Hizi ni hoja zilizoibuka mara tu baada ya Kikwete kumaliza hotuba yake! Wewe una hoja gani?

nilichokiona rais hakuja kuhutubia bunge ama kuzindua bali alikuja kumjibu Warioba na kuonyesha msimao wa ccm.nilitarajia yy kama kiongozi wa nchi kutoonyesha upande bali jukumu lingeeachwa kwa wajumbe kulumbana kwa hoja ili kutupa katiba ya kuwafaa watanzania
 
mambo manne:-


1. nadhani maoni ya Raisi yamechelewa, kwasababu hatua hiyo imeshafanywa. na sidhani ilikuwa ni jambo la busara kutoa maoni yake, akijua kabisa kwamba kwa nafasi yake maoni yake yanaweza kufunika maoni ya watu wengine wote, hasa majority.


2. kwanini Tume imewakilisha sample ya kura za watu wachache, na kujichanga, kuna tofauti kubwa sana kati, "ASILIMIA 60 YA WAZANZIBAR" na "ASILIMIA 60 YA WAZANZIBARI WALIOPIGA KURA" tofauti ya namba kati ya hizo sentensi mbili ni KUUUUBWA MNO.


3. ILI kuondoa mizizi ya fitina, kwanini tusipige kura ya maoni (kila mtu apige) nchi nzima, kwenye polling stations (vituo vya kupigia kura, ili tuwe na rekodi sahihi kabisa, ili hapo mbele watu wasijisikie kama vile walifanyiwa uhuni. kura za kule CRIMEA jumapili iliyopita.


4. Serikali tatu zinawezekana, GREAT BRITAIN ina nchi nne, Northern Ireland, Scotland, England na Wales. hizi nchi zote zina nyimbo yao, bendera yao, wanachagua mashindano ya pamoja na wanachagua mashindano ya kitaifa. WIZARA NYETI (kama ulinzi na fedha) ZINAUNDWA PAMOJA, na Wizara ndogo kama education na locality, zinasimamiwa na nchi moja moja kivyake.


Watanzania tusitake kufanya mambo yawe magumu, hivi vitu vimefanyika na tunaweza kuiga mambo mazuri.
 
Tanganika bado kuna Ibada za wafu na Watu wanakwenda kuomba na kulia kwenye kaburi la Nyerere. Kwa kifupi Nyerere ni nabii kwa baadhi ya watanganyika.

Ila kwangu mimi binafsi Nyerere ni kama mjumbe wa Mwenyezi Mungu aliyeasi maagizo ya Mungu.
Ni kama nabii Yona(Yunus).Alitumwa kwa Watu wa ninawi akakimbilia Tarashishi akamezwa na samaki.
Nyerere alitumwa kwa WATANGANYIKA akaasi na kutamani kuichukua Zanzibar,East Afrika na Afrika Nzima. Akamezwa na samaki(ZANZIBAR)4

Nyerere Hakufanana kabisa kama Manabii watiifu:
Mfano Musa kwa wana Waisrael tu.Issah kwa Waisrael, walipomkataa ndo akaenda kwa wengine,Muhammad( Nabii wa haki) kwa watu wa lugha yake ili aeleweke vizuri.Baada ya kufanya vizuri kwa watu wake ndipo waliowafuata waliamua kutangaza mema yao kwa mataifa mengine tena baada ya wao kuondoka.
Sasa Nyerere aliamua kupiga Mruzi akiwa na maji mdomoni.Nyerere ni mjenzi (mason) aliyejenga nyumba kila eneo mpaka kwenye MCHANGA bila kuwa na uwezo wa kujenga misingi imara;matokeo yake ni baadhi ya majengo kusombwa na maji na mengine ukarabati wa kila siku na kusaba gharama kubwa.

Japo Umemtusi Nyerere kiaina Lakini Moyoni unamkubali .najua lazima utakuwa ni Mzanzibar wewe . Jaribu kuchunguza kiundani utabaini Nyerere aliwaletea Muungano wenye kuwapendelea Nyie wana Visiwa wahamiaji Enzi za Utumwa wa kiaraabu . Kwani wanaofaidi Matunda ya muungano ni Wazanzibar wana wabunge wengi kwenye Visiwa vidogo wana baraza la wakilishi wabunge wao wanavuna posho zenji na Dodoma Pesa ya kuwalea inatoka Tanganyika yote Wao chao ni chao lakini cha Tanganyika ni cha wote . Wazanzibar wengi wanamshukuru Nyerere kwa muungano huu ,ambao umewafanya wao waishi Tanganyika na kumiliki Ardhi na nyumba huku Watanganyika hawaruhusiwi kumiliki Ardhi Zanzibar .
 
Ndugu zangu Watanzania;
Kama nilivyoeleza, nimeona yafuatayo katika hotuba ile:
(1) Mh. Rais alijua tangu mwanzo kabla ya kuunda tume ya Warioba kuwa ni nini alitaka kukifanya kwa habari za wale waliokuwa wanalilia katiba mpya.
(2) Mh. Rais aliamua kwa moyo wake bila woga kuiingiza nchi katika hasara kuubwa ya kuiunda kamati ya Warioba na kuwapa uhuru wa kuizunguka Tanzania nzima kumbe ni kiini macho tu kwamba alitaka kupata maoni ya Watanzania kumbe mhhh.
Nayasema hayo kwa sababu zifuatazo:
Haiwezekani, hata kabla ya Hotuba ya Warioba Bungeni, tayari CCM ilikuwa imekwisha toa msimamo wa kuiponda na akaja M/Kiti wake akaiponda vivyo hivyo. Ule msimamo wa CCM ndio msimamo wa Rais aliyeiteua hiyo tume ya Warioba.
Jingine ni kwamba; Sababu zoote alizozitoa Rais hakuna hata moja yenye mashiko kuhusu kwa nini Zanziba wao tu wawe na uwezo wa kuwa nchi huru na utaifa wao, ati Tanganyika ijinyamazie kwa kuwa ati ni nchi kubwa kuliko Zanziba. Haiingii akilini kwamba mimi kuitwa Mtanganyika ni ujinga ila Mzenj kuitwa Mzanzibari ni fahari. Nasema, haingii akilini.
Haiingii akilini kuwa, ni gharama sana kuendesha serekali 3 ili Tanganyika ionekane kwenye huo muungano, lakini nchi ndogo ka Zanziba iweze kuiendesha serekali yake iliyo jiundia yenyewe nje ya muungano. Wao wana uwezo gani sisi Tanganyika hatuuwezi? Wao wana mbinu gani sisi hatutaziweza?
Kwa nini tusiamini kuwa Tanganyika tumepumbazwa na neno Tanzania ili Zanziba wasichangie chochote kwani wanasema hayo ni ya kwao sisi tujue yetu? Kwa nini, wizara zisizo za Muungano ziongozwe na wazenj wakati Tanganyika tunao watu wenye uwezo mkuubwa tu wasizipewe wakati kule Zenj wao hakuna hata msaidizi kutoka Tanganyika?
Kwa nini ilikuwa ngumu sana kwa JK kulitamka hata hilo jina Tanganyika ila rahisi kwake kutamka Zanziba?
Nashauri Bunge hilo livunjwe kwani tunajadili kitu kisichokuwepo. Katiba inaitwa ya muungano huku Zanziba hawajui waliungana na nani. Nasema hakuna nchi iitwayo Tanzania Bara. Kama serekali tatu ni gharama, basi gharama inayotumika kuendesha serekali ya Zanziba iingizwe kwenye pato la taifa. Tuvunje hiyo serekali tuwe na serekali moja na Taifa moja lililoundwa na nchi 2 Tanganyika na Zanziba.
Kinacho nitisha nikwamba wanazani watanganyika niwajinga na wataukubali ujinga huu
 
SHIKAMOO SAIDI KUBENEA!!! LEO
KWENYE KIPINDI CHA STAR TV
TUONGEE ASUBUHI
KUBENEA WA -----------
AMEJADILI NA KUULIZA MASWALI
YANAYOFANANA NA HAYA KUHUSU
HOTUBA YA RAIS JANA.
# kama tume ya Rais ya mabadiliko
ya katiba chini ya Jaji JOSEPH SINDE
WARIOBA hikuwa sahihi mbona
ilikuhusisha kila hatua waliyofikia,na
hukusema chochote zaidi ya
kuwaamuru waendeleee???
# Na kama ofisi ya waziri mkuu
iliyochini yako ilitoa maoni
yanayofanana na yaliyopo kwenye
tume ya mabadiliko ya katiba " yaani
serikali 3" unawezaje kuyakataa kiasi
hicho, au unataka kutuambia kuwa
taasisi za serikali pia zilikusaliti? ama
hazijui chochote kuhusu changamoto
za muungano???
# Pia kama mshauri mkuu wa Tume
kuhusu mapato ya serikali hasa
kwenye ,muundo wa muungano wa
serikali 3 ni mamlaka ya mapato
Tanzania yaani "TRA" ambao ni
wataalamu wetu kwenye mambo ya
mapato ,wewe mh,umeshauriwa na
akina nani kuhusu mapato ?? na
kama ni hao hao TRA kwanini
wamekupa ushauri tofauti na
Walioipa tume??? ukizingatia
umeonyesha hofu kubwa kwenye
suala la mapato ya serikali3??
#Na kama wewe na chama chako
kama ulivyosema jana mnaamini
serikali 2 mpaka hatua hii ambayo
muda wa kutoa maoni kwa mujibu wa
sheria ya mabadiliko ya katiba
umepita hamunoni mnaingilia maoni
ya wananchi kwa kutumia nafasi yenu
kuwa madarakani???
# Lakini pia jana ulionyesha hofu
kuwa inawezekana kwa muundo wa
serikali 3 wanajeshi na polisi kuasi
labda kwasababu wanadai mishahara
yao au posho zao, ukiwa umesahau
kuwa Jeshi la polisi linamadai
makubwa kuliko walimu kwenye
muungano huu wa serikali 2 lakini
hawajapindua. eti mh unasemaje
kuhusu hili???
# Na kwanini jana umekwenda
kulihutubia bunge kama mjumbe wa
bunge maalumu la katiba na sio
kufungua bunge kama tulivyotaarifiwa
kwani ulikwenda kuichambua
Rasimu,na kuna umuhimu gani Bunge
kuwepo kama umeshaelekeza mambo
yanavyopaswa kufanyika?? si
waondoke ukae na watu wachache
ikulu mtengeneze katiba tuepushe
gharama zisizo na maana ??
# Mwisho umetutisha kuwa serikali 3
zinaweza kusababisha jeshi kupindua
na wanajeshi kuongoza nchi na
baadae kuvua magwanda na
kugombea Urais, umesahau kuwa
wewe pia ni Luteni wa jeshi uliyevua
magwanda na kugombea Urais ??? na
tena kwa mujibu wa katiba yetu wewe
ni mkuu wa vikosi vyote nchini???
tatizo liko wapi?? mpaka ututishe???
Nakushauri mh,ufute kauli zako za
jana ili mchakato uendeleeb kwa
uhuru zaidi!

Sasa Unataka Nini Tena Zaidi Ya Ukweli Huo? Na Kwa Kuongezea tu Hakuwepo Peke Yake bali Alikuwepo Na Mwandishi Mtani Wangu Wa Kihaya Bwana Balile na Wamechambua Vizuri Mno Issues na Upuuzi Wa Hotuba Ya MJOMBA Jana. Hakika Kubenea na Balile Leo Wamenifanya Nisikie Furaha na Wamenikuna. Hawaogopi, Wakweli na Wanajiamini. Nimewafuatilia Mwanzo Mwisho huku Dotto Bulendu Akikandamiza Kwa Logic Analysis Zake. MJOMBA Amejishusha Thamani Jana na Amejidhalilisha na Kutuonyesha Uwezo Wake Butu wa Kufikiri na Kuona Mambo.
 
SHIKAMOO SAIDI KUBENEA!!! LEO
KWENYE KIPINDI CHA STAR TV
TUONGEE ASUBUHI
KUBENEA WA -----------
AMEJADILI NA KUULIZA MASWALI
YANAYOFANANA NA HAYA KUHUSU
HOTUBA YA RAIS JANA.
# kama tume ya Rais ya mabadiliko
ya katiba chini ya Jaji JOSEPH SINDE
WARIOBA hikuwa sahihi mbona
ilikuhusisha kila hatua waliyofikia,na
hukusema chochote zaidi ya
kuwaamuru waendeleee???
# Na kama ofisi ya waziri mkuu
iliyochini yako ilitoa maoni
yanayofanana na yaliyopo kwenye
tume ya mabadiliko ya katiba " yaani
serikali 3" unawezaje kuyakataa kiasi
hicho, au unataka kutuambia kuwa
taasisi za serikali pia zilikusaliti? ama
hazijui chochote kuhusu changamoto
za muungano???
# Pia kama mshauri mkuu wa Tume
kuhusu mapato ya serikali hasa
kwenye ,muundo wa muungano wa
serikali 3 ni mamlaka ya mapato
Tanzania yaani "TRA" ambao ni
wataalamu wetu kwenye mambo ya
mapato ,wewe mh,umeshauriwa na
akina nani kuhusu mapato ?? na
kama ni hao hao TRA kwanini
wamekupa ushauri tofauti na
Walioipa tume??? ukizingatia
umeonyesha hofu kubwa kwenye
suala la mapato ya serikali3??
#Na kama wewe na chama chako
kama ulivyosema jana mnaamini
serikali 2 mpaka hatua hii ambayo
muda wa kutoa maoni kwa mujibu wa
sheria ya mabadiliko ya katiba
umepita hamunoni mnaingilia maoni
ya wananchi kwa kutumia nafasi yenu
kuwa madarakani???
# Lakini pia jana ulionyesha hofu
kuwa inawezekana kwa muundo wa
serikali 3 wanajeshi na polisi kuasi
labda kwasababu wanadai mishahara
yao au posho zao, ukiwa umesahau
kuwa Jeshi la polisi linamadai
makubwa kuliko walimu kwenye
muungano huu wa serikali 2 lakini
hawajapindua. eti mh unasemaje
kuhusu hili???
# Na kwanini jana umekwenda
kulihutubia bunge kama mjumbe wa
bunge maalumu la katiba na sio
kufungua bunge kama tulivyotaarifiwa
kwani ulikwenda kuichambua
Rasimu,na kuna umuhimu gani Bunge
kuwepo kama umeshaelekeza mambo
yanavyopaswa kufanyika?? si
waondoke ukae na watu wachache
ikulu mtengeneze katiba tuepushe
gharama zisizo na maana ??
# Mwisho umetutisha kuwa serikali 3
zinaweza kusababisha jeshi kupindua
na wanajeshi kuongoza nchi na
baadae kuvua magwanda na
kugombea Urais, umesahau kuwa
wewe pia ni Luteni wa jeshi uliyevua
magwanda na kugombea Urais ??? na
tena kwa mujibu wa katiba yetu wewe
ni mkuu wa vikosi vyote nchini???
tatizo liko wapi?? mpaka ututishe???
Nakushauri mh,ufute kauli zako za
jana ili mchakato uendeleeb kwa
uhuru zaidi!
Yote sawa, lakini la muhimu ni hili. Kwanza huo ufunguzi uliwekewa mazingira ya vitisho CCm wakidai ati wamegundua njama za rais kuzomewa. Pili zilipita kampeni za ajabu za jinsi ya kumshangilia Kikwete na CCm yake. Katika yote aliyosema Kubenea, muhimu ni hili. Hakuna haja ya kuendelea na bunge hilo ikiwa wengine na chama chao wameshatoa msimamo wao. Wao wakiwa madarakani nani atazuia maoni yao? Sioni umuhimu wa Bunge hili kuendelea na kuharibu pesa za bure, labda kama CCM wanafanya wanachojua. Kwa hiyo wapo hapo Dodoma kucopy na kupaste
 
Kwa hotuba ya jana ya Mh Rais nawashauri wajumbe wenye nia njema na Nchi hii waungashe virago warudi makwao kukwepa kumaliza hela za madawati na madawa huko mahospitalini, ila kama wana vichwa ngumu nakuamua kubaki basi wahakikishe wanaufanyia kazi ule msemo maneno "uamuzi wako usiwe wa kuambiwa na akili za kuambiwa changanya na zako"hapo wanaweza kubaki, vinginevyo h Rais keshaonyesha anataka Katiba ya aina gani yeye na CCM yake.
 
Hapa naona ni kama tunarusha ngumi hewani tu,kwa kuwa msimamo umewekwa wazi na rais,yatupasa tukubaliane tufanye nini ili kuzuia mchakato huu wa kihuni usiendelee!kama ni Mtikila kwnda mahakamani akazuie tumuunge mkono.kama ni UKAWA kuitisha maandamano tujue

Tatizo la mh Rais ambalo hakuwatendea haki wananchi wake ni kwakutoa maoni yake ndani ya bunge na huku akijaribu kusisitizia misimamo yake ambayo kiuhalisia ilikuwa ndio msimamo wa chama chake. Kwakupata katiba ya sawa yenye maoni ya wananchi kwa nchi yetu bado kuna safari ndefu sana. Rais namjua ni mtu ambaye msimamo wake waTANZANIA tunaujua kuwa huyu yuko after the country lakini misimamo ya chama chake ndio imemfanya azungumze yale aliyozungumza. Chakunishangaza zaidi ni kuwa hata vyama vya upinzani kama CHADEMA kilichotangaza kuunga mkono muundo wa serikali 3 wapo mamluki kibao wanaotaka muundo wa serikali 2. Inashangaza sana na kwakweli hatutoipa Katiba yaTANZANIA yenye maoni ya wananchi.
 
Kuna swali hapa najiuliza juu ya maoni ya tume zote zilizowahi kuundwa kutatua kero za Muungano na majibu yake! Tume zote zimekuja na solution ya serikali tatu hakuna hata tume moja iliyokuja na solution au pendekezo la serikali mbili au moja wote wanasema tatu na mara zote serikal tatu zimekuwa zikipingwa na serikal (CCM) lakini ndo huwa zinajirudia rudia.
Kwanini hili hutokea?!
 
kwamfano labda KUBENEA angekua raisi, je angeacha onyesha upande wa chama chake na kuwaongoza wananchi na wanachama wake juu ya nini cha kufanya.?? Ni UPU MBAVU kufikiri kwamba angeacha.

Therefore, akae kimya. Sanasana ataonekana mnafiki na mpoteza muda.
 
Hivi huyu mtatiro anaakili kweli eti anasema wajumbe wengi hawana weledi na hawajui kuchambua hivi wewe mtatiro unaweledi gani zaidi ya kuwadanya vijana wa cuf na kupotosha jamii kwenye mambo ya msingi,kwa sasa hatudanganyiki tena rais kafungua njia tafadhali tuheshimiane na tuishi kwa adabu.

hivi wewe jamaa unafikr hii tanzania ni ya ccm na ndugu zko ebu fikiria maisha yako ya baadae bila ccm mwenzio kaja na mawazo mazuri lakini wewe una mbeza hivi uko timamu kweli yan nataman watanzania wote tungekuwa na akili kama zangu mngefkria kama mimi sio kama hili jamaa limelidhika na ccm
 
Kuna swali hapa najiuliza juu ya maoni ya tume zote zilizowahi kuundwa kutatua kero za Muungano na majibu yake! Tume zote zimekuja na solution ya serikali tatu hakuna hata tume moja iliyokuja na solution au pendekezo la serikali mbili au moja wote wanasema tatu na mara zote serikal tatu zimekuwa zikipingwa na serikal (CCM) lakini ndo huwa zinajirudia rudia.
Kwanini hili hutokea?!
 
Baada ya Hotuba ya jana ya MH; JK iliyoonekana dhahiri kumjibu Warioba baadhi ya vipengere, Wadau nawashauri someni kitabu AN ENEMY OF THE PEOPLE na mwandishi Ibsen, mpate majibu ya namna wanasiasa siku zote wasivyoweza kukubaliana na tafiti na maoni ya wataalamu kwa gharama yoyote ile na haitatokea, hata kama ni ndugu wa damu tumbo moja, Kitabu hiki kizuri pia kipo ktk. fasihi na usomwa na vijana wa kidato cha sita Tanzania mchepuo wa Lugha/languages
 
Kuna swali hapa najiuliza juu ya maoni ya tume zote zilizowahi kuundwa kutatua kero za Muungano na majibu yake! Tume zote zimekuja na solution ya serikali tatu hakuna hata tume moja iliyokuja na solution au pendekezo la serikali mbili au moja wote wanasema tatu na mara zote serikal tatu zimekuwa zikipingwa na serikal (CCM) lakini ndo huwa zinajirudia rudia.
Kwanini hili hutokea?!

Ndiyo suluhisho pekee, yaani hamna namna. Hata ikiundwa nyingine jawabu litabaki hilo tu!
 
Labda iundwe tume ya wenye upeo mdogobwa kiccm kama kina nape ndiyo itasema serikali 2
 
Back
Top Bottom