Hivi Waganda wana matatizo gani na Kiswahili

Kweli wanaboa. Pia kingereza chenyewe na accent yao tofauti. Kuna binti alisoma mlimani 4 yrs law, siku nikamtumia email ya kiswahili, eti akajibu nimempa wakati mgumu. Ila si wote
nimesoma nao hapo UDSM tulikuwa tunaishi hall four wote, wana tabia ya kujitenga sana hawa jamaa na kufanya mambo yao kwa siri kama wachawi
 
Na kweli umesema. Hawa Waganda mambo yao sielewi kabisa. Watajifanya hawajui Kiswahili lakini kadri mnavyo endelea na mazungumzo, unasikia atoa contribution. Swala langu ni hili, kama huelewi lugha mbona unachangia katika mazungumzo? Huo sio utapeli kweli au ndio sophistication.

Kuna difference between "kuelewa" na "kuongea" kwa hivyo husiwahukumu.
 
Ni kweli ndugu wengi hawajui kiswahili... ni ajali ya kihistoria ikiwa ni pamoja na madhara ya vita Tz waliyopigana kumg'oa Iddi Amin Uganda.Askari wetu walikuwa wanaongea kiswahili lakini pia majambazi na wahalifu wakawa wanaitumia lugha hiyo katika matukio.Hii ikajenga chuki dhidi ya kiswahili ambapo kilionekana ni lugha ya majambazi!
Uko sawa kabisa most of my friends waganda wananiambia the same
 
kuna baadhi ya maeneo wapo vizuri kwenye kiswahili kwa mfano maeneo ya kusini mashariki ya ug!
 
Mkuu, hapa umenena! Waganda si tu kwamba wengi wao hawakijui kiswahili, lakini pia hawakipendi. Unajua kwa nini? kwa sababu waganda kwa tabia yao ni watu wa kujisikia bora sana, na wanaona vyao tu ndiyo bora na vizuri. Nakumbuka nilikuwa na rafiki yangu mmoja hap Tz mganda daima alikuwa anasifia vya kwao tu: mara konyagi yao ni bora kuliko ya TZ, bia ya kwao umegemwa vizuri zaidi, kahawa ya kwao juu, wasichana wa kwao bomba, nk, nk. Ajabu na kweli!

Kumbe wana aina ya majivuno na madharau kwa watu wengine. wao kujifunza na kuongea kiswahili wanaona ni kujidhalilisha, kujishusha, kutoonekana wa maana.

design ya wahaya fulani hivi

makabila yote 51 ya uganda wanalazimika kujifunza ki Luganda ambalo ndilo kabila kubwa kabisa na poweful, sasa washakuwa watumwa wa ndani ya nchi yao, tena waje kwa kiswahili inakuwa ngumu

kuna semina/warsha nyingi zinawahimiza wajifunze kiswahili
 
mkuu usiumie hii lugha inazungumzwa kuanzia uingereza hadi marekani sembuse hapo kampala. achana nao watashtuka kumekucha
 
Tatizo kubwa kiswahili uganda kilikuwa kinatumiwa na majambazi mfano vunja mlango,kaa chini,toka nje, fungua mlango etc hivo waganda wakachukia kiswahili pia ata jeshi la id amin mpaka sasa lugha inayotumiwa kufundisha polis na wanajesh uganda ni kiswahili
 
Ee wakenya kiswahili chao ndiyo hivo tena. Ila cha ajabu kule ng'ambo wakenya ndiyo wanaotambuliwa zaidi kwamba ndiyo wazungumzaji wa Kiswahili na si watanzania. Aisee, wale jamaa wanajua kujiweka mbele na kujitangaza.

Kuna msemo kuwa: 'Kiswahili kilizaliwa Tanzania, kikakulia Kenya na kikafia Uganda'
 
nimekaa kidogo kampala kwa kipindi fulani, kumbukumbu zangu ni nzuri tu kutaka kupewa mke na rafiki yangu wa kiganda..
 
Kuna difference between "kuelewa" na "kuongea" kwa hivyo husiwahukumu.
hapo kwenye red, siku nyingine andika "usiwahukumu" na sio husiwahukumu. au na wewe ni mganda? ndio maana operation kimbunga ilifanikiwa, ni kumwambia tu mtu ongea kiswahili au imba wimbo wa taifa....
 
Kuna mmoja nimesoma nae chuo miaka kibao na mpaka leo hii tumemaliza hajui kuongea kiswahili.., zaidi ya kudokoadokoa neno moaja moja..
 
Mimi kuna kijana nimemfundisha kiswahili na sasa anaongea vema kabisa,, niiishi nae kwangu dar na nikapiga marufuku kiigereza home off course familia yangu ya kiswahili na kwa vile nilikua mtu wa kusafiri ika mlazimu ajifunze ili awasiliane na wana familia ,, leo aninishukuru sana ,, anasema lugha hii ni nzuri ila anasema hawakuipenda maana ilikua ni lugha ya Idd Amini na wanajeshi ,, so kiswahili hukiona kama lugha ya watu katili na wajanja wajanja... kwa Kongo hasa mashariki ya kongo lingala inakufa kwa dhana hihii maana ni lugha ya FRDC (jeshi la Kongo) so watu hasa generation mpya wanapenda kiswahii na French kuliko lingala
 
watu tumekwenda mpk komoro n tukakikuta kiswahili kama dawa.lugha tamu hii asikwambie mtu
 
Kweli wanamiss kitu, wanashindwa kuangalia nchi karibu zote zinazowazunguka wanazungumza Kiswahili. Pia, sijajua kama hii documentary ya Iddi Amin ni kweli au la, achana na ile movie yake, kuna documentary ya Iddi Amini. Alikuwa anakung'uta kiswahili mpaka basi. Watoto wake wadogo lugha ya nyumbani anawaongelesha Kiswahili. Hawa Waganda wa sasa sijui vipi? Alafu Museven yeye anakibamiza ka mTz.
 
ni ukweli usiopunguka kuwa wakenya ndio wanaoongea kiswahili fasaha na ndio wanaoitendea haki sarufi. lafudhi yao ndio kivutio kikubwa kwa wamagharibi japo sio nzuri ila ni orijino

hapw kwetu ZnZ wanajitwhidi

kwa hapa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom