Ndugu wanajamvi hili nimekuwa kimya kwa mda kidogo baada ya uchaguzi wa Arusha niliona niwaache wanachadema mtambe mtambike mara baada ya ushindi huo mlioupata.
Nina kila sababu yakuwapongeza wananchi wa Arusha kwakufanya uchaguzi kwa amani kwani amani ndiyo tunu na kitambulisho pekee ya Taifa letu,bila kuvisahau vyombo vya usalama kwakuhakikisha zoezi linafanyika kwa amani.
Mosi kwakuzingatia dhana ya utawala bora na uongozi bora inayotakay chama chochote cha kisiasa kukubali matokeo hata kama yamekuwa kinyume na matarajio waliyokuwa wameyatarajia,ni wazi kwamba CCM ni chama pekee chenye ukomavu wa kisiasa wa hali ya juu ukilinganisha na vyama vingine vya kisiasa ambavyo hulazimisha matokeo ya chaguzi yawe kama vile wao watakavyo hata kufikia kufanya fujo na vurugu zinazohatarisha amani ya nchi yetu.
Pili napenda kutoa himizo kwa wanaccm na viongozi wote walioshiriki uchaguzi wa Arusha kuwa kuvunjika kwa mpini sio mwisho wa uhunzi,tumejaribu,tumeweza na sasa tusonge mbele katika kuwatumikia watanzania kwani ilani iliyoko madarakani ni ya CCM.
Hakuna sababu yakukata tamaa kwa matokeo haya ya Arusha kwakuzingatia kwamba hata mbuyu ulianza kama mchicha, tujikumbushe kwamba kata hizo zilikuwa zinamilikiwa na chadema tangu awali na isitoshe kura tulizopata ni nyingi kuliko zile tulipata 2010 hii ni ishara ya wazi sasa kwamba wapo watu wengi walioichagua chadema 2010 lakini sasa wamegeuka na kuichagua CCM ishara ya kwamba sasa wanakiunga mkono chama cha mapinduzi.
Jukumu tulilonalo ni kujisahihisha pale tulipokosea na kuzitumia kura hizo kama mtaji wetu katika kipindi hiki kifupi kabla yakufikia uchaguzi mkuu ujao.kwakufanya hivyo tutakuwa tumejiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kushinda.
Tatu napenda kuwapa hongera na pole chadema kwakujisahaulisha kuwa uchaguzi huu umefanyika katika mikoa mingi na sio Arusha pekeyake na matokeo ya awali CCM ilishinda kwa kishindo kwa kata 16 chadema kata 4 tu,iweje muwe wepesi wakusahau mapema hivyo?ukizingatia kwamba pamoja na ninyi kushinda kata 4 za Arusha na kuwafanya muwe na kata 8 bado CCM ni iyena iyena nambari wani.
Nadhani kuna swali la kujiuliza hapa sisi kama watanzania kwamba kuna nini kati ya chadema na Arusha?ukizingatia kuwa kuna mikoa mingine chadema ilifanya chaguzi na kushinda lakini matumizi ya helicopter yalifanyika Arusha tu. Niwakumbushe kwamba kunapotokea na chaguzi kinachoangaliwa ni matokeo ya jumla ya maeneo yote yaliyofanya uchaguzi na sio matokeo ya mkoa mmoja.
Chadema ingeonyesha kwamba ni chama makini endapo ingefurahia ushindi wa Arusha huku wakijitathimini sababu zilizopelekea CCM kupata kura nyingi kipindi hiki kuliko 2010 badala ya wao kuanza kubeza wanaccm,kubeza viongozi wa ccm walioshiriki uchaguzi huo pamoja na kubeza CCM bila kuzingatia kwamba mpaka sasa CCM wameibuka kidedea katika uchaguzi huu mdogo.
Waswahili walisema 'akipendacho chongo huita kengeza' ushindi wa chadema Arusha ni sawa na chongo ila wao wanang'ang'ania kuuita ni kengeza kutokana na CCM kushinda kata 16 chadema 8 halafu mnajiita mashujaa huku nikulazimisha chongo kuwa kengeza.
Kwani hata kipofu akiona mawingu hudhani kuwa kaona mbingu,kumbe ni mawingu tu na yatapita.
Ni vema mkatambua kuwa wa awali ni wa awali tu.
Naomba kuwasilisha,wenye hoja karibuni wanaotumia matusi kama kinga yao pia karibuni.
CCM umoja ni ushindi.
Viva CCM
Juliana Shonza, Mtu wa Shamba ametoa tathmini hii hapa: Tembelea uzi huu Chaguzi ndogo 16/6 na 14/7 majumuisho na tathmini
Unasemaje kuhusu nafasi ya CCM hapo?
Tofautisha mtu na chama au taasisi, yawezekana kabisa kuna mengi yamefanywa na mtu kipindi akiwa ccm lakini kwa sasa ni chadema, sasa utasema alofanya mtu akiwa ccm basi kilifanywa na ccm? jibu ni HAPANA.
Ndo maana tunashindwa kuwaelewa walobaki ccm kama kweli wana uwezo mzuri wa kufikiri au wamekaririshwa tu. Huwa nashindwa kumwelewa mtu anayesimama kwa mavazi ya njano na kijani akatamba kwamba wao ndo wenye nchi.
Hapo sasa mbuyu kama mchicha kwa chama chao wapi na wapi? hapo kapotokaUmeandika vizuri isipokuwa hapo kwenye ''hata mbuyu ulianza kama mchicha.'' CCM ni chama kikongwe kuliko vyama vyote hapa nchini. Hiyo nahau sidhani kama inaendana na ukongwe wake. Ni dalili ya kuanza kukata tamaa kuilinganisha CCM na mchicha ambao baadaye utakuwa hadi kuwa kama mbuyu. Mlipaswa tayari kuwa mmekuwa hadi mmefikia ukubwa wa ubuyu. Hiyo kauli ilitakiwa kutolewa na vyama vinavyoanza kukua.
Wewe ni mmoja wa watu waliokuwa arusha mkiipigia debe chadema kwa raslimali za ccm. Na kujishaua kote mkapigwa vituo vyote. Eti makapi ya cdm ndio keki za ccm. Dada wa watu nakuhakikishia, mwaka huu hautakwisha bila ya nyinyi kutolewa kwenye reli. Eti hata mbuyu ulianza kama mchicha. Ccm ilikuwa mbuyu wakati mwigulu anawasajili. Wewe na wenzako ndio mnaifanya iwe mchicha. Vipi lakini, sombetin mwigulu ataenda?
Ndugu wanajamvi hili nimekuwa kimya kwa mda kidogo baada ya uchaguzi wa Arusha niliona niwaache wanachadema mtambe mtambike mara baada ya ushindi huo mlioupata.
Nina kila sababu yakuwapongeza wananchi wa Arusha kwakufanya uchaguzi kwa amani kwani amani ndiyo tunu na kitambulisho pekee ya Taifa letu,bila kuvisahau vyombo vya usalama kwakuhakikisha zoezi linafanyika kwa amani.
Mosi kwakuzingatia dhana ya utawala bora na uongozi bora inayotakay chama chochote cha kisiasa kukubali matokeo hata kama yamekuwa kinyume na matarajio waliyokuwa wameyatarajia,ni wazi kwamba CCM ni chama pekee chenye ukomavu wa kisiasa wa hali ya juu ukilinganisha na vyama vingine vya kisiasa ambavyo hulazimisha matokeo ya chaguzi yawe kama vile wao watakavyo hata kufikia kufanya fujo na vurugu zinazohatarisha amani ya nchi yetu.
Pili napenda kutoa himizo kwa wanaccm na viongozi wote walioshiriki uchaguzi wa Arusha kuwa kuvunjika kwa mpini sio mwisho wa uhunzi,tumejaribu,tumeweza na sasa tusonge mbele katika kuwatumikia watanzania kwani ilani iliyoko madarakani ni ya CCM.
Hakuna sababu yakukata tamaa kwa matokeo haya ya Arusha kwakuzingatia kwamba hata mbuyu ulianza kama mchicha, tujikumbushe kwamba kata hizo zilikuwa zinamilikiwa na chadema tangu awali na isitoshe kura tulizopata ni nyingi kuliko zile tulipata 2010 hii ni ishara ya wazi sasa kwamba wapo watu wengi walioichagua chadema 2010 lakini sasa wamegeuka na kuichagua CCM ishara ya kwamba sasa wanakiunga mkono chama cha mapinduzi.
Jukumu tulilonalo ni kujisahihisha pale tulipokosea na kuzitumia kura hizo kama mtaji wetu katika kipindi hiki kifupi kabla yakufikia uchaguzi mkuu ujao.kwakufanya hivyo tutakuwa tumejiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kushinda.
Tatu napenda kuwapa hongera na pole chadema kwakujisahaulisha kuwa uchaguzi huu umefanyika katika mikoa mingi na sio Arusha pekeyake na matokeo ya awali CCM ilishinda kwa kishindo kwa kata 16 chadema kata 4 tu,iweje muwe wepesi wakusahau mapema hivyo?ukizingatia kwamba pamoja na ninyi kushinda kata 4 za Arusha na kuwafanya muwe na kata 8 bado CCM ni iyena iyena nambari wani.
Nadhani kuna swali la kujiuliza hapa sisi kama watanzania kwamba kuna nini kati ya chadema na Arusha?ukizingatia kuwa kuna mikoa mingine chadema ilifanya chaguzi na kushinda lakini matumizi ya helicopter yalifanyika Arusha tu. Niwakumbushe kwamba kunapotokea na chaguzi kinachoangaliwa ni matokeo ya jumla ya maeneo yote yaliyofanya uchaguzi na sio matokeo ya mkoa mmoja.
Chadema ingeonyesha kwamba ni chama makini endapo ingefurahia ushindi wa Arusha huku wakijitathimini sababu zilizopelekea CCM kupata kura nyingi kipindi hiki kuliko 2010 badala ya wao kuanza kubeza wanaccm,kubeza viongozi wa ccm walioshiriki uchaguzi huo pamoja na kubeza CCM bila kuzingatia kwamba mpaka sasa CCM wameibuka kidedea katika uchaguzi huu mdogo.
Waswahili walisema 'akipendacho chongo huita kengeza' ushindi wa chadema Arusha ni sawa na chongo ila wao wanang'ang'ania kuuita ni kengeza kutokana na CCM kushinda kata 16 chadema 8 halafu mnajiita mashujaa huku nikulazimisha chongo kuwa kengeza.
Kwani hata kipofu akiona mawingu hudhani kuwa kaona mbingu,kumbe ni mawingu tu na yatapita.
Ni vema mkatambua kuwa wa awali ni wa awali tu.
Naomba kuwasilisha,wenye hoja karibuni wanaotumia matusi kama kinga yao pia karibuni.
CCM umoja ni ushindi.
Viva CCM
Afadhali Shonza ana interest tunazozijua kutoka kwa Mwigulu mzee wa kuovertake,na kina radhia,simiyu yetu n.k,wao interest zao ni zipi ndani ya ccm,nijuzeni tafadhali.
Nashindwa kumwelewa huyu mdada, kati ya cdm na ccm kipi kilianza kama mchicha? kumbe ni kweli shoza alijifukuzisha cdm baada ya kujikuta elimu yake ni ndogo kulinganisha na wenzake, kweli huyu ni bulula kweli.
Kabla ya matokeo kutanganzwa mkatoka NDUKI -- wewe na Kamanda wa Green Guards.sijui mlikimbilia wapi maana dar mmeonekana jana.
Mbona uchaguzi ulifanyika kata 26.Umeandika kuwa CCM walishinda kata 16 na CHADEMA kata 8 vipi kata zilizobakia 2 zilichukuliwa na chama gani?.
Radhia sweety.....kumbe ukitulia unakua na sweety ideas wakati mwingine...Umeandika vizuri isipokuwa hapo kwenye ''hata mbuyu ulianza kama mchicha.'' CCM ni chama kikongwe kuliko vyama vyote hapa nchini. Hiyo nahau sidhani kama inaendana na ukongwe wake. Ni dalili ya kuanza kukata tamaa kuilinganisha CCM na mchicha ambao baadaye utakuwa hadi kuwa kama mbuyu. Mlipaswa tayari kuwa mmekuwa hadi mmefikia ukubwa wa ubuyu. Hiyo kauli ilitakiwa kutolewa na vyama vinavyoanza kukua.