita vya Ufisadi"..
Mkuu,kama ndivyo jiulize swali hili nani alimpa nafasi hiyo? na je huyo aliyempa nafasi hiyo analiona hilo uliloliona? na kama analiona amechukua hatua gani?Kama anaona na hachukui hatua basi yeye ndiye fisadi namba moja.Ameweka watu ili walinde maslahi yake.
 
Angekuwapo MZALENDO MWAL.J.K.FATHER OF THE NATION angesema kwa kizanaki wote lao moja.AACHE KUTUDHARAU KWANI NI SIKU NYINGI ANALALAMIKA,ALISHAKARIRIWA NA WEAKLEAKS AKILALAMA LAKINI KWA ULAFI NA UBINAFSI WAKE UNAOCHANGIWA NA KUNUFAIKA NA MFUMO ULIOPO ANAOULALAMIKIA LEO,ALIKANUSHA KI-style.,SASA LEO ANALALAMA NINI?TULIONA USANII, KIBOGOYO AKIPEWA MENO AKAJA AKAONGEZEWA TENA KWA MBWEMBWE,TUKAAMBIWA SASA KIBOGOYO ATAKULA HATA NYAMA YENYE MFUPA AMBAO HAUJAIVA VIZURI.,SASA TANGU WAKATI ULE HADI LEO KAMA ANAKWAMISHWA KATIKA UTENDAJI WAKE WA KILA SIKU,ANANG'ANG'ANIA NINI HICHO KITI?ANANGOJA NINI KAMA YEYE NI MSAFI??KAMA ANAZIRUKA KAULI ZAKE,TUMUAMINI KWA LIPI KATIKA HILI ALISEMALO LEO???
 
Jamani, hivi Hosea katenda dhambi kuwataarifu kwamba ziko kesi 60 ambazo DPP amezikalia? Badala ya kumwandama DPP na kumuuliza kwa nini amekalia kesi hizo anaandamwa mtoa habari! We are not serious.
Ar U serios???bora maisha means KANYAGA TWENDE?It doesn't matter where were going,bora liende,mradi kuna maisha???WOTE LAO MOJA HAMNA WA KUMSEMA MWENZAKE,HAMNA WA KUMFUNGA PAKA KENGELE.NI USANII TU KAMA KAWA WATU WANAIMBISHWA WIMBO NAO WANAITIKIA BILA YA KUUJUA,WALA KUJUA KUSUDI NA MAANA WIMBO WENYEWE.
 
Si aliombwa mdahalo na DPP aeleze ni mafaili gan hayo na yamekaa kwa DPP kwa muda gani akaingia mitini huyu...!!? kesi ni ushahidi, mwenyewe hapo anaeleza hakukua na ushahidi sasa inakuaje alalamikie tena DPP!!?
 
Wana jamvi nimesikia Takukuru karibu wanaanza kuwafikisha vigogo wakubwa, mapapa na manyangumu mahakamani kwa pilato. Kimsingi kauli za bwana Hosea zinanitibua sana nyongo, na zinatia kichefuchefu. mkikumbuka wikileaks kipindi cha nyuma kidogo ilitoa siri ya kwamba Dr.Hosea ameshakatazwa na Mh.Rais kuwafikisha manyangumi na vigogo kwa pilato (mahakamiani) hata iwe kwa dawa ya ngw'anamalundi. sasa najiuliza huyu bwana kuleta kaulizi za kukejeri raia anamanisha nini hasa. wa tz nawaombeni muwe watu wa kutunza kumbukumbu, yaani viongozi hawa wameifanya tz kama dangulo.
 
nafikiri hajasikika mda mrefu kwenye vyombo vya habari ndo hivyo tena anatumia fursa .serikali hii imekuwa ni ya matamko tu bila hatua zozote kuchukuliwa
 
Back
Top Bottom