Hizi ndio ndege za Magufuli

Bodi ilioshindwa kuendesha shirika lenye ndege moja litaweza kuendesha shirika lenye ndege mbili? Sijasikia wakiongelea business plan au wanataka zikifika ndio wanze kujipanga? Viongozi wa hii nchi sio wa kuwaamini kwenye mambo ya biashara.
Mkuu heshima yako,umegonga utosini,majitu yalienda kusoma ili kukariri na kushinda mitihani,unakuta mtu ana shahada gunia zima lakini taaluma au ujuzi ni bure kabisa.Basi hizi ndege za Magufuli wacha zije na zigeuke SAMAKI WA MAGUFULI.
 
Wala sio ujuaji niambie serikali imefanikiwa wapi kuendesha shirika la kibiashara?
Serekali ilishindwa kuendesha viwanda na biashara zooote alizoacha mkoloni,tena mkoloni aliacha biashara zikiwa na ufanisi mkubwa mp
Bila shaka atazipangia nauli mwenyewe.
Kabisa Mkuu,maana rais anafanya kila kazi,mpaka kupanga bei ya sukari na wapi ikanunuliwe,na nani apewe kibali cha kuagiza sukari.
 
Wala sio ujuaji niambie serikali imefanikiwa wapi kuendesha shirika la kibiashara?
Serekali ilishindwa kuendesha viwanda na biashara zooote alizoacha mkoloni,tena mkoloni aliacha biashara zikiwa na ufanisi mkubwa mpaka Tanganyika wakati ule iliongoza kwa export na pesa za kigeni aliacha zimejaa hazina kiasi cha kupelekea dola ya kimarekani kuwa chini ya Tanganyika shs,tukazichoma zote kupigana vita ya Uganda kumtoa Idd Amin Dada ili kumsaidia swahiba wetu Dr Milton Apollo Obote arudi kwenye madaraka kwa gharama ya sisi watanzania wooote kuwa masikini omba omba.CCM JUU,JUU,JUU ZAIDIIIIIIIIII.
 
Soma uelewe alichoandika,umekula MICHEMBE sasa unategemea akili yako itaelewa kitu kweli?,mtu kaeleza kwa ufasaha na wewe NGOSHA unajibu kwa hisia zako butu,umeishaambiwa serekali hii ya Tanzania haiwezi kufanya chochote chenye TIJA,na mifano ipo,sana sana wataendesha shirika hilo kwa miaka mitatu au chini yake natutaambiwa shirika limekufa kutokana na sababu zisizo zuilika,hata ndege zikinunuliwa zitanunuliwa ndege chakavu zilizopakwa rangi na pesa itaingia mifukoni mwa MAHESHIMIWA mazinzi na malevi,sasa wewe tokwa mapovu ukojoe ukalale.

Mkuu chini ya MAGUFULI watu wameshaanza kunyooka sasa mtaani na makazini watu wameaanza kuheshimiana ,sidhani kama kuna watu wataingilia utendaji wa wengine,mbona kwenda nje ya nchi watu hawaondoki usimaji sasa ni mzuri kuliko huko nyuma
 
Wabongo bwana heti kelele angani kwani kuna ndege inatembea kimyakimya angani?.bora tuanze na hivyo.tatizo nyie kila kitu ni wakatisha tamaa
Mh hapana hebu tuwe wakweli hapa kupanda chatter ya Dar Arusha ni tofauti na kupanda Boeing au airbus
 
Ndio maana huwa nawasifu sana watu wa Kilimanjaro na Arusha kwa uwezo wa kiakili waliojaaliwa na MUNGU,bro umegusa pale pale,hizo ndege chakavu zikianza kazi chini ya serekali,basi ujue zitaenda tupu na kurudi tupu mpaka shirika litasambaa bila kurudisha hata pesa ya toilet paper za ndani ya ndege,ukitaka ticket utaambiwa ndege imejaa,mpaka utoe rushwa,na hizo ndege zikienda service mara moja, wataandika zimeenda mara saba.

ukitaka toilet paper watasema utumie maji yakunywa ambayo umeleta mwenyewe kutawazia
 
Mkuu chini ya MAGUFULI watu wameshaanza kunyooka sasa mtaani na makazini watu wameaanza kuheshimiana ,sidhani kama kuna watu wataingilia utendaji wa wengine,mbona kwenda nje ya nchi watu hawaondoki usimaji sasa ni mzuri kuliko huko nyuma
Mkuu,Magufuli kweli anafanya kazi vizuri sana lakini kumbuka ni yeye tu peke yake,waliomzunguka wote ni vibaka na wanajifanya kumsaidia kupasua majipu lakini hiyo ni nguvu ya soda kulinda vibarua vyao tu,kwa hiyo hakuna chochote kitafanikiwa mpaka wananchi wa Tanzania wawe na uchungu wa nchi yao,kitu hicho ni ndoto kwa Watanzani.
 
Serekali yetu haina uwezo wa kuendesha hata biashara ya boda boda,inachoweza ni kugawa kanga,kofia,pombe ya kienyeji,supu ya makongoro na ngoma ya bugobogobo kwa wananchi waimbe,wacheze ngoma halafu waende wakasambaze ukimwi na kuzaa watoto nje ya ndoa wasio wajua baba zao baaasi.


Mti wa mbuyu ulianza Kama mchicha.
Hivi mashirika makubwa ya ndege dunia yalianzaje? Waliajiri waataalamu wa ndege Na wakafanikiwa.Wewe unachuki ya kuwa MTanzania Au hujipendi.
Hii Tanzania itasonga mbele tu Hata tukiagiza mitumba ya ndege.
 
ukitaka toilet paper watasema utumie maji yakunywa ambayo umeleta mwenyewe kutawazia
Si ajabu hata vyoo vikaharibika na hakuna ukarabati,vitafugwa kufuli,na abiria tutaambiwa ukitaka kujisaidi subiri ndege ikitua utaenda kujisaidia nyumbani kwa sababu hata vyoo vya airport ni vibovu kama ilivyo JKIA.
 
Bado tuna mind ya kijamaa, mambo ya kufanya
1. Maliza madeni yote ya atc
2. Uza baadhi ya share kwa wazawa na mashirika ua umma kama nssf etc
3. Serikali isiwe majority ila watu binafsi washughlikie maswala ya biashara
4. Badili jina la shirika na nembo hata ukiita hapa kazi tuu airlines au majipu airlines sawa tuu ili mradi tujibrand upya
 
Mti wa mbuyu ulianza Kama mchicha.
Hivi mashirika makubwa ya ndege dunia yalianzaje? Waliajiri waataalamu wa ndege Na wakafanikiwa.Wewe unachuki ya kuwa MTanzania Au hujipendi.
Hii Tanzania itasonga mbele tu Hata tukiagiza mitumba ya ndege.
Na ile miti minene ya mibuyu isio na idadi ulioachiwa na Wakoloni wewe Mtanzania,mbona ulishindwa hata kuangua ubuyu tu bila kuitunza,sasa huo mchicha utakaopanda leo ili ikue kama mibuyu ndio utaweza?,labda kwa msaada wa watu wa Marekani,na msaada wa bure hakuna duniyani,ni lazima uiname tu au ushike ukuta,watakusaidia kulima mchicha na kabla haijageuka mibuyu madini yoote yatakuwa yamesainiwa mikataba ya miaka 200 ya kuvunwa na Wazungu,wewe utapewa chandaru aina ya ngao.
 
Badala ya hizo mbili ndogo angenunua moja kubwa kuliko hivyo vitoroli
24f2a5420ec83b78c30ee9023a29f4fd.jpg

Kwa soko lipi la ku-operate na hiyo monster? 50-70 seater ndio inayotufaa mpaka tutakaposimama.

Tutahitaji dedication ya hatari kuisimamisha ndege yetu, luxury ambayo kwa sasa Tanzania hakuna.
 
Bado tuna mind ya kijamaa, mambo ya kufanya
1. Maliza madeni yote ya atc
2. Uza baadhi ya share kwa wazawa na mashirika ua umma kama nssf etc
3. Serikali isiwe majority ila watu binafsi washughlikie maswala ya biashara
4. Badili jina la shirika na nembo hata ukiita hapa kazi tuu airlines au majipu airlines sawa tuu ili mradi tujibrand upya
Hapana mkuu,jina la shirika la ndege liwe MWADECO bhana,au labda MWADILA,halafu waganga wote wa kule GAMBOSHI waletwe ili wafanye zindiko na kuweka tunguli kila kona ya ndege,maana Kenya ,Uganda,Rwanda wametuloga sana na kusababisha tuwe nyuma yao kimaendeleo,na bila kusahau kule BANDARINI nako pageuzwe GAMBOSHI ili kukinga.
 
JPM ametangaza kwamba soon ATCL itapata ndege mbili aina za Bombadier Q400 kwa ushauri aliopewa kutoka Rwanda.Hivi kweli wataalamu wetu walishindwa kumshauri Rais? Specification za ndege hizo ni kama ifuatavyo


Bombardier Q400
Price - Current Price $ 27 million U.S.*
The NextGen Passenger Turboprop the Bombardier Q400 NextGEN...
Manufactured from -
1983 - Present
Seating Chart /Seats -
78

Travel Range -
2,522.00 Kilometer
1,362 Nautical Miles

Country of Manufacture -
Canada
  • Engine -
  • 2 X Pratt and Whitney PW150A
  • Power -
  • 5,071.00 Horsepower
  • Avionics -
  • Rockwell Collins Pro Line Fusion
  • Maximum Cruising Speed -
  • 666.25 km per hr 414.00 mph
  • Service Ceiling -
  • 7,620.00 metres 25,000.00 feets
  • Rate of Climb -
  • 457.20 mpm 1,500.00 fpm
  • Numbers Ordered/Sold -
  • 250
  • Cabin Height -
  • 1.95 metres 6.40 feets
  • Cabin Width -
  • 2.51 metres 8.23 feets
  • Cabin Length -
  • 18.80 metres 61.68 feets
  • Exterior Length -
  • 32.84 metres 107.74 feets
  • Wingspan / Rotor Diameter -
  • 28.42 metres 93.24 feets
  • Fuselage Diameter -
  • 2.69 metres 8.83 feets
  • Baggage Volume -
  • 14.20 cubic metre 501.47 cubic feet

  • Maximum Take Off Weight -
  • 29,257.20 kgs 64,500.00 lbs
  • Maximum Payload -
  • 8,669.20 kgs 19,112.00 lbs
  • Fuel Tank Capacity -
  • 1,697.00 gallon 6,423.82 litres
  • Fuel Economy -
  • 0.34 km per litre 0.80 NM per gallon
  • Minimum Take Off Distance -
  • 1,402.08 metres 4,600.00 feets
  • Minimum Landing Distance -
  • 1,286.56 metres 4,221.00 feets

source:Bombardier Q400 Turboprop Aircraft - Seating, Price, Safety Record - NextGENView attachment 362099 View attachment 362100 View attachment 362101 View attachment 362099 View attachment 362100 View attachment 362101

Dah umri wa ndege umenizidi!
 
Back
Top Bottom