GE2025 Hizi ndio sababu kwanini watu wa Morogoro haina sababu za kumnyima kura Samia Suluhu

GE2025 Hizi ndio sababu kwanini watu wa Morogoro haina sababu za kumnyima kura Samia Suluhu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Getrude Mollel

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2022
Posts
308
Reaction score
424
Muda mfupi baada ya Rais Samia Suluhu kuingia madarakani 2021, alifanya ziara ndogo mkoani Morogoro, na akaongea na watu pale Msamvu tarehe 7-04-2021.

Pale Rais Samia Suluhu aliwatoa watu wa Morogoro hofu na kuwaambia ya kwamba, mambo mengi mazuri yanakuja kwenye mkoa huo, ajira, mikopo, viwanda na miradi mingine ya maendeleo.

Rais Samia Suluhu akatimiza ahadi yake, Agosti 2021, alifanya ziara ya kitaifa sasa mkoani humo ambapo, alizindua Bwawa kwa ajili ya umwagiliaji katika Kiwanda cha Sukari Mtibwa ambapo, maendeleo hayo yatakuza uzalishaji wa sukari kutoka wastani wa tani 20,446 kwa mwaka hadi tani 85,000.

Hakuishia hapo, Rais Samia Suluhu aliweka jiwe la msingi la utanuzi wa kiwanda cha sukari Kilombero ambapo, utanuzi huo utaongeza zaidi uzalishaji kutoka wastani wa tani 126,000 kwa mwaka hadi tani 271,000 kwa mwaka mradi ukikamilika na hapa, zaidi ya watu 5000 wataajiriwa.

Ndani ya muda mfupi tu, Rais Samia Suluhu ameleta mageuzi makubwa sana kwenye sekta ya kilimo, ajira, viwanda na miundombinu mkoani Morogoro ambapo, faida kubwa imepatiakana kwa watu hao.

Watu wa Morogoro kwa makubwa hayo na mengine mengi yanayokuja, hawana sababu ya kumyima kura Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.
 
Lami ya nanenane-Tungi imemalizika juzi tu hapa, miradi ya maji
 
1. Uzinduzi Bwawa la Umwagiliaji la Kiwanda cha Sukari mtibwa ambapo hii imechangia uzalishaji kutoka tani 20,946 hadi tani 85,000

2. Aliweka jiwe la msingi la utanuzi kiwanda cha Kilombera Sugar ambapo kitaongeza uzalishaji kutoka 126,000 - 271,000.

3. Alizindua kiwanda cha Sukari Mkulazi Mbigiri

4. Rais Samia Suluhu aliweka Jiwe la Msingi la Kiwanda cha Sigari cha Mkwara Leaf

5. Alizindua Daraja la Berege katika wilaya ya Kilosa ambayo ni njia fupi kuelekea Kilindi - Tanga

6. Rais Samia alizindua barabara ya Rudewa - Kilosa yenye urefu wa km 142

7. Alizindua Daraja la Ruaha

8. Rais Samia alizindua Barabara ya Kidatu Ifakara km 61
 
Back
Top Bottom