Hoja za Kihiyo uamuzi wa NECTA kuachana na utaratibu wa kutangaza top 10 na mwanafunzi bora

Tanzania Nchi Yetu Sote

JF-Expert Member
Mar 12, 2017
505
854
Nimefuatilia kwa karibu mitizamo kinzani ya wadau wa elimu na wanaharakati mbalimbali baada ya Baraza la mitihani Tanzania kutangaza matokeo kidato cha nne 2022, na hoja kubwa iliyoleta mjadala mtandaoni ni ile ya Baraza la mitihani Tanzania kuondoa utaratibu wa kutangaza shule kumi bora kitaifa (Top 10) na mwanafunzi bora kitaifa kama ambavyo imezoeleka kwa miongo mingi kwa kile kilichoitwa ni kutoa publicity/marketing kwa baadhi ya shule zilizofanya vizuri na pia kuwa siyo sawa kutangaza mwanafunzi mmoja bora kuliko wote ikiwa walisoma katika mazingira tofauti.

Kufuatia hoja hiyo Baraza la mitihani kumeibuka makundi mawili kinzani, wapo wanaokosoa hoja hiyo na wapo wanaounga mkono Baraza la mitihani, makundi yote mawili yanaweza kuwa na hoja za msingi na kila upande haupaswi kuhitimisha mjadala huu.

Nimefanikiwa kuona baadhi ya maandiko ya upande unaokosoa uamuzi wa Baraza la mitihani wa kuachana na utaratibu wa kutangaza Top 10 na mwanafunzi bora kitaifa, miongoni mwa baadhi ya sababu zilizotajwa na upande huu usiyokubaliana na utaratibu mpya ni kuwa;

Mosi, Wameona shule za serikali hakuna zilizofanya vizuri zimeburuzwa na shule binafsi

Pili, imetolewa mifano mbalimbali kuonyesha kuwa Baraza halikupaswa kuacha kuendelea na utaratibu wa kutangaza kwasababu ya hoja zilizotolewa na Baraza kuonekana hazina tija.

Kundi la pili linalokubaliana na utaratibu kwa bahati mbaya wao sijabahatika kuona andiko zaidi ya comments tu mitandaoni ambazo kimsingi zinaonyesha ama hawajataka kuwa wazi kwanini wanakubaliana na uamuzi Baraza au hawana hoja ya msingi kwanini wanakubaliana.

NINI MAONI YANGU KUHUSU UAMUZI WA BARAZA LA MITIHANI?

Binafsi napongeza uamuzi wa Baraza la mitihani kuachana na utaratibu wa kutangaza shule 10 bora na mwanafunzi bora kitaifa.

Naunga mkono utaratibu wa Baraza la mitihani kuachana na utangazaji wa top 10 na mwanafunzi bora kwasababu zifuatazo;

Mosi, Kazi kuu ya Baraza la mitihani pamoja na majukumu mengine ni kumtahini mwanafuzi katika level husika na kutoa vyeti kwa watakaokuwa wamefaulu kupata daraja I-IV baada ya kutahini na kutangaza matokeo.
Kimsingi hoja ya kutangaza top 10, ilikuwa inamnufaisha nani? Mwalimu, mwanafunzi, serikali au shule?. Baraza la mitihani ni Taasisi ya Umma kutangaza matokeo ni jukumu lake la msingi lakini utaratibu wa kupanga shule 10 bora kitaifa na mwanafunzi bora kitaifa siyo kanuni na wala haipaswi kugombewa, ni sawa na binti wa kazi nyumbani uliyempa majukumu ya kukuandalia chakula, wajibu wake wa msingi ni kuandaa chakula, ikitokea akakuzoesha kuandaa chakula, mboga na kachumbari utamuona ni mnyumbulifu siku akiondoa kachumbari ukahoji utakuwa na nongwa zako binafsi, nataka kusema uandaaji wa taarifa ya kutangaza matokeo kwamba iwekwe top 10 au top 100, wanafunzi bora 10 au 100 siyo kanuni au sheria ni utaratibu tu, lakini kutangaza matokeo ni LAZIMA maana ndiyo kazi mahususi Baraza la mitihani

Pili, Baraza la mitihani linaunda sera za mitihani kwa kufuata sera ya Elimu yenye lengo la kuwajengea watahiniwa uwezo wa kujitegemea, sera ya elimu na Baraza la mitihani linatahini wanafunzi wote (binafsi na serikali) kwa mtihani moja wala HALISHINDANISHI WANAFUNZI au SHULE, hoja ya kushindana ibaki kwa walimu mashuleni kama inawajengea chachu kufanya vizuri na kwasababu kila mmoja ana access ya matokeo ya shule zote Tanzania, afungue kuona shule alizozishinda anazoshindana nazo, Baraza libaki na kazi ya kuatahini, kutoa matokeo na vyeti kwa waliofaulu tu.

Tatu, Kwakuwa hakuna cheti huwa kinandikwa shule ya serikali au binafsi, mwanafunzi bora au top 10 , bali huandikwa matokeo kwa kadiri mtahiniwa alivyofaulu, sioni sababu ya mjadala wa mwanafunzi bora na Top 10, ukitazama kwa jicho la tatu mjadala wa top 10 na mwanafunzi bora haukuwa fair, mazingira yanayozunguzwa ni mengi siyo tu ya miundombinu, walimu, vitabu nk pia yapo mazingira ya utahini bado changamoto, mfano kuna masomo maswali yake ni ya kimazingira yaani nikiwa na wanafunzi 100 wanafunzi 50 wanatoka mwanza na 50 wanatoka mbeya/Iringa, fikiria wote wamepata alama A masomo 5, lakini somo la Jiografia likatoka swali la picha ya pamba na Bailojia likatoka swali la samaki (Tilapia) nani atafaulu zaidi? Kwa hakika aliyekuwa exposed na mazingira hayo utajibu kwa ufasaha hasa hawa wa Mwanza na hawa wengine hawatafanya vizuri, Je, ukipima ufaulu wa jumla kwa alama inatosha kusema huyu wa Mwanza ni mwanafunzi bora kitaifa au tubaki tu matokeo, ili kuendelea kutafuta namna bora zaidi ya upimaji wa kuwajengea uwezo wa kujitegea? Nadhani dhana pama ya mazingira iliyozunguzwa na Baraza siyo tu miundombinu , maslahi kwa walimu, vitabu nk.

Mwisho, Mjadala ulipaswa kuangazia Sera ya Elimu inakidhi vigezo vya kumjengea mwanafunzi uwezo wa kujitegemea na inaendana na matakwa ya dunia ya sasa? Kuendelea kuuliza maswali ya label Tilapia fish imepitwa na wakati, kuliko kuja na hoja Top 10 na mwanafunzi bora haijatanzwa kwasababu shule za serikali zimeburuzwa na binafsi so what? Yaani top 10 ikitangazwa kinaongezeka nini? kama kuna kundi lilinufaika kwa kutangaziwa biashara kupitia top 10 na mwanafunzi bora kitaifa, ni vema kuwa waungwana kwa kushukuru kwa nyakati walizonufaika na kukubali kuanza kufanya promotion sasa, kuliko kuona kama kuna sheria imekiukwa.

...leongange262@gmail.com
 
Ndefu ila Necta wamechelewa sana kufanya haya maamuzi watu walikuwa wanaiba sana mitihani ili shule zao ziwe top
 
HOJA ZA KIHIYO UAMUZI WA NECTA KUACHANA NA UTARATIBU WA KUTANGAZA TOP 10 NA MWANAFUNZI BORA

Hiyo ilikua njia mmoja yapo ya kuibia wazazi, hasa kwa shule binfsi, ukifuatilia mbinu zinazo fanywa ili shule ipate kua kwenye top 10, zinaumiza mzazi na mwanafunzi, nashukuru sana kwa mara ya kwanza Necta kuachana na ujinga huo.
 
Zipo cosenquence nyingi zilizowazi na zisizowazi kwa baraza hilo kuachana na utaratibu huo. Kuna shule za upande fulani zimekuwa zinafanya vibaya na za taasisi fulani nazo zimekuwa hazina matokeo mazuri, hivyo basi utaratibu huu utaficha aibu kwa shule hizo. Hili la kuzipa promo shule kinara ni cover tu lakini ndani ya cover kuna mengi yaliyosababisha uamuzi huo
 
Back
Top Bottom