Tuhuma kipindi cha Clouds 360 kutokuwa na mizania

Suphian Juma

Senior Member
Apr 2, 2019
133
546
KUHUSU KUSHAMBULIWA MTANDAONI CLOUDS, MWANDISHI KIJAH.

Nimeongea na moja ya Watayarishaji wa Kipindi cha CLOUDS 360 (jina nalihifadhi).

Mnamshambulia bure Mtangazaji Kijah Yunus na Clouds kwamba hawa-balance Stori na hivyo wanawapendelea CCM na kuwatenga CHADEMA kwa kurejea Interview zao na Spika Ndugai, Lazaro Nyalandu na DC Sabaya.

Mtayarishaji anasema Clouds wamesumbuka sana kumtafuta Mwenyekiti wa CHADEMA, Mbowe miaka kadhaa sasa. Mtayarishaji anaendelea kusema aliwahi kwenda mpaka Ledger Plaza kwa ajili ya kumuomba aende 360 miaka miwili iliyopita lakini bado alimrusha

Aidha kuanzia mwaka jana Mtayarishaji anasema Clouds walimwita Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika ila akawarusha kila siku na mpaka wiki iliyopita wamemtafuta hajawapa ushirikiano.

Sasa nyie vijana na wafuasi wa CHADEMA mnataka Clouds wafanyaje? Wafunge kipindi au wasialike watu wa vyama vingine sababu ninyi hamtaki?

Tukiachana na hoja yenu ya Mwandishi Kijah kwamba eti ni CCM ambayo haina mashiko kwani hakuna sheria inayowakataza waandishi wa Habari kujihusisha na Siasa; Lakini pia hebu tutafakari, kama Clouds wanaibeba CCM vipi Zitto ni CCM? Lakini Prof Jay je? Boniphace Jacob? Mchungaji Msigwa? Halima Mdee, Upendo Peneza, Heche? Hawa wote wamehojiwa 360 je walikuwa CCM?


Halafu kama ni hoja ya maswali aliyoulizwa leo DC Sabaya kwamba yalikuwa bias, hivi bias ni Watangazaji kumhoji maswali kuhusu shutuma karibia zote zinazomkabali? Why msingejikita kujadili majibu aliyoyatoa DC Sabaya?

WITO WANGU: Vijana na wafuasi wa CHADEMA acheni kuwashambulia watu wasio na hatia. Washaurini Viongozi wenu wakahojiwe. Nami pia nawaomba Viongozi wa CHADEMA waende kuhojiwa waache kukwepa interviews, na kusababisha chuki kwa chombo cha Habari bila sababu.

Kama hawataki, basi wawajulishe wafuasi wao ili lawama hizi zisizotokee tena kwa Waandishi na vyombo vyao vya habari badala yake wajikite kujibu hoja za viongozi watakaohojiwa.

Mnapigania Uhuru wa vyombo vya Habari halafu nyie hamtaki kuhojiwa? Ooops!! DISGUSTING!!!


Suphian Juma,
Singida, Tanzania.
0717027973.


IMG_20210510_161148.jpg
 
Ukada umewazidi na hivyo balance lazima iwe ishu,chakukumbuka ni kuwa kama back mmekwamia swami iliyopita tokeni huko tuko awamu ya sita yenye uhuru wa maoni na habari, isiyo na ubaguzi na inayohitaji kuuona umoja wa kitaifa unaimarika Bila kujali itikadi.
 
Tulia wewe, unalelewa kwa watu unaazimwa hata sabuni ya kuogea unafikiri hatujui? Mbona unalelewa na wanaume wenzio hatusemi unapata wapi Authority ya kuwasema CHADEMA? Pany.a buku wa Minyughe wewe.
 
Huwezi kujadili issue binafsi za mtu ambae unajua upande wa pili hauwezi kumpata azijibu.

Sabaya hata mtoto wa mwaka mmoja anajua tabia zake. Sio mgeni material kumhoji kwenye media.

Clouds hata mlipo muita Nyalandu tuliwa ambia mna feli mahali. Acheni siasa za maji taka. Mtapotea kama Tbc.
 
Mjinga mkubwa, umeweka na no za cm ilitukupigie kwa lipi? kama CCM inaleta maendeleo ufukara mlionao Singida unatokana na nini? basi Sindiga na Dodoma kusingekuwa na nyumba za tembe
Sufiani Juma anatapatapa,alishindwa kumpa uteuzi mwendazake. Sasa hivi Kila uzi anaweza namba za simu,ili awamu ya 6 imkumbuke,
Atakula nyama za punda hadi aludi Dar akaolewe.
 
Kwa maoni yangu, kwenye vipindi kama hivi (sijasikiliza kusikia washiriki wa kipindi hiki walisema nini) si taaluma ya uandishi wa habari kuruhusu mshiriki wa kipindi kuongelea habari za mtu mwingine, ambazo zinaweza kuwa zinamchafua machoni pa jamii, kama yeye hayupo kusemea upande wake.

Anayeongoza kipindi inabidi auelekeze mjadala kwenye issues na si kwa mtu au watu fulani ambao hawapo isipokuwa kama jambo linaloongelewa lina masilahi kwa taifa (kiasi kwamba kutoongelea habari hizo kutakuwa na madhara kwa taifa au umma).

Vyombo vya habari vikijifunza kufanya hivyo, baadhi ya manung'uniko kwamba chombo fulani cha habari kinawabeba watu fulani au kinatumiwa kuwachafua watu wengine, yatapungua na mwongoza au waongoza kipindi watakuwa wameonyesha ukomavu katika kusimamia maadili ya uandishi wa habari.

Vyombo vya habari vyetu vijifunze kuwa 'habari njema' kwa umma na kwa watu binafsi. Sisis wote tunapitia ujana, utu uzima na kisha uzee. Ni jambo la faraja kwa baadaye baada ya kustaafu kuwa unajikumbusha mambo uliyofanya ukiwa bado mwandishi wa habari na kupata faraja kwamba ulisimamia maadili ya kazi yako, kuliko kusikitika kwamba "hapa sikupaswa kufanya hivyo nilivyofanya au nilitumiwa kumchafua mtu mwingine".
 
Huyu bwana kipindi ni Afisa habari wa ACT kulitokea habari fulani fulani hizi nadhani zina ukweli kabisa maana akili yake inaonyesha ni kweli anafanyiwa hivyo
Musiba alisema huyu jamaa Suphian Juma Ni chicha mwiba hata Mimi sasa naonganisha dots na kukubaliana na musiba kwa mara ya Kwanza.
 
Back
Top Bottom