Hoja ya Spika Ndugai: Nitawafukuzaje wabunge ambao Rufaa zao hazijasikilizwa na Baraza kuu kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA?

Katiba ambayo Spika haijui maana ametaka apelekewe nakala? Hamna Katiba ya Chadema inayozungumzia viambatishi. Na Chadema hawajampelekea Spika madai bali wamempa taarifa. Wanachokidai sasa ni afuate Katiba ya nchi ( sio ya CDM) inavyosema kuhusu sifa ya mbunge.

Amandla..
Wasikilize CDM vizuri tgen msikilize spika vizuri. Kama umewasikiliza bgasi rudi tena ukawasikilize tena vizuri tgen urudi hapa
 
Hao chadema wako very very selfish Yani wew mwanaume unapigania mwanamke afukuzwe kazi yake kisa wew huna that's very foolishness and stupidity, Spika kawajibu kwa hoja sana sana huwezi tu kumfukuza kazi mtu hivi hivi bila a fair justice never..

Kiingereza nacho jamani?! Kumbe hujui hii issue - umefahamu kutoka kwa Spika tu. Barua ya Chadema kwa Spika ni kuwa watu hao hawakuteuliwa na chama kuwa wabunge (kumbuka wengi wao walikuwa wagombea majimboni na walishindwa). Ndani ya Chadema kulikuwa na list ya wabunge wa kuteuliwa tayari!! Kama ilivokuwa kwa vyama vingin!! Baada ya kukiuka taratibu za chama na wao kuandika barua kwa ofisi ya Spika, waliitwa na kuhojiwa na kupatikana na hatia na kufukuzwa. Wakakata rufaa na bado haijaamuliwa.

Ungekuwa hata na ufahamu nusu ungefahamu pia kuwa huu ulikuwa ni mpango wa Tume ya Uchaguzi na Spika kuingiza wabunge bungeni, sio wa Chadema. Katibu wa Chadema hakuwahi kuandika barua kuwatambulisha akina Mdee na ndio maana aliandika barua ya kukataa uteuzi wa kughushi na kueleza kuwa hao si wanachama tena. Spika anakataa makusudi kuzungumzia mamlaka ya uteuzi na anazungumzia rufaa ya uanachama kwa sababu anajua kuna watu na wewe!! Si ni huyuhuyu alikwambia hana taarifa za kufukuzwa kwao? Sasa amejua wapi kuwa walifukuzwa na anahimiza mchakato wa rufaa?

Tuna safari ndefu sana kama nchi!! Hata uelewa wa mambo madogo tu ni mbinde. Mambo mengine yanazidi uwezo, msiwe mnayashadidia. Hili si suala la jinsia. Hata watakaochukua nafasi zao (kama sheria ilifuatwa) ni wanawake pia.
 
Wasikilize CDM vizuri tgen msikilize spika vizuri. Kama umewasikiliza bgasi rudi tena ukawasikilize tena vizuri tgen urudi hapa
Kwenye issue hii nakumbuka Chadema walisema hivi: 1) Chadema hawajamteua mbunge yeyote wa viti maalum kwenda bungeni 2) Wabunge 19 waliodai wameteuliwa "walijiteua wenyewe" 3) Kwa sababu hiyo, waliojiteua wamekiuka utaratibu wa chama na hivyo wamefukuzwa uanachama. Kwa upande wa 'walioteuliwa au waliojiteua', baada ya kuona kama wamefukuzwa chama, wakakata rufaa kwa ngazi ya juu ya chama. Kwa maoni yangu, kukata kwao rufaa ni ushahidi kwamba wanatambua kuwa wamefukuzwa uanachama na hiyo inawafanya pia wakose sifa ya kuwa wabunge wa chama cha siasa kama walivyokuwa wakidai kuwa wako bungeni kwa baraka za chama chao. Na rufaa hiyo ndiyo ingeweza kuwarudishia uanachama endapo kama ingetupilia mbali uamuzi wa chama. Alternatively, rufaa nyingine nje ya chama (mfano mahakamani), ingeweza pia kuwarudishia uanachama endapo ingetupilia mbali uamuzi wa chama. Kwa vile uamuzi wa A au B haujafanyika, bado uamuzi wa chama unabaki kama ulivyo.
 
hivi kuna ugumu gani CDM wakatimiza spika anacho waelekeza? Mbona jambo dogo sana hilo!
 
Kwa maoni yangu, hoja zao (za x na y) zinakinzana na ndiyo maana rufaa ina'make sense' kunapokuwa na hoja kinzani.
Ni kweli, ila mi naona CDM ndio wameamua kulifanya hili jambo kuwa story/habari ili watengeneze headlines & kufanya km nafasi ya kuendeleza popularity yao
 
hivi kuna ugumu gani CDM wakatimiza spika anacho waelekeza? Mbona jambo dogo sana hilo!
Spika hana mamlaka ya kuelekeza chama ambacho sio chake. Mamlaka yake yanaishia Bungeni. Aidha, barua inajibiwa kwa barua. Kama vile yeye alivyosema kuwa hana habari kuwa Lissu anaugua kwa sababu hajaandikiwa formal letter vile vile Katibu Mkuu wa Chadema hawezi kufanyia kazi kitu ambacho hakipo kwenye maandishi. Taratibu zinasema Spika alipaswa kujibu barua aliyoandikiwa akiweka sababu zinazomfanya ashindwe kuikubali. Hajafanya hivyo. Mbaya zaidi muda wote huu walikuwa wanajifanya hawajapokea barua yeyote kutoka Chadema. Na mbaya zaidi zaidi amesema hata akipewa hivyo viambatisho itabidi avipeleke kwanza kwa wataalamu wavichunguze na hata kama wataalam wakisema vikoja sahihi atachukua muda wake kufanyia kazi hiyo barua na hamna wa kumlazimisha afanye uamuzi haraka iwezekanavyo. Yote haya bado unataka Chadema waamini kuwa Spika anakusudia kutenda haki katika suala hili?

Chadema wako sahihi kumuacha afanye anachotaka maana hana mamlaka juu yao.

Amandla...
 
hivi kuna ugumu gani CDM wakatimiza spika anacho waelekeza? Mbona jambo dogo sana hilo!
Nyuma ya pazia kuna maswali yanayohitaji majibu kutoka kwa Viongozi wakuu wa CHADEMA:
1) Kwa nini suala hilo limeshikiwa bango na BAWACHA na siyo Kamati Kuu iliyowafukuza?
2) Kwa nini rufaa yao haisikilizwi?
3) Je, ruzuku ya hao Wabunge 19 CHADEMA inapokea?
 
Spika hana mamlaka ya kuelekeza chama ambacho sio chake. Mamlaka yake yanaishia Bungeni. Aidha, barua inajibiwa kwa barua. Kama vile yeye alivyosema kuwa hana habari kuwa Lissu anaugua kwa sababu hajaandikiwa formal letter vile vile Katibu Mkuu wa Chadema hawezi kufanyia kazi kitu ambacho hakipo kwenye maandishi. Taratibu zinasema Spika alipaswa kujibu barua aliyoandikiwa akiweka sababu zinazomfanya ashindwe kuikubali. Hajafanya hivyo. Mbaya zaidi muda wote huu walikuwa wanajifanya hawajapokea barua yeyote kutoka Chadema. Na mbaya zaidi zaidi amesema hata akipewa hivyo viambatisho itabidi avipeleke kwanza kwa wataalamu wavichunguze na hata kama wataalam wakisema vikoja sahihi atachukua muda wake kufanyia kazi hiyo barua na hamna wa kumlazimisha afanye uamuzi haraka iwezekanavyo. Yote haya bado unataka Chadema waamini kuwa Spika anakusudia kutenda haki katika suala hili?

Chadema wako sahihi kumuacha afanye anachotaka maana hana mamlaka juu yao.

Amandla...
Lets wait and see!
 
Nyuma ya pazia kuna maswali yayohitaji majibu kutoka kwa Viongozi wakuu wa CHADEMA:
1) Kwa nini suala hilo limeshikiwa bango na BAWACHA na siyo Kamati Kuu iliyowafukuza?
2) Kwa nini rufaa yao haisikilizwi?
3) Je, ruzuku ya hao Wabunge 19 CHADEMA inapokea?
Nadhani issue kubwa ni maslahi ndani ya chama.
 
Nadhani issue kubwa ni maslahi ndani ya chama.
Tangu wamefukuzwa ni muda mrefu na wanaendelea kushiriki shughuli za Bunge, lakini Viongozi walioamua wafukuzwe wamekaa kimya, kulikoni?

Kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA (2016), kukoma kwa uanachama kuna mkanganyiko mkubwa.
5.4.6 Kufukuzwa uanachama wa Baraza la Vijana au Wanawake au Wazee kwa utovu wa nidhamu.
5.4.7 Taarifa ya mwanachama aliyefukuzwa na Baraza ngazi husika itawasilishwa kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji cha ngazi hiyo na Kamati Kuu kwa ngazi ya Taifa.

Lakini leo BAWACHA wanadai wamewafukuza uanachama. Je, kwa nukuu hapo ya Katiba ya CHADEMA (2016), BAWACHA wana uwezo wa kuwavua uanachama au ni kuwavua uongozi na kama uanachama wamezingatia Katiba ya chama?
 
Tangu wamefukuzwa ni muda mrefu na wanaendelea kushiriki shughulu za Bunge, lakini Viongozi walioamua wafukuzwe wamekaa kimya, kulikoni?

Kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA (2016), kukoma kwa uanachama kuna mkanganyiko mkubwa.
5.4.6 Kufukuzwa uanachama wa Baraza la Vijana au Wanawake au Wazee kwa utovu wa nidhamu.
5.4.7 Taarifa ya mwanachama aliyefukuzwa na Baraza ngazi husika itawasilishwa kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji cha ngazi hiyo na Kamati Kuu kwa ngazi ya Taifa.

Lakini leo BAWACHA wanadai wamewafukuza uanachama. Je, kwa nukuu hapo ya Katiba ya CHADEMA (2016), BAWACHA wana uwezo wa kuwavua uanachama au ni kuwavua uongozi na kama uanachama wamezingatia Katiba ya chama?
1. Madai/maelezo ya BAWACHA ni kwamba wao hawajawavua uongozi bali wamevuliwa uanachama.

2. Spika kawaambia yeye hawezi kuwatafsiria katiba yao, hivyo ni wajibu wao kufuata & kutekeleza yaliyomo kwenye katiba yao
 
lissu alikuwa anajifanya kuwa kila mtu anajuwa kuwa anaumwa kumbe akasahau kuwa taarifa ya maandishi lazima halafu akawa anadanganya bado anaumwa huku anaendelea kuzurura ulaya na kuichafua nchi huyo mhuni
Acha kujitoa ufahamu wewe,wakati anapakiwa ndani ya ndege kupelekwa DSM Hadi Nairobi kwa matibabu,ndugai so alikuepo,?
Au alijipakia mwenyewe?
 
lissu alikuwa anajifanya kuwa kila mtu anajuwa kuwa anaumwa kumbe akasahau kuwa taarifa ya maandishi lazima halafu akawa anadanganya bado anaumwa huku anaendelea kuzurura ulaya na kuichafua nchi huyo mhuni
Mwenyezi Mungu ni fundi sana. Subirini atakapochukua spana zake, ndio mtajua virusi havilindwi na bunduki wala haitishwi kwa ubabe wa madaraka!
 
Spika wa bunge mh Job Ndugai hana tatizo na wabunge wa viti maalumu wa Chadema akina Halima Mdee na wenzake bali anachotaka ni utaratibu wa natural justice kufuatwa.

Kwa mujibu wa katiba ya Chadema Baraza kuu ndio lenye maamuzi ya mwisho ya kumvua mtu uanachama endapo hajaridhika na utaratibu wa awali.

Anachohoji Spika Ndugai ni kama wabunge hao akina Halima Mdee walipewa fursa ya kusikilizwa na kama ndio ameomba mihtasari ya vikao husika ili ajiridhishe na kuchukua maamuzi stahiki.

Ni vema JJ Mnyika akatoka na kuzijibu hoja za Spika Ndugai kwa mujibu wa katiba na siyo blah blah.

Mnyika aseme tu kwanini anasita kuitisha kikao cha baraza kuu ili kukata mzizi wa fitina?

Pia J J Mnyika aufahamishe Umma iwapo wabunge wote 19 hawakuridhika na maamuzi ya kamati kuu hivyo walikata rufaa au kuna baadhi waliridhika na maamuzi hayo kama alivyokiri mjumbe wa kamati kuu mh Jesca Kishoa.

Hili swala linatutia doa kama taifa ni vema likamalizwa sasa.

Tusisahau kufuatilia hotuba ya Rais Samia bungeni leo.

Kazi Iendelee!
Hao wabunge walikanwa na CHADEMA. Sasa kama CHADEMA imedai haikuwateua kuwakilisha CHADEMA swala la kufukuzwa siyo lazima liwe sababu kuu ya Ndugai kutowaondoa. Siyo kazi ya Ndugai kutafsiri katiba ya CHADEMA. Ndugai siyo mwanachama wa CHADEMA na haitii katiba ya CHADEMA.
 
Ndugai kuwa na ufahamu, unapowatetea hao uwe na kumbukumbu wengine uliwatendeaje, linganisha mwenyewe halafu tumia akili ya darasa la pili, usitumie elimu ya chuo kuchukuwa hatua!
 
Back
Top Bottom