CCM: Nini ubaya wa REFORMS zinazodaiwa na CHADEMA?

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
711
Reaction score
1,165
Leo natamani kupata maoni ya makada wenzangu wa Chama Cha Mapinduzi, waliopo humu jukwaani.

Kuna ubaya gani wa kuwapa CHADEMA reforms wanazozitaka ili washiriki uchaguzi bila manung'uniko?

Mm binafsi sijapata kusikia mtu hata mmoja, ndani na nje ya CCM akisema hivi, reform hii inayodaiwa na CHADEMA ubaya wake ni huu, na reform ile ubaya wake ni ule! Ninachokisikia ni muda hautoshi kana kwamba CHADEMA wameanza kudai reforms zao leo.

Kwenye uchaguzi huu, CCM itakuwa na mtaji wa kura 13milioni za kuanzia za wanachama wake, na kura yangu ikiwepo, mafanikio ya ilani 2020-2025 ya kuyanadi, Sh. 86 bilioni kwaajili ya kampeni, mabalozi wenye hamasa waliowezeshwa baiskeli, watendaji wa CCM kata wenye hamasa waliowezeshwa pikipiki, mabasi ya kisasa n.k. Chama gani kitatushinda?

Mm nadhani, kutokuwapa CHADEMA reforms wanazozitaka sio sawa. Inaleta imani kuwa CCM inategemea madhaifu ya sheria zetu kushinda chaguzi badala ya nguvu yake ya kisiasa na imani ya wananchi.

CCM ni kubwa sana, ushindi wake kwenye uchaguzi hauwezi kuhatarishwa na reforms wanazozitaka CHADEMA. Tuwape reforms, tuwashinde uchaguzi, tutakuwa tumewaziba midomo.

View: https://vm.tiktok.com/ZMALV8XcR/
 
THE FALL OF CCM 1995-2025.✍️📌
 
1755755826511.png

1755755874772.png
CCM inaongozwa na huyu mmiliki wa maliasili zetu asiyetaka Reforms nor fair Elections
 
CCM hata Dunia ipinduke mara nne haiwezi kuruhusu hizo reforms. Wanajua hawapendwi na wananchi kwa hiyo watakuwa wametoa nchi kwa Chadema. Samia hakubaliki na serikali yake yote.
Kwa takwimu zipi, CCM itashindwa na CHADEMA? CCM ndio maisha ya wananchi ya kila siku, huku tunakoishi mitaani, wananchi wote wanaona mabalozi wa CCM ndio viongozi wao karibu zaidi na hawa ndio wanaowahimiza wanachama wa CCM kwenda kupiga kura.
 
Hivi kumbe watu wenye akili bado wapo kwenye hiko chama??? Natamani wenzako wote wasome hiko ulichokiandika hapa umeandika kitu Cha maana sana na Nina imani utakua umejiondoa katika hiyo dhambi ya kukandamiza wanyonge... hongera sana.

Chama kinajinadi kina wanachama wengi kuliko chama kingine chochote Sasa uoga unatoka wapi Ina maana hata wenyewe Kwa wenyewe hamuaminiani??
 
Back
Top Bottom