Hongera CCM

Hongera CCM

Mods napendekeza huu uzi ulioletwa na Juliana Shonza ufutwe kwa kuwa umetolewa au kwa kutokuelewa vizuri idadi ya kata ambazo Chadema walishinda kwenye uchaguzi wa kata 26 uliofanyika hivi karibuni na/au umepotoshwa kwa makusudi kwani maelezo yake hayana usahihi...Chadema walishinda kata kumi na sio nane kama alivyoeleza.

Pia napendekeza Juliana Shonza ambaye ni mleta mada apigwe ban kwa kufuata sheria za JF kwa kupotosha jamii kwa taarifa za uongo!!!

Cc Invisible Moderator
 
Ndugu wanajamvi hili nimekuwa kimya kwa mda kidogo baada ya uchaguzi wa Arusha niliona niwaache wanachadema mtambe mtambike mara baada ya ushindi huo mlioupata.

Nina kila sababu yakuwapongeza wananchi wa Arusha kwakufanya uchaguzi kwa amani kwani amani ndiyo tunu na kitambulisho pekee ya Taifa letu,bila kuvisahau vyombo vya usalama kwakuhakikisha zoezi linafanyika kwa amani.

Mosi kwakuzingatia dhana ya utawala bora na uongozi bora inayotakay chama chochote cha kisiasa kukubali matokeo hata kama yamekuwa kinyume na matarajio waliyokuwa wameyatarajia,ni wazi kwamba CCM ni chama pekee chenye ukomavu wa kisiasa wa hali ya juu ukilinganisha na vyama vingine vya kisiasa ambavyo hulazimisha matokeo ya chaguzi yawe kama vile wao watakavyo hata kufikia kufanya fujo na vurugu zinazohatarisha amani ya nchi yetu.

Pili napenda kutoa himizo kwa wanaccm na viongozi wote walioshiriki uchaguzi wa Arusha kuwa kuvunjika kwa mpini sio mwisho wa uhunzi,tumejaribu,tumeweza na sasa tusonge mbele katika kuwatumikia watanzania kwani ilani iliyoko madarakani ni ya CCM.

Hakuna sababu yakukata tamaa kwa matokeo haya ya Arusha kwakuzingatia kwamba hata mbuyu ulianza kama mchicha, tujikumbushe kwamba kata hizo zilikuwa zinamilikiwa na chadema tangu awali na isitoshe kura tulizopata ni nyingi kuliko zile tulipata 2010 hii ni ishara ya wazi sasa kwamba wapo watu wengi walioichagua chadema 2010 lakini sasa wamegeuka na kuichagua CCM ishara ya kwamba sasa wanakiunga mkono chama cha mapinduzi.

Jukumu tulilonalo ni kujisahihisha pale tulipokosea na kuzitumia kura hizo kama mtaji wetu katika kipindi hiki kifupi kabla yakufikia uchaguzi mkuu ujao.kwakufanya hivyo tutakuwa tumejiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kushinda.

Tatu napenda kuwapa hongera na pole chadema kwakujisahaulisha kuwa uchaguzi huu umefanyika katika mikoa mingi na sio Arusha pekeyake na matokeo ya awali CCM ilishinda kwa kishindo kwa kata 16 chadema kata 4 tu,iweje muwe wepesi wakusahau mapema hivyo?ukizingatia kwamba pamoja na ninyi kushinda kata 4 za Arusha na kuwafanya muwe na kata 8 bado CCM ni iyena iyena nambari wani.

Nadhani kuna swali la kujiuliza hapa sisi kama watanzania kwamba kuna nini kati ya chadema na Arusha?ukizingatia kuwa kuna mikoa mingine chadema ilifanya chaguzi na kushinda lakini matumizi ya helicopter yalifanyika Arusha tu. Niwakumbushe kwamba kunapotokea na chaguzi kinachoangaliwa ni matokeo ya jumla ya maeneo yote yaliyofanya uchaguzi na sio matokeo ya mkoa mmoja.

Chadema ingeonyesha kwamba ni chama makini endapo ingefurahia ushindi wa Arusha huku wakijitathimini sababu zilizopelekea CCM kupata kura nyingi kipindi hiki kuliko 2010 badala ya wao kuanza kubeza wanaccm,kubeza viongozi wa ccm walioshiriki uchaguzi huo pamoja na kubeza CCM bila kuzingatia kwamba mpaka sasa CCM wameibuka kidedea katika uchaguzi huu mdogo.

Waswahili walisema 'akipendacho chongo huita kengeza' ushindi wa chadema Arusha ni sawa na chongo ila wao wanang'ang'ania kuuita ni kengeza kutokana na CCM kushinda kata 16 chadema 8 halafu mnajiita mashujaa huku nikulazimisha chongo kuwa kengeza.
Kwani hata kipofu akiona mawingu hudhani kuwa kaona mbingu,kumbe ni mawingu tu na yatapita.

Ni vema mkatambua kuwa wa awali ni wa awali tu.

Naomba kuwasilisha,wenye hoja karibuni wanaotumia matusi kama kinga yao pia karibuni.

CCM umoja ni ushindi.

Viva CCM

PUMBA TUPU Juliana Shonza, wapi ndugu yako Mwapamba?Nawaonea huruma sana, poleni sana MALAYA WA KISIASA.
 
Last edited by a moderator:
Chama cha mapinduzi kingekuwa kinauwezo wa kusema baadhi ya wanachama wangeumbuka,maana CHAMA kingewakataa katika majukwaa,ukisoma katiba ya chama cha mapinduzi wachache sana wana sifa ya kuwa wanachama wa chama hiki
*Katiba ya chama mapinduzi nitanukuu
(Toleo la februari 1997) Fungu la kwanza
""Mtu atakayekubaliwa kuingia katika CCM au Kuendelea kuwa Mwanachama,ni yule anayetimiza masharti yafuatayo-
Mosi,kuwa mtu anayeheshimu watu
Pili,kuwa mtu anayefanya juhudi ya kuielewa,kuieleza,kuitetea na kuitekeleza ITIKADI na siasa ya CCM
Tatu,kuwa mtu mwenye kuamini kuwa kazi ni kipimo cha utu,na kuitekeleza imani hiyo kwa vitendo
Nne,kuwa mtu anaependa kushirikiana na wenzake
Tano,Kuwa mtu ambaye siku zote yuko mstari wa mbele katika utekelezaji wa mambo yote ya umma,kulingana na miongozo ya CCM
Sita,kuwa wakati wote ni mfano wa tabia nzuri kwa vitendo vyake na kauli yake,kuwa mwaminifu,na kutokuwa mlevi au mzururaji
Saba,kuwa ama mkulima,mfanyakazi au mwenye shughuli nyingine yoyote halali ya kujitegemea
"VV"
 
Duh! Hivi UDSM kinatoa makapi kiasi hiki?
Hata IGP wa green guards aka mwigulu naye ni mhitimu wa pale, tena first class!

Bi juliana msalimie mwigulu huko mafichoni.
 
Tofautisha mtu na chama au taasisi, yawezekana kabisa kuna mengi yamefanywa na mtu kipindi akiwa ccm lakini kwa sasa ni chadema, sasa utasema alofanya mtu akiwa ccm basi kilifanywa na ccm? jibu ni HAPANA.

Ndo maana tunashindwa kuwaelewa walobaki ccm kama kweli wana uwezo mzuri wa kufikiri au wamekaririshwa tu. Huwa nashindwa kumwelewa mtu anayesimama kwa mavazi ya njano na kijani akatamba kwamba wao ndo wenye nchi.

Ni sawa mkubwa. Tunaweza pia kuangalia dhamana ya kuboresha maisha ya Watanzania ambayo imekuwa mikononi mwa ccm kwa miaka zaidi ya hamsini sasa. Tunapotoa dhamana ya uongozi wa nchi kwa chama, tunategemea ufanisi wa kiwango kikubwa katika nyanja mbali mbali za maendeleo na taswira yake ionekane katika maisha ya Mtanzania.

Angalia hadi sasa ccm imeshindwa kutoa huduma bora za afya kwa Watanzania wanalipa kodi kubwa kila kukicha.

Viwango na ubora wa elimu unasidi kushuka hadi wana standardize matokeo ya mitihani ya taifa halafu wanasingizia watu wamefaulu huku uelewa ukiwa ule ule wa kupanda mikwaju na mibuyu.

Huduma za maji safi na salama imekuwa ndoto hata mijini ambako serikali imetandika mabomba tu lakini kinachopita katika hizo bomba ni siri ya vyura.

Majority hadi leo hawana makazi sahihi.

Tatizo la vifo vya wanawake na wfatoto, achana na wanaume wanaokufa kiume limeendelea kuwa tatizo huku eti takwimu zikisemwa limedhibitiwa.

Kushuka kwa democrasia nchini kunakofanywa makusudi kwa maslahi ya watawala kumekuwa kisu shingoni kwa mtanzania wa kawaida. imebidi aendelee kunyamaz hata anapoona hapawi sawa kwa hofu ya kutendewa yasiyotarajiwa wala kuelezewa.

Raslimali za nchi kuwa mikononi kwa jina la mwa wageni kwa jina la uwekezaji na watu wachache wenye asili ya kiasia na kunaacha uzao wa Watz na tumaini la kuwa kama wahindi wekundu.

Angalia jinsi tasnia ya habari inavyodhibitiwa ili kuwanyima wananchi taarifa sahihi na muhimu ambazo zingewasaidia kupanga na kufanya maamuzi sahihi.

Mgawanyo mbovu wa mapato ya serikali , rushwa, ufisadi na kukosa uwajibikaji katika sekta ya umma, kumejenga wingu jeusi la kutisha katika anga la Tz. Watu wanaishi wakingojea siku zao zifike basi.

Utekelezaji mbovu wa mipango dhaifu ya maendeleo, mipango mibovu na miji na ukosefu wa miundo mbinu sahihi ya technolojia, uzalishaji, usafirishaji, masoko na nishati, ni vyanzo vya mauti kwa wananchi.

Haya na mengine mengi, yanahitaji serikali makini inayoelewa, inayojali na yenye nia za dhati za kuboresha ustawi wa taifa. Siyo ccm iliyoshindwa kwamiaka 50.

Hapa ndipo tunaona kwamba, kama kuna mtu mmoja ni dhaifu, akafanya maamuzi yasiyokubalika, mfumo wa serikali umbane na kurekebisha alipokosea. Kama mfumo nidhaifu, watu wataendelea kujiamulia kufanya kle wanataka, kuchukua maamuzi ya ovy na kuyatelekeza, matokeo yake ndiyo tunakuwa na hawa wanaotukanwa na Sweety Radhia kwamba wamezaliwa kariakoo.

Kumbe kama seriakli ya ccm ingekuwa ni kwa ajli ya wananchi, isingeruhusu hali yoyote, mtu yeyote, taasisi yoyote ama chombo chochote, kutenda kinyume na malengo ya maendeleo hadi kuzalisha tabaka linalosemwa na kuzaliwa kariakoo.

Njia pekee ya kuhakikisha nchi yetu inapiga kasi katika maendeleo ni kuunganisha nguvu za pamoja ili kupata serikali itakayotengeneza mfumo sahihi unaohitajika kwa sasa katika kubadilisha uozo wa serikali ya ccm na kuleta maendeleoa. Yote haya yanayotusumbua yanahusiana moja kwa moja na Serikali dhaifu ambayo ni ya ccm and ndiyo maana tunasema ccm imejenga matabaka ya watu wanaoitwa wamezaliwa kariakoo.
 
Umeandika vizuri isipokuwa hapo kwenye ''hata mbuyu ulianza kama mchicha.'' CCM ni chama kikongwe kuliko vyama vyote hapa nchini. Hiyo nahau sidhani kama inaendana na ukongwe wake. Ni dalili ya kuanza kukata tamaa kuilinganisha CCM na mchicha ambao baadaye utakuwa hadi kuwa kama mbuyu. Mlipaswa tayari kuwa mmekuwa hadi mmefikia ukubwa wa ubuyu. Hiyo kauli ilitakiwa kutolewa na vyama vinavyoanza kukua.
Hapo sasa mbuyu kama mchicha kwa chama chao wapi na wapi? hapo kapotoka
 
Wewe ni mmoja wa watu waliokuwa arusha mkiipigia debe chadema kwa raslimali za ccm. Na kujishaua kote mkapigwa vituo vyote. Eti makapi ya cdm ndio keki za ccm. Dada wa watu nakuhakikishia, mwaka huu hautakwisha bila ya nyinyi kutolewa kwenye reli. Eti hata mbuyu ulianza kama mchicha. Ccm ilikuwa mbuyu wakati mwigulu anawasajili. Wewe na wenzako ndio mnaifanya iwe mchicha. Vipi lakini, sombetin mwigulu ataenda?

Thubutu yake amepewa za uso ataenda tena? anyway akienda asisahau kuchukua komedi yake, Mwigulu ni mtaji kwa CDM
 
Juliana shonza, wewe ni mchumia tumbo, mnafiki, zakubimbi na ndumilakuwili. Wewe na Mwampamba ndiyo mnachangia kuibomoa CCM. Hata wana ccm wenyewe wanafahamu ila 'wanawapaisha' kinafiki wakidhani kwamba Chadema itasikitika kuwapoteza, bila kutambua kuwa mmetemwa na Chadema kama makapi tu. Mpo CCM kiushabiki wa kisiasa tu ijapokuwa mnachangia kuibomoa ccm zaidi kuliko kuijenga. Ni watu wenye akili za kuku tu, kama Mwigulu wanaoweza kukubali kuwakumbatia. Shame upon all of you.
 
Ndugu wanajamvi hili nimekuwa kimya kwa mda kidogo baada ya uchaguzi wa Arusha niliona niwaache wanachadema mtambe mtambike mara baada ya ushindi huo mlioupata.

Nina kila sababu yakuwapongeza wananchi wa Arusha kwakufanya uchaguzi kwa amani kwani amani ndiyo tunu na kitambulisho pekee ya Taifa letu,bila kuvisahau vyombo vya usalama kwakuhakikisha zoezi linafanyika kwa amani.

Mosi kwakuzingatia dhana ya utawala bora na uongozi bora inayotakay chama chochote cha kisiasa kukubali matokeo hata kama yamekuwa kinyume na matarajio waliyokuwa wameyatarajia,ni wazi kwamba CCM ni chama pekee chenye ukomavu wa kisiasa wa hali ya juu ukilinganisha na vyama vingine vya kisiasa ambavyo hulazimisha matokeo ya chaguzi yawe kama vile wao watakavyo hata kufikia kufanya fujo na vurugu zinazohatarisha amani ya nchi yetu.

Pili napenda kutoa himizo kwa wanaccm na viongozi wote walioshiriki uchaguzi wa Arusha kuwa kuvunjika kwa mpini sio mwisho wa uhunzi,tumejaribu,tumeweza na sasa tusonge mbele katika kuwatumikia watanzania kwani ilani iliyoko madarakani ni ya CCM.

Hakuna sababu yakukata tamaa kwa matokeo haya ya Arusha kwakuzingatia kwamba hata mbuyu ulianza kama mchicha, tujikumbushe kwamba kata hizo zilikuwa zinamilikiwa na chadema tangu awali na isitoshe kura tulizopata ni nyingi kuliko zile tulipata 2010 hii ni ishara ya wazi sasa kwamba wapo watu wengi walioichagua chadema 2010 lakini sasa wamegeuka na kuichagua CCM ishara ya kwamba sasa wanakiunga mkono chama cha mapinduzi.

Jukumu tulilonalo ni kujisahihisha pale tulipokosea na kuzitumia kura hizo kama mtaji wetu katika kipindi hiki kifupi kabla yakufikia uchaguzi mkuu ujao.kwakufanya hivyo tutakuwa tumejiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kushinda.

Tatu napenda kuwapa hongera na pole chadema kwakujisahaulisha kuwa uchaguzi huu umefanyika katika mikoa mingi na sio Arusha pekeyake na matokeo ya awali CCM ilishinda kwa kishindo kwa kata 16 chadema kata 4 tu,iweje muwe wepesi wakusahau mapema hivyo?ukizingatia kwamba pamoja na ninyi kushinda kata 4 za Arusha na kuwafanya muwe na kata 8 bado CCM ni iyena iyena nambari wani.

Nadhani kuna swali la kujiuliza hapa sisi kama watanzania kwamba kuna nini kati ya chadema na Arusha?ukizingatia kuwa kuna mikoa mingine chadema ilifanya chaguzi na kushinda lakini matumizi ya helicopter yalifanyika Arusha tu. Niwakumbushe kwamba kunapotokea na chaguzi kinachoangaliwa ni matokeo ya jumla ya maeneo yote yaliyofanya uchaguzi na sio matokeo ya mkoa mmoja.

Chadema ingeonyesha kwamba ni chama makini endapo ingefurahia ushindi wa Arusha huku wakijitathimini sababu zilizopelekea CCM kupata kura nyingi kipindi hiki kuliko 2010 badala ya wao kuanza kubeza wanaccm,kubeza viongozi wa ccm walioshiriki uchaguzi huo pamoja na kubeza CCM bila kuzingatia kwamba mpaka sasa CCM wameibuka kidedea katika uchaguzi huu mdogo.

Waswahili walisema 'akipendacho chongo huita kengeza' ushindi wa chadema Arusha ni sawa na chongo ila wao wanang'ang'ania kuuita ni kengeza kutokana na CCM kushinda kata 16 chadema 8 halafu mnajiita mashujaa huku nikulazimisha chongo kuwa kengeza.
Kwani hata kipofu akiona mawingu hudhani kuwa kaona mbingu,kumbe ni mawingu tu na yatapita.

Ni vema mkatambua kuwa wa awali ni wa awali tu.

Naomba kuwasilisha,wenye hoja karibuni wanaotumia matusi kama kinga yao pia karibuni.

CCM umoja ni ushindi.

Viva CCM

Nimeshindwa kujizuia, potelea mbali, umeandika hoja za kitoto sana, baadhi yake nimezipaka rangi. Inasikitisha kuona kuwa uwezo wako wa kujenga hoja umeishia hapo.
 
yaani kwa hiki ulichokiandika inaonyesha una upeo mdogo Sana wa kufikiria.
Hata sisi wengine tusiofatilia siasa sana tunajua CCM wamepoteza huu uchaguzi wewe unasema eti wameibuka kidedea???seriously??Kupoteza kata mlizokuwa mnazishikilia ni kuibuka kidedea?
Dada yangu siasa ni science kama science nyingine,inahitaji uwezo wa kufikiria na kudadavua mambo.
Ningekuwa mimi ni wewe ningeandika maneno machache tu
"wana arusha mliotupigia kura tunashukuru kwa kura zenu, tutaendelea kufanya jitihada ili kurudisha imani mliyokuwa nayo kwa CCM"
Nape mwenzio anaujua ukweli ndio maana kakaa kimya hajataka kuongelea lolote. Ila wewe na kiherehere chako unatoka huko unakuja kuandika utumbo hapa. Dada yangu sometimes kukaa kimya ndio JIBU SAHIHI ZAIDI. unajishushia hadhi yako kidogo uliyokuwa nayo.

Wewe na mwenzio Mtela mlikuwa mnapimwa tu ni kiasi gani mnaweza kusaidia chama, ila kwa matokeo haya ambayo mmeshindwa kutoa ushawishi na ushindi hata kwa kituo kimoja inaonyesha kazi yenu ni UTUMBO mtupu na kinachofuata ni kutupwa kama mpira wa kiume unavyotupwa baada ya matumizi (maana hata jinsi unavyoshikwa before matumizi ni tofauti unavyoshikwa baada ya matumizi).

kaa chini jitafakari, hivyo viposho visikupe kiburi. wenzio akina wassira washazeeka washakula vya kutosha.

WATCH OUT!!!!!!
 
Afadhali Shonza ana interest tunazozijua kutoka kwa Mwigulu mzee wa kuovertake,na kina radhia,simiyu yetu n.k,wao interest zao ni zipi ndani ya ccm,nijuzeni tafadhali.

Buku Saba si haba
 
Degree nyingine ni hadi uwe bingwa wa kutanua!
Mleta mada anaamini CCM imepata kura nyingi kuliko mwaka 2010 wakati wapiga kura wa Arusha walikuwa asilimia karibia 20??!
Kama ndivyo, basi CCM inajifia bure!
Halafu ungalileta takwimu zinazoonesha kabla ya chaguzi zote nani alikuwa na kata ngapi na amebakiwa na ngapi!
Vinginevyo ni kuonesha kwamba bodi ya mikopo haikopeshi fedha peke yake ila hata akili!
 
Nashindwa kumwelewa huyu mdada, kati ya cdm na ccm kipi kilianza kama mchicha? kumbe ni kweli shoza alijifukuzisha cdm baada ya kujikuta elimu yake ni ndogo kulinganisha na wenzake, kweli huyu ni bulula kweli.
 
Kati ya yote ili la CCM kuwa mchicha nimeniacha hoi, mchicha oyeeeeeee haya ndio majembe ya CCM.
 
Kabla ya matokeo kutanganzwa mkatoka NDUKI -- wewe na Kamanda wa Green Guards.sijui mlikimbilia wapi maana dar mmeonekana jana.

Walienda kujifuta machozi chobisi!
Si mnamjua mzee wa vodosho!?
 
Ulijisikiaje siku ulipofukuzwa uanachama wa CHADEMA? bora tuanzie hapo make usomeki kabisa sijui unaandika ukiwa na jazba sijui hasira au ndo jinsi unavyojenga hoja?
 
Mbona uchaguzi ulifanyika kata 26.Umeandika kuwa CCM walishinda kata 16 na CHADEMA kata 8 vipi kata zilizobakia 2 zilichukuliwa na chama gani?.

Huyu binti nikati ya watanzania wanaomiliki makaratasi yanayoitwa degree!
Yeye na mchumi namba moja wanakidhalilisha UDSM!
Ngh!
 
Umeandika vizuri isipokuwa hapo kwenye ''hata mbuyu ulianza kama mchicha.'' CCM ni chama kikongwe kuliko vyama vyote hapa nchini. Hiyo nahau sidhani kama inaendana na ukongwe wake. Ni dalili ya kuanza kukata tamaa kuilinganisha CCM na mchicha ambao baadaye utakuwa hadi kuwa kama mbuyu. Mlipaswa tayari kuwa mmekuwa hadi mmefikia ukubwa wa ubuyu. Hiyo kauli ilitakiwa kutolewa na vyama vinavyoanza kukua.
Radhia sweety.....kumbe ukitulia unakua na sweety ideas wakati mwingine...
 
Back
Top Bottom