Swali zuri sana hilo!!, Kwa muda nilokaa hapa JF, nimeona watu walio komaa sana, hata inafika wakati wale wanaopangusa kamasi wakiingia wanapigwa na MOSHI wa hekima nzito nzito mpaka wanayeyuka na kupotea mitini. Pia mimi nimetembelea hizo Sites ulizo taja hapo lakini sijapata mambo ya maana ndani yake. Ni juzi juzi nimealikwa Harusi ya kijana mtaani, wameonana na kujuana na mpenzi wake wa kike kwenye FB, kumbe ndo mambo ya kisasa, watu wakabaki kuulizana kama maisha ya wanandoa ndio pia yatakua huko 'CYBERSPACE' ama vipi, hapo ndio twasubiri!!!.
Tuje kwa jibu la swali lako, Hapa JF kupata mtu wa kuchakachua, sio eti haiwezekani, lakini naona ni vigumu sana, ila fanya bidii na jitihada utafanikiwa Dogo!