Hizi sio ndoto za kawaida

wainga

Member
Mar 30, 2017
53
125
Mkuu mimi kuna wakati nilikuwa naota nyoka wananitambaa mwilini mpaka nasisimka kwa hofu, sijuwi hiyo ndoto inamaanisha nini?
Ya pili ni hii,naota naporomoka kutoka katika maporomoko ya maji na kwenda mpaka chini,ndoto hiyo nayo inamaanisha nini mkuu?
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
170,195
2,000

Nyoka ni ulinzi wa kiroho... Hayo maporomoko sio ile udenda kweli? Lakini kuna Wakati roho zetu hututoka na kwenda kuivinjari dunia huko hukutana na milima na mabonde
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
170,195
2,000
Habari mshana Jr
Nimeota njozi moja sijui maaana yake
Nilikua nimelala na mpenzi wangu na nikaota nachunga wanyama wengi sana ila katika hao wanayama kuna mbuzi na mtoto wake mweupe wamenisumbua sana , nikawachapa sana mpaka wakashindwa kutembea...
Mbuzi ni mnyama msumbufu na asiyetulia kuna mambo yanakuzonga na bado hujayapatia ufumbuzi
 
kamituga

JF-Expert Member
May 31, 2019
1,199
2,000
Mkuu mimi kuna wakati nilikuwa naota nyoka wananitambaa mwilini mpaka nasisimka kwa hofu, sijuwi hiyo ndoto inamaanisha nini?
Ya pili ni hii,naota naporomoka kutoka katika maporomoko ya maji na kwenda mpaka chini,ndoto hiyo nayo inamaanisha nini mkuu?
Hizo ndoto zote zina mahusiano

1.tuanze kwa kujua tafasiri ya vitu ulivyo viona
a) nyoka- kibiblia ni shetan
Sasa unapo ona nyoka amekuzunguka kuna uwezekano umezungukwa na maroho machafu ya shetani ktk maisha yako

2.unaota huko juu alafu unaanguka mpka kwenye maji
b) maji ni dunia
Sasa ndoto yako ikiwa Ina maana kuna anguko ktk uchumi wako ambalo linatokana na roho chafu ulizotumiwa kushambulia maishaa yako kutoka juu mpka chini uko uliko anguka

Ndoto uwa zinaleta taarifa ya mambo yaliopo au yatakayo kuja badae na ukiona unatakiwa kuchukua hatua za kiroho kuzuia ayo mashambulizi yasije kwenye mwili

Angalia khali yako ya kiuchumi tangu umeanza kuota izo ndoto ukilinganisha na kabla ya hapo utapata majibi.
 
kamituga

JF-Expert Member
May 31, 2019
1,199
2,000
Mara unaota umekamatwa mateka unaenda kuuwawa! Mara niote nimeangusha mtoto! Mara yaani am very frustrated
Tuanze kwanza kwa kujua maana ya mambo ulio yaona kwenye ndoto kibiblia km ni mfuasi wa bible lakini.

Mtoto-bahati
Chui - adui
Sasa kwenye iyo ndoto kuna mambo ambayo ukija kuangalia kwenye maisha yako yawezekana yanaendelea au yatakuja kutokea kwa baadae.

Kuna vita inaendelea kwenye maisha yako unaweza kukuta ni sehemu ya kazi au biashara na watesi wako wanataka wakuteke usifulukute kabisa na iyo khali ni mbya inaamaana nafsi yako inapokua imekamatwa mateka na ulimwengu wa Giza akuna ambacho kita fanikiwa kwako na unapoota unadodosha mtoto ina maana bahati au kitu kizuri Una poteza na hiii ni kutokana na mashambulizi ya vita izo ulizo kua unapigana ndio chanzo cha kupoteza bahati kifupi unashambuliwa na ulimwengu wa Giza.
 
Dinazarde

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
39,575
2,000
Ni kweli kabisa

Jr

mim juzi nimeota nna mimba naumwa uchungu nataka kujifungua lakin mtoto hatoki mara niondoke hospital nikampumzike kisha nikiumwa naaanza kutafuta hospital nyingine huduma hakuna uchungu unaniuma huku damu zikimwagika nikawa natamani iwe ndoto nilivyoshtuka asubuji nilishuruku
Sasa sijui ina maana gani sijui natamani sana mtoto
 
BabaDesi

JF-Expert Member
Jun 30, 2007
4,292
2,000
...Mkuu Mshana, kuna wakati kama miaka minne\mitano nyuma ilikuwa kila wiki Mara moja ama mbili no lazima niote kuhusu ajali ya ndege kuanguka bila Mimi kuwrmo katika ndege hizo Bali inatokea kama nipo tu njiani na ninaona ndege inaruka na ninajisemea tu kuwa ndege ile itaanguka na kweli inakuwa hivyo!

Ajabi ni kuwa baada ya ndege kuanguka tu basis ndoto inaishia japo bila kuona majeruhi ama maiti kutokana na ajali hiyo!

Miaka ya karibuni ndoto za kuiota ndoto hiyo zimepungua kasi ingawaje ni vigumu sana kupitisha mwezi mzima bila kuiota!

Niseme tu pia kwamba hakuna jambo lolote LA ziada ambalo limetokea kwenye ratiba ya maisha yangu ambalo lingeweza kunifanya nidhani kwamba labda ni kutokana na ndoto yangu hii, pamoja na kwamba bado ninaendelea kuiota japo kasi ya kuiota imepungua lakini haipotei moja kwa moja!
Haya utasemaje Mkuu Mshana...?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Koffi Annan

JF-Expert Member
Dec 23, 2018
781
1,000
Mara nyingi huwa naota napita mahali kisha nakua sioni macho au naona kwa shida sana
Au nataka kuvuka barabara au nakimbizwa na kitu ila miguu inatembea kwa tabu sana. Najivuta mda mwingine natambaa ila huwa nafika ninapotaka kufika japo kwa shida na nikishtuka nakua hadi roho inauma kwa nini nashindwa kutembea au kuona.
Ndoto hizi naota tokea nikiwa mdogo hata jana pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
170,195
2,000
mim juzi nimeota nna mimba naumwa uchungu nataka kujifungua lakin mtoto hatoki mara niondoke hospital nikampumzike kisha nikiumwa naaanza kutafuta hospital nyingine huduma hakuna uchungu unaniuma huku damu zikimwagika nikawa natamani iwe ndoto nilivyoshtuka asubuji nilishuruku
Sasa sijui ina maana gani sijui natamani sana mtoto
Ukiachana na la kupata mtoto kuna mambo unayafanya lakini hayafikii tamati

Jr
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
170,195
2,000
mim juzi nimeota nna mimba naumwa uchungu nataka kujifungua lakin mtoto hatoki mara niondoke hospital nikampumzike kisha nikiumwa naaanza kutafuta hospital nyingine huduma hakuna uchungu unaniuma huku damu zikimwagika nikawa natamani iwe ndoto nilivyoshtuka asubuji nilishuruku
Sasa sijui ina maana gani sijui natamani sana mtoto
Ukiachana na swala la hamu ya kupata mtoto kuna mambo huyakamilishi ama hayakamiliki pamoja na kuyaanza vema

Jr
 
Abby Newton

JF-Expert Member
Nov 12, 2017
1,196
2,000
Ukiachana na swala la hamu ya kupata mtoto kuna mambo huyakamilishi ama hayakamiliki pamoja na kuyaanza vema

Jr
Mshana nasumbuliwa na hizi ndoto
1.kuota mara kwa mara nipo shule ya msingi nafanya mtihani na classmates wenzangu ambao nilisoma nao miaka zaidi ya 15 iliyopita wakati tayari nmeshamaliza chuo.
2.Kuota nakula vyakula mbalimbali ila si nyama
3.Kuota nakimbizwa na Simba,au mtu(watu) wenye hasira kali
4. Mara kadha natokewa na rafiki ambaye sasa ni marehemu.
5.Mara nyingi naota nipo chini ya mwembe mkubwa nikiwa na rafiki zangu wa utotoni,tukiwa tunachuma maembe. Wakati mwingine tukiwa juu ya mti Simba hutokea chini ya mti na kuanza kupanda kutufuata,lakini hunifuata hasa mimi mwisho naishia kushituka.
5.Mara chache pia huwa naota niko kwenye uwanja wa vita nikiwa na wanajeshi wengi.

Najitahidi kuomba kila ninapolala lakini baada ya mda inajirudia tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom