ndugu manyerere, kwa bahati mbaya, nyerere aliongea kuna audio nyingi sana zinazothibitisha kuwa alikuwa mshirikina sana sana. kuna siku alikuwa akihutubia wazee, akaeleza kuwa alishawahi kupelekwa kuchinja kondoo/mbuzi bagamoyo na maneno mengine kama hayo, AKAKIRI KUWA "KWENYE MASUALA HAYO NILIKUWA MTUNDU" kwa wale waliokwisha kusikiliza hotuba zake, amekiri kabisa kuwa alikuwa mtundu kwenye mambo ya kishirikina.
hata hivyo, si nyerere tu, hakuna kiongozi tz ambaye walau anaanzia kuwa mkurugenzi na kwenda juu....makatibu, mawaziri wote, wabunge wote, marais wote...hakuna hata mmoja ambaye sio mshirikina. pale ikulu kama wewe huna Mungu wa Ibrahim Isaka na Yakobo, ukienda kichwakichwa hata siku moja hauwezi kuishi. ni uchawi umejaa. tuache unafiki...
ukiona mtu anafichaficha kuongelea ukweli kuhusu uchawi, ujue yeye pia ni mshirikina tu. ndio maana hadi leo wachawi ukiongea nao huwa wanasema hakuna uchawi duniani ni uongo tu kumbe usiku wanawanga.