Waraka kwa Mkurugenzi wa mashtaka DPP

Mangi Mkubwa

Senior Member
Jan 3, 2014
107
29
WARAKA KWA MKURUGENZI WA MASHTAKA - DPP.

TAKUKURU IUNDIWE TAKUKURU-JAJI LUBUVA.

Kwa muda mrefu sasa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa - PCCB wamekuwa wakitenda mambo ya ajabu na kukomoa watanzania utadhani sio raia wa nchi hii.

Mwezi may 2021,Mkurugenzi wa mashtaka nchini Silvester Mwakitalu aliyaondoa mahakamani mashauri takribani 140, yaliyofungulia na idara hiyo, ambapo watu hao ilipendekezwa washitakiwe kwa makosa ya utakatishaji wa fedha ili tu wasipate dhamana.

Katika awamu hii ya sita,kwa kiwango kikubwa na hasa baada ya Mh. Rais Samia Suluhu kukemea wazi tabia hii, angalau mashtaka haya yamepungua. ila ukweli unabaki wazi kwamba bado kuna watu wanashikiliwa magerezani na mifano mingine ni waliokuwa wanasiasa,watumishi na wafanyabiashara ambao upelelezi wa mashauri yao wanaambiwa ama 'UPELELEZI HAUJAKAMILIKA AU USIKILIZWAJI UNASUA SUA' na hili ni kwa kuwa hawawezi kuthibitisha hayo makosa hasa wanayozuia dhamana.na sasa wanategea wahanga wachoke na kukata tamaa waamue kukubali makosa ili tu kununua uhuru wao.

Takukuru kwa mujibu wa sheria haihusiki na utambuzi,ufuatiliaji na upelelezi wa makosa kama kuunda magenge ya kihalifu na utakatishaji fedha,lakini utashanga sehemu ya mashtaka mengi wanaopeleleza hao ni makosa hayo.Mbaya zaidi wapo Active kupendekeza hayo makosa kwa DPP,hasa yanayohusu watu binafsi kuliko kuhangaika na mifumo ya wizi iliyoibuliwa na CAG au kama ile aliyoeleza Mhe. Rais aliyoielezea katika shughuli za mwenge wa uhuru kule kagera juu ya wizi wa bandarini.

hebu fikiria kama sio Rais na DPP kuamua kufuta hayo mashtaka 140 nini kingetoke?vipi kuhusu hali za magereza?familia zao? maisha yao je!

Kati ya mashtaka tunayosikia kutowahi kuthibitishwa ni haya mashtaka yanayopendekezwa na kuletwa na taasisi hii na kuchunguzwa nao,LAKINI kama alivyowahi kueleza Mhe. Rais, Mtu anaambiwa huna hatia baada ya kusota gerezani kwa muda mrefu,ametengwa na ndugu na familia.wahanga na ndugu zao wamepitia machungu na maumivu makubwa bila sababu;je hii ni kwa gharama ya nani!

Ndugu DPP kama mtu anazuia dhamana miaka miwili mwishoni anaachiwa huru huoni anakuwa amefarakanishwa na ofisi yako 'JAMUHURI' na anaishia kuilaumu serikali kwa makosa ya baadhi ya watu katika taasisi.AMA KWA KUKOMOA AU KUTOKUWA WAADILIFU.

Mabadiliko yanayoendelea polisi sasa sio yawaguse PCCB tu ila ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka inayopaswa kusimamia haki za pande zote izifundishe taasisi hizi kwa vitendo kwamba hatimaye lawama na manunguniko hayo ambayo Mhe. Rais ameyaeleza wazi yanaiendea ofisi yake na wakatae yote yanayofanywa kwa mihemko na hisia badala ya uhalisia na HAKI.

Unao sasa mifano mingi ya watu waliopelekwa mahakamani kwa mbwembwe wakadhalilishwa chini ya mitutu na baadae mahakama inasema tena kwa upole SHITAKA HALIJATHIBITISHWA huko PCCB na ofisi ya mashtaka wapo wanasheria ambao wangeweza kuwa mahakimu na majaji , je HAWAYAONI HAYA? au ndio kujitetea kuwa kesi ni pata potea!!na taaluma yenu mnaiweka wapi! lile wazo la kufanya kesi nje ya mahakama kuamua kama wanaweza kushinda kortini ambalo ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka ilimueleza Mhe.Rais lifanyike sasa kwa kesi walizopeleleza TAKUKURU, na kuwa watu wanaosota magerezani maana kutofanya hivyo ni kujifanya tunatafuta haki ya upande mmoja huku tunasigina upande mwingine.

DPP muda umefika sasa ujue uma na Mhe.Rais na hata wewe hatupendelei sana kusikia kelele hizi za upelelezi bado,au mtu ameomba rushwa na kabla hata halijakamilika anawekewa shitaka la kizamani la utakatishaji fedha ili kuteswa kimkakati akubali.Mtu apambane na mashtaka yake ya haki mahakama itaweka mzani.

Hayo ndiyo yanawaibua watu wa heshima katika mihimili ya haki kama jaji Lubuva kuona hii taasisi haiwatendei haki watu.labda ila vetting aliyoagiza Rais itasaidia hawa watu kujua hii nchi ni yakwetu sote
 
Hayo ndiyo yanawaibua watu wa heshima katika mihimili ya haki kama jaji Lubuva kuona hii taasisi haiwatendei haki watu.labda ila vetting aliyoagiza Rais itasaidia hawa watu kujua hii nchi ni yakwetu sote.
 
Back
Top Bottom