Hoja ya Spika Ndugai: Nitawafukuzaje wabunge ambao Rufaa zao hazijasikilizwa na Baraza kuu kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,977
Spika wa bunge mh Job Ndugai hana tatizo na wabunge wa viti maalumu wa Chadema akina Halima Mdee na wenzake bali anachotaka ni utaratibu wa natural justice kufuatwa.

Kwa mujibu wa katiba ya Chadema Baraza kuu ndio lenye maamuzi ya mwisho ya kumvua mtu uanachama endapo hajaridhika na utaratibu wa awali.

Anachohoji Spika Ndugai ni kama wabunge hao akina Halima Mdee walipewa fursa ya kusikilizwa na kama ndio ameomba mihtasari ya vikao husika ili ajiridhishe na kuchukua maamuzi stahiki.

Ni vema JJ Mnyika akatoka na kuzijibu hoja za Spika Ndugai kwa mujibu wa katiba na siyo blah blah.

Mnyika aseme tu kwanini anasita kuitisha kikao cha baraza kuu ili kukata mzizi wa fitina?

Pia J J Mnyika aufahamishe Umma iwapo wabunge wote 19 hawakuridhika na maamuzi ya kamati kuu hivyo walikata rufaa au kuna baadhi waliridhika na maamuzi hayo kama alivyokiri mjumbe wa kamati kuu mh Jesca Kishoa.

Hili swala linatutia doa kama taifa ni vema likamalizwa sasa.

Tusisahau kufuatilia hotuba ya Rais Samia bungeni leo.

Kazi Iendelee!
 
Hoja kuu sio kufukuzwa. CHADEMA wanadai hawajawateua hao wabunge kupitia vikao vyao vya kikatiba. Hapo Mh Dugai mbona anapakwepa? Kufukuzwa likikuwa ni zao la kukiuka taratibu za chama.

Chama chao kimesema hakijawateua kwa kuwa hakuna vikao vilivyokaa. Mbona hakikusikilizwa? Vikao vya rufaa ndio muhimu sasa?

Hata kama utaratibu wa kuwafukuza haukufuatwa, lakini hilo la kuteuliwa na vikao ama la ni factual issue. Kwa hivyo hoja kuu ni kuwa hawakuteuliwa na Chadema kama sheria inavyotaka, hiyo ya kutokuwa wanachama wa chama cha siasa ni nyongeza ambayo haina athari kwenye hoja kuu.

Pathetic!
 
Mbowe mjanja sana!

Amemwambia spika awe anapiga danadana ili mambo yaende maana Mbowe ndio injinia hili sakata
 
Hao chadema wako very very selfish Yani wew mwanaume unapigania mwanamke afukuzwe kazi yake kisa wew huna that's very foolishness and stupidity, Spika kawajibu kwa hoja sana sana huwezi tu kumfukuza kazi mtu hivi hivi bila a fair justice never..
 
Hoja kuu sio kufukuzwa. CDM wanadai hawajawateua hao wabunge kupitia vikao vyao vya kikatiba. Hapo Mh Dugai mbona anapakwepa? Kufukuzwa likikuwa ni zao la kukiuka utaratibu za chama...
Hoja kuu yako inamuhusu Dr Mahera siyo Ndugai bwashee!
 
Back
Top Bottom