Hizi sio ndoto za kawaida

Mshana nasumbuliwa na hizi ndoto
1.kuota mara kwa mara nipo shule ya msingi nafanya mtihani na classmates wenzangu ambao nilisoma nao miaka zaidi ya 15 iliyopita wakati tayari nmeshamaliza chuo.
2.Kuota nakula vyakula mbalimbali ila si nyama
3.Kuota nakimbizwa na Simba,au mtu(watu) wenye hasira kali
4. Mara kadha natokewa na rafiki ambaye sasa ni marehemu..,
Namba moja na namba nne huwa naziota sana akikujibu naomba nitag mkuu
 
niwe tu mkweli, mimi sijawahi kuamini katika ndoto kabisa kwa sababu kuna wakati naweza kaa hata wiki mbili sijaota chochote na hata nikiota ni mambo tu ambao huwa hayamake sense hasa yale marudio ya vitu ambavyo naexperience katika maisha ya kila siku, siku nitakayoamini kuwa ndoto ina maana ni pale itakapojirudia zaidi ya mara moja vile vile bila kubadilika chochote ila ikiwa leo hivi kesho vile nitaipotezea tu.

aim for the stars
 
Kuna rafiki yangu mmoja alifariki mwaka 2017

Huwa namuota mara kwa mara katika mazingira ya huku ulimwenguni, hii inaashiria nini mkuu?
Alifariki katika mazingira gani? Wakati wa kufariki mlikuwa na mawasiliano ya karibu?
Kuna wakati memory ya kitu fulani huganda na ku stick sehemu moja bila sababu zingine zozote

Jr
 
Mshana nasumbuliwa na hizi ndoto
1.kuota mara kwa mara nipo shule ya msingi nafanya mtihani na classmates wenzangu ambao nilisoma nao miaka zaidi ya 15 iliyopita wakati tayari nmeshamaliza chuo.
2.Kuota nakula vyakula mbalimbali ila si nyama
3.Kuota nakimbizwa na Simba,au mtu(watu) wenye hasira kali...
Ndoto zako nyingi ni za mapambano ya kimaisha
Ukiota uko shule maana yake ni kwamba kuna jambo hujalimaza ama kuna hatua fulani hujaivuka
Ndoto za kuwa chini ya mwembe ni ishara ya amani na shibe kwakuwa mwembe huleta kivuli na pia hutoa matunda mazuri yafaayo kuliwa
Ndoto za Simba ni ukakamavu na ushindi kwenye harakati zako za maisha.. Imagine uote unafukuzwa na konokono
Lakini kumbuka pia ni lazima tuote na baadhi ya ndoto huwa hazina tafsiri moja

Jr
 
Mtumishi wa mambo ya giza giza mimi huwa naota nagonga misosi misosi naiti kali... ni njaa inanisumbua ama nini?
 
Mshana Jr ndoto ni uongo na kuamini kisichokuwepo sawa na utabiri wa nyota kwa nini tuendelee kutoa maelezo ya jambo lisilo na uhalisia au just for coincidence in real life

Ukiamini ndoto unaamini hakuna Mungu
 
Ukiamini ndoto unaamini hakuna Mungu..!!! Hapa hukuwaza wema au huna uelewa wa kutosha

“Wanaodhania ya kuwa wanawasahaulisha watu wangu jina langu kwa ndoto zao, wanazomhadithia kila mtu jirani yake, kama vile baba zao walivyolisahau jina langu, kwaajili ya baali. Nabii aliye na ndoto, na aseme ndoto yake; na yeye aliye na neon langu, na aseme neon langu ka uaminifu. Makapi ni kitu gani kuliko ngano? Asema Bwana. Yeremia 23:27-28

Jr
 
Mshana Jr ndoto ni uongo na kuamini kisichokuwepo sawa na utabiri wa nyota kwa nini tuendelee kutoa maelezo ya jambo lisilo na uhalisia au just for coincidence in real life

Ukiamini ndoto unaamini hakuna Mungu
“[Nabii wa Mungu] Danieli aliona ndoto . . . kitandani mwake. Ndipo akaandika ndoto hiyo; akasimulia masimulizi kamili ya mambo hayo.”—Danieli 7:1.

Jr
 
“[Nabii wa Mungu] Danieli aliona ndoto . . . kitandani mwake. Ndipo akaandika ndoto hiyo; akasimulia masimulizi kamili ya mambo hayo.”—Danieli 7:1.

Jr
Safi sana
Umeeleza ndoto kama ufunuo wa mungu na si kama kazi ya ubongo

Hapa jukwaan tunaeleza ndoto za Mungu au kazi ya ya ubongo?

Tunaifafanua ndoto kama ufunuo wa Mungu kwa watu au ndoto kama mawazo ya utendaji wa mwanadamu unaongozwa na utashi!

Ybs 34:1-8 alishaonya
Pitia hapo

Na ndiyo maana yesu alipofika hakukuta wayaudi wamebaki kwenye ndoto, uchawi au utabiri wa nyota isipokuwa mafundisho ya manabii ambayo ni ufunuo wa Mungu kwa njia ya ndoto nk
 
Safi sana
Umeeleza ndoto kama ufunuo wa mungu na si kama kazi ya ubongo

Hapa jukwaan tunaeleza ndoto za Mungu au kazi ya ya ubongo?...
Ramark Bible ni kitabu chenye ufunuo wa ki Mungu ndio maana ili ukisome vizuri na kukielewa angalau nusu yake inahitaji miaka mine... Ukiwa mtu wa kudonyoa donyoa tu vifungu kuna mahali hutapaelewa

Jr
 
Niliota Siku chache nipo kwenye barabara ya lami mahali fulani katikati ya mji na nikamuona hasimu wangu kibiashara anakuja nyuma yangu punde nageuka kulia kwangu ng'ambo ya barabara naona maji mengi na mawimbi makubwa sana yamefunika mpaka magorofa cha ajabu maji hayavuki upande wa pili kabisa nikawa naogopa sana,

kidogo yule hasimu wangu akanisogelea na kuniuliza vp waelekea wapi na huyaoni hayo maji? sikumjibu ila natetemeka nikaanza kukimbia ila kule ninakolekea ndo maji yanazidi .
Niliamka nikajikuta naingia kwenye sala haraka sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom