Duble Chris
JF-Expert Member
- May 28, 2011
- 3,481
- 564
Hadithi ni ndefu. Sema ulikuwa na ban
Ndugu wanajamvi hili nimekuwa kimya kwa mda kidogo baada ya uchaguzi wa Arusha niliona niwaache wanachadema mtambe mtambike mara baada ya ushindi huo mlioupata.
Nina kila sababu yakuwapongeza wananchi wa Arusha kwakufanya uchaguzi kwa amani kwani amani ndiyo tunu na kitambulisho pekee ya Taifa letu,bila kuvisahau vyombo vya usalama kwakuhakikisha zoezi linafanyika kwa amani.
Mosi kwakuzingatia dhana ya utawala bora na uongozi bora inayotakay chama chochote cha kisiasa kukubali matokeo hata kama yamekuwa kinyume na matarajio waliyokuwa wameyatarajia,ni wazi kwamba CCM ni chama pekee chenye ukomavu wa kisiasa wa hali ya juu ukilinganisha na vyama vingine vya kisiasa ambavyo hulazimisha matokeo ya chaguzi yawe kama vile wao watakavyo hata kufikia kufanya fujo na vurugu zinazohatarisha amani ya nchi yetu.
Pili napenda kutoa himizo kwa wanaccm na viongozi wote walioshiriki uchaguzi wa Arusha kuwa kuvunjika kwa mpini sio mwisho wa uhunzi,tumejaribu,tumeweza na sasa tusonge mbele katika kuwatumikia watanzania kwani ilani iliyoko madarakani ni ya CCM.
Hakuna sababu yakukata tamaa kwa matokeo haya ya Arusha kwakuzingatia kwamba hata mbuyu ulianza kama mchicha, tujikumbushe kwamba kata hizo zilikuwa zinamilikiwa na chadema tangu awali na isitoshe kura tulizopata ni nyingi kuliko zile tulipata 2010 hii ni ishara ya wazi sasa kwamba wapo watu wengi walioichagua chadema 2010 lakini sasa wamegeuka na kuichagua CCM ishara ya kwamba sasa wanakiunga mkono chama cha mapinduzi.
Jukumu tulilonalo ni kujisahihisha pale tulipokosea na kuzitumia kura hizo kama mtaji wetu katika kipindi hiki kifupi kabla yakufikia uchaguzi mkuu ujao.kwakufanya hivyo tutakuwa tumejiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kushinda.
Tatu napenda kuwapa hongera na pole chadema kwakujisahaulisha kuwa uchaguzi huu umefanyika katika mikoa mingi na sio Arusha pekeyake na matokeo ya awali CCM ilishinda kwa kishindo kwa kata 16 chadema kata 4 tu,iweje muwe wepesi wakusahau mapema hivyo?ukizingatia kwamba pamoja na ninyi kushinda kata 4 za Arusha na kuwafanya muwe na kata 8 bado CCM ni iyena iyena nambari wani.
Nadhani kuna swali la kujiuliza hapa sisi kama watanzania kwamba kuna nini kati ya chadema na Arusha?ukizingatia kuwa kuna mikoa mingine chadema ilifanya chaguzi na kushinda lakini matumizi ya helicopter yalifanyika Arusha tu. Niwakumbushe kwamba kunapotokea na chaguzi kinachoangaliwa ni matokeo ya jumla ya maeneo yote yaliyofanya uchaguzi na sio matokeo ya mkoa mmoja.
Chadema ingeonyesha kwamba ni chama makini endapo ingefurahia ushindi wa Arusha huku wakijitathimini sababu zilizopelekea CCM kupata kura nyingi kipindi hiki kuliko 2010 badala ya wao kuanza kubeza wanaccm,kubeza viongozi wa ccm walioshiriki uchaguzi huo pamoja na kubeza CCM bila kuzingatia kwamba mpaka sasa CCM wameibuka kidedea katika uchaguzi huu mdogo.
Waswahili walisema 'akipendacho chongo huita kengeza' ushindi wa chadema Arusha ni sawa na chongo ila wao wanang'ang'ania kuuita ni kengeza kutokana na CCM kushinda kata 16 chadema 8 halafu mnajiita mashujaa huku nikulazimisha chongo kuwa kengeza.
Kwani hata kipofu akiona mawingu hudhani kuwa kaona mbingu,kumbe ni mawingu tu na yatapita.
Ni vema mkatambua kuwa wa awali ni wa awali tu.
Naomba kuwasilisha,wenye hoja karibuni wanaotumia matusi kama kinga yao pia karibuni.
CCM umoja ni ushindi.
Viva CCM
HaasbunaAllahu Waneema 'Lwakil.
Binti Juliana Shonza najua hii thread umeianzisha kwa maelekezo ya bosi wako. Pamoja na hayo na kwa faida ya vilaza wa hesabu wenzako hapo lumumba ngoja nikusaidie kufanya hesabu ya darasa la kwanza. Kwa akili yako ndogo unashindwa kujua kwamba kama ccm ilishinda kata 16 na Chadema imeshinda kata 8 basi jumla ya kata zilizofanya uchaguzi ni 24 (16+8=24!hesabu ya darasa la kwanza hii)sasa sijui kata 2 umezipeleka wapi!!??
Jumla ya kata zilizopaswa kufanya uchaguzi tarehe 16/06/2013 ni kata 26.
Kata zilizofanya uchaguzi tarehe hiyo 16/06 zilikuwa kata 22 (baada ya policcm kulipua bomu mkutano wa Chadema na hivyo NEC kuahirisha uchaguzi katika kata 4 za Arusha).
Katika kata 22 zilizofanya uchaguzi awali ccm ilishinda kata 16 na Chadema ikashinda kata 6 (Chadema ilirudisha mikononi kata zake 2 na kuchukua 4 kutoka kwenu ccm).
Katika uchaguzi uliofanyika Arusha juzi tarehe 14/07/2014 Chadema imewagaragaza vibaya ccm kwa kujinyakulia kata zote 4.
Kwa ujumla msimamo wa ushindi wa kata kwa ujumla ni kwamba Chadema 10 ccm 16. Lakini pia kwa uwiano wa wingi wa kura Chadema ina 46% huku ccm ikiwa na 49%. Sasa nataka uanzie hapo uniambie kama ccm imeongeza idadi ya wapiga kura toka 2010 au imeporomoka? sitarajii kwamba mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dsm unaweza kushindwa hata kuunga unga hesabu ndogo kama hizi, unless uniambie hiyo degree uliipata kwa mlango wa dharura.
ukitaka kuona graduate anapata aibu afanye mitiani ya bodi siku hizi degree ni kama makalio kila mtu anayo sishangai shoza anavyoandika bila kutafakari
Kiukweli tulikuwa tunaidharau jf, lakini amini usiamini, mabandiko kama haya, yamesaidia saidia, huwezi jua!. Zamani nilikuwa napitia mabandiko yako kwa dharau na kujibu kwa kejeli, lakini baada ya uteuzi, sasa napitia mabandiko yako yote kwa makini zaidi, heshima na adabu haswa kwa kuzingatia wewe sasa ndio bosi wangu kwenye tasnia ya habari.Ndugu wanajamvi hili nimekuwa kimya kwa mda kidogo baada ya uchaguzi wa Arusha niliona niwaache WanaCHADEMA mtambe mtambike mara baada ya ushindi huo mlioupata.
Nina kila sababu yakuwapongeza wananchi wa Arusha kwakufanya uchaguzi kwa amani kwani amani ndiyo tunu na kitambulisho pekee ya Taifa letu,bila kuvisahau vyombo vya usalama kwakuhakikisha zoezi linafanyika kwa amani.
Mosi kwakuzingatia dhana ya utawala bora na uongozi bora inayotakay chama chochote cha kisiasa kukubali matokeo hata kama yamekuwa kinyume na matarajio waliyokuwa wameyatarajia,ni wazi kwamba CCM ni chama pekee chenye ukomavu wa kisiasa wa hali ya juu ukilinganisha na vyama vingine vya kisiasa ambavyo hulazimisha matokeo ya chaguzi yawe kama vile wao watakavyo hata kufikia kufanya fujo na vurugu zinazohatarisha amani ya nchi yetu.
Pili napenda kutoa himizo kwa wanaCCM na viongozi wote walioshiriki uchaguzi wa Arusha kuwa kuvunjika kwa mpini sio mwisho wa uhunzi,tumejaribu,tumeweza na sasa tusonge mbele katika kuwatumikia watanzania kwani ilani iliyoko madarakani ni ya CCM.
Hakuna sababu yakukata tamaa kwa matokeo haya ya Arusha kwakuzingatia kwamba hata mbuyu ulianza kama mchicha, tujikumbushe kwamba kata hizo zilikuwa zinamilikiwa na CHADEMA tangu awali na isitoshe kura tulizopata ni nyingi kuliko zile tulipata 2010 hii ni ishara ya wazi sasa kwamba wapo watu wengi walioichagua CHADEMA 2010 lakini sasa wamegeuka na kuichagua CCM ishara ya kwamba sasa wanakiunga mkono chama cha mapinduzi.
Jukumu tulilonalo ni kujisahihisha pale tulipokosea na kuzitumia kura hizo kama mtaji wetu katika kipindi hiki kifupi kabla yakufikia uchaguzi mkuu ujao.kwakufanya hivyo tutakuwa tumejiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kushinda.
Tatu napenda kuwapa hongera na pole CHADEMA kwakujisahaulisha kuwa uchaguzi huu umefanyika katika mikoa mingi na sio Arusha pekeyake na matokeo ya awali CCM ilishinda kwa kishindo kwa kata 16 CHADEMA kata 4 tu,iweje muwe wepesi wakusahau mapema hivyo?ukizingatia kwamba pamoja na ninyi kushinda kata 4 za Arusha na kuwafanya muwe na kata 8 bado CCM ni iyena iyena nambari wani.
Nadhani kuna swali la kujiuliza hapa sisi kama Watanzania kwamba kuna nini kati ya CHADEMA na Arusha? ukizingatia kuwa kuna mikoa mingine CHADEMA ilifanya chaguzi na kushinda lakini matumizi ya helicopter yalifanyika Arusha tu. Niwakumbushe kwamba kunapotokea na chaguzi kinachoangaliwa ni matokeo ya jumla ya maeneo yote yaliyofanya uchaguzi na sio matokeo ya mkoa mmoja.
CHADEMA ingeonyesha kwamba ni chama makini endapo ingefurahia ushindi wa Arusha huku wakijitathimini sababu zilizopelekea CCM kupata kura nyingi kipindi hiki kuliko 2010 badala ya wao kuanza kubeza wanaCCM, kubeza viongozi wa CCM walioshiriki uchaguzi huo pamoja na kubeza CCM bila kuzingatia kwamba mpaka sasa CCM wameibuka kidedea katika uchaguzi huu mdogo.
Waswahili walisema 'akipendacho chongo huita kengeza' ushindi wa CHADEMA Arusha ni sawa na chongo ila wao wanang'ang'ania kuuita ni kengeza kutokana na CCM kushinda kata 16 chadema 8 halafu mnajiita mashujaa huku nikulazimisha chongo kuwa kengeza.
Kwani hata kipofu akiona mawingu hudhani kuwa kaona mbingu,kumbe ni mawingu tu na yatapita.
Ni vema mkatambua kuwa wa awali ni wa awali tu.
Naomba kuwasilisha,wenye hoja karibuni wanaotumia matusi kama kinga yao pia karibuni.
CCM umoja ni ushindi.
Viva CCM
Uteuzi wa kupeana peana tuKiukweli tulikuwa tunaidharau jf, lakini amini usiamini, mabandiko kama haya, yamesaidia saidia, huwezi jua!. Zamani nilikuwa napitia mabandiko yako kwa dharau na kujibu kwa kejeli, lakini baada ya uteuzi, sasa napitia mabandiko yako yote kwa makini zaidi, heshima na adabu haswa kwa kuzingatia wewe sasa ndio bosi wangu kwenye tasnia ya habari.
Karibu Boss, Mheshimiwa saba, Bi Juliana Shonza.
Paskali.
Nimekusoma mkuu ovaUteuzi wa kupeana peana tu
Ova