Stand alone
Member
- Feb 27, 2017
- 64
- 153
Pombe ilikuwa imemwingia kichwani kiasi flani na kumfanya ajiskie kuwa ni jasiri kwa namna moja ama nyingine, aliamua kunyanyuka na kusogeleaa chumba kingine ambacho ndani yake kulikuwa kuna tukio la sherehe lililokuwa likiendelea, tukio la kuchagua baadhi ya wanafunzi wa chuoni pale ili waweze kufanyiwa mchujo wa kuweza kujiunga katika club hiyo iliyokuwa ikifanya tukio lile.
Eduardo Saverin mwanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo kikuu kile kiichwato Harvard aliamua kuingia ndani ya chumba kile kilichokuwa kikiogofya kwa wingi wa watu kiasi kwamba alihisi kuishiwa ujasiri na kushindwa aanzie wapi ndani mle, aliangaza macho huku na kule na kuona meza karibu na alipokuwa amesimama, ni meza ambayo ilikuwa imekaliwa na watu wanne ambao aliangaza na kumwona mmoja wao akiwa amevalia mavazi yaliyomtambulisha kuwa yeye ni mwanachama wa club ile,
aliamua kupiga moyo konde na kusogelea meza ile ili aweze kuongea na yule mwanachama ili kusudi na yeye apate mwaliko wa kuchaguliwa kujiunga na klabu ile ambayo alitaka sana kuwa mwanachama kwani aliona kuwa ingemsaidia sana katika maisha yake ya baadae kutokana na kuwa msingi wa klabu ile ulikuwa ni kufundisha netwworking na socialization, kwa kuwa mwanachama katika club ile ungeweza kuongea na watu mbalimbali,
kukutana na kuongea na wasichana warembo pia kutumia weekend yako katika maeneo ya hali ya juu chuoni pale ikiwa ni pamoja na jumba maalumu lililopo kwa ajili ya club hiyo ambapo pia ungeweza kunywa na kufanya starehe za aina mbalimbali, kiukweli ilikuwa ni fahari kuwa mwanachama katika club ile kwani walijulikana kama 'Social king stars of the school' ambapo kulikuwa na vigezo na masharti mbalimbali ili kuweza kujiunga,
ilikuwa ni mpaka uwavutie kweli kweli ndio upate mwaliko wa kujiunga na Club ile ambapo pia ungefanyiwa interview mbalimbali na kuwa mwanachama kamili baada ya kushinda na kufuzu vigezo na masharti yake, katika watu mia mbili wanaoweza kuitwa ni ishirini pekee ambao wangehitajika katika club ile iliyoitwa the Phoenex ambayo ilikuwa ni moja kati ya club tofauti tofauti zilizopo chuoni pale na kila club ikiwa na misingi na malengo yake binafsi.
EDUARDO SAVERIN mototo kutoka familia ya kitajiri iliyotawaliwa na biashara alikuwa amefundishwa umuhimu wa social networking na connection katika kupata unachokitaka hivyo alikuwa ni mtaalamu wa kumwaga maneno na bla bla ili kumwingia mtu akilini, na hivyo basi baada ya kumsogelea mwanafunzi yule aliweza kuongea nae na kukoleza bla bla nyingi ili kuweza kumfurahisha na kwa kuzingatia kuwa mwanafunzi yule alionesha kumfahamu.
Baada ya kutoka katika tukio la sherehe ile, Eduardo Saverin, alikuwa ndani ya chumba anachoishi chuoni pale akijaribu kukumbuka matukio mbali mbali yaliyotokea katika tukio la sherehe usiku ule, alikumbuka mapambo mbalimbali yaliyokuwa yamepambwa ndani mle, alikumbuka watu mbalimbali aliowaona katika tukio lile, aliweza pia kumkumbuka mtoto mmoja,
mwanafunzi ambaye tangu yeye aingie ndani ya chumba kile alimwona akiwa amesimama kwenye kona akiwa peke yake, alikumbuka mtoto/mwanafunzi yule alikuwa ni mwembamba mwenye nywele za curl zikiwa na rangi ya brown kwa mbali na akiwa pia ni mwenye uso ulio mwembamba, tangu Eduardo aingie ndani mle mpaka tukio linaisha mtoto yule alikuwa amesimama pale pale kwani alionekana kuwa ni mwoga asieweza kuzungumza na watu wala asiejua aanzie wapi ili aweze kujichanganya na watu kirahisi,
Eduardo aliwaza mtoto yule alikuwa amefuata nini mle ndani maana alionekana kuwa hapamfai, mle ndani hapakuwa pa watu wa aina yake, Eduardo aliwaza kwa namna moja ama nyingine mtoto yule asingeweza kupata nafasi ya kujiunga na the Phoenex kwa maana watoto wa namna ile hawakuwa aina ya club kama the Phoenex hata klabu nyingine asingeweza kuingia.Eduardo aliamua kutopoteza muda mwingi kumfikiria mtoto yule na badala yake aliamua kufanya mambo yake mengine pasipo kujua kuwa mtoto yule siku moja angeweza kubadilisha kitu maishani mwake.
***
Ilikuwa ni siku nyingine katika tukio jingine, Eduardo alikuwa amesimama akitazama mandhari mbalimbali ya ukumbi ule, karibu yake walisimama wanafunzi wanne wa kiume wawili wakiwa katika usawa wake mmoja akiwa upande wake wa kushoto na mwingine akiwa mbali kidogo katika upande wake wa kulia, alikuwa ni mwembamba mwenye nywele za curly na mwenye uso mwembamba,alikuwa amevaa sandels miguuni na kaptura japokuwa kulikuwa kuna baridi kali la kutovaa namna ile,
Eduardo aliweza kumtambua kuwa ndie mwanafunzi aliemuona kwenye kona katika tukio lililopita siku chache nyuma, na tangia pale aliweza kumuona sehemu mbali mbali lakini hakuwahi kumwelewa katika sehemu yoyote ile aliyomwona kwani katika sehemu zote alizomwona hakuna hata sehemu moja aliyomwona akiwa comfortable na hata usiku huo pia katika tukio hilo alionekana kama alilazimishwa kuwepo mahali pale kutokana na kuonekana kuwa hakuwa na amani na hii ilitokana na uoga wake wa kuzungumza na watu.
Jina lake aliitwa MARK ZUCKERBERG, alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa pili chuoni pale. Mark alikuwa ni mtoto aliekulia katika mtaa wa kawaida ulioitwa Dobbs Ferry uliopo jijini New York Marekani akiwa ni mtoto wa daktari wa meno ambae ni baba'ke na pia mtoto wa mwanasaiklojia ambae ni mama'ke. Pamoja na Eduardo kutomfahamu Mark, alikuwa amewahi kuskia sifa flani flani kumhusu, kwamba Mark ni mwanafunzi wa mwaka wa pili akisoma masomo ya computer science, alipokuwa high school alikuwa akiongoza kwa hacking yaani alikuwa ni mtaalamu wa kuingia kwenye computer system za sehemu mbalimbali pasipo ruhusa,
Eduardo hakuweza kuthibitisha kama ni ukweli au ni uongo lakini ilisemekana pia kuwa Mark aliwahi kutengeneza program ya software iliyoitwa synapse ambayo ilihusika na maswala ya MP3 player, Mark aliweza kuruhusu program hiyo iwe katika mtandao na kuweza kupakuliwa bure na watumiaji, kutengeneza program ile kulimfanya Mark apokee simu nyingi kutoka katika makampuni mbalimbali yakimtaka aende kuyafanyia kazi na tetesi zilikuwa kuwa kampuni ya Microsoft ilimwahidi dollar million mbili ili aende akaifanyie kazi lakini Mark aliweza kuikataa ofa ile.
Eduardo hakuingiwa akilini hata kidogo na kitendo cha mtu kupiga chini dollar million mbili,kitendo ambacho kilimchanganya na kufanya kuendelea kumwona Mark kuwa ni mtu wa ajabu na huenda akawa ni genius maana chuoni pale alikuwa ametengeneza program aliyoitwa 'course match' program ambayo ilimsaidia mwanafunzi kuingia online na kutafuta mwanafunzi aliyesoma nae course moja na kuweza kurahisisha mwingiliano na mawasiliano kutokana na kuwa chuoni pale kulikuwa na watu wengi waliosoma course tofauti tofauti na kuishi sehemu tofauti tofauti ambapo ilikuwa ni kazi kutambuana.
Eduardo aliwaza kuwa mtu kuweza kukataa dollar million huenda kutakuwa kuna sehemu anaelekea hivyo aliona kuwa mtu kama yule ndo mtu muafaka aliehitaji kufanya nae urafiki.
Eduardo akiwa amesimama pale aliwapigisha story huku wakiwajadili wasichana waliokuwa wamesimama karibu yao na yalikuwa maongezi ambayo yalivutia mpaka Mark aliongea
"kweli inafurahisha" Eduardo pia alijibu "yeah" japo hakuweza kuielewa voicetone ya Mark kwamba alikuwa kwenye mood ipi, uso wake wala sauti yake haikuashiria chochote kile kama ni furaha, utani au ni nini.
Muda ulifika wale wanafunzi watatu waliondoka, Eduardo akaona kuwa huo ndo muda muafaka wa yeye kuweza kumsogelea Mark, alimtajia dorm aliloishi kisha akamuuliza yeye aliishi dorm lipi, Mark alimjibu na kuelewa kuwa waliishi mabweni yanayopita njia moja japo yalikuwa ni tofauti hiyvo wakakubaliana kuwa waondoke
Walipokuwa wakitoka nje, Eduardo aliweza kumwambia Mark kuwa kulikuwa kuna sherehe bwenini kwake hivyo kama atataka waende wote kwenye sherehe ile, Mark alimwambia kuwa inawezekana lakini hayupo tayari kwenda sababu wote walijua ni nini cha kutegemea kwenye sherehe za bweni, chumba kidogo watu kibao huku wakivuta na kunywa pombe.
***
Walikuwa ni mapacha wawili waliofanana, Cameron Winklevoss na Tyler Winklevoss wakiwa ni wanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo hicho cha Harvard.
Cameron na Tyler walikuwa ni watoto wa tajiri ambao walijua ni nini wanataka, walikuwa ni wenye muonekano wa kuvutia na waliojibidisha katika mchezo wa kusukuma mtumbwi, siku zote walitaka kufanya mambo makubwa ili kuweza kuleta heshima kama walivyolelewa katika familia yao yenye fedha nyingi, wote walikuwa ni wanachama wa club iliyoitwa Porcellian,
club ya hali ya juu iliyokuwa na misingi ya kufundisha namna ya kutawala dunia, kufanya mambo makubwa na kuongoza ulimwengu na si kufanya starehe kama club ya the phoenix, hata pia kuna baadhi ya watu maarufu ambao walisoma chuoni hapo waliwahi kuwa wanachama katika club hiyo huku Raisi wa 32 wa Marekani Franklin D. Roosevelt ambae alisoma chuoni hapo nakukataliwa kuwa mwanachama katika club hiyo aliwahi kukaririwa akisema kuwa kitendo cha yeye kukataliwa katika club ile kilikuwa ni kitendo cha kumfadhaisha maisha yake yote.
Kutokana na kwamba Tyler na Cameron walikuwa ni watu walio busy waliobanwa na ratiba huku muda wao mwingi wakiutumia kufanya mazoezi ya mchezo wao pamoja na kuhudhuria darasani hawakuweza kukutana na watu wengi hasa wasichana, hawakuwa huru kuchagua msichana bora Zaidi kwa kuwa hawakuwa na muda wa kutembea sehemu zingine na kuona wasichana wengine tofauti na wale walioishi nao sehemu moja chuoni pale,
Hivyo basi kwa kutumia kigezo hicho wakaingiwa na wazo kuwa watengeneze website ambayo itakutanisha watu na kuweza kujenga urafiki na kubadilishana mawazo huku upande mwingine utakuwa ni upande wa mahusiano, ambapo mtu ataweza kutafuta mpenzi anaemtaka na hivyo basi website hiyo wataiita 'Harvard connection' yaani website ya kuunganisha wanafunzi wa Harvad.
Tyler na Cameron waliamua kushirikiana na rafiki yao wa kihindi aliyeitwa Divya, kwa kuwa hawakuwa wataalamu sana wa kompyuta waliamua kumtafuta mtu mwingine ambae aliitwa Victor, Victor alianza kazi ya kutengeneza website ile lakini kabla ya kumaliza aliweza kuondoka chuoni pale na kufanya Winklevoss twins na Divya wasitishe kutengeneza website ile mpaka pale watakapopata mtaalamu mwingine hasa katika codes na programming, genius ambae ataelewa ni nini wanataka kukitengeneza, walipanga pia wabandike tangazo mahali waliposoma computer science ili compyuta science waweze kuliona na ikiwezekana apatikane mmoja wa kufanya nae kazi hiyo
***
Eduardo aliingia ndani ya darasa ambalo hakujua ni darasa gani, lakini kwa kuwa watu walikuwa wamejaa sana alijua litakuwa ni darasa la muunganiko ambalo wanafunzi mbalimbali kutoka course mbalimbali husoma kwa pamoja kama sehemu ya sheria ya chuo mwanafunzi kuhudhuria angalau moja kati ya madarasa ya aina hiyo yafundishayo masomo mbali mbali kama vile Sanaa historia na lugha,
Eduardo aligundua darasa lile lilikuwa ni la historia, aliangaza huku na kule darasani mle, haikuchukua muda alimuona Mark akiwa peke yake nyuma ya darasa huku mistari mitatu ya mbele yake ikiwa haina watu, aliona miguu ya Mark ikining'inia ikiwa imevaa sandels aina ya adidas na alivaa kaptura huku juu akiwa amevaa sweta la kofia ambayo alizamisha kichwa chake na kusinzia,
Eduardo alipenya na kwenda kuketi pembeni ya Mark huku akiwa na tenga dogo lenye kuku ambao aliambiwa atembee nao popote pale aendapo kwa muda wa wiki nzima akiwahudumia na wakiendelea kuwa hai hilo likiwa ni moja ya sharti na jaribio ili aweze kufuzu kuwa mwanachama wa The Phoenix, kuku walianza kupiga kelele Mark alishtuka usingizini, manyoya ya kuku yalitoka yakiwapeperukia na watu waligeuka kuwashangaa,
Eduardo aliona kuwa aondoke kabla hali haijazidi Zaidi, alimwambia Mark kuwa usiku waonane kwani amekutana na msichana mrembo ambae alikuwa na rafiki yake hivyo alimwambia msichana yule usiku ule aje na rafiki yake na hivyo watakuwa wanne wakipata kinywaji sehemu flani, Mark alionekana kufurahia kwani vitu kama hivyo hapo nyuma havikuwezekana kwake, alimuuliza Eduardo tena kuwa msichana aliitwa nani, Eduardo alimjibu na kuongezea kwa msisitizo kuwa ni mrembo sana,Eduardo alimwambia Mark pia kuwa avae vitu vizuri ili abadilishe muonekano wake
***
Usiku ule ulikuwa ni Mbaya kwa Mark, Mark alikuwa amekataliwa na kuambiwa maneno mabaya na ya kukosolewa na msichana aliyekuwa ameenda nae out, Mark aliona sio sahihi kabisa, yeye ambae tokea high school amekuwa akijiona yupo sawa na hajawahi kutendewa hivyo inakuwaje yeye amtendee namna ile, alikasirka sana na kuona kuwa ameaibishwa sana
Alikimbia mpaka bwenini kwake chumbani kwake na kufika juu ya meza kulipokuwa kuna laptop yake huku pembeni pakiwa kuna desktop ya chuo, aliketi na kuwasha laptop yake, kwa haraka alifungua blog mpya na kuiita jina 'Havard Face mash' na kisha alianza kuandika maneno ya moyoni mwake moja wapo ni kumtukana msichana yule
Alianza-
"Flani (aliandika jina lake) ni mshenzi sana, nahitaji kufikiria kitu kingine ili nimuondoe akilini kwangu, nahitaji kufikiria kitu ambacho kitatawala akili nyangu, ni rahisi na inawezekana ila sasa nahitaji wazo"
Alichukua chupa ya pombe aliyokuwa ameifungua mezani na kunywa kwa hasira,aliigeukia desktop ambayo ilikuwa wazi ikionesha sura/picha za wanafunzi waliokuwa wakiishi bweni hilo, ulikuwa ni utaratibu wa chuo kuweka katika mtandao mahususi kwa kila bweni picha za sura za wanafunzi wa bweni husika, mtandao ulikuwa ukiitwa 'Facebook'. Mark aliigeukia laptop yake na kuendelea kuandika
"Nimelewa kidogo siwezi kudanganya, Kirkland (jina la bweni alilokuwa akiishi) facebook ipo wazi katika compyuta mezani kwangu na baadhi ya hawa watu picha zao ni sura mbaya na zenye kuogofya mpaka nataka niweke picha za hawa watu karibu na picha za wanyama wa kufuga ili watu waweze kupiga kura ni sura ipi inavutia Zaidi"
Mark rafiki yake mkubwa alikuwa ni kompyuta, mbele ya kompyuta yake ndipo palipompa Amani kuliko sehemu nyingine yeyote, marafiki zake wengi ambao alisoma nao waliwasiliana kwa njia ya email na si kupiga simu maana pia walikuwa busy na kompyuta zao kama yeye, isipokuwa Eduardo ambae ndo mara nyingi angeweza kuwasiliana nae kwa simu, alipata kuwasiliana na baadhi ya marafiki zake na kisha aliendelea kuandika
"Sio wazo zuri na pengine sio la kufurahisha lakini Billy(rafiki yake) amekuja na wazo la kufananisha watu wawili kutoka katika facebook na pengine labda kuweka mnyama katikati yao,vizuri sana, nafikiri Billy anawazo"
Mark alianza kuandaa wazo la kutengeneza website ya kuweza kufanyia hicho kitu
"Ndio! Sijui hasa ni kwa namna gani wanyama wa kufuga wataweza kufaa katika hii shughuli yote,kamwe huwezi kuwa na uhakika na wanyama wa kufuga lakini nimependa wazo la kufananisha watu wawili kwa pamoja kwani linaleta mtazamo mzuri maana hata watu hawatapiga kura moja kwa moja bali watachagua namba itakayowakilisha uzuri wa kila mtu, itakuwa kama kwenye hotornot.com.
Kitu kingine, zinahitajika picha nyingi sana kama iwezekanavyo ila kwa bahati mbaya Harvard huwa haina facebook ya umma hivyo picha zote ntaenda kuzichukua kwenye facebook ya kila bweni na watu wake wote waliomo"
Ilikuwa hairuhusiwi kuchukua information kutoka katika compyuta systems za chuo na kwa namna yeyote ile ilikuwa haiwezekani kuingia na kuweza kuchukua picha kwa kuwa kulikuwa kuna security systems zilizowekwa ila Mark kwake yeye aliona inawezekana,aliandika
"Let the hacking begin"
Aliweza kuingia kwenye facebook ya bweni moja baada ya jingine na kukusanya picha na kuziweka katika laptop yake kisha alitumia siku kadhaa kutengeneza website ambayo aliiita 'Facemash.com' na baada ya kumaliza aliwarushia baadhi ya rafiki zake link ya website ile ili waweze kuona alichofanya ikiwezekana wampe mawazo juu ya hicho kitu na kisha aliondoka kuelekea darasani
Baadae alirudi kutoka darasani ili aweze kusoma emails zake, alifika mezani ambapo aliiacha laptop yake ikiwa wazi, hakuweza kuamini baada ya kuona laptop yake imeganda ikiwa inaact kama server ya Facemash.com, kulikuwa kuna jam katika website yake kwani alipowatumia rafiki zake nao pia waliwatumia wengine na mzunguko ukaendelea hivyo hivyo,
watu wengi sana waliweza kuingia katika website ile huku wakaka wakipigia kura picha za wasichana ambazo ndo zilikuwa zikishindanishwa, walipiga kura wakichagua ni nani alikuwa mrembo zaidi kati yao. taarifa zilienea, pia zilifika katika taasisi mbalimbali za maswala ya wanawake kwani kitendo cha yeye kusema kutaka kuzifananisha picha za wasichana na picha za wanyama kiliiwachukiza wasichana wengi
Mark aliogopa sana japo hakuwa na uhakika kama kitu kile hakikuwa sahihi, kwa haraka aliizima website ile na kisha kujitupa kwenye kochi huku moyo wake ukidunda, pengine hakufikiria matokeo yake yangekuaje ila alisukumwa na hisia kufanya vile
***
Mark aliitwa kwenye kamati ya nidhamu pamoja na bodi ya chuo, alishtakiwa kwa makosa ya kuhack systems za chuo na kuchukua picha za wanafunzi, Mark aliweza kujitetea kuwa sio kosa lake bali information zilikuwa zinapatikana kirahisi ndio maana aliweza kuzipata kwa hiyo ni kosa la chuo kuwa na security sysytems dhaifu kiasi kwamba ameweza kuwaingilia kirahisi, hivyo badala ya kumlaumu aliwaambia wamshukuru kwa kuonyesha udhaifu na makosa katika security zao na hivyo alisema kuwa atajitolea kuwarekebishiia kama watataka.
Chuo kilimsamehe Mark na kumfutia adhabu ambayo ingekuwa kufukuzwa chuo
Taarifa zilikuwa zimefika kila kona chuoni hapo kuhusu website ya kufananisha wasichana na kupiga kura ni wasichana wapi walikuwa ni warembo zaidi chuoni pale, taarifa zilifika mpaka kwenye gazeti la chuo lililoitwa 'The Crimson' na kuamwandika Mark kwa sifa mbaya ya alichokifanya.
wasichana wengi walimchukia Mark, Mark alipokea email nyingi au hata barua kutoka kwa wasichana ambao walimtukana, baadhi ya wavulana pia walichukia kwa girlfriend zao kuzidiwa kura na wasichana wengine. Mpaka hapo Mark alikuwa hajaelewa kosa lake ni nini, kwa nini walichanganyikiwa kiasi hicho, hakuweza kuona kama kuna tatizo lolote kwa yeye kufanya vile ambapo yeye anaona alikuwa akijifurahisha tu
Mark alikosa amani, kila sehemu aliyoenda alihisi wasichana wanahasira nae na hivyo watamfuata ili wamtukane alijihisi pia popote alipopita huenda walimtazama na kumnyooshea vidole.
***
Divya alikuwa na gazeti la the crimson mkononi, alienda moja kwa moja mpaka alipokuwa Tyler na kuanza kumsomea habari ya Mark, Tyler alimwita Cameron na kisha kusoma habari ile gazetini, Divya aliwaambia kuwa ni Mark mwenyewe ndie alietengeza website hiyo na kisha kuizima mwenyewe baada ya mambo kuona ndivyo sivyo kutokana na watu kuchukia kitendo kile, aliwaambia kuwa Mark ndie alietengeneza website ya 'course match' kwa kifupi Mark alikuwa ni mtaalamu, Tyler alifurahi kuskia vile na wakajiuliza kuwa watampata wapi Mark, Divya aliwaambia kuwa ameambiwa na Victor kuwa Mark anasoma compyuta science na ni ndio anaweza kuwatengenezea website wanayoitaka lakini Victor pia alimwonya kuwa Mark ni mtoto wa ajabu kidogo, wakaulizana kivipi, Divya akawaambia kuwa ni 'mwoga wa watu'
"mtafte basi huyo Mark tuone kama anataka kuwa sehemu ya historia" aliongea Tyler
***
Mark alikuwa ameketi chumbani kwake, alimwita Eduardo na kumwonesha email aliyotumiwa, Eduardo alianza kuisoma email ile iliyoandikwa kuwa imetoka kwa Divya, Cameron na Tyler Winklevoss, katika email hiyo walieleza kuhusu website ambayo walitaka kuitengeneza na kuomba waonane na Mark ili wazungumze kwani wangependa sana kushirikiana nae katika hicho kitu hivyo awataarifu kwa email au simu waliyoandika hapo ni lini wataweza kuchat au kuonana ili waweze kuzungumza zaidi.
Mark alimuuliza Eduardo kuwa anafikiriaje kuhusu suala hilo, Eduardo alimwambia kuwa aachane nao, Mark alijibu kwa nini isiwe, japo Mark alionesha uhakika lakini Eduardo hakuwa na imani kwani alimfahmu Mark, aliwaza kuwa Mark na watoto kama wale wapi na wapi, walikuwa ni watu wawili tofauti, alifahamu pia ilihitajika kazi ya ziada pamoja na muda kumwelewa Mark hivyo aliwaza watapatana vipi! ila kwa vyovyote vile, Eduardo hakutaka kufikiria sana aliamua kumwachia Mark na maamuzi yake maana siku zote hufanya anachoamua na kujiskia
***
Cameron na Tyler waliweza kukutana na Mark na moja kwa moja kuanza kuzungumza kuhusu suala lao
"Tutaiita Harvard connection, itakuwa na site mbili, moja ya mahusiano na nyingine ya kuunganisha marafiki, utakuwa ni mtandao ambao wanafunzi wa Harvard wataweza kukutana, kutafutana na kubadilishana taarifa mbalimbali, wanafunzi wataweza kuweka picha zao na maelezo yao binafsi ili kuweza kutaftana na wenzao wanaowafahamu"
Tyler aliendelea kuelezea kwa undani kuhusu website hiyo na kumweleza Mark kuwa hicho kitu wanachotaka kukifanya ni kikubwa kwani kitajulikana chuo kizima mapaka gazetini na hivyo itasaidia kumsafisha Mark na sifa yake ya website yake iliyofananisha wasichana, Tyler alimwambia " utweza kurudi gazetini kwa sifa nzuri na sio kama mwanzo, hivyo utaweza kujisafisha"
Mark alionekana kuvutiwa na kuelewa vizuri hicho kitu walichokitaka, aliomba ajue ni wapi yule aliyekuwa ameanza kufanya aliishia, cameroon aliweza kumwambia ajionee mwenyewe, Mark aliweza kuangalia na kuona ilikuwa ni kazi ndogo tu iliyopo ambayo ingechukua masaa kama kumi na matano na kuweza kumaliza, aliwaambia kuwa yupo tayari na hivyo atafanya kazi hiyo.
Tyler na Cameron waliondoka wakiwa na furaha wakijua siku chache wataenda kutimiza kitu kitakachobadilisha maisha yao ambacho wamekuwa wakikiwaza muda mrefu
***
Masaa yalipita siku zikapita na wiki zikapita, mwezi ukakatika, chuo kikafungwa na wanafunzi wakaenda majumbani kupumzika kwa ajili ya sikuu ya christmas na mwaka mpya, Mark pia alienda nyumbani kwao huku Eduardo yeye akibaki chuo
Chuo kilifunguliwa Mark na wanafunzi wengine walirudi chuo. Siku zote hizo Mark amekuwa akiendelea kufanya mawasiliano na kina Divya, Cameron and Tyler kuhusu kutengeneza website yao aliyosema ataitengeneza, kila siku aliwaambia kuwa ataitengeneza na kuwaambia kuwa amebanwa na masomo na project nyingine hivyo waendelee kumvumilia, waliendelea kumvumilia huku wakiendelea kuwasiliana nae
***
Eduardo alikuwa ndani ya bar ya chuoni hapo, alikuwa amekunywa kiasi flani ili kutuliza akili, alikuwa anaskia uchovu uliotokana na shughuli za siku hiyo nzima, baada ya kumaliza alisimama na kuamua kuondoka kwenda kupumzika, alipokuwa akitoka alimwona Mark akiwa anazunguka zunguka mle bar huku akiangaza angaza, ni dhahiri kuwa ailikuwa akimwangaza Eduardo.
Eduardo alimfuata na kusimama mbele yake, Mark alishangaa kumwona Eduardo mbele yake, Mark alimvuta Eduardo na kwenda kuketi kwenye viti, Eduardo aliona uso wa Mark ukiwa wenye kutaka kusema jambo tena lililomvutia.
Mark alianza
" Nafikiri nimekuja na kitu akilini mwangu"
Mark alielezea, alianza kwa suala lililopita mwezi wa nyuma juu ya tukio la website yake ya Facemash, alimwambia Eduardo kuwa amekuwa na wazo ambalo amekuwa akilifanyia kazi kichwani mwake tangu siku ya tukio la Facemash, alieleza kuwa katika tukio lile aliona jinsi watu walivyoingia katika website yake na kuweza kupiga kura,
Aliona jinsi watu walivyovutiwa na kufurahia kufanya vile hii ni kutokana na kuwafahamu watu waliowaona katika mtandao ule maana kuna mitandao mingi inapost picha za watu warembo kama wangetaka wangeenda kuwaangalia warembo kule lakini watu wengi walivutiwa na Facemash kutokana na kuwa watu hupenda kutazama mtandaoni watu wanaowafahamu.
Hivyo alistaajabu na kufikiria kuwa kama watu wengi wanapenda kuingia mtandaoni na kuangalia watu wanowafahamu ni kwanini asitengeneze website ya kufanya hivyo? itakuwa ni jamii ya marafiki mtandaoni ambao wataweza kuweka picha, profiles na vingine vyovyote, yaani itakuwa kama mtandao wa kijamii, utahitaji kumfahamu mtu ambae utakuwa ukimtafuta katika mtandao huo na yaani itakuwa ni mawasiliano ya marafiki walio halisi katika dunia,
mtandao huu hautakuwa kama Facemash ila wenyewe utakuwa tofauti kwani watu wenyewe wataweza kuweka information zao na picha zao kwa hiari na sio hacking tena, watasema wanaishi wapi, wanasoma wapi, wamekulia wapi, wanavutiwa na nini na wanatafuta nini na pia mtu atakuwa na uwezo wa kumwalika rafiki yake kuweza kujiunga nae.
Mark alimalizia "nafikiri tutarahisisha na kufupisha kwa kuuita mtandao huu 'Facebook'
Eduardo alitoa macho kwa mshangao kwa maelezo yale aliyoyaskia aliona lilikuwa ni wazo moja zuri sana, alijaribu kutafakari mitandao mingine ya kijamii na kuona wazo hili la Mark ilikuwa na utofauti mkubwa sana na mitandao mingine, watu mbalimbali walikuwa na mawazo ya kutengeneza mitandao ya kijamii lakini wazo la Mark ililikuwa ni la aina yake, Eduardo aliweza kuwaza na kufikiria mtandao wa Cameron na Tyler waliomwambia Mark awetengenezee, aliona kuwa ulikuwa na utofauti na hili wazo la Mark na alitambua kuwa Mark alikuwa bado hajawafanyia kazi yoyote ile mapacha hao,Mark hakuwahi kumwelezea Eduardo kiundani kuhusu mtandao wa mapacha hao bali alikuwa akitaja tu kuwa ni mtandao wa mahusiano
Eduardo alijua kuwa Mark bado aliendelea kuwasiliana nao japo kazi alikuwa hajaifanya,hakujua ni kwa nini Mark alifanya vile, Eduardo alijua siku zote Mark ni mtu wa tofauti sana, asingeweza kupoteza muda wake kuwatengenezea mapacha wale website yao ili kusudi awafurahishe au apate sifa nzuri kwani Mark ni mtu asiejali na hufanya anachoamua, Eduardo alihisi pengine wale mapacha hawakumwelewa Mark, kwamba walifikiri Mark atakimbilia kuwatengenezea website ile ili ajipaishe aonekane na yeye na watoto wale, Mark hakuwa wa namna ile ,
Eduardo aliwaza kuwa huenda Mark anataka kushindana na watoto wale waliotaka kutumia uwezo wake kutengeneza website yao wenyewe, watoto ambao walifikiri kuwa wanatawala Dunia yote, huenda walitawala Dunia na kujulikana katika jamii lakini katika dunia ya website na kompyuta Mark alikuwa ni mfalme wao.
"Yeah ni wazo zuri sana" Eduardo alimjibu Mark, Mark ambae alikuwa na shauku kubwa na project yake hiyo aliyotaka kuitengeneza ambayo anamwomba Eduardo washirikiane.
Eduardo alijiuliza ni kwa nini Mark amechagua kutaka kushirikiana na yeye wakati yeye hana maarifa yoyote yale kuhusu kompyuta, alijiuliza kwa nini amchague yeye asie na ujuzi wa kompyuta na kumwacha roommate wake aitwaye Dustin Moskovitz ambae pia alisoma kompyuta science na alikuwa na ujuzi mzuri tu wa maswala ya kompyuta na kidogo pia nae alikuwa ni genius!
Mark aliendelea, na ndipo Eduardo akagundua sababu ni kwa nini
"Lakini tutahitaji pesa ya kuanzia ili tuweze kufanikisha project yetu" Mark alimwambia Eduardo.
Mark alihitaji pesa ili aweze kufanikisha project yake nzima, alihitaji pesa ili aweze kukodi servers na kuwa online na ndio sababu kubwa ya yeye kumshirikisha Eduardo, yeah familia ya Eduardo ilikuwa ni familia tajiri na hata Eduardo mwenyewe pia alikuwa na pesa, Eduardo hakusita kukubali
"Ndio niko tayari kushirikiana nawe" Eduardo alijibu huku akimshika Mark mkono, alikubali kuwa atatoa pesa pamoja na ushauri na pia atawezakumwongoza Mark katika project hiyo kwa jinsi hata ambavyo Mark asingeweza kufikiri, kumwongoza katika njia ya biashara kwani Mark hakuwa na akili ya biashara hata kidogo
Eduardo alimwuliza kingehitajika kiasi gani katika wakati huo, Mark alimtajia, Eduardo akasema hakuna shida kwani kilichopo ni kwenda tu bank na kuchukua pesa.
"Tutagawana kampuni asilimia sabini kwa thelathini" Mark mwenyewe alijiwahi kusema
"asilimia sabini za kwangu, thelathini za kwako. Utakuwa CFO (Chief financial officer) wa kampuni" Mark alisema.
Eduardo aliona kuwa ilikuwa ni sahihi ukizingatia wazo lilikuwa ni la Mark mwenyewe, japo hakujua kama project hiyo itazaa matunda au la alikubali kujiitolea bila kujali kwani aliona dalili za mafanikio kutokana na wazo la website hiyo kuwa tofauti na website ziingine
" Hii itavutia sana" alisema Eduardo
ITAENDELEA.........
Sehemu ya pili ipo hapa: THE ACCIDENTAL BILLIONAIRES- The founding of facebook: a tale of money,genius and betrayal
Sehemu ya tatu ipo hapa: THE ACCIDENTAL BILLIONAIRES- The founding of facebook: a tale of money,genius and betrayal
Sehemu ya nne ipo hapa: THE ACCIDENTAL BILLIONAIRES- The founding of facebook: a tale of money,genius and betrayal
Sehemu ya tano ipo hapa: THE ACCIDENTAL BILLIONAIRES- The founding of facebook: a tale of money,genius and betrayal