gspain
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 2,892
- 5,946
Mimi nadhani Chadema wanajivuta kusikiliza rufaa kwa sababu watakapoisikiliza tu na uamuzi unaotegemewa ukatolewa, wakata rufaa wataweza kwenda Mahakamani na Mahakama ina mamlaka ya kuzuia utekelezaji wa hukumu yeyote. Kwa maneno mengine, inaweza kusema wakina Halima watabaki kuwa wanachama wa CHADEMA na viongozi wa Bawacha mpaka kesi yao itakapoamuliwa. Wakishindwa hapo wanapanda Mahakama ya Rufaa na mara tayari 2025 na uamuzi bado. Wakina Halima wanajiuzulu Chadema na kujiunga na CCM na wanapewa ubunge wowote wanaoutaka. Mchezo umekwisha. Kwa hii danadana ni vigumu kwa wakina Halima kwenda Mahakamani.
Amandla...
Maelezo yako yana mantiki, possibly ndicho Chadema wanacho kikwepa.
Maana mahakama ikizuia utekelezaji wa kuvuliwa uanachama, baadhi ya covid-19 ambao ni wajumbe wa kamati kuu waendelee kuhudhuria vikao vya chama kama kawaida huku wakiwa mguu mmoja CCM na mguu mwingine CDM.