Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,550
- 6,062
Ni kweli ndugu wengi hawajui kiswahili... ni ajali ya kihistoria ikiwa ni pamoja na madhara ya vita Tz waliyopigana kumg'oa Iddi Amin Uganda.Askari wetu walikuwa wanaongea kiswahili lakini pia majambazi na wahalifu wakawa wanaitumia lugha hiyo katika matukio.Hii ikajenga chuki dhidi ya kiswahili ambapo kilionekana ni lugha ya majambazi!
WOS,
Hili jambo la history ni kweli. Ila angalia maneno ya JAFAR hapa chini yanatofautiana kidogo na yako. Pia askari wa Tanzania hawakukaa sana Uganda kiasi kwamba hilo tatizo liwe la muda mrefu. Ni sawa na shangazi yangu alikuwa akisema kuwa walivamiwa na askari wenye PUA kubwa kama domo la bata na walikuwa wakiwaita MA-KUYA. Nilikuja baadaye kugungua walikuwa Wacongo hasa baada ya kumuona Urlus Mabele na pua lake na wap hawasemi KUJA ila KUYA. Ila kwa kuwa walikaa kwa muda mfupi, husikii hata leo hii madhara ya Wacongo kuchukiwa Tanzania.
Usiwalaumu sana Waganda, actually tunatakiwa tuwasaidie kukijua kiswahili. Waganda kutopenda kiswahili kinatokana na historia ya nchi yao. Enzi zile za Idd Amin Dada (RIP), kiswahili kilikuwa kinatumika sana na watu wake wa karibu, hasa hasa Jeshi. Kwa kuwa wanajeshi walikuwa wanyanyasaji, wabakaji na sifa zote mbaya walikuwa nazo, hivyo basi huko mtaani ukiongea kiswahili ulikuwa unatengwa, maana inawezekana 100% wewe ni wa Amin na unahatarisha maisha ya watu. Idd Amin mwenyewe alikijua kiswahili.
Historically, mpaka leo waganda wana kasumba hiyo.
Jafar,
Kuna rafiki yangu mmoja aliniambia juu ya hiyo kesi. Akasema enzi hizo ukisema Kiswahili, basi hata Polisi watakuachia. Jamaa akikuta mnacheza mpira na aseme kiswahili kuwa na yeye anataka kucheza, basi alipewa namba na mmoja wenu kuondoka. Hawa jamaa (askari wa Amini wenye kuvaa mashati ya vitenge) walikuwa WANAOGOPWA sanaana. Sidhani neno WALITENGWA lilikuwepo. Walichotaka wao walipata ila sema hata kama watu walikuwepo nao basi hao watu WALIKUWA WANACHEKA husu USO UMEKUNJAMANA na hofu juu ya kwamba utasema neno jamaa akugeuzie kibao. Hawa jamaa walikuwa kama miung watu, wakifanya watu chochote wanachokitaka.
Ila sasa wameanza kubadilika. Hebu msikie Jose Camelleon, jama ana-rap Mashairi kama hana akili vile..... "alisema yeye halagi UGALI, nikamkimbia na kumuacha KIGALI,........"