Hizi tetesi ni kweli kuhusu Nyerere?

Hizi tetesi ni kweli kuhusu Nyerere?

Zamani tunasadikishwa kuwa yule Mzee wetu JK wa kwanza (Mungu amlaze pema peponi) ,alikuwa ni mtaalamu sana wa hizi kamati za ufundi wa mambo ya asili ya mwafrika (uchawi).....

Zipo hadithi mbali mbali tulizokuwa tunasimuliwa kuhusu yeye kwamba:- alikuwa na saa/rada (vyovyote iwavyo) kila alipokuwa anataka kusafiri anakwenda kuiangalia, akikuta ina rangi nyeupe basi ilimaanisha kuwa safari yake ni nzuri....na kama cku hiyo akiikuta ina rangi nyekundu au nyeusi basi hasafiri maana safari hiyo itakuwa na mkosi....

Kuna uzushi mwingine kuwa eti hata kile kifimbo chake kilikuwa ni maalumu kwa ajili yake tu na wasimuliaji wakaenda mbali zaidi kwa kusema kuwa ipo walikuwa mkutanoni huko Arusha na baada ya mkutano kumalizika akakisahau mezani kile kifimbo watu wakajaribu kukiiba lakin kikagoma kung'oka pale mezani!!

Na watu wakazidi kudai kwamba eti hata kushinda kwa ile vita ya kagera kulichangiwa kwa kiasi kikubwa na zile kamati zake za ufundi........kuna hayo na madai mengine mengi tu sasa mi binafsi cjafahamu lolote ktk hayo kuna anaejua zaidi?
Katika ile vita nasikia kweli uchawi ulihusika sana na wanajeshi walijipatia umaarufu kwa maajabu waliokua wanafanya Kwa mfano Jen. Marwa aliitwa kambale eti akikamatwa na maadui alikua anateleza km kambale akawa hashikiki hivyo hivyo Mzee msuguri aliitwa mti mkavu Kwa umahiri wake wa kuwatoka maadui kimaajabu...wenye kufahamu habari hii atujuze zaidi maana nimesimuliwa tu na waliokuwepo enzi hizo ikiwa nimebakisha miaka mi3 kutoka kusikojulikana kuja duniani!!
 
nasikia yule mzee alikua ni mtata wanasema ata alipo kufa waligundua kwenye saa yake wanasema ilibadika rangi na wanasema kila raisi wa nchi hii lazima awe mkubwa wa wachawawi si unaona viongozi wetu wana mawazo ya kichawi chawi unakuta wanaongea vitu ambavyo havipo

Inawezekana japo hilo pia cjalithibitisha
 
Katika ile vita nasikia kweli uchawi ulihusika sana na wanajeshi walijipatia umaarufu kwa maajabu waliokua wanafanya Kwa mfano Jen. Marwa aliitwa kambale eti akikamatwa

Kuna moja ndio kali sasa......
Eti kuna ndege ya jeshi la Uganda ilikuwa ktk doria mpakani, basi mwalimu akafanya makeke na ghafla ile ndege ikawa na bendera ya Tz,basi lile jeshi la wahuni wa Uganda walipoiona wakaamua kuiwahi kuitungua kumbe ilikuwa ni ya kwao!!!
 
wamasema kwanza ile saa ilikua ni jini na ile fimbo ilkua ni jini na kuna jini alikua nalo kwa ajili ya kuongea ambolo lilikua linampa mawazo ndio maana mpaka leo hotuba za nyerere ukizikiliza leo unaona kama sio mtu wa kawaida wanasema kama kweli nyerere zile akili zilikua ni za kwake mwenyewe kikawaida binadamu huwa anavina saba kwanini hakuna mtoto wake hata mmoja alie lisi akili zake
 
Hivi wakuu ikitokea nikaanza kucheka kwa hii thread na baadhi ya michango ,nitaonekana nakamua chuchu za fisi?
 
Kuna moja ndio kali sasa......
Eti kuna ndege ya jeshi la Uganda ilikuwa ktk doria mpakani, basi mwalimu akafanya makeke na ghafla ile ndege ikawa na bendera ya Tz,basi lile jeshi la wahuni wa Uganda walipoiona wakaamua kuiwahi kuitungua kumbe ilikuwa ni ya kwao!!!

😀
Hii imenifurahisha zaidi!!
 
Nyerere alikuwa Mkatoliki safi tangu utoto. Karibu kila siku aliyokuwa Dar alikuwa hakosi kwenda kusali St. Peters.

Licha ya hilo, alielimika kiasi cha kujua kwamba kuwa Mkatoliki safi hakuna maana ya kutojihusisha na mila kabisa, after all alikuwa mtoto wa Chifu.

Kuna hotuba moja aliongelea jinsi alivyofukizwa makaburini kwa Jumbe Tambaza Upanga Dar es salaam. Huku wazee wa TANU wakinyunyiza damu ya Mbuzi aliyechinjwa na kumkemea kwa nuizo Gavana Sir Edward Twining ashindwe na Nyerere atupatie Uhuru.

Bila ya shaka alikubali matambiko haya kimila na kisiasa zaidi - alikuwa mgeni pwani, na wazee wa pwani ndio walimtaka kufanya matambiko haya, kulikuwa na haja ya kuonyesha umoja na kutojifanya msomi sana.

Nyerere will almost always be a legend in Tanzania. Hususan kwa sababu wabongo wanapenda sana habari za uchawi.

Kusema Nyerere alikuwa na nguvu za kichawi kunaonyesha Watanzania wanavyofikiri zaidi ya nguvu alizokuwa nazo Nyerere.
 
Zamani tunasadikishwa kuwa yule Mzee wetu JK wa kwanza (Mungu amlaze pema peponi) ,alikuwa ni mtaalamu sana wa hizi kamati za ufundi wa mambo ya asili ya mwafrika (uchawi).....

Zipo hadithi mbali mbali tulizokuwa tunasimuliwa kuhusu yeye kwamba:- alikuwa na saa/rada (vyovyote iwavyo) kila alipokuwa anataka kusafiri anakwenda kuiangalia, akikuta ina rangi nyeupe basi ilimaanisha kuwa safari yake ni nzuri....na kama cku hiyo akiikuta ina rangi nyekundu au nyeusi basi hasafiri maana safari hiyo itakuwa na mkosi....

Kuna uzushi mwingine kuwa eti hata kile kifimbo chake kilikuwa ni maalumu kwa ajili yake tu na wasimuliaji wakaenda mbali zaidi kwa kusema kuwa ipo walikuwa mkutanoni huko Arusha na baada ya mkutano kumalizika akakisahau mezani kile kifimbo watu wakajaribu kukiiba lakin kikagoma kung'oka pale mezani!!

Na watu wakazidi kudai kwamba eti hata kushinda kwa ile vita ya kagera kulichangiwa kwa kiasi kikubwa na zile kamati zake za ufundi........kuna hayo na madai mengine mengi tu sasa mi binafsi cjafahamu lolote ktk hayo kuna anaejua zaidi?

Mwenyewe umeshasema uzushi sasa sisi unataka tukusaidiaje?
 
uchawi ni mambo ya kufikirika wala hayana ukweli yani hayapo

Acha utani! ulisha wahi kulogwa? nilisha wahi kulogwa kila siku asubuh najikuta nipo juu ya tawi la mgomba siku nyingine naamka asubuh najikuta nipo ndani ya pipe la bomba la maji! Nilisha wekwa chini ya bahari wiki nzima bila kutoka juu! ndugu zangu mim naamini 100% uchawi upo
 
Mh......... Chini ya bahari...wiki nzima!!!
 
Umesahau na hii, Alimtoa kafara mwanae wakati wa vita ya kagera ili tushinde vita ile. Hii nayo inazungzwa sana huku mtaani
 
Huo wote ni uzushi tu. Mwalimu hakuwa na tabia za aina hiyo. Mwalimu alikuwa Mkristo Mkatoliki safi. Anaweza kuwa na upungufu wake, lakini kiimani alikuwa timamu kweli kweli. Lakini pia aliheshimu sana mila za asili.

Nakumbuka alishiriki maadhimisho ya mila za Kizanaki kama Wazanaki wengine. Alifanya hivyo kwa kuamini kuwa pamoja na dini za kimapokeo, bado Waafrika wana mila nzuri zinazopaswa kuenziwa. Huyo ndiye Mwalimu.
ndugu manyerere, kwa bahati mbaya, nyerere aliongea kuna audio nyingi sana zinazothibitisha kuwa alikuwa mshirikina sana sana. kuna siku alikuwa akihutubia wazee, akaeleza kuwa alishawahi kupelekwa kuchinja kondoo/mbuzi bagamoyo na maneno mengine kama hayo, AKAKIRI KUWA "KWENYE MASUALA HAYO NILIKUWA MTUNDU" kwa wale waliokwisha kusikiliza hotuba zake, amekiri kabisa kuwa alikuwa mtundu kwenye mambo ya kishirikina.

hata hivyo, si nyerere tu, hakuna kiongozi tz ambaye walau anaanzia kuwa mkurugenzi na kwenda juu....makatibu, mawaziri wote, wabunge wote, marais wote...hakuna hata mmoja ambaye sio mshirikina. pale ikulu kama wewe huna Mungu wa Ibrahim Isaka na Yakobo, ukienda kichwakichwa hata siku moja hauwezi kuishi. ni uchawi umejaa. tuache unafiki...

ukiona mtu anafichaficha kuongelea ukweli kuhusu uchawi, ujue yeye pia ni mshirikina tu. ndio maana hadi leo wachawi ukiongea nao huwa wanasema hakuna uchawi duniani ni uongo tu kumbe usiku wanawanga.
 
Back
Top Bottom