Hizi tetesi ni kweli kuhusu Nyerere?

Hizi tetesi ni kweli kuhusu Nyerere?

Zamani tunasadikishwa kuwa yule Mzee wetu JK wa kwanza (Mungu amlaze pema peponi) ,alikuwa ni mtaalamu sana wa hizi kamati za ufundi wa mambo ya asili ya mwafrika (uchawi).....

Zipo hadithi mbali mbali tulizokuwa tunasimuliwa kuhusu yeye kwamba:- alikuwa na saa/rada (vyovyote iwavyo) kila alipokuwa anataka kusafiri anakwenda kuiangalia, akikuta ina rangi nyeupe basi ilimaanisha kuwa safari yake ni nzuri....na kama cku hiyo akiikuta ina rangi nyekundu au nyeusi basi hasafiri maana safari hiyo itakuwa na mkosi....

Kuna uzushi mwingine kuwa eti hata kile kifimbo chake kilikuwa ni maalumu kwa ajili yake tu na wasimuliaji wakaenda mbali zaidi kwa kusema kuwa ipo walikuwa mkutanoni huko Arusha na baada ya mkutano kumalizika akakisahau mezani kile kifimbo watu wakajaribu kukiiba lakin kikagoma kung'oka pale mezani!!

Na watu wakazidi kudai kwamba eti hata kushinda kwa ile vita ya kagera kulichangiwa kwa kiasi kikubwa na zile kamati zake za ufundi........kuna hayo na madai mengine mengi tu sasa mi binafsi cjafahamu lolote ktk hayo kuna anaejua zaidi?

Ngoja Tuwaachie Waganga Na Watabiri Waliopo Humu Walisemee Na Sisi Watakatifu Tutulie Kimya!!!!!!!!
 
Hahahahaha Mkuu Sio Arusha Story ilitokea Sumbawanga kwa wakina Pinda kule Maana ndipo palisadikiwa kuwa na Uchawi mkubwa ukifuatiwa na Tanga japo Lindi na Mtwara ndio Balaa... huko sumbawanga Kifimbo kilipoachwa watu walikinyanyua wakashindwa wakaitwa Mapower yakashindwa ikaletwa Landlover wakafunga Minyororo wapi likaja Winchi nalo likashindwa ndipo wakamuita Rais mwenyewe na alipofika alikinyanyua tu na kukiweka Kwapani kilaini hahaha...

Ila Jamaa alikuwa anaogopewa sana na maneno mabovu yote alikuwa akipewa Kawawa kwa kutokusoma kwake... ilikuwa ni aibu alipokuwa akisafiri Nje ya nchi...
 
Viongozi wengi kote duniani lazima wana means of protecting themselves, Ikulu huwezi kaa hivihivi uongozi mamilioni ya watu, Usimwone kiongozi anakwenda kanisaani au msikitini ukasema huyu anamwabudu mungu tu, kuna Siri kubwa numa ya pazia, Ushawahi sikia Hirizi ya Simba, Akipewa kiongozi anatisha kama Simba, Akiingia mkutanoni watu wote humweshimu na kumsikiliza, Hivyo amini usiamini mambo hayo yapo!
 
Katika ile vita nasikia kweli uchawi ulihusika sana na wanajeshi walijipatia umaarufu kwa maajabu waliokua wanafanya Kwa mfano Jen. Marwa aliitwa kambale eti akikamatwa na maadui alikua anateleza km kambale akawa hashikiki hivyo hivyo Mzee msuguri aliitwa mti mkavu Kwa umahiri wake wa kuwatoka maadui kimaajabu...wenye kufahamu habari hii atujuze zaidi maana nimesimuliwa tu na waliokuwepo enzi hizo ikiwa nimebakisha miaka mi3 kutoka kusikojulikana kuja duniani!!

ya msuguri sijajua lakn jenerali Marwa yule alikuwa hatari aliweza kuongoza platoon tatu na kila platoon alionekana kama platoon kamanda.
 
mambo ya kiswahili yapo hata kule kwetu Tanga siku moja katk harakat zangu nilikuwa nimevaa viatu ya kutumbukiza na soksi hatimae ile nshtuka nakuta soksi hakuna bana
 
mambo ya kiswahili yapo hata kule kwetu Tanga siku moja katk harakat zangu nilikuwa nimevaa viatu ya kutumbukiza na soksi hatimae ile nshtuka nakuta soksi hakuna bana

Duuh...hiyo hatariii!!
 
mtoa mada hauko serious. kwanini hakuenda kuangalia hiyo rada kabla hajapanda ndege kwenda london? maana kule ndo alimalizwa kirahisi
 
Nyerere alikuwa Mkatoliki safi tangu utoto. Karibu kila siku aliyokuwa Dar alikuwa hakosi kwenda kusali St. Peters.

Licha ya hilo, alielimika kiasi cha kujua kwamba kuwa Mkatoliki safi hakuna maana ya kutojihusisha na mila kabisa, after all alikuwa mtoto wa Chifu.

Kuna hotuba moja aliongelea jinsi alivyofukizwa makaburini kwa Jumbe Tambaza Upanga Dar es salaam. Huku wazee wa TANU wakinyunyiza damu ya Mbuzi aliyechinjwa na kumkemea kwa nuizo Gavana Sir Edward Twining ashindwe na Nyerere atupatie Uhuru.

Bila ya shaka alikubali matambiko haya kimila na kisiasa zaidi - alikuwa mgeni pwani, na wazee wa pwani ndio walimtaka kufanya matambiko haya, kulikuwa na haja ya kuonyesha umoja na kutojifanya msomi sana.

Nyerere will almost always be a legend in Tanzania. Hususan kwa sababu wabongo wanapenda sana habari za uchawi.

Kusema Nyerere alikuwa na nguvu za kichawi kunaonyesha Watanzania wanavyofikiri zaidi ya nguvu alizokuwa nazo Nyerere.

Ni kweli kuacha mila ni kupotoka.....hata kile kifimbo si uchawi na inasemekana alipewa na Bibi kule kwetu Kolero.....!
 
Huo wote ni uzushi tu. Mwalimu hakuwa na tabia za aina hiyo. Mwalimu alikuwa Mkristo Mkatoliki safi. Anaweza kuwa na upungufu wake, lakini kiimani alikuwa timamu kweli kweli. Lakini pia aliheshimu sana mila za asili.

Nakumbuka alishiriki maadhimisho ya mila za Kizanaki kama Wazanaki wengine. Alifanya hivyo kwa kuamini kuwa pamoja na dini za kimapokeo, bado Waafrika wana mila nzuri zinazopaswa kuenziwa. Huyo ndiye Mwalimu.

Tena ukatoliki ndio upagani wenyewe ndugu.Watchout
 
Kuhusiana na kifimbo , niliwahi kusoma mahojiano ya mama Maria Nyerere akisema kwamba Mwalimu alivyoacha kuvuta sigara alianza kushika kifimbo kama njia ya kucope na withdrawal
 
Hahahahaha Mkuu Sio Arusha Story ilitokea Sumbawanga kwa wakina Pinda kule Maana ndipo palisadikiwa kuwa na Uchawi mkubwa ukifuatiwa na Tanga japo Lindi na Mtwara ndio Balaa... huko sumbawanga Kifimbo kilipoachwa watu walikinyanyua wakashindwa wakaitwa Mapower yakashindwa ikaletwa Landlover wakafunga Minyororo wapi likaja Winchi nalo likashindwa ndipo wakamuita Rais mwenyewe na alipofika alikinyanyua tu na kukiweka Kwapani kilaini hahaha...

Ila Jamaa alikuwa anaogopewa sana na maneno mabovu yote alikuwa akipewa Kawawa kwa kutokusoma kwake... ilikuwa ni aibu alipokuwa akisafiri Nje ya nchi...

saga tu hyo
 
Back
Top Bottom