Hivi Watangazaji wa Clouds FM wana shida gani?

Hivi Watangazaji wa Clouds FM wana shida gani?

Hawa watu wamegoma kusoma magazeti ya leo eti kisa yameripoti habari za Lowassa.

Eti wanasema kilichotokea jana kila mtu alishughudia hivyo hakukuwa na haja magazeti kuripoti leo.

Kweli clouds?

Walichoamua eti bora tusome uhuru(jarida la CCM). Ambalo limeripoti ''Magufuli ushindi wa Tsunami''
Kwa design hii waandishi wa clouds na media zenu wekeni wazi kuwa ninyi ni vyombo ya propaganda za CCM.
Lakini hii mbona inajulikana mkuu, shida ni kwamba wanawaza je Oktoba maCCM wikibwagwa itakuwaje?!
 
Mnajua humu jamaa na rafiki pengine ndugu za wafanyakazi na wamiliki wanaingia na kuona mawazo yetu.Clouds ina mambo ya kipuuzi,kikauzu,kitoto.Clouds sina hakika kama kuna mbwajajaji mwenye elimu ya chuo cha juu.watangazaji wake hawatumii taaluma,ni uzoefu wa soga za mtaani.low level education,thinking capacity,determination and poor performance.

Hata wao wenyewe wanapita humu hao matahira
 
Haina shida after October 25th lazima watasoma tuu matokeo na hapo ndo itakuwa mwisho wa hicho kijarida cha Uhuru ambacho hakiko huru
 
Mawingu fm ni wafanya biashara msiwalaumu kwa deal walilopokea kutoka kwa system cuz kuna ka-studio ka taifa kalipitia mlango wa nyuma kisha kakawa mali yao.Nadhani hizo ni fadhila katika masuala ya kibiashara illegally na ndio maana kwenye deal la malaria walimfanyisha jingle father house ili hata aliyedhurumiwa aogope kutia mikono..
 
Huu ndiyo Ukweli harisi Ruge na January walimzunguka Sugu kijanja Kwa kumwingiza JK kwenye Dili Leo ili lionekane ni suala la Kitaifa , hata hii ya Juzi ya Wasanii kumuaga JK pia ulikuwa mchongo wa January na Ruge na Pesa ya kugharamia shughuri itakuwa imetoka huko huko Ofisi Kuu.
 
leo wamepata aibu polisi na wananchi wamekanusha kuwa hakuna duka lililoporwa wala watu kuibiwa jana kwenye maandamo ya Lowasa kuchukua fomu
. Maana wakina Hando asbh walishadadia balaa kuwa yale maandamano yalikuwa ya wahuni na watu waliibiwa.
 
Kinachomchanganya Gerald ni ndoto kuwa naye siku moja atapata ukuu wa wilaya. Jamaa ni mnafiki sana na huwa anapenda sana kucrash matukio yanahusu UKAWA. Hana tofauti na Ephraim Kibonde.

Kibonde huwa ni mwanachama wa NCCR mageuzi na Gerard ni Chadema huenda wanafanya kazi Kwa kumfurahisha Ruge lakini mionyoni mwao woote ni Ukawa.
 
leo wamepata aibu polisi na wananchi wamekanusha kuwa hakuna duka lililoporwa wala watu kuibiwa jana kwenye maandamo ya Lowasa kuchukua fomu
. Maana wakina Hando asbh walishadadia balaa kuwa yale maandamano yalikuwa ya wahuni na watu waliibiwa.

Watakuwa wamelazimishwa na Ruge ambaye ni ccm lakini Kama wanaingia JF watakuwa wamepata Ujumbe wao.
 
Wewe Ruge waache watangazaji wawe huru kubalance vyama vyote acha kulazimisha ccm ipendelewe hapo kwenu clouds , Watu wa sasa wapo makani sana ukifanya Upendeleo watakuadhibu kwa kuacha kusikiliza Radio yenu.
 
Other countries have Mafia. In Tz the Mafia have a country, political parties and the media houses.
 
Hivi Hiyo Clouds bado ipo?. Mimi nilishaacha kuisikiliza mwaka wa tatu sasa. Tangu walipojipa jukumu la kumfanyia birthday jk niliwashangaa sana.

Mimi huwa nasikiliza Radio One tu, nikiwa kwenye gari yangu au nyumbani. Na mke wangu sasa hivi naye ameniunga mkono kutoisikiliza clouds mwaka wa pili sasa.Radio One ndio mpango mzima, wana vipindi vilivyopangwa na vya uhakika.

Mkuu kumbe na wewe mzee...
 
Usibishane nao people could not tell the difference mambo yote mkude simba na mr panjuani E fm!
 
Muwe mna sikikiliza magic fm 12:30 ni wazuri sana kwenye magazeti na uchambuzi

Clouds nilishasahau kama kama powerbreakfast...labda kipindi cha michezo...
 
Back
Top Bottom