Mkuu hapa kwenye wanaoenda nje hawakumbuki nyumbani si kweli hata kidogo.Ujamaa ulikuwa na faida nyingi sana kuliko unavyofikiri wewe. Hata kiswahili ni lugha inayotuunganisha. Tatizo hapa ni watu kukosa uzalendo. Hasa nyie mnaoenda nje ya nchi hamkumbuki nyumbani.
wanajamvi!
Tuseme ukweli wakenya wametuzidi kwa mengi. Wanajituma kwenye kazi, zaidi si spenders kama sisi(kuanzia serikali mpaka mtu binafsi mfano kwao waziri anapanda passat(saloon car),unaweza kukuta mkenya tajiri mwenye majumba kila kona na makampuni kadhaa anatembelea toyota probox. Tembea kenya hususani miji mikubwa (nairobi, kisumu, mombasa) uhesabu investments kubwa kubwa real estates,apartments,majengo makubwa,supermarkets,kampuni kubwa za insurance, constructions, media houses (tv stations, publishing), airlines, kampuni za mabasi yanayosafiri ndani na nchi jirani kwa aslimia kubwa yanamilikiwa na wakenya wenyewe na wameajiri wakenya wenzao(suala la kabila gani ndo wanaajiriwa usiniulize leo, mimi naanagalia wakenya ndo walioajiriwa). Sasa njoo tanzania serikalini matumizi ni makubwa kupitiliza magari ya kifahari, watanzania wa kawaida ni spenders mtu anatembelea toyota land cruiser v8 lakini hana investment ya maana. Zaidi watanzania ni wavivu kupitiliza, nenda hoteli hapa tanzania ukimka asubuhi ya saa 12 ukiuliza chai unaambiwa bado. Nenda kalale hoteli za kenya saa 12 kasoro chai tayari so unakunywa chai then kama unasafiri muda huo unaendelea na safari zako.
Kubwa kupita yote, kenya wanathamini elimu kuliko vitu vyote (nikisema elimu simaanishi elimu ya vyuo vikuu tu) kuanzia shule ya msingi, sekondari na kuendelea) kwao mpaka mtu wa saloon anasomea na ukienda saloon utaona tofauti na saloon za kibongo). Lugha ya kiingereza nayo imetufanya tujione wanyonge sana mbele yao. Wakenya ni wepesi kutafuta opportunities hapa usa wakenya wamejaa, ukienda uk ndo usiseme, saudi arabia, south sudan, tz, uganda, south africa ndo balaa na wakipata hela zao wanaenda ku-invest kenya. Ndio maana makaburu (south africa) wanashindwa/wanapata wakati mgumu kuinvest kenya maana competition kenya tofauti na tz hakuna competition na watz hawathamini bidhaa za kwao(tz).
Hata kama ni hivyo mbona wametuzidi mambo mengi wakati tuna rasilimali nyingi kuliko wao bwanaNa wewe unakiri kushundwa??. yaani huna confidence, una longo longo huwezi kudeliver??. Hakuna watu wenye longolongo kama wakenya,.
Tulishindwa kuweka misingi imara katika kila nyanja baada ya kupata Uhuru, kwa miaka 24 tumetawaliwa kidikteta nakila alichosema Rais tulilifata "blindly", maamuzi mengi yaliyofanywa wakati huo ndio yamekuwa chachu ya maporomoko ya kila kitu Tanzania.
Baada ya kugundua hilo tufanye nini maana miaka 24 unayosema ni ile ya baba wa Taifa ambapo mwisho wake ilikuwa 1984, na kutoka 1984 mpaka sasa ni miaka 28. Toka 1984 tumefanya nini kubalisha hiyo hali na tufanye nini baada ya kugundua tatizo hilo
Shule za Sekondari zaidi ya 5,000 kwa sasa (zilikuwa chini ya 500 wakati wa Nyerere (na zote za kurithi kwa mkoloni), wanafunzi vyuo vikuu zaidi ya 300,000 (wa ndani tu ya nchi) mbali wanaosoma kwa jitihada zao nje ya nchi.
Huu ni msingi mwema sana. Tumeshaanza kuona manufaa yake inabidi sasa tuongeze ufanisi kwa kuziboresha na kuziboresha kutaanza kuwa na maana pale tu tutakapo anza kupata waalim waliosoma ambao ndio hao tunawasomesha sasa..
Anyway, hilo li super highway wamejengewa na waChina. Kuanzia wazo mpaka kulijenga na kuchora hiyo mistari wamefanya wachina.
Ukweli ni kwamba hakuna namna mwaafrika atakaa awaze na kujenga barabara kama hilo. Na akijaribu, huo mradi hautafika mwisho kabla hela zote hazijaibwa. Hata umsimamie na mtutu wa bunduki haitasaidia
Safi sana mkuu kwa maneno mazuri ila hata hivi vyuo tulivyonavyo tunahitaji kuvitanua kwani idadi ya wanachuo in relation to facilities haiendeni, shule nyingi za msingi zina wanafunzi kuanzia 800 mpaka 1500 wakati sera inatuambia shule moja wanafunzi 560 ukienda shule za serikali za secondari nyingi ni double session yaani idadi ya wanafunzi waliopo nao ni kubwa kulinganisha na majengo. Nadhani kwa kuanzia si mbaya ila tunahitaji tukimaliza la waalimu nadhani bado kazi ya ujenzi wa shule na madarasa ya kutosha unahitajika ili darasa moja liwe na watu 40 kuanzia primary school to university. Kwa utaratibu huu wa wanafunzi wengi facilities chache mwisho wa siku tunapata wataalamu ambao si makini mfano mzuri siku hizi multiple choice questions in exams ni kuanzia primary school to university kwa kuwa walimu wana wanafunzi wengi hivyo anaona akitoa mtihani wenye maswali ya kupima general knowledge atapata wapi muda wa kusahihisha wakati ana wanafunzi 400 anafundisha kwa madarasa tofauti, mwisho wa siku tunapata wataalamu ambao hawajaumiza vichwa kufikiri hence poor performance, otherwise contribution yako nzuri.
Ndio kwanza tumeanza kuweka misingi ambayo haikuwekwa na waliopewa madaraka mwanzoni, itatuchukuwa muda kuweka kila kitu sawa, ndio kwanza tunaanza kuwaelimisha raia wetu kwa kiwango cha juu, waliopewa madaraka mwanzoni waliishia kuwasomesha wengi kwa kiwango cha kujuwa kusoma magazeti na kuandika barua za kifamilia.
Sasa tunaona Serikali ya awamu hii, ikikazana kutuondoa huko na kutupeleka kwenye kisomo cha juu, ni hii miaka 7 tu iliyopita tumeona zaidi ya shule za sekondari 5,000 zikijengwa, vyuo vikuu vipya karibu viwili kila mwaka kwa miaka 7 sasa ya Kikwete.
Waliopita wangeyanfanya hayo, saa hizi tunaongea mingine. Tuna safari ndefu lakini ni vizuri kuw Kikwete kaanza kuifupisha hiyo safari.
Hapo kwenye red: "uswahili" mwingi. Uswahili si lugha tu bali ni utamaduni pia. Sisi watz tu waswahili si kwa kuwa tunaongea lugha (kiswahili tu) bali pia tu waswahili wa utamaduni licha ya wingi wa makabila yetu. Na moja ya sifa ya waswahili ni upigaji wa domo, soga bila kuwa siriaz kwenye kazi za maendeleo. Sifa hii imewajaa wengi. Tunakosa seriousness ktk kazi, kujiamini kudogo, kuridhika kwa sana kwa mafanikio kidogo, kukosa ambition ya maendeleo, kupenda vya dezo na starehe bila jasho. Kwa kifupi wengi ni dull. Ndiyo uswahili huo.fikra za ujamaa na uswahili mwingi. Maendeleo hayaji kwa lelemama, yanahitaji kujituma. Lets be serious, otherwise ni aibu tupu. Hivi nchi hii Mungu ametupa kila kitu tunaweza kumlaumu nani kwa umaskini na aibu hii. Nipo nje ya nchi na ninapokutana na watu ukiwaambia umetoka tz, they associate it na umaskini, what a shame. Leaders ndio kila wakati kuzurura kuombaomba wakati sisi ndio tungetakiwa kuombwa.
Kinachotokea tanzania ni kwamba kutakuwa na tabaka la wale walio matajiri kutokana na juhudi zao, na lile la umaskini wa kutisha ambao wataendelea kulaumu kila mtu kwa hali zao. And then there will be a fight between. Kwakuwa tabaka la juu litakuwa na nguvu, wajipanga kujihami kama ilivyo marekani, mabunduki kila mahali