Hivi Wakenya wametushinda nini?

Hatuna Viongozi wenye mipango.Nathubutu kusema kwamba Kenya kuongozwa na Rais kama Kenyatta junior ni bonge la bahati kwakweli.Kenyatta is a typical Nationalist anayepambana kuijenga Kenya kuwa an economic force to be reckoned with.Sifa kubwa zimwendee Rais Mchumi Bwana Mwai Kibaki kwa kuweka mipango mizuri ya uchumi wa kisasa na sasa Kenyatta anataka kuimalizia mipango ya Predecessor wake na hata kwenda mbele extra miles.Natamani Tanzania tungekuwa na Intelligent & smart leader kama Kagame.Kagame anaiangalia Dunia kama ninavyoiangalia mimi.Kwa mtazamo wangu vita vya kiuchumi wa kileo vinapiganwa katika uwanja wa Information Technology(IT).Masoko,Ajira,Elimu na biashara na uchumi kwa ujumla vinaendeshwa ki-electronic zaidi eneo ambalo Kagame wa Rwanda ameliona na ameanza kulichangamkia lakini sisi huku Tanzania Serikali ndio kwanza inali-discourage hili eneo nyeti kwa kuli-stiffle na kodi pamoja na tozo zisizokuwa na kichwa wala miguu.Hii ni ishara kwamba Serikali haijajua umuhimu wa IT katika kukuza uchumi.
 


hivikwa nini hizi multinationals zinaenda nairobi na sio dar?

 
Tunatakiwa tujifunze toka kwa wenzetu wakenya, kuna kitu wametuzidi inapokuja mambo ya national interest na pia ambitions ya wakenya kwa ujumla.
Lazima vitu vingine tukubali.
Wakenya wangekuwa kama walivyo sasa ila BILA ukabila, wangekuwa mbali sana!
 
ujamaa ndio chanzo cha yote haya. wao wanaitana bwana sisi ndugu. Meneja unamwandikia barua ya onyo mfanyakazi unaanza ndugu,yahusu kuchelewa kazini. Hivi ndugu atakuelewa kweli. Kuwepo kwa bahari kumeleta jamii za kivivu sana kazi ni kuvua samaki basi na kulala hamna kwenda shule wala kulima.Kenya kila mtu kivyake na watu wanapigana vita sana kugombea fursa hata kama inamuongezea senti chache. Mtu akiipata fursa anaitumikia maana watu wamemtolea macho. Tanzania kuna ulevi unaoitwa amani . Kwa ajili ya amani usiandamane, usigome, ukiibiwa hata kura unyamaze,wakininiii escrow mshangilie mkinyamaza mnaukabila au mnaonea wivu dini nyingine na summary yake ni uvunjifu wa amani. Ifikapo 2015 November kama siasa hazitobadilika nitachukua maamuzi magumu
 
ccm wanajua kuficha hela ulaya na kupiga dili
 
ccm wanajua kuficha hela ulaya na kupiga dili

ule uwanja wa dar unavuja
 


nimecheka sana heheeeee
 
Si tulichagua sura. Na hb kaitembeza kweli sura. Kikwete namchukia sana, najua alikua na nia nzuri lakini lazima angejitambua kuwa uwezo HANA. Wabongo hawa sio wakukenuliwa meno tu hovyo siku zote. A leader in africa needs 1st to be feared then respected. Sasa an airhead yule dah. Anyways we got what we deserved. Ila tusifanye ujinga huo tena jamani CCM HAWATUFAI tutaendelewa kuachwa mpaka na Burundi hapa tubaki kuongoza kwenye big brother na mtv africa.
 
Tatizo la Tanzania kuwa nyuma ni viongozi tunaowachagua. Tunakimbilia kuchagua watu kwasababu hatujui makabila yao eti kwa kuogopa ukabila, hivyo tunajikuta tunawapa urais kwa upendeleo na sio utendaji kazi wao.

Wakati umefika kuchagua watu wanaochapa kazi na walio aggressive, watu wanaojua uchumi ni kitu gani, watu wanaojua biashara zinafanywa vipi, watu wenye uchungu na fedha na rasilimali za nchi hii, watu wenye uzoefu na uwekezaji, watu wasiowaonea mafisadi aibu.

Hadi tutakapofanya hayo, tutabaki tukiwaona wenzetu wakitimua mbio angali tumesimama.
 
Tofauti: Viongozi wa Kenya waiba na kujenga. Viongozi wa Tanzania waiba lakini hawajengi.

Kote kuna rushwa. Kenya wanakula lakini kusudio linatimia. Tanzania wanakula rushwa lakini kusudio halitimii.
 
CENTER]KAA has welcomed China's biggest Airline, China Southern Airlines to Jomo Kenyatta International Airport












​
[/CENTER]
 
Uhuru tours JKIA and directs KAA to improve the passenger handling capacity
NTV Kenya | 17 June 2015


​
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…