Hivi weupe ndio urembo au?

Habari zetu warembo na watanashati.
Hii tabia imeota mizizi sasa sijui kwa nini wanawake tunakuwa hivi...tena siku hizi vipodozi vya kubadilisha rangi vinatangazwa hadharani kabisa afadhali siku za nyuma watu walikuwa wanajichubua kwa kujificha.
Hivi ni kweli hivi vipodozi vya kubadilisha ngozi havina madhara kiafya? Kama vina madhara mamlaka zinazohusika zimeshindwa kuwashughulikia wanaofanya biashara hizi? Kwa kweli nashindwa kuelewa hivi huyu dada ukimuangalia picha yake ya kushoto na kulia kuna tofauti yoyote? Ipo inayovutia kuliko nyingine? Mimi naona mtu ni yule yule tu nothing more nothing less. Naombeni maoni yenu wadau
View attachment 526690
Toooooba!
 
Ndiyo, kwenye jamii nyingi, hususan za watu weusi [walio na asili ya Afrika] rangi nyeupe ya ngozi huhusishwa na urembo.

Naamini ni ukweli ambao watu wengi hatuupendi, lakini ndo hivyo tena. Ukweli mara nyingi huwa ni mchungu na tulio wengi huwa tunajitahidi kuukataa waziwazi.

Hapo juu umezungumzia watu kujichubua ili kujibadili rangi ya ngozi na wawe weupe zaidi. Vipi kuhusu nywele bandia zilizonyooka? Ina maana nywele asilia za kipilipili ni mbaya, siyo?

Na vipi kuhusu majina ya kigeni siku hizi?

Unakuta mtu anaitwa Anthony Francis wakati baba ni Mgogo na mama ni Mnyiramba!

Au Maxwell John wakati baba ni Mmakonde na mama ni Mzaramo!

Hiyo mifano inanileta kwenye hoja ya kuhusisha Uafrika na uduni na Uzungu na ubora.

Hata watu wenye tabia za kishenzi huwa tunawaita 'waswahili'. Halafu tabia flani flani zinazoonekana au kudhaniwa kuwa ni za kistaarabu ndo zinaonekana ni za 'kizungu'.

Ni ndivyo tulivyo tu.
Mkuu umenena vyema kabisa!
 
Wewe hujawahi kusikia ila zipo. Na mashiko yangu mimi wewe unaweza kuona ni upuuzi...ndo hivyo tunatofautiana

Naam, na ndivyo hivyo hivyo kwenye kujichubua na kushonea nywele bandia.

Wewe unaweza usione mashiko ya sababu za mtu kujichubua ilhali yeye anaona akijichubua ndo atakuwa mzuri zaidi.
 
Ndiyo maana wachina, wazungu, waarab wanatucheka sana kwa kutuletea kemikali zilizo oza huku Afrika. Pia inashangaza unaweza ona mwanamke jeusiiii limevaa wigi ya kijani, nyekundu, njano, sielewi wanaona uzuri gani. Yaani baada ya kuonekana mzuri anakuwa anatisha kuwa a zombie.

3ae690469e32405eaf2e9b5510547aa8.jpg
 
Wewe unataka uzungu unaficha Sanga unabaki na Josephine Goodluck Paul mwingine anajichubua. Wote lengo ni moja- Uzungu ila njia tofauti.
Hahaa sawa mkuu kumbe mtu unaweza kujikataa asili yako kwa namna nyingi
 
Waafrika ni wahanga na watumwa wa mapokeo ya tamaduni na mila za kigeni, tangu tulipoaminishwa kuwa za kwetu ni za kishenzi na ki mizimu na ukweli tumekuwa watumwa mpaka tunagombana wenyewe kwa wenyewe, kugombea imani za kigeni inakera.

Ukiangalia mabara mengine yamebaki na tamaduni na mila zao achilia mbali majina yao pia. Shida iko Africa. Ukija kwa wake zetu na binti zetu wao ndiyo kabisaa wameukana asili yao eg rangi, nywele. Huwezi kuona mambo haya mabara mengine sisi tumepokea kila kitu. Mpaka utu wetu umekosa maana mbele ya jamii nyingine
 
Sio urembo wala nini ni ULIMBUKENI tu, wanaojichubua kutoka weusi kwenda weupe wengi wao HAWAJIAMINI
 
Habari zetu warembo na watanashati.
Hii tabia imeota mizizi sasa sijui kwa nini wanawake tunakuwa hivi...tena siku hizi vipodozi vya kubadilisha rangi vinatangazwa hadharani kabisa afadhali siku za nyuma watu walikuwa wanajichubua kwa kujificha.

Hivi ni kweli hivi vipodozi vya kubadilisha ngozi havina madhara kiafya? Kama vina madhara mamlaka zinazohusika zimeshindwa kuwashughulikia wanaofanya biashara hizi? Kwa kweli nashindwa kuelewa hivi huyu dada ukimuangalia picha yake ya kushoto na kulia kuna tofauti yoyote?

Ipo inayovutia kuliko nyingine? Mimi naona mtu ni yule yule tu nothing more nothing less. Naombeni maoni yenu wadau
View attachment 526690
wakati mweusi alikua very beautiful and young, since ajibadilishe amekua ugly and old. lol.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom