Hivi weupe ndio urembo au?

Ndiyo, kwenye jamii nyingi, hususan za watu weusi [walio na asili ya Afrika] rangi nyeupe ya ngozi huhusishwa na urembo.

Naamini ni ukweli ambao watu wengi hatuupendi, lakini ndo hivyo tena. Ukweli mara nyingi huwa ni mchungu na tulio wengi huwa tunajitahidi kuukataa waziwazi.

Hapo juu umezungumzia watu kujichubua ili kujibadili rangi ya ngozi na wawe weupe zaidi. Vipi kuhusu nywele bandia zilizonyooka? Ina maana nywele asilia za kipilipili ni mbaya, siyo?

Na vipi kuhusu majina ya kigeni siku hizi?

Unakuta mtu anaitwa Anthony Francis wakati baba ni Mgogo na mama ni Mnyiramba!

Au Maxwell John wakati baba ni Mmakonde na mama ni Mzaramo!

Hiyo mifano inanileta kwenye hoja ya kuhusisha Uafrika na uduni na Uzungu na ubora.

Hata watu wenye tabia za kishenzi huwa tunawaita 'waswahili'. Halafu tabia flani flani zinazoonekana au kudhaniwa kuwa ni za kistaarabu ndo zinaonekana ni za 'kizungu'.

Ni ndivyo tulivyo tu.
 
Hapo kwenye majina pananikera sana, unakutana na mtu mzima bila aibu eti anaitwa Peter Paul au Mohammed abdallah, seriously!! Hii ipo zaidi Tanzania kuliko nchi nyingine yeyote ile Africa. Nigeria ni aibu mtu kuwa na jina la kigeni hata mnigeria azaliwe wapi ataitwa Babatunde, Yemi na majina yao ya asili hali kadhalika South Africa wanatumia sana majina yao, wakenya pia ni sisi tu ndo tumekengeuka.

Kuna mtoto mtanzania toka Mwanza mwaka jana alienda UN kuhutubia anatumia majina mawili yote ya kigeni hadi wale watu walimshangaa. Nilikua naangalia TV ila niliona aibu peke yangu.

Ni wabongo tu ambao wakienda mbele kama anaitwa Musa atajiita Moses, Hashimu Thabiti kawa Hasheem Thabeet. Tumekuwa whitewashed hadi aibu
 
Mimi siutamani weupe..Ila natamani Sana Yumbo flat. Naumbo zuri Sana shida Ni tumbo TU..nikiwaona wadada Instagram...nawatamani sana.
Pole sanaa...tumbo mbna linapunguzwa vzur tu...ukizingatia mazoezi na mlo Basi ni dawa tosha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom